KATIBU TAWALA WA KOA WA TANGA, BW. BENEDICT OLE KUYAN (KATIKATI) AKIWA NAYE NI MIONGONI MWA VIONGOZI WALIOFIKA KWENYE HOSPITALI HIYO. KUSHOTO KWAKE NI BREGEDIA GENERAL MWANGWAMBA. |
BWANA AFYA MKUU WA MKOA WA TANGA BW. JUMANNE MAGOMA (KUSHOTO) AKIWEMO KWENYE MSAFARA HUO AKIWEMO MKUU WA MAGEREZA MKOA. |
WANANCHI WALIOFURIKA KATIKA HOSPITALI HIYO WAKIWA KATIKA ENEO LA MAPOKEZI AMBAKO MKUU WA MKOA ALIFIKA NA KUINGIA KUMUONA DAKITARI WA WATOTO KAMA YUPO. |
MADAKTARI na wauguzi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo, wametii amri ya serikali ya kuwataka kurejea kazini kufanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa lakini pamoja na kurejea huko, wameanza mgomo baridi wakiwa kazini.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika hospitali hiyo asubuhi kufuatilia madaktari na wauguzi ambao hawakufika, lakini wote walifika na kwenda kwenye maeneo yao ya kazi kama kawaida.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo Dkt Fred Mtatifikolo, alipoulizwa kuhusu madaktari kurejea kazini alisema wameanza kazi jana na kwamba wote waliokuwa kwenye mgomo ulioanza katika hospitali hiyo Ijumaa wiki iliyopita kuunga mkono wenzao, wapo kazini na wanaendelea na kazi kama kawaida.
"Tuliitisha Roucall saa mbili asubuhi, tukakuta madaktari wote na wauguzi wamefika kazini, mgomo ulikuwepo hapa katika hospitali yetu Ijumaa na Jumamosi iliyopita lakini ulihusu madaktari hawa wa Intershirp kuunga mkono wenzao, lakini leo wote wapo kazini sasa kama hawafanyi kazi siwezi kujua kwa vile mimi kama Mganga Mkuu Mfawidhi siwezi kutembelea maeneo yote kuona utendaji wao wa kazi," alisema Dk Mtatifikolo.
Hata hivyo, pamoja na madaktari hao kurejesa kazini lakini kwa ujumla hawaonekani kufanya kazi kama kawaida na baadhi yao walisema kuwa suala la mgomo baridi lipo kwa vile wamelazinishwa kurejea kazini bila kusikilizwa huku wakiw ana madai yao ya msingi kama malimbikizo ya nyongeza zao za mishahara na posho nyingine.
"Sisi ni madaktari unapotulazimisha kufanya kazi bila madai yetu ya msingi kuyasikiliza na kutulipa kile tunachodai halafu unatutishia kutufukuza kazi sidhani kama umetatua mgogoro uliopo baina yetu na serikali, tutakuja kazini lakini suala la kufanya kazi ni jingine sisi tupo tupo tu hapa, hadi kieleweke kwa maana ya kwamba serikali ikubali kutulipa madai yetu, iache kusingizia siasa," alisema Dkt mmoja ambaye kama mwenzake walikataa kutaja majina yao wala kupigwa picha.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama walifika kwenye hospitali hiyo majira ya saa 6:00 mchana kutembelea wodi mbalimbali ikiwemo sehemu ya kupokelea wagonjwa wa nje kuona kama maeneo hayo madaktari kama walikuwa kazini na kisha baadaye mkuu huyo alizungumza na wafanyakazi wote wakiwemo madaktari wa hospitali hiyo.
Akizungumza na wafanyakazi hao mkuu huyo wa mkoa aliwaambia kwamba anayetaka kazi aendelee na kazi kama daktari hataki kazi aondoke apishe wengine ambao watafanya kazi kwa moyo wote wa kuwatibia wananchi wanaofika.
No comments:
Post a Comment