Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Friday, April 26, 2013

YANGA yatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, baada ya timu ya Azam kutoka sare ya kufungana bao 1-1, na wenyeji Coastal Union mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Katika mchezo huo, ulichezesha na mwamuzi Adrew Shamba kutoka Pwani ambaye alilalamikiwa kushindwa kulimudu pamano hilo kutokana na maamuzi yake, wageni ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao, liliwekwa kimiani ni beki Agrey Moriss kwa penalti dakika ya 60.

Morris alifunga penalti hiyo iliyotokana na mchezaji wa Coastal Yusuph Chuma kugongana na mchezaji wa Azam Gaudence Mwaikimba na mwamuzi huyo ambaye hakuwa ameonesha kuwa ni pigo la penalti lakini baadaye akasema mpira huo upigwe kuwa penalti.

Coastal ambao wachezaji wake walikuwa wakicheza bila ya kuwa na 'presha', walisawazisha bao hilo lililofungwa na mtokea benchi Danny Lyanga ambaye mpira wake wa kwanza kuugusa alifunga bao hilo baada ya kuukuta mpira uliokuwa umepigwa na Pius Kisambale na kuiandikia timu yake bao la kusawazisha na kuifanya Yanga itawazwe kuwa bingwa wa ligi hiyo.

Azam ikishinda michezo yake yote iliyobakia itafikisha pointi 54 ambazo tayari zimepitwa na yanga waliokuwa na pointi 56 na michezo miwili mkononi dhidi ya Coastal Union Jijini Dar mei Mosi mwaka huu kisha na mahasimu wao Simba.

POST HII WAPENDWA WAPENZI TUMEIWEKA KWA MAJARIBIO KABLA YA KURUDI TENA KWA KASI YA AJABU PINDI TATIZO LINALOSABABISHA BLOGU YAKO HII YA MZEE WA BONDE ISIWE HEWANI KUMALIZWA.