Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, July 12, 2011

SHEREHE ZA IDADI YA WATU DUNIANI ZAFANA MUHEZA

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Meja Jenerali (mstaafu) Said Kalembo akisoma hotuba yake kwenye sherehe za kitaifa za maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani iliyoadhimishwa kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza ilikofanyika Kitaifa hapa nchini,kulia kwa Bw. Kalembo ni Waziri wa Fedha, uchumi na Mpango wa Maendeleo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Omar Yusuph Mzee, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilayani Muheza Bw. Peter Jambele.

Maofisa wa kamati ya ulinzi na usalama kutoka kushoto Kaimu RPC Tanga Mohamed Jafar, mwakilishi wa ofisi ya RSO mkoani Tanga, Mwakilishi wa magereza wakifuatilia kwa makini sherehe hizo.

Mkuu wa mkoa meja jenerali Said kalembo pamoja na waziri wa fedha, uchumi na mpango wa maendeleo wa serikali ya mapinduzi zanzibar Bw. Omar yusuph mzee wakiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za Tanga pamoja na wenyeviti wa halmsauri hizo mara baada ya Mkuu wa mkoa kusoma hutuba kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani iliyofanyika kitaifa wilaya ni Muheza.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Bw. Salim Sinani (kushoto) akiteta jambo na Meya wa Jiji la Tanga Bw. Omar Guled kwenye sherehe za idadi ya watu duniani zilizofanyika wilayani Muheza.

No comments:

Post a Comment