Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Sunday, July 31, 2011
HATIMAYE UBINGWA WA POOL WATOKA DAR WAENDA DODOMA
MWENYEKITI WA POOL TAIFA BW. ISAACK TCHOGOSHO AKIMKABIDH KITITA CHA SHILINGI MILIONI KIONGOZI WA MKOA WA MWANZA AMBAO WAMETWAA USHINDI WA TATU KATKA MASHINDANO HAYO. |
MABINGWA WAPYA WA MASHINDANO YA SAFARI LAGER NATIONAL POOL CHAMPIONSHIRP MKOA WA DODOMA. |
Saturday, July 30, 2011
BILION 121 ZAHITAJIKA KUKARABATI MRADI WA MAJI WA HTM HANDENI
ADAM MGANGA MPIGA NGOMA YA UFUNGILO AKIASHIRIA KUANZA KWA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI, JULY 28 MWAKA HUU. |
WAHESHIMIWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI WAKIWA KATIKA MKUTANO WAO WA BARAZA LA MADIWANI (FULL-COUNCIAL) WILAYANI HANDENI. |
MADIWANI WAKIFUATILIA MKUTANO HUO WA BARAZA LA MADIWANI NA KUCHANGIA HOJA MBALIMBALI. |
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI BW. HASSAIN MWACHIBUZI (kulia), MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO BW. RAMADHANI DILIWA NA KULIA KWAKE NI MAKAMO WAKE. |
NGOMA YA UFUNGILO HANDENI
Tuesday, July 26, 2011
KAZI YA BWANA AFYA WA JIJI AIFANYA KALEMBO, UWASA HARAKA WAUZIBUA MFEREJI ULIOKUWA UKITIRIRISHA MAJI BARABARANI
KALEMBO ATEMBELEA MFEREJI AFRITEX (CIC) UNAOMWAGA KEMIKALI ZA SUMU
Na Mwandishi Wetu,Tanga
MKUU wa mkoa wa Tanga Meja Jererali (Mstaafu), Said Kalembo ameuagiza uongozi wa Jiji la Tanga kuchukua hatua za haraka juu ya tatizo la viwanda vinavyotiririsha maji yenye kemikali na kusababsiha madhara kwa binadamu katika mfereji mama unaopita kata sita za Jiji hilo kwenda baharini, unapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
MKUU wa mkoa wa Tanga Meja Jererali (Mstaafu), Said Kalembo ameuagiza uongozi wa Jiji la Tanga kuchukua hatua za haraka juu ya tatizo la viwanda vinavyotiririsha maji yenye kemikali na kusababsiha madhara kwa binadamu katika mfereji mama unaopita kata sita za Jiji hilo kwenda baharini, unapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Akizungumza juzi wakati mkuu huyo na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya mkoa walipotembelea mfereji huo kuona namna maji yanayodaiwa kuwa na kemikali yakimwagwa kutoka viwandani na kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine wanaotumia mfereji huo kuufanyia usafi.
Awali Ofisa Afya wa Jiji hilo, Yusuph Gumbo akimsomea taarifa mwenyekiti huyo wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, alisema kuwa Julai 11 mwaka huu vibarua 14 waliokuwa wakifanya usafi kwenye mfereji huo kwa kuingia katikati, walipata madhara makubwa ya kuungua miguuni kwa kubabuka ngozi baada ya kuingiwa na maji yanayodhaniwa kuwa kemikali zenye sumu.
Alisema vibarua hao walipokuwa wakisafisha mfereji huo wenye urefu wa kilomita nane, licha ya kuvaa viatu virefu (Gum Boots) hata hivyo maji ya mfereji huo yaliwaingia na kujisikia kuwashwa baada ya muda wa masaa mawili walipotoka katika mfejei huo na kisha kuanza kubabuka na hali zao kuwa mbaya.
“Kwa vile vibarua wale walikuwa wakipokezana kuingia ndani ya mfereji waliamua kutoka ili wenzao wengine waingie waendelee na usafi, lakini wale waliotoka mferejini baada ya kuvua viatu muwasho ulizidi na mmoja kati yao ambaye aliungua vibaya na ngozi ilibabuka na kufanya awe na vidonda kuanzia magotini hadi miguuni,” alisema Gumbo.
Aliongeza kwamba mfereji huo uliojengwa miaka ya 1970 kwa ajili ya kusaidia kutoa maji ya mvua na kuyapeleka maharini lakini sasa umekuwa ukitumiwa na viwanda kumwaga mabaki ya takataka zao na kuvitaja viwanda hivyo kuwa ni kiwanda cha nguo cha Afritex, Kiwanda cha kusindika samaki cha Sea Food Products, Kiwanda cha foma, Kiwanda cha Vioo (Tansilica), karakana ya Tanroads na karakana za magari zilizopo eneo la viwanda Gofu.
Hata hivyo, alisema hatua ambazo halmashauri ya jiji imechukua hadi sasa ni kuwapa notisi ya kisheria wenye viwanda hivyo na kuwataka kuwa na mitambo ya kusafishia majitaka wanayoyatiririsha kabla ya kumwagwa baharini na kiwanda cha Afritex tayari kimenunua mtambo huo lakini bado haujaanza kusafisha maji hayo.
Mwana mazingira wa Envirocare Haika mcharo ambaye ni ofisa habari wa taasisi hiyo inayojihusisha na suala la mazingira hapa nchini, alimweleza Mkuu wa huyo wa mkoa katika ziara hiyo kwamba serikali inatakiwa kuchukua hatua juu ya tatizo hilo kwa ajili ya kulinda viumbe hai vya baharini na binadamu na wananchi wanaoishi pembezoni mwa mfereji huo.
“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa kabla ya kufanya ziara hapa na kamati yako, juzi (Alhamisi) nilitembelea kiwanda cha Afritex nikiwa na waandishi wa habari kuona namna kiwanda hiki kinavyojiendesha hasa sual la mazingira tumeona maji yao wanayoyatitiisha lakini tunadhani wakati mwingine maji yanakuja kwenye mfereji huu bila kusafisha, ni vema serikali ya mkoa ikatilia mkazo suala hili mapema kabla ya athari kubwa haijapatikana,” alisema mcharo.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa mkoa alimwagiza viongozi wa Jiji pamoja na Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi kuhakikisha wanachukua hatua za haraka ikiwezekana kuvifungia viwanda walivyobainika kumwaga kemikali hizo zenye sumu kwani tayari madhara kiafya yamepaikana kwa vibarua hao waliobabuka ngozi kuliko kukaa na kulalamikia suala hilo.
MWISHO
MSHIKE MSHIKE WA KUDAKA ABIRIA STENDI YA TANGA
Sunday, July 24, 2011
KAMANDA MPYA WA POLISI TANGA AANZA KAZI KWA KUKAMATA SMG NA BASTOLA
KAMANDA MPYA WA POLISI MKOANI TANGA ACP CONSANTINE MASAWE AKIWAONYESHA SILAHA WALIZOKAMATA HUKO MTONI BOMBO WILAYANI KOROGWE BAADA YA KUMKAMATA JAMBAZI SUGU |
KAMANDA MPYA WA POLISI MKOANI TANGA ACP CONSTANTINE MASAWE AKIJARIBU KUIPIGA SILAHA AINA YA SMG WALIYOIKAMATA KWA JAMBAZI MMOJA HUKO KOROGWE |
PROFESA J AWARUSHA WANAFUNZI ONESHO LA MALARIA HAIKUBALIKI
Friday, July 15, 2011
SIMBA VIDEO COACH YATOA MABASI MAPYA
Wednesday, July 13, 2011
DC ACHELEWA BAADA YA GARI LAKE KUHARIBIKA
Tuesday, July 12, 2011
SHEREHE ZA IDADI YA WATU DUNIANI ZAFANA MUHEZA
Maofisa wa kamati ya ulinzi na usalama kutoka kushoto Kaimu RPC Tanga Mohamed Jafar, mwakilishi wa ofisi ya RSO mkoani Tanga, Mwakilishi wa magereza wakifuatilia kwa makini sherehe hizo. |
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Bw. Salim Sinani (kushoto) akiteta jambo na Meya wa Jiji la Tanga Bw. Omar Guled kwenye sherehe za idadi ya watu duniani zilizofanyika wilayani Muheza. |
Saturday, July 2, 2011
COASTAL UNION YAPATA UONGOZI MPYA
KLABU ya Coastal Union ya Jijini Tanga, leo imefanya uchaguzi wake wa kikatiba wa kuchagua viongozi wake watakaoiongoza klabu hiyo kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu baada ya miaka takribani taisa kuongozwa na kamati za muda.
waliochaguliwakatika mkutano huo ambao awali ulikuwa ufanyike wiki iliyopita lakini ulisimamishwa na TFF (shirikisho la soka nchini) baada ya kuwaengua wagombea saba ambao hawakuwa na sifa za kuwania nafasi hizo ni pamoja na Mwenyekiti Ahmed Hilal 'Aurora' ambaye hakuwa na mpinzani baada ya kujizolea kura 52 kati ya wajumbe 55 waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo.
Wajumbe waliochaguliwa kura zao zikiwa kwenye mabano ni pamoja na Kweli Nahashon (48), Albert Peter (47), Salim Amir (42), Julius Benjamin (42) na James Mwinchande ambaye alipata kura 36.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa kamati ya uchaguzi wa klabu hiyo Abdallah Yahya alisema kuwa watu waliojiandikisha kupiga kura kwa maana wanachama halali walikuwa 77 lakini kwenye uchaguzi huo wamefika wanachama 55 hivyo uchaguzi huo ulifanyika kutokana na koram ya wajumbe kutimia.
Alisema kwa mujibu wa katiba ya Coastal Union viongozi wanatakiwa kuwa tisa kwa maana Mwenyekiti, Makamo Mwenyeki na wajumbe saba lakini kutokana na kwamba kumebaki nafasi tatu za makamo mwenyekiti na wajumbe wa tatu uchaguzi mwingine utaitisha mara baada ya wanachama ambao walienguliwa kukamilisha taratibu za kuwasilisha vyeti wakikamilisha.
Wanachama ambao waliomba lakini walienguliwa ni pamoja na Makamo Mwenyekiti Steven Mghuto na Titus Bandawe, Yakob Nuru, Jawa Bakari Jawa, Ayub Athumani na Kilo Rashid.
Kwa mara ya mwisho klabu hiyo ilifanya uchaguzi wake wa kikatiba mwaka 2002 ambapo marehemu Zacharia Kinanda 'Arrigo Sacchi' aliachaguliwa kuwa Katibu Mkuu na wakati huo huo akiwa kocha mkuu wa timu hiyo na Mbwana Abushiri 'Director' akiwa mwenyekiti.
MWISHO
MASIKINI BANDARI YA TANGA HIVI NI KWELI WAFANYABIASHARA HAWAPENDI KUITUMIA SABABU YA TRA?
WADAU WATAKA TAMASHA LA FILAMU TANGAMANO LIFANYIKE KILA MWAKA
FAX JAZZ INAVYOKONGA NYOYO ZA WATU TANGA HOTEL
MSHABIKI MAARUFU WA MUZIKI UNAOAPIGWA TANGA HOTEL MR RASTA AKISAKATA MUZIKI WA FAX AKIWA NA MKEWE KWENYE UKUMBI HUO WA TANGA HOTEL. |
MRATIBU WA UKIMWI WA JIJI LA TANGA MR MOSES NAYE HAKUBAKI NYUMA ALIKUTWA NA KAMERA YETU AKISAKATA MUZIKI WA FAX HUKU AKIMWAGA SERA ZA UPIMAJI WA HIARI WA VIRUSI VYA UGONJWA FAKIRI WA UKIWMI. |
SHIRIKA LA SAHiRNGON YAJIKITA MUHEZA KUFUNDISHA NAMNA YA UFUATILIAJI WA FEDHA ZA KILIMO ZINAZOTUMWA NA SERIKALI WILAYANI HUMO
Friday, July 1, 2011
MASHINDANO YA POOL MKOANI TANGA KUANZA SPLENDID NA MAGROVE JULY 7 HADI 10 KWA VILABU VINANE KUCHUANA
WATAALAM WA KAMPUNI YA INTERGRETED YA JIJI DAR ES SALAAM INAYOHUSIKA NA MATANGAZO YA BIA YA SAFARI LAGER WAKITOA MATANGAZO YAO KUHUSU KUANZA RASMI KWA MASHINDANO YA POOL MKOANI TANGA. |
Subscribe to:
Posts (Atom)