WAKUU WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WALIKUWEPO KATIKA SHEREHE YA SIKU YA SHERIA NCHINI AMBAPO MGENI RASMI ALIKUWA JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA, JAJI MUSSA KIPENKA. |
JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA, JAJI MUSSA KIPENKA AKIZUNGUMZA KWENYE SHEREHE YA SIKU YA SHERIA ILIYOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA MAHAKAMA JIJINI TANGA. |
HAKIMU MKAZI MFAWIDHI WA MAHAKAMA YA WILAYA MKOANI TANGA RM INCHARGE MR. CHUMA AKITOA UFAFANUZI WA MAMBO MBALIMBALI KUHUSU SIKU YA SHERIA ILIPOFANYIKA JIJINI TANGA. |
JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga, Jaji Mussa Kipenka, amewataka watumishi wa mahakama nchini kuwaelewesha wananchi kuhusu taratibu mbalimbali za mahakama wakati mchakato wa kutoe elimu kwa jamii ukiandaliwa.
Akizungumza katika siku ya sheria iliyofanyika kwenye viwanja vya mahakama Kuu kanda ya Tanga, Jaji Kipenka alisema wananchi kutokana na kutokujua taratibu za mahakama wamekuwa wakipoteza muda mwingi kutafuta haki ama kufungua kesi au kukata rufaa kuitafuta haki katika mamlaka zisizohusika.
“Changamoto kubwa iliyopo mbele yetu ni kuboresha eneo hili la elimu kwa umma ili taratibu na shuguli za mahakama ziwe wazi kwa wananchi…Hivyo ni vema sasa watumishi na watendaji wote wa mahakama wawajibike kwa kutoa maelekezo kwa wananchi kuhusu taratibu za mahakama pale zinapohitajika,” alisema Jaji Kipenka.
Hata hivyo, Jaji huyo alikiri kuwepo kwa tatizo la kuhusiana na sheria ya mwenendo wa mashauri ya kesi za madai ambazo amedai kutokana na taratibu zake imekuwa ni vigumu kueleweka hasa kwa mwananchi ambaye hajasomea fani ya sheria.
Akifafanua Jaji Kipenka alisema kwa kiwango kikubwa mapungufu yaliopo katika sheria hiyo yamekuwa yakisababisha ‘wadaawa’ (wanaofungua kesi za madai) kutofahamu hatua muhimu za kuchukua kabla au baada ya kufungua mashauri hayo ambayo wengi wamekuwa wakikosea sana.
“Elimu kwa umma ni changamoto kubwa kwa mahakama ya Tanzania na ipo haja ya kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na mahakama kuanzisha programu mahususi ya elimu kwa umma ili kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli zetu za kimahakama,” alisema Jaji Kipenka.
Katika sherehe hiyo iliyoongozwa na kuandaliwa vema na Msajili Mfawidhi wa wilaya wa mahakama Kuu kanda ya Tanga, Bw. Benedict Mwingwa, kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilikuwa ni “Umuhimu wa elimu kuhusu mahakama kama hatua ya msingi ya utatuzi wa migogoro katika jamii”.
No comments:
Post a Comment