MWILI WA NAHODHA HUYO UKIONEKANA BAADA YA KUJINYONGA |
MELI YA MVU TIGER IKIWA IMETIA NANGA KWENYE BANDARI YA TANGA |
TIMU YA MAOFISA WA SERIKALI AKIWEMO MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOANI TANGA, RCO MOHAMED JAFAR (kulia mwenye glovu za bluu) AKIWA NA MAOFISA HAO KUCHUNGUZA MWILI WA MAREHEMU HUYO |
NAHODHA ADAM AKIONEKANA KWENYE MTI HUO AKIWA AMEJINYONGA TAYARI |
NAHODHA HUYO AKINING'INIA HUKU OFISA WA KIKOSI CHA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOANI TANGA, AFANDE JOHN AKIUTAZAMA MWILI HUO KUONA KAMA NI KWELI ALIJITUNDIKA HAPO AU ULIWEKWA NA MTU |
MABAHARIA WA MELI HIYO PAMOJA NA MAOFISA WA SERIKALI WAKIUSHUSHA MWILI WA NAHODHA HUYO KUTOKA MAHALI AMBAKO ALIJINYONGEA KWENYE MELI HIYO |
MELI YA TIGER INAVYOONEKANA PICHANI KATIKA ENEO LAKE LA NDANI JUU KABISA YA KICHWA CHA NAHODHA HUYO |
MWILI WA NAHODHA HUYO UKIWA UMEFUNGWA TAYARI KWA KUTOLEWA NCHI KAVU KWENYE KUHIFADHIWA KWENYE HOSPITALI YA BOMBO. |
MAOFISA HAO WAKIWA NA WAHUDUMU WA AFYA WA MAMLAKA YA BANDARI NCHINI BANDARI YA TANGA WAKIUBEBA MWILI KUUTOA NJE YA MELI HIYO WAKITUMIA BOTI NYINGINE |
NAHODHA MSAIDIZI WA MELI HIYO BW. COLGOLF AKITOA MAELEZO KWA MAOFISA WA SERIKALI KUFUATIA KUJINYONGA KWA NAHODHA HUYO |
MWILI UKIWA UMEFUNGWA VIZURI TAYARI KUPELEKWA KWENYE HOSPITALI YA BOMBO KUHIFADHIWA |
MWILI UKIWA UMEBEBWA NA MAOFISA HAO NA KUUPAKIA KWENYE BOTI ILI WAUTOE NJE NA KUUPELEKA HOSPITALINI BOMBO |
MAOFISA HAO WAKIUTOA MWILI HUO NJE YA BOTI WALIMOMPAKIA NA KUUPELAKA BOMBO HOSPITALI. |
Na Mzee wa Bonde,Tanga
Nahodha wa meli ya kigeni akutwa amejinyonga melini
NAHODHA wa Meli ya shehena ya MV Tiger Monrovia,Pakulski Radoslav Adam (47) jana alikutwa akiwa amejinyonga ndani ya meli hiyo katika mazingira ambayo hayajajulikana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe alisema jana kuwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana Alhamisi wakati meli hiyo ikiwasili katika bandari ya Tanga ikitokea Dar es salaam.
Alisema wafanyakazi wa meli hiyo wamesema kuwa Nahodha huyo alipanda ngazi hadi kwenye nguzo za bendera ya meli hiyo na kujinyonga kwa kutumia kamba.
Alisema wanfanyakazi hao wamedai kuwa hawakuwa wamejua mwenzao alikokuwa hadi ilipofika ilipofika alfajiri baada ya mmoja wa wafanyakazi melini kupanda juu na kuukuta mwili wake ukining’inia.
Alisema kufuatia tukio hilo, wafanyakazi hao wameweza kuwasiliana na ndugu zake walioko nchini Poland pamoja na mmliki wa meli hiyo ambao ili kujua nini kifanyike juu ya mwili huo.
Mwandishi wa habari hizi alishihudia shughuli za utoaji wa mwili huo uliokuwa ndani ya meli iliyotia nanga mbali na bandari ya Tanga,zikifanywa na maafisa wa jeshi la Polisi,Bandari ya Tanga,uhamiaji,TRA pamoja na mawakala wa meli hiyo ambapo ilichukua zaidi ya masaa saba hadi kuutoa na kuupeleka Hospitali ya Bombo.
Wakala wa meli hiyo,Abas Mohamed wa kampuni ya CMA CGM (T) Ltd alisema imebeba makontena ya bidhaa mbalimbali ambazo zimetoka nchi za Ulaya na bara la Asia na kwamba ilipita Dar es salaam na ingekaa banadari ya Tanga kwa siku mbili kabla ya kwenda Mombasa na Colombo nchini Malasia.
Afisa afya wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Happiness Byabato alisema baada ya kuufanyia uchunguzi mwili huo ambaini kuwa amejinyonga mwenyewe.
Kwa mujibu wa Massawe ni kuwa mwili huo umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga,Bombo kusubiri maamuzi ya ndugu wa marehemu kama asafirishwe au azikwe Tanga.
Alisema pamoja na kwamba taarifa za awali zinaeleza kuwa nahodha huyo kajinyonga lakini jeshi hilo bado linafanya uchunguzi wa kitaalamu kujua chanzo cha tukio hilo.
No comments:
Post a Comment