Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Tuesday, January 31, 2012
Monday, January 30, 2012
MH GALLAWA AWAPASHA MADAKTARI NA MANESI BOMBO, ASIYETAKA KAZI AONDOKE
KATIBU TAWALA WA KOA WA TANGA, BW. BENEDICT OLE KUYAN (KATIKATI) AKIWA NAYE NI MIONGONI MWA VIONGOZI WALIOFIKA KWENYE HOSPITALI HIYO. KUSHOTO KWAKE NI BREGEDIA GENERAL MWANGWAMBA. |
BWANA AFYA MKUU WA MKOA WA TANGA BW. JUMANNE MAGOMA (KUSHOTO) AKIWEMO KWENYE MSAFARA HUO AKIWEMO MKUU WA MAGEREZA MKOA. |
WANANCHI WALIOFURIKA KATIKA HOSPITALI HIYO WAKIWA KATIKA ENEO LA MAPOKEZI AMBAKO MKUU WA MKOA ALIFIKA NA KUINGIA KUMUONA DAKITARI WA WATOTO KAMA YUPO. |
MADAKTARI na wauguzi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo, wametii amri ya serikali ya kuwataka kurejea kazini kufanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa lakini pamoja na kurejea huko, wameanza mgomo baridi wakiwa kazini.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika hospitali hiyo asubuhi kufuatilia madaktari na wauguzi ambao hawakufika, lakini wote walifika na kwenda kwenye maeneo yao ya kazi kama kawaida.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo Dkt Fred Mtatifikolo, alipoulizwa kuhusu madaktari kurejea kazini alisema wameanza kazi jana na kwamba wote waliokuwa kwenye mgomo ulioanza katika hospitali hiyo Ijumaa wiki iliyopita kuunga mkono wenzao, wapo kazini na wanaendelea na kazi kama kawaida.
"Tuliitisha Roucall saa mbili asubuhi, tukakuta madaktari wote na wauguzi wamefika kazini, mgomo ulikuwepo hapa katika hospitali yetu Ijumaa na Jumamosi iliyopita lakini ulihusu madaktari hawa wa Intershirp kuunga mkono wenzao, lakini leo wote wapo kazini sasa kama hawafanyi kazi siwezi kujua kwa vile mimi kama Mganga Mkuu Mfawidhi siwezi kutembelea maeneo yote kuona utendaji wao wa kazi," alisema Dk Mtatifikolo.
Hata hivyo, pamoja na madaktari hao kurejesa kazini lakini kwa ujumla hawaonekani kufanya kazi kama kawaida na baadhi yao walisema kuwa suala la mgomo baridi lipo kwa vile wamelazinishwa kurejea kazini bila kusikilizwa huku wakiw ana madai yao ya msingi kama malimbikizo ya nyongeza zao za mishahara na posho nyingine.
"Sisi ni madaktari unapotulazimisha kufanya kazi bila madai yetu ya msingi kuyasikiliza na kutulipa kile tunachodai halafu unatutishia kutufukuza kazi sidhani kama umetatua mgogoro uliopo baina yetu na serikali, tutakuja kazini lakini suala la kufanya kazi ni jingine sisi tupo tupo tu hapa, hadi kieleweke kwa maana ya kwamba serikali ikubali kutulipa madai yetu, iache kusingizia siasa," alisema Dkt mmoja ambaye kama mwenzake walikataa kutaja majina yao wala kupigwa picha.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama walifika kwenye hospitali hiyo majira ya saa 6:00 mchana kutembelea wodi mbalimbali ikiwemo sehemu ya kupokelea wagonjwa wa nje kuona kama maeneo hayo madaktari kama walikuwa kazini na kisha baadaye mkuu huyo alizungumza na wafanyakazi wote wakiwemo madaktari wa hospitali hiyo.
Akizungumza na wafanyakazi hao mkuu huyo wa mkoa aliwaambia kwamba anayetaka kazi aendelee na kazi kama daktari hataki kazi aondoke apishe wengine ambao watafanya kazi kwa moyo wote wa kuwatibia wananchi wanaofika.
Saturday, January 28, 2012
MADAKTARI, WAUGUZI HOSPITALI YA BOMBO NAO, WAANZA MGOMO
WAFANYAKAZI WA KITENGO CHA UPASUAJI WA HOSPITALI YA BOMBO WAKIWA WAMEKAA NJE YA HOSPITALI HIYO KAMA SEHEMU YA MGOMO WAO WALIOUANZA LEO KATIKA HOSPITALI HIYO KUUNGA MKONO WENZAKO NCHI NZIMA. |
MADAKTARI NA WAUGUZI WAKIWA WAMEKUSANYIKA KATIKA UKUMBI MDOGO WA KITENGO CHA MAZOEZI YA VIUNGO WAKISOMEWA TAARIFA YA KWANINI WANATAKIWA KUGOMA |
BAADHI YA MADAKTARI NA WAUGUZI WAKISIKILIZA MKUTANO HUO. |
WAKISIKILIZA KWA MAKINI MKUTANO HUO |
HAWA NDIYO WALIOKUWA WAKISOMA BARUA ILIYOKUWA NA MADAI YA MADAKTARI AMBAYO WANAIDAI SERIKALI |
MADAKTARI na wauguzi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo, nao wameanza mgomo wao jana, kuunga mkono wenzao waliogoma nchini kote kwa ajili ya kuishinikiza serikali iwalipe malimbikizo yao ikiwemo posho zao wakiwa kazini.
Mgomo huo umeanza jana ambapo huduma mbalimbali kwa wagonjwa zilisimama, na wagonjwa katika wodi ya wazazi walibaki pekee yao asubuhi bila kuwa na waauguzi wowote halkadhalika wagonjwa waliokuwa wodini ambao huwa wanapitiwa na madaktari kujua namna walivyolala, lakini waliamka bila kumuona daktari hali ambayo ilileta usumbufu mkubwa kwa wagonjwa hao.
Hata hivyo, katika kikao chao walichofanya jana katika hospitali hiyo kitengo cha viungo ambapo mwandishi wa habari hizi alifika eneo hilo bila kupata ushirikiano kutoka kwa madaktari huo, wakieleza kwamba waandishi waliokutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda walishindwa kumbana suala la msingi la kugoma kwao badala yake, wanazungumzia suala la uraisi wa 2015.
"Jamani nyie waandishi issue ni mgomo wa madaktari nyie mnazungumza na Waziri Mkuu suala la Urais hamuoni kwamba mnatumika katika masuala makubwa ya Kitaifa mnaingiza mambo ambayo hata wakati wenyewe haujafika, kwanini msimbane kuhusu mgomo na ni kwanini serikali inapiga chenga kukutana na viongozi wetu?," alihoji mmoja wa madaktari hao ambaye hakutaka jina lake lianikwe gazetini.
Abdallah Kubo mgonjwa aliyelazwa katika wodi ya Galanos, alilalamika kukosa matibabu baada ya kupata ajali juzi usiku ambako alifikishwa katika hospitali hiyo, majira ya saa tano usiku na kwamba alitarajia jana asubuhi angeonwa na daktari kisha kwenda kupatiwa x-ray kuangaliwa kama amevunjika katika viungo vyake.
"Kwa kweli mwili wangu unauma sana, nimeanguka na pikipiki baada ya kuwashiwa taa na gari kubwa kisha nikaparamia msingi nikaanguka nimeleta hapa sijitambui, nimeamka muda huu simuoni daktari, ndugu zangu wanataka nikapigwe x-ray lakini hatujaambiwa chochote twasikia leo (jana) madaktari wamegoma," alisema Kubo.
Mwanamke mwingine aliyejitambulisha kwa jina Bi Rose Mwaimu alisema alifika katika hospitali hiyo asubuhi jana, kwa ajili ya kuonana na daktari katika kitendo cha mazoezi ya viungo, lakini hakuweza kupata msaada wowote baada ya kuelezwa kwamba madaktari hawafanyi kazi
kufuatia mgomo waliouanza.
"Baba nimekuja hapa tangu asubhi nasubiri huduma lakini sijapata msaada wowote mguu wangu unaendelea kuvimba sijui sitafanyaje, kwa kweli tunaomba watuonee huruma jamani tunateseka," alisema Rose.
Alisema hospitali hiyo ya Bombo haina madaktari wa kutosha, hivyo mgomo huo utaathiri huduma za kiafya kutokana na kwamba wakati wakiwa wote hospitali hiyo huduma zao zimekuwa haziridhishi hivyo kugoma huko kutasababisha wagonjwa kupoteza maisha.
Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Dkt Mchomvu, alikiri mgomo huo kuanza katika hospitali hiyo leo (jana) lakini alisema huduma za dharura zitaendelea kama kawaida isipokuwa huduma nyingine wagonjwa hawatapata matibabu kama ilivyokuwa awali.
"Ni kweli tumegoma kuanzia leo (jana) kuunga mkono wenzetu nchini kote lakini huduma za Emergence (dharura) zitaendelea iwapo kutakuwa na wagonjwa wa aina hiyo," alisema Dkt Mchomvu.
Thursday, January 19, 2012
WATENDAJI WA VIJIJI HANDENI, KILINDI WAPATIWA SEMINA ELEKEZI KUHUSU UTUNZAJI MAZINGIRA
OFISA AFYA MKUU WA MKOA WA TANGA, BW. JUMANNE MAGOMA AKIZUNGUMZA KATIKA SEMINA HIYO KUELEZEA JINSI MKOA HUO ULIVYOJIPANGA KUHUSU USAFI KATIKA WILAYA ZAKE. |
OFISA AFYA YA MZINGIRA KATIKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII BW. ANYITIKE MWAKITALIMA AKIZUNGUMZIA NAMNA WIZARA HIYO ILIVYOJIPANGA KUHAKIKISHA INASHUGHULIKIA SUALA LA USAFI NCHINI. |
BW. MWAKITALIMA (KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BW. MASHAKA MHANDO MWANDISHI WA GAZETI LA MAJIRA (KATIKATI) NA BW. SONYO MWENKALE WA GAZETI LA NIPASHE. |
RC GALLAWA ALIVYOTEMBELEA KIWANDA CHA SARUJI TANGA
MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA KIWANDA CHA SARUJI SIMBA CEMENT ALIPOTEMBELEA KUONA SHUGHULI ZA UZALISHAJI IKIWEMO CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO. |
KIWANDA CHA SARUJI TANGA |
MH. GALLAWA ATAKA KIWANDA CHA SARUJI KUTAFUTA MAWAKALA KILA WILAYA MKOANI TANGA WA KUSAMBAZA SARUJI
Friday, January 13, 2012
MADC KOROGWE NA LUSHOTO WAKUTANA KUMALIZA TATIZO LA UHARIBIFU WA MSITU
Subscribe to:
Posts (Atom)