MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (mstaafu) CHIKU GALLAWA AKIFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA MAOFISA WA TAKUKURU MAKAO MAKUU, MIKOA NA WILAYA ULIOFANYIKA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT-TANGA |
Na Mashaka Mhando,Tanga
MKUU wa mkoa wa Tanga, luteni (mstaafu) Chiku Gallawa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuongeza kasi ya kufuatilia fedha zinazopelekwa na serikali katika halmashauri nchini ili ziweze kutumika vizuri kwenye miradi mikubwa ysa maendeleo iliyokusudiwa.
Akifunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa takukuru kwenye hoteli ya Tanga beach Resort kwa maofisa wa taaisis hiyo kutoka mikoa yote ya tanzania bara, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa takukuru wamebeba dhamana kubwa ya kustawisha maendeleo kwa kufautilia watendaji kwenye halmasauri ambao wanatumia vibaya fedha zinazoolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo.
Amesema serikali hasa ya awamu ya nne, imekuwa ikitoa fedha nyingi katika halmashauri kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maeneleo hasa ya elimu, afya, barabara na kujenga majengo mbalimbali lakini fedha hizo wakati mwingine zimekuwa zikitumika visivyo na hivyo kuleta malalamiko kutoka kwa wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa pamoja na kuipongeza taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuokoa fedha za serikali kiasi cha shilingi bilioni 97.5, lakini ameitaka takukuru kuhakikisha inaongeza kasi ya mapambano ya rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi.
Kuhusu wananchi mkuu huyo wa mkoa amewataka kutoa ushirikiano kwa taaisis hiyo na waache kulalamikia masuala ya ufisadi wakati kama watatoa ushirikiano masula hayo yanaweza kudhibitiwa kwa watu kuogopa fedha za umma hatua ambayo mwelekeo wa taasisi hiyo inakoelekea na kwamba waongeze jitihada kutumia nyenzo walizokuwa nazo katika mapambano hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala la mapambano ya rushwa ikiwemo kuwafundisha watumishi wake kwenda sambamba na mabadiliko ya teklonojia katika masuala ya rushwa.
MWISHO
Mkuu tupo pamoja,
ReplyDelete