Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Sunday, July 31, 2011

YANGA YAIKACHA COASTAL LEO KUOGOPA MAKWANJA

MABINGWA WA SOKA TANZANIA BARA, YANGA SPORTS CLUB WAMEINGIA MITINI KWA KUAHIRISHA MCHEZO WAO WA KIRAFIKI DHIDI YA 'WAGOSI WA KAYA' COASTAL UNION AMBAYO KWA SASA IPO FITI ASILIMIA 90 KUKABILIANA NA MIKIMIKI YA LIGI KUU YA VODACOM ITAKAYOANZA MWEZI UJAYO. YANGA WAMEAAHIRISHA MECHI HIYO WAKIELEZA KWAMBA KUCHEZA MCHEZO HUO KUTAVURUGA MAANDALIZI YAO YA MCHEZO WA NGAO YA HISANI HAPO AGOSTI 17 MWAKA HUU WATAKAPOCHEZA NA WAPINZANI WAO WAKUBWA SIMBA. HATA HIVYO HABARI ZILIZOZAGAA KATKA MITAA YA NGAMIANI ZINASEMA YANGA WAMEUKACHA MCHEZO HUO ULIOKUWA UPIGWE LEO KWENYE UWANJA WA CCM MKWAKWANI, KUTOKANA NA KUAMINI KWAMBA COASTAL NA SIMBA NI KITU KIMOJA HIVYO WACHEZAJI WA COASTAL WANAWEZA KUTUMIWA NA UONGOZI WA SIMBA KUWAAMUMIZA WACHEZAJI WAO ILI WASHINDWE KUCHEZA VYEMA SIKU HIYO YA NGAO YA HISANI, MANENO HAYO!!! 

No comments:

Post a Comment