TAMASHA la wazi la sinema ambalo linafikia kelele chake leo kwenye uwanja wa Tangamano huku filamu iliyoongozwa na Single Mtambalike (Richie) na kuzalishwa na Suleiman Said Barafu ya Senior Bachelor ndiyo iliyofunga pazia la tamasha hilo huku wadau wa filamu wakiomba tamasha hilo lifanyike kila mwaka mjini hapa.
Tamasha hilo ambalo lilikuwa la wiki moja ambalo limedhaminiwa na Grand Malt Tanzania lilianza Juni 27 katika viwanja ya Tangamano Mjini Tanga, lilihudhuriwa na maelfu wa Jiji la Tanga na wilaya jirani ambao wameweza kuwaona wasanii waliokuwa wakiwaona tu luningani.
Filamu hiyo ambayo ilioneshwa kwenye uwanja huo ilitanguliwa na maelezo kutoka kwa muigizaji wake Jacob Steven maarufu kama JB ambaye ameshajizolea umaarufu mkubwa kupitia filamu kadha alizoigiza. | |
| |
|
No comments:
Post a Comment