Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Monday, June 20, 2011

UWANJA WA SABASABA TANGA ULIVYOJAA BAR NA NYAMA CHOMA

ENEO LA BANDARI AMBALO WATU WENGI WALIKUWA WAKIFIKA KUONA SHUGHULI ZA BANDARI YA TANGA WAKATI ULE WA SABASABA, LEO LIMEBAKI KUWA GEREJI TU.

UKUMBI HUU ULIKUWA SANA UNATUMIKA KWA MUZIKI ENZI MIMI NIKIWA MKUBWA NILIWAHI KUSHUHUDIA BENDI YA TANGA INTERNATIONAL CHINI YA NA MWIMBAJI WAKE MAHIRI KALOJI IKIPOOMOSHA MUZIKI WAKATI WA SABASABA LEO LIMEBAKI KUWA GOFU BADO MWEKEZAJI WA BAR HAJAPAONA LAKINI WAKIPAONA WANAWEZA KUPACHUKUA NASIKIA DJ MMOJA NI ENEO LAKE.

WADAU HAWA WA UWANJA WA SABASABA AMBAO SASA UMEJAA BAR AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIUZA VINYWAJI NA NYAMA CHOMA ZA KILA AINA UNAZOZIJUA HAPA DUNIANI WAKIONGOZWA NA KIONGOZI WAO MWENYE PUA KUBWA HAPA JAMAA HAWA, BAADA YA KUSHIBA SASA WANASHUSHIA VINYWAJI VYAO BAADA YA KULA NYAMA, AISEE WANAFAII KWELI.



UWANJA WA SABASABA ULIOPO ENEO LA GOFU JUU HIVI LEO UMEBAKI KUWA NA BAR, MAKANISA, GERAGE NA NYUMBA ZA KUSIHI BAADA YA KUFUNGWA MIAKA YA 1994 HADI LEO UMEKUWA NI UWANJA WA VINYWAJI NA NYAMA CHOMA.

ENEO HILI KWA MUJIBU WA UTAFITI NI KWAMBA KUNA BAR ZIPATAZO 49, MAKANISA 8, NYUMBA ZA KUISHI 12 NA GAREGE ZIPATAZO SITA.

UWANJA HUU HAPO ZAMANI KWA KWELI ULIKUWA KIVUTIO KIKUBWA KWA KUTANGAZA BIDHAA ZA MASHIRIKA, MAKAMPUNI YALIYOKUWEPO MKOANI TANGA NA PIA WANANCHI HASA WATOTO WALIKUWA WAKIPATA BURUDANI SAFI ZA KUSAFIRISHWA NA KITOLOLI PALE KWENYE BANDA ZA TRC ENZI HIZO NA UKIENDA KWENYE BANDA LA BANDARI WATU WALIKUWA WAKIINGIA KWENYE MFANO WA MELI AMBAYO ILIKUWA IKIWAFURAHISHA WENGI.

LEO HII KWENYE UWANJA HUO NI ENEO LA WATU WACHACHE NDIYO WANAOFIKA HUKO KUNYWA POMBE NA KULA KITI MOTO AMBACHO AMA KWA HAKIKA KUMEKUWEPO NA MABANDA MENGI AMBAYO YANASHINANA KUTENENEZA NYAMA HIYO AMBAYO INAONEKAN SASA KULIWA NA WATU WA DINI ZOTE KUTOKANA NA KWAMBA WAISLAMU NA WAKRISTO (wasabato) AMBAO HAWALI LAKINI NAO UTAWAKUTA WAKILA BILA HOFU.

JE MDAU WA MAENDELEO UNADHANI CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) AMBACHO NDICHO KINAMILIKI UWANJA HUU WA SABASABA WALIKUWA SAHIHI KUWAKODISHA WATU HAWA AU KINATAKIWA KUBUNI MRADI WA JENGO KUBWA AMBALO LITAKUWA KITEGA UCHUMI CHAO ITAKACHOWAINGIZIA FEDHA KWA AJILI YA KUWASAIDIA KATIKA KAMPENI ZA VYAMA VINGI AU MAWAZO YAKO NI NINI?

No comments:

Post a Comment