|
HOTEL MPYA YA NYUMBANI HOTEL & RESTAURANT INAVYOONEKANA. |
|
MGENI RASMI KATIKA SHEREHE FUPI YA UFUNGUZI WA HOTELI MPYA YA NYUMBANI HOTEL & RESTAURANT ENG. OMARI NUNDU (Katikati mwenye taji) AMBAYE NI MBUNGE WA TANGA, KULIA NI MKURUGENZI MTENDAJI WA HOTELI HIYO BW. ALOYCE KIMARO MBUNGE WA ZAMANI WA JIMBO LA VUNJO (CCM). |
|
NAIBU MEYA WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA BW. MUZAMINI SHEMDOE AMBAYE NI DIWANI WA KATA YA MABAWA (wa kwanza kushoto) DIWANI WA KATA YA CENTRAL BW. KHALID ABDALLAH (katikati). |
|
WADAU MBALIMBALI WALIFIKA KATIKA UZINDUZI HUO WA HOTELI YA NYUMBANI AKIWEMO MMILIKI WA HOTELI YA DOLPHIN INN ILIYOPO ENEO LA CHUDA BI ANNA MAARUFU ANNA DOLIPHIN (katikati) AKIWA NA RAFIKI ZAKE. |
|
NAIBU MHARIRI WA GAZETI LA MWANANCHI BW. MIDRAJ IBRAHIMU (kushoto) AKIWA NA OFISA MMOJA WA JIJI LA TANGA KITENGO CHA BIASHARA NA MASOKO WAKIWA MIONGONI MWA WATU WALIOHUDHURIA UZINDUZI HUO. |
Na Mzee wa Bonde,Tanga
MMILIKI wa hoteli mpya inayojulikana kwa jina la NYUMBANI Hotel & Restaurant Bw. Aloyce Kimaro aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, amewataka wafanyabiashara na wananchi wa Jiji la Tanga, kumuunga mkono katika uwekezaji wake mpya wa sekta ya hoteli ili kusaidia kuongezeka kwa pato la uchumi la mkoa wa Tanga.
Akitoa neno la shukurani kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopo mkabala ya jengo la posta katikati ya Jiji la Tanga, mbunge huyo wa zamani alisema alipata wazo la kufungua hoeli hiyo mkoani Tanga, kushirikiana na wana-jamii kuongeza pato la mkoa hasa kutokanana uwepo wa bandari na shughuli nyingine za kiuchumi.
Alisema kutokana na uwepo wa bandari na kukua kwa shughuli nyingi za kibiashara alionelea kufungua hoteli hiyo hivyo amewataka wananchi na wafanyabiashara kushirikiana naye kumsapoti katika kuhakikisha hoteli hiyo inatoa huduma za kisasa na za kimaaifa.
Bw. Kimaro ambaye anaendesha hoteli hiyo akiwa na wakurugenzi wengine Bw. John Kessy na Mansfeld, wanatarajia kufungua hoteli zenye jina hilo katika mikoa yote nchini ili kuhakikisha wanawekeza katika sekta hiyo wakiwa kama Watazania na kusaidia kukua kwa uchumi wa Tanzania. Hoteli hiyo ya Tanga inafuatia kuwepo kwa hoteli nyingne zenye jina hilo la nyumbani katika miji ya Mwanza na Moshi.
Akizindua hoteli hiyo Waziri wa Uchukuzi, Injinia Omar Nundu ambaye ni mbunge wa jimbo la Tanga, alisema katika kutembea kwake Ulaya hoteli hiyo inaingana kabisa na ambazo amezishuhudia na kwamba hoteli ya Nyumabni ni moja ya hoteli yenye hadhi kubwa mkoani Tanga na ambayo itafungua ukurasa mpya kwa wawekezaji wengine.
"Mbunge wenu mnajua nimemaliza huko Ulaya, lakini hoteli hii nilipoingai kwenye vyumba nimekuta vitu ambavyo nikiwa huko Ulaya kwenye mahoteli makubwa nimekutana na mambo makubwa mabyo yamo humu ndani, hii ni changamoto kwa wawekezaji wengine kuona umuhimu wa kuwekeza mahoteli makubwa kama haya katika Jiji letu," alisema Injinia Nundu.