Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Thursday, June 30, 2011

UKUMBI UNAOFANYIA MIKUTANO YA BARAZA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA MDOGO

MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA WAKIENDELEA NA MJADALA WA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI HIYO, LEO KWENYE UKUMBI WA HALMASHAURI HIYO AMBAYO BAADHI YA WADAU WAMEULALAMIKIA UKUMBI HUO WAKIDAI KWAMBA NI MDOGO UNAPASWA KUJENGWA UKUMBI MKUBWA KWA FAIDA YA VIONGOZI WAJAO.
DIWANI WA KATA YA NKUMBA (wa kwanza kushoto) AKIWA NA DIWANI WA KATA YA TONGWE WAKISIKILIZA KWA MAKINI MJADALWA WA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KILICHOFANYIKA LEO KWENYE UKUMBI AMBAO NI MDOGO SANA WA HALMSHAURI HIYO.

Tuesday, June 28, 2011

TANGA CEMENT YATOA MSAADA WENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 57 KWA KITUO CHA WALEMAVU MOROGORO

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA TANGA CEMENT ERIK WESTERBERG (mwenye shada la maua kulia) AKIMKABIDHI FUNGUO ZA BWALO LA KULIA CHAKULA NA JIKO PADRI BEATUS SEWANDO AMBAYE NI  MKURUGENZI WA KITUO CHA KUWAHADUMIA WALEMAVU CHA AMANI KILICHOPO WILAYANI MVOMELO MKOANI MOROGORO, MSAADA HUO UMEGHARIMU KIASI CHA SHILINGI MILIONI 57.

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA TANGA CEMENT ERIK WESTERBERG (mwenye shati nyeupe) AKISHIKANA MIKONO NA MMOJA YA WATOTO WANAOLELEWA KATIKA KITUO HICHO CHA AMANI, IMA KAMOTA.

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA TANGA CEMENT ERIK WESTERBERG (kushoto) AKISHIKANA MIKONO NA MAMA JOSEPHINE MAKITA AMBAYE NI MWANZILISHI WA KITUO HICHO CHA AMANI KILICHOPO WILAYANI MVOMELO MKOANI MOROGORO KATIKA HAFLA HIYO FUPI YA KUKABIDHI JENGO LA CHAKULA NA JIKO

Wednesday, June 22, 2011

KAMATI ANGALIENI MAHAKIMU WANAOKIUKA MAADILI YAO-JAJI MKUU AIAMBIA KAMATI YA WATUMISHI WA MAHAKAMA

JAJI  MKUU OTHMAN RASHID CHANDE AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA WATU,MISHI WA MAHAKAMA WA WILAYA ZA KOROGWE, HANDENI, KILINDI NA LUSHOTO KATIKA MKUTANO AMBAO ULIKUWA MAALUMU WA KUZINDUA KAMATI HIYO ULIOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO (IJA) KUSHITO KWA JAJI MKUU NI MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO BI SOPHIA MJEMA.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA (kushoto), KAMPTENI (mstaafu) SEIF MPEMBENWE DC HANDENI NA MKUU WA WILAYA YA KILINDI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI JAJI MKUU HAYUPO PICHANI AKIELEZEA UMUHIMU WA KAMATI YA UTUMISHI WA MAHAKAMA INAVYOWEZA KUTOA AHABU KWA MAHAKIMU WANAOKWENDA KINYUME NA SHERIA

MSAJILI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA BW. BENEDICTOR MWINGA (kushoto), HAKIMU MKUU MKAZI WA MAHAKAMA ZA MKOA WA TANGA BW. CHUMA WAKIFUATILIA KWA MAKINI TAARRIFA NA NA MAELESZO YA JAJI MKUU WA TANZANIA JAJI OTHMAN CHANDE HAYUPO PICHANI KWENYE MKUTANO WA KUZINUA KAMATI YA WAJUMBE HAO.

MAHAKIMU WAKAZI NA WA WILAYA WAKIMSIKILIZA JAJI MKUU KATIKA MKUTANO HUO AMBAO ULIFANIKA KWENYE CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA IJA WILAANI LUSHOTO.

WAJUMBE WA KAMAT HIYO YA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAKIMSIKILIZA JAJI MKUU HAWA NI VIONGOZI WA DINI NA WATU MASHUHURI KUTOKA KATIKA WILAYA HIZO.

Monday, June 20, 2011

UWANJA WA SABASABA TANGA ULIVYOJAA BAR NA NYAMA CHOMA

ENEO LA BANDARI AMBALO WATU WENGI WALIKUWA WAKIFIKA KUONA SHUGHULI ZA BANDARI YA TANGA WAKATI ULE WA SABASABA, LEO LIMEBAKI KUWA GEREJI TU.

UKUMBI HUU ULIKUWA SANA UNATUMIKA KWA MUZIKI ENZI MIMI NIKIWA MKUBWA NILIWAHI KUSHUHUDIA BENDI YA TANGA INTERNATIONAL CHINI YA NA MWIMBAJI WAKE MAHIRI KALOJI IKIPOOMOSHA MUZIKI WAKATI WA SABASABA LEO LIMEBAKI KUWA GOFU BADO MWEKEZAJI WA BAR HAJAPAONA LAKINI WAKIPAONA WANAWEZA KUPACHUKUA NASIKIA DJ MMOJA NI ENEO LAKE.

WADAU HAWA WA UWANJA WA SABASABA AMBAO SASA UMEJAA BAR AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIUZA VINYWAJI NA NYAMA CHOMA ZA KILA AINA UNAZOZIJUA HAPA DUNIANI WAKIONGOZWA NA KIONGOZI WAO MWENYE PUA KUBWA HAPA JAMAA HAWA, BAADA YA KUSHIBA SASA WANASHUSHIA VINYWAJI VYAO BAADA YA KULA NYAMA, AISEE WANAFAII KWELI.



UWANJA WA SABASABA ULIOPO ENEO LA GOFU JUU HIVI LEO UMEBAKI KUWA NA BAR, MAKANISA, GERAGE NA NYUMBA ZA KUSIHI BAADA YA KUFUNGWA MIAKA YA 1994 HADI LEO UMEKUWA NI UWANJA WA VINYWAJI NA NYAMA CHOMA.

ENEO HILI KWA MUJIBU WA UTAFITI NI KWAMBA KUNA BAR ZIPATAZO 49, MAKANISA 8, NYUMBA ZA KUISHI 12 NA GAREGE ZIPATAZO SITA.

UWANJA HUU HAPO ZAMANI KWA KWELI ULIKUWA KIVUTIO KIKUBWA KWA KUTANGAZA BIDHAA ZA MASHIRIKA, MAKAMPUNI YALIYOKUWEPO MKOANI TANGA NA PIA WANANCHI HASA WATOTO WALIKUWA WAKIPATA BURUDANI SAFI ZA KUSAFIRISHWA NA KITOLOLI PALE KWENYE BANDA ZA TRC ENZI HIZO NA UKIENDA KWENYE BANDA LA BANDARI WATU WALIKUWA WAKIINGIA KWENYE MFANO WA MELI AMBAYO ILIKUWA IKIWAFURAHISHA WENGI.

LEO HII KWENYE UWANJA HUO NI ENEO LA WATU WACHACHE NDIYO WANAOFIKA HUKO KUNYWA POMBE NA KULA KITI MOTO AMBACHO AMA KWA HAKIKA KUMEKUWEPO NA MABANDA MENGI AMBAYO YANASHINANA KUTENENEZA NYAMA HIYO AMBAYO INAONEKAN SASA KULIWA NA WATU WA DINI ZOTE KUTOKANA NA KWAMBA WAISLAMU NA WAKRISTO (wasabato) AMBAO HAWALI LAKINI NAO UTAWAKUTA WAKILA BILA HOFU.

JE MDAU WA MAENDELEO UNADHANI CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) AMBACHO NDICHO KINAMILIKI UWANJA HUU WA SABASABA WALIKUWA SAHIHI KUWAKODISHA WATU HAWA AU KINATAKIWA KUBUNI MRADI WA JENGO KUBWA AMBALO LITAKUWA KITEGA UCHUMI CHAO ITAKACHOWAINGIZIA FEDHA KWA AJILI YA KUWASAIDIA KATIKA KAMPENI ZA VYAMA VINGI AU MAWAZO YAKO NI NINI?

Sunday, June 19, 2011

ULIPATA KUMUONA ALUU ALLY AKICHEZA MPIRA?

KHALID ABDALLAH MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF (kushoto) AKIWA NA MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA NA TAIFA STARS ALUU ALLY 'SPOILER' AMBAYE KWA SASA YUPO NCHINI ABUDHABI BAADA YA KUSTAAFU KUCHEZA SOKA, HAPA WALIKUWA KWENYE UWANJA WAQ MKWAKWANI WAKIFATILIA MCHEZO WA KIRAFIKI BAINA NA YA COASTAL UNION NA TIMU MOJA YA MOMBASA.

MCHEZAJI WA COASTAL UNION SAID AKIJARIBU KUMTOKA MCHEZAJI WA TIMU YA MOMBASA ILIYOKUWA JIJINI TANGA KWA MCHEZO WA MMOJA WA KIRAFIKI NA TIMU HIYO, COASTAL ILISHINDA 2-1

KIWANDA CHA MBAO CHA SIKH SAW MILLS KWELI KIMEKUFA?

LANGO KUU LA KUINGILIA KATIKA KIWANDA CHA MBAO CHA SIKH SAW MILLS AMBACHO KWA SASA KINAONEKANA KUFA BAADA YA SERIKALI KUKIUZA KWA MWEKEZAJI MZAWA AMBAYE HATA HIVYO HAKUNA JITIHADA ZA KUKIFUFUA.

HIVI NDIVYO INAVYOONEKANA KWA NJE JENGO ZURI LA KIWANDA CHA SIKH SAW MILLS KILICHOKUFA.

Friday, June 17, 2011

RAS OLE KUYAN AONGOZA WATUMISHI TANGA KUPIMA UKIMWI

KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. BENEDICT OLE KUYAN AKIWAONGOZA WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TANGA KUPIMA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI AMBAPO KATI YA WATUMISHI 77 WALIOHUDHURIA SEMINA YA UKIMWI 70 WALIPIMA AMBAPO KATI YA HAO 45 WALIPIMA NA KUCHUKUA MAJIBU YAO PAPO HAPO NA WENGINE WALIOBAKI HAWAKUCHUKUA MAJIBU YAO NA WATUMISHI 7 HAWAKWENDA KUPIMA KWA UWOGA.

Friday, June 10, 2011

Komradhi wasomaji wetu wa Blogu hii ya Mzee wa Bonde

Komradhi wasomaji wetu wa Blogu hii ya mzee wa Bonde ya watu na matukio kutokana na kutokuwepo hewani kwa muda mrefu hii inatokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu, tunawaomba radhi sana.

lakini katika kipindi ambacho hatutakuwa hewani tunafanya maboresho madogo katika Blogu hii ili siku ikianza kazi zake basi itoke kwa ufanisi na kukufahamisha matukio mbalimbali hapa Mkoani Tanga na nje ya mkoa huu na mengine nje ya nchi.

Asanteni Utawala blogu ya mzee wa bonde.