Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Wednesday, December 7, 2011

TUTUMIE FURSA ZILIZOPO KATIKA MKOA WETU WA TANGA-RC GALLAWA ASEMA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WILAYANI MUHEZA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU. WA KWANZA KUSHOTO MKUU WA WILAYA YA MUHEZA METHEW NASEI, MWENYEKITI WA CCM WILAYANI MUHEZA PETER JAMBELE NA KATIBU TAWALA WA TANGA BENEDICT OLE UYAN

Sunday, December 4, 2011

TAKUKURU FUATILIENI FEDHA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI HALMASHAURI-GALLAWA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (mstaafu) CHIKU GALLAWA AKIFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA MAOFISA WA TAKUKURU MAKAO MAKUU, MIKOA NA WILAYA ULIOFANYIKA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT-TANGA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (Mstaafu) CHIKU GALLAWA (mwenye koti jekundu na sketi ya bluu) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA NGAZI YA JUU WA TAASISI YA KUZUAI NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU) MARA BAADA YA KUFUNGA MKUTANO WAO WA MWAKA.


Na Mashaka Mhando,Tanga
MKUU wa mkoa wa Tanga, luteni (mstaafu) Chiku Gallawa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuongeza kasi ya kufuatilia fedha zinazopelekwa na serikali katika halmashauri nchini ili ziweze kutumika vizuri kwenye miradi mikubwa ysa maendeleo iliyokusudiwa.

Akifunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa takukuru kwenye hoteli ya Tanga beach Resort kwa maofisa wa taaisis hiyo kutoka mikoa yote ya tanzania bara, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa takukuru wamebeba dhamana kubwa ya kustawisha maendeleo kwa kufautilia watendaji kwenye halmasauri ambao wanatumia vibaya fedha zinazoolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo.

Amesema serikali hasa ya awamu ya nne, imekuwa ikitoa fedha nyingi katika halmashauri kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maeneleo hasa ya elimu, afya, barabara na kujenga majengo mbalimbali lakini fedha hizo wakati mwingine zimekuwa zikitumika visivyo na hivyo kuleta malalamiko kutoka kwa wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa pamoja na kuipongeza taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuokoa fedha za serikali kiasi cha shilingi bilioni 97.5, lakini ameitaka takukuru kuhakikisha inaongeza kasi ya mapambano ya rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi.

Kuhusu wananchi mkuu huyo wa mkoa amewataka kutoa ushirikiano kwa taaisis hiyo na waache kulalamikia masuala ya ufisadi wakati kama watatoa ushirikiano masula hayo yanaweza kudhibitiwa kwa watu kuogopa fedha za umma hatua ambayo mwelekeo wa taasisi hiyo inakoelekea na kwamba waongeze jitihada kutumia nyenzo walizokuwa nazo katika mapambano hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala la mapambano ya rushwa ikiwemo kuwafundisha watumishi wake kwenda sambamba na mabadiliko ya teklonojia katika masuala ya rushwa.
MWISHO

Wednesday, November 30, 2011

RC-TANGA AONGOZA KIKAO CHA KWANZA CHA BODI YA BARABARA TANGA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI CHIKU GALLAWA AKIFUNGUA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA TANGA

BAADHI YA WAJUMBE WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA KUTOKA WILAYA YA KOROGWE WAKIONGOZWA NA DC WAKE BW. ERSTO SIMA (KATIKATI) WAKISIKILIZA KWA MAKINI UWASILISHAJI WA MADA MBALIMBALI KUHUSU BARABARA ZA MKOA WA TANGA

KAIMU MENEJA WA WAKALA WA BARABARA MKOA WA TANGA TANROADS INJINIA ALFRED NDUMBALO AKIWASILISHA TAARIFA YA UFANYAJI KAZI WA WAKALA HIYO KATIKA KIKAO CHA BODI YA BARABARA

MAOFISA WA MKOANI WAKIENDELEA NA ZOEZI LA KUREKODI ORODHA YA WAJUMBE WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA

BAADHI YA WAJUMBE KUTOKA WILAYA YA MUHEZA MBUNGE WA JIMBO LA MUHEZA BW. HERBERT MNTANGI (kulia) NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO BW. AMIR KIROBOTO

MAKAMO MPYA WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA TANGA BW. SALEH PAMBA (KUSHOTO), MWENYEKITI WA CCM MKOA WA TANGA BW. MUSSA SHEKIMWERI NA MWENYEKITI WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA NA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTEN CHIKU GALLAWA WAKIFUATILIA KWA MAKINI HOJA ZA KIKAO HICHO 

Friday, November 25, 2011

MWENGE WAKIMBIZWA TANGA KISHA WAKABIDHIWA MOROGORO

MKUU WA MKOA WA KUSINI PEMBA (aliyeshika Mwenge), MEJA (mstaafu) JUMA K TINDWA AKIMKABIDHI MWENYE WA UHURU MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (mstaafu) CHIKU GALLAWA MARA BAADA YA MWENGE HUO KUWASILI KATIKA UWANJA WA NDEGE UKITOKEA KISIWANI PEMBA.

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (mstaafu) CHIKU GALLAWA AKIWA TAYARI AMEUPOKEA MWENGE WA UHURU KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA KUSINI PEMBA, MEJA (mstaafu) JUMA TINDWA, ANAYEWATAZAMA NI MMOJA WA WAKIMBIZA MWENGE BW. DEOGRATIUS BULLAYI DAFI.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIPOKEA MWENGE WA UHURU KWA HESHIMA BAADA YA MKUU WA MKOA WA TANGA KUSOMA TAARIFA YAKE YA NAMNA MWENGE HUO UTAKAVYOKIMBIZWA KATIKA WILAYA ZA TANGA MJINI NA KILINDI, WA KWANZA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA MKINGA BW. RASHID NDAILE.

WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA TANGA WAKISHUHUDIA TUKIO LA KUKABIDHIWA MWENGE WA UHURU MWAKA HUU MKOANI TANGA AMBAO NI MAALUM KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU

MKUU WA MKOA WA MOROGORO BW. JOEL BENDERA AKIWA AMEUPOKEA MWENGE WA UHURU KUTOKA KWA KAIMU MKUU WA MKOA WA TANGA KAMPTENI (mstaafu) SEIF MPEMBENWE ALIYEUKABIDHI MWENGE HUO MKOANI HUMO KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA ALIYEKUWA NA MAJUKUMU MENGINE YA KITAIFA.

Tuesday, November 15, 2011

WANANCHI TANGA WATOA RAMBIRAMBI KWA WALIOKUFA KWA AJLI YA MELI YA MV SPICE ISLENDARS

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GALLAWA AKIMKABIDHI MAKAMU WA PILI WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLI IDD HUNDI YA SHILINGI MILIONI 11.2 KAMA MCHANGO WA RAMBIRAMBI KWA WANANCHI WA ZANZIBAR KUFUATIA KUZAMA KWA MELI YA MV. SPICE ISLANDERS ILIYOZAMA MIEZI MIWILI ILIYOPITA.
Na Mashaka Mhando,Zanzibar
MKUU wa mkoa wa Tanga, luteni (mstaafu) Chiku Gallawa, amesema wananchi wa mkoa huo, waliupokea kwa masikitiko makubwa msiba wa wananchi waliokuwemo kwenye meli ya Mv Spice Islanders iliyozama miezi miwili iliyopita kwenye mkondo wa Nungwi Visiwani humo, na kwamba wameguswa hasa kutokana na ukaribu wake na visiwa hivyo.

Akizungumza juzi wakati wa kukabidhi rambirambi ya michango kwa ajili ya watu waliopeza maisha kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi, Seif Alli Idd, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wanachi wa mkoa wa Tanga waliuopokea kwa masikitiko makubwa msiba huu mzito kutokana na mkoa huo kuwa na mahusiano ya karibu kutokana na kutenganishwa na bahari ya Hindi.

Alisema kuwa msiba huo utazidi kuwaunganisha wananchi wa mkoa huo na Visiwani humo katika kipindi chote cha raha, tabu na majonzi ya kuwakumbuka ndugu zao waliopoteza maisha kwenye jali hiyo na kwamba wataendelea kuwaombea ili mwenyezi Mungu awalale mahali pema peponi.

"Tanga na Zanzibar ni karibu sana na wanachi wa pande zote mbili wana mahusiano ya karibu sana.wameguswa na msiba huu na wameomba tuwasilishe pole nyingi sana pamoja na rambirambi hii ya hundi ya sh 11,288,250, msiba huu utazidi kuwaunganisha katika kipindi chote cha raha na taabu, wameomba mwenyezi mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu," alisema Mkuu huyo wa mkoa.

Luteni Gallawa aliwataka wale waliokabidhiwa dhima ya kusafirisha abiria katika vyombo vya usafiri wawe wanajali maisha ya watumiaji wao na kwamba wakati mwingine majanga ya namna hiyo yamekuwa yakiepukika lakini kutokana na wasafiishaji kujaza watu kupita kiasi hupelekea matatizo ambayo husababisha maafa kama yaliyotokea kwenye meli hiyo.

Kwa upande wake Makamu wa rais, alishukuru mchango huo kutoka kwa majirani zao wa karibu na kwamba rambirambi hiyo ni kielelezo tosha cha Muungano uliotukuka baina ya wananchi wa visiwani na bara kwa kujaliana katika shida na raha hasa katika ajali hiyo ambayo haiwezi kusauliwa kutoka na uwingi wa vifo vya watu waliopoteza maisha.

"Ulikuwa ni msiba mkubwa katika historia ya Zanzibar, watu 203 walithibitika kufariki na 619 waliokolewa, serkali zote mbili ya Muungano na ya Mapinduzi Zanzibar zilishirikana katika kipidi chote cha janga hili, na kuwasaidia wahanga hao," alisema Makamu huyo wa Rais.

Alisema tume imeundwa kuchunguza mkasa huu na serikali ya SMZ itatoa majibu yake hadharani kwa wananchi ili kuepusha janga kama hilo lisitokee tena na kwamba michango yote itapokelewa na kutumiwa kwa makusudi kwa kadri itakavoamriwa na serikali.

Ujumbe wa Tanga kwenda visiwani humo uliongozwa na Mkuu huyo wa mkoa, pia walikuwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa Bw. Mussa Shekimweri Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi, Mkuu wa wilaya ya Muheza Bw. Methew Nasei na mwakilishi wa wafanyabiashara mkoani Tanga Bw.Salim Abdallaziz  kutoka kampuni ya unga wa ngano ya Pembe.

Sunday, November 6, 2011

KUMBE KUNA SAMAKI WAKUBWA KIASI HIKI!

VIJANA WA KIJIJI CHA BAGAMOYO KILICHOPO WILAYANI KOROGWE WAKIVUA SAMAKI KATIKA DARAJA MOJA WAPO AMBALO LINAJENGWA NA KAMPUNI YA KICHINA YA SINOHYDRO, DARAJA HILO LIPO JIRANI NA MTO PANGANI AMBAO MAJI YA MTO HUO YAMEKATISHA BARABARA HIYO NA VIJANA HAO KUPATA NAFASI YA KUVUA SAMAKI

JUMA (KUSHOTO) NA SUFIANI WAKIVUA SAMAKI

ADAM NA SAID WAKIVUA SAMAKI KWA CHANDARUA KILICHOTOLEWA KWA AJILI YA KUJIKINGA NA MALARIA, LAKINI WANAKITUMIA KUVULIA SAMAKI.

VIJANA WAKIVUA HUKU WAKICHEZA KATIKA DARAJA HILO

SAMAKI WALIOVULIWA KATIKA DARAJA HILO

"...TUNAPATA SAMAKI HAPA, WEEE USICHEZE SI UNAWAONA HAWA...SHULE KWANINI BANA SI NAVUA NIKIUZA NITAPATA PESA...,ANASEMA GUMBO MLIMBO

Wednesday, November 2, 2011

TICTS YAKUTANA NA WADAU WAKE KWENYE HOTELI YA TANGA BEACH RESORT

OFISA MTENDAJI MKUU WA TICTS BW. NEVILLE BISSETT AKIELEZEA NAMNA KAMPUNI HIYO YA KUPAKUA MAKONTENA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM JINSI ITAKAVYOWEZA KUONGOZA KATIKA KAZI YA KUPAKUA MAKONTENA KATIKA NCHI ZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA.

WADAU WA MKUTANO ULIOITISHWA NA TICTS KWENYE HOTELI YA TANGA BEACH RESORT KUZUNGUMZIA CHANGAMOTO ZA KAMPUNI HIZO.

WADAU WAKISIKILIZA KWA MAKINI MKUTANO WA WADAU WA TICTS

WADAU WAKIPIA PICHA YA PAMOJA KWENYE HOTELI YA TANGA BEACH RESORT JIJINI TANGA.

Saturday, October 29, 2011

MKUU WA MKOA ATEMBELEA MGODI WA KUZALISHA UMEME WA HALE, AKUTANA NA CHANGAMOTO

MKUU WA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA NEW PANGANI FALLS POWER STATION INJINIA PAKAYA MTEMAKAYA AKIMSOMEA TAARIFA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GALLAWA ALIPOTEMBELEA KAIKA MGODI WA KUZALISHA UMEME ULIOPO HALE WILAYANI KOROGWE.

WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KOROGWE PAMOJA NA MSAIDIZI WA MKUU WA MKOA WA TANGA, BW. JOSEPH SURA (KULIA), WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA LUTENI CHIKU GALLAWA (HAYUPO PICHANI) ALIPOTEMBELEA MGODI WA KUZALISHA UMEME HALE.

INJINIA PAKAYA MTEMAKAYA (ALIYENYOOSHA MKONO JUU) AKIMWELEZA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI CHIKU GALLAWA (KUSHOTO) NAMNA UZALISHAJI UNAVYOFANYIKA KWENYE MGODI HUO WA KUZALISHA UMEME HALE.


INJINIA PAKAYA MTEKAYA AKIMWELEZA MKUU WA MKOA NAMNA ABAVYO CHANAMOTO ZA UZALISHAJI UMEME ZINAVYOSABABISHA WAKAI MWININE WASHINDWE KUZALISHA KWA UFANISI

MKUU WA MKOA LUTENI CHIKU GALLAWA NA WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALMA YA WILAYA YA KOROGWE WAKITEMBEA NDANI YA MGODI WA UZALISHAJI UMEME WA HALE WILAANI KOROGWE AMBAKO WALIJIONEA KAZI MBALIMBALI ZINAZOFANIKA ZA UZALISHAJI UMEME.

INJINIA PAKAYA MTEMAKAYA AKIELEZA KWAMBA KITUO HICHO TANGU KIMEJENGWA MIAKA YA 1995 KIMEKUWA KIKIFANYA KAZI VIZURI ISIPOKUWA KOMPYUTA ZINAZOENDESHA MITAMBO ZIMEHARIBIKA NA HIVYO MITAMBO KUENDESHWA KWA KUTUMIA USIMAMIZI WA WATU

MKUU WA MKOA AKITOA MAELEKEZO YA NAMNA YA KUANGALIA CHANGAMOTO WANZOKABILIANA NAZO WATENDAJI WA MGODI WA KUZALISHA UMEME HALE HUKU WATENDAJI HAO WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI.

INJINIA MUSIMU MAKUNGA MSIMAMIZI WA MGODI WA KUZALISHA UMEME WA PANGANI FALLS AKITOA MAELEKEZO WA JINSI WANAVYOWEZA KUENDESHA MITAMBO HIYO YA KUZALISHA UMEME KATIKA MAJUKUMU YAO YA KILA SIKU.

MKUU WA MKOA NA WENYEJI WAKE WA MGODI WA KUZALISHA UMEME WALIPATA FURSA YA KUTEMBELEA MGODI WA ZAMANI WA KUZALISHA UMEME WA OLD PANGANI FALLS KWA KUPANDA KIBERENGE KAMA WANAVYOONEKANA KATIKA PICHA.

HAPA MKUU WA MKOA LUTENI CHIKU GALLAWA AKIWA NA MSAFARA WAKE WAKIANGALIA KINA CHA MAJI KATIKA BWAWA LILILOZUIWA KWA AJILI YA KUPELEKA MAJI KATIKA MGODI HUO

Friday, October 28, 2011

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA BARABARA YA TANGA/HOROHORO, BANDARI YA TANGA

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIUNDOMBINU INJINIA OMARI CHAMBO, AKITOA UFAFANUZI KWA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WALIOKUWA KWENYE MKUTANO KWENYE JENGO LA BANDARI HOUSE TANGA

WATENDAJI WA BANDARI YA TANGA WAKIFUATILIA KWA MAKINI MICHANGO YA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIUNDOMBINU INJINIA OMARI CHAMBO (KATIKATI) AKIELEZEA JAMBO KWA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WALIOTEMBELEA BANDARI YA TANGA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI

MJUMBE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU BW. HERBERT MNTANGI AMBAYE NI MBUNGE WA MUHEZA (BONDE) AKIWAELEKEZA WAJUMBE WENZAKE JINSI KISIWA KILICHOPO JIRANI NA BANDARI YA TANGA KINAVYOWEZA KUZIDISHA KUJAA KWA MCHANGA KATIKA BANDARI YA TANGA

HAPA WAJUMBE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WAKIWA NA WAFANYAKAZI WA BANDARI YA TANGA, WAKIPATA MAELEZO KATIKA ENEO LA KUINGIA KATIKA ENEO AMBALO LITAJENGWA BANDARI MPYA SEHEMU YA MWAMBANI

WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU NA WAFANYAKZI WA BANDARI YA TANGA, WAKITAZAMA ENEO AMBALO LITAJENGWA BANDARI YA KINA KIREFU KATIKA SEHEMU YA MWAMBANI

MTAALAMU WA TANROADS INJINIA EDWARD AKIWAELEKEZA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU JINSI KAMPUNI YA KICHINA YA SINOHYDRO ILIVYOJIDHATITI KATIKA KUHAKIKISHA INAMALIZA BARABARA YA TANGA/HOROHORO KUWEKA LAMI NA KUIMALIZA KWA WAKATI

WAHESHIMKWA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WAKITEMBEA KWA MIGUU KWENDA KUANGALIA DARAJA LA NDOYO AMBALO WACHINA WA KAMPUNI YA SINOHYDRO WAMELIJENGA KWA UBORA WA HALI YA JUU

MWENYEKITI WA KAMATI PETER SERUKAMBA (MBELE) AKIWAONGOZA WABUNGE WENZAKE KUTEMBELEA BARABARA YA TANGA/HOROHORO

Thursday, October 27, 2011

MKUU WA MKOA WA TANGA, ATEMBELEA VIWANDA NI ZIARA YAKE YA KWANZA TANGU ATEULIWE KUWA RC MPYA

MKUU WA MKOA WA TANGA, LUTENI (Mstaafu) CHIKU GALAWA (kushoto) AMEANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VIWANDA VILIVYOPO JIJINI TANGA, KUONA SHUGHULI MBALIMBALI WANAZOZIFANYA IKIWA NI ZIARA YAKE YA KUJIFUNZA NAMNA VIWANDA VILIVYOPO HAPA VINAVYOKABILIWA NA MATATIZO, PICHA HII RC HUYO ALIIPIGA WILAYANI PANGANI ALIKOKWENDA KUTAMBULISHWA NA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA HUU, MEJA GENERALI SAID KALEMBO (katati) WALIYEKUWA NAYE NI MDAU WA TEKLONOJIA YA ELETRONIKI MOHAMED HAMMIE 'ANKO MO'.

Monday, October 24, 2011

KILA LA KHERI COASTAL UNION LEO ISHINDWE DHIDI YA POLISI DODOMA

KIKOSI CHA COASTAL UNION AMBACHO LEO KITAPAMBANA NA TIMU YA POLISI DODOMA KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI MAJIRA YA SAA 10:00 JIONI MCHEZO AMBAO UNATARAJIWA KUWA MKALI HASA KUTOKANA NA POLISI KUFUNGWA BAO 3-1 NA AZAM KWENYE UWANJA WA CHAMANZI JIJINI DAR ES SALAAM NA 'WAGOSI WA KAYA' KUWA KATIKA KIWANGO KIZURI TANGU WALIPOISARAMBATISHA VILLA SQUAD KWA MABAO 6-1 NA TIMU HIYO KUPUMZIKA MUDA MREFI HIVYO WATAINGIA UWANJANI WAKIW ANA ARI YA KUENDELEZA USHINDI CHINI YA KOCHA WAO MAHIRI JAMHURI KIHWELO 'JULIO'. MARA YA MWISHO TIMU HIZO KUCHEZA KWENYE UWANJA HUO ILIKUWA MWAKA 2008 AMBAPO POLISI WALIIFUNGA COASTAL BAO 1-0 BAO LILILOFUNGWA NA BANTU ADIMIN KIPINDI CHA PILI, JE COASTAL WATAFUNJWA MWIKO WA KUFUNGWA NA TIMU HIYO KWENYE UWANJA WAKE WA NYUMBANI?

UNAPOWAPA WATOTO CHAKULA SHULENI UWEZO WAO WA KUFIKIRI UNAONGEZEKA

WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI KATIKA SHULE YA MSINGI LWENGERA ESTATE WAKIWA KWENYE FOLENI YA CHAKULA MARA BAADA YA KUMALIZA VIPINDI VYAO VYA MASOMO SHULENI HAPO, WANAOWAANGALIA NI MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU' (MWENYE SUTI NYEUPE) ALIYEFIKA SHULENI HAPO KWENYE MAHAFALI YA DARASA LA SABA MWAKA HUU, WENGINE NI MAOFISA WA SHULE NA KATA YA KWAGUNDA ILIPO SHULE HIYO.

MMOJA WA WALIMU WA SHULE YA LWENGERA ESTATE AKIWAPAKULIA CHAKULA 'WALI' WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI WA SHULE HIYO MARA BAADA YA KUMALIZA VIPINDI VYAO VYA MASOMO.

"NTILIE MWINGI MWALIMU, LEO NINA NJAA MAANA NIMESOMA SANA' NDIVYO INAVYOELEKEA KUSEMA HIVI MWANAFUNZI WA DARASA LA AWALI LA SHULE YA LWENGERA ESTATE , BATULI RAJABU (KUSHOTO) AKIMWELEZA MWALIMU WAKE AMJAZIE CHAKULA HICHO.

WALI MAHARAGE WANAFUNZI HAWA WA DARASA LA AWALI LA SHULE YA MSINGI LWENGERA ESTATE WAKIPAKULIWA CHAKULA CHA MCHANA MARA BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAO SHULENI HAPO. UTARATIBU HUO NI MZURI KWANI UNAMFANYA MTOTO AFURAHI MASOMO NA WAKATI HUO KUKUA UWEZO WAKE WA KUFIKIRI NA KUKARIRI SABABU YA KUPATA CHAKULA SHULENI.