Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Sunday, July 24, 2011

KAMANDA MPYA WA POLISI TANGA AANZA KAZI KWA KUKAMATA SMG NA BASTOLA

KAMANDA MPYA WA POLISI MKOANI TANGA ACP CONSANTINE MASAWE AKIWAONYESHA SILAHA WALIZOKAMATA HUKO MTONI BOMBO WILAYANI KOROGWE BAADA YA KUMKAMATA JAMBAZI SUGU

KAMANDA MPYA WA POLISI MKOANI TANGA ACP CONSTANTINE MASAWE AKIJARIBU KUIPIGA SILAHA AINA YA SMG WALIYOIKAMATA KWA JAMBAZI MMOJA HUKO KOROGWE

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WALIOFIKA KWENYE OFISI YA KAMANDA MPYA WA POLISI MKOANI TANGA KUKUTANA NAYE KWA MARA YA KWANZA AMBAPO ALIWAPA HABARI YA KUKAMATA BUNDUKI AINA YA SMG NA BASTOLA (KULIA) NI WILLIAM MNGAZIJA AKIMSIKILIZA KWA MAKINI KAMANDA HUYO (KUSHOTO).

PROFESA J AWARUSHA WANAFUNZI ONESHO LA MALARIA HAIKUBALIKI

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI USAGARA WAKIFUATILIA KWA MAKINI ONESHO LA KAMPENI YA KUPIGA VITA MALARIA HAIKUBALIKI LIKIONGOZWA NA WASANII WA THT AKIWEMO PROFESA J AMBAYE ALITOA BURUDANI ILIYOFURAHIWA NA WANAFUNZI WENGI WALIOHUDHURIA.

PROFESA J AKITOA BURUDANI KWENYE UWANJA WA SHULE YA SEKONDARI YA USAGARA SEKONDARI JIJINI HAPA AKISHIRIKIANA KUIMBA NA MWANAFUNZI MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA ZENNA WIMBO WA 'ZARI LA MENTALI' KIBAO AMBACHO KWA HAKIKA KILIWABURUDISHA IPASAVYO WANAFUNZI.

PROFESA J AKIIMBA PAMOJA NA MMOJA WA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI GALANOSI AMBAYE ALIKUWA AKISHINDANA NAYE KUIMBA KIBAO 
 MCHANGANYIKO.
Professor Jay and Ditto meet with studnets in Tanga using performance to fight malaria
July 21st 2011.
On the 21stof July, students from ten schools came together at Usagara Secondary School in Tanga town to take part in malaria themed song, theatre and poetry competitions. The competition was a part of the Zinduka! club initiative, in which youth are empowered with the knowledge and tools to drive forward the fight against malaria in local communities. The judges were treated to a spectacle of talent as they witnessed an array of performances including poetry readings, songs and even theatrical performances
On reaching the final round, Tanzanian artist, Ditto, took to the stage to talk to the students about how important it is to protect themselves from malaria to ensure they secure their future, before the artist sang the malaria he had written for the Zinduka! campaign which has now become an anthem for a generation fighting against malaria.
The students were then surprised when another guest Bongo fleva rapper and Zinduka! goodwill ambassador Professor Jay joined Ditto on stage to sing the anthem. The artist has been a prominent figure in the fight against malaria, featuring in the launch of the Zinduka! campaign in 2010 and making regular appearances for the campaign in the field and on TV.Professor Jay then took time to hand out awards to the lucky competition winners.
Professor J had this to say, “I joined the Zinduka! campaign with the hope that through my music I could help to fight malaria in Tanzania. But to see kids wanting to get involved and using music as the platform to fight malaria in their communities, that’s what makes me most proud of the work we have done.
Professor Jay and Ditto then invited youth to join him as he visited a number of houses near Tanga town, where the youth spoke to households about what measures they use to protect themselves from malaria and what they think needs to be done to eradicate malaria in Tanzania.

The Malaria Haikubaliki Campaign is led by the Tanzanian Government behind the leadership of President JakayaKikwete. It is supported by partners including Malaria No More, Tanzania House of Talent (THT), Johns Hopkins University, Population Services International and United Against Malaria. The goal of the program is to achieve universal bed net coverage and eliminate malaria deaths by urging all Tanzanians to Zinduka! (“Wake up!”) to the threat of malaria and protect themselves against the disease.


 
              











Friday, July 15, 2011

SIMBA VIDEO COACH YATOA MABASI MAPYA

KWA USAFIRI WA RAHA SAFIRI NA BUS LA SIMBA VIDEO COACH KWA SAFARI ZAKO ZA DAR ES SALAAM, DODOMA, MOROGORO NA ARUSHA

BUS JIPYA LA SIMBA VIDEO COACH LINAVYOONEKANA KWA NDANI

Wednesday, July 13, 2011

DC ACHELEWA BAADA YA GARI LAKE KUHARIBIKA

Katibu Tawala (DAS) wa wilaya ya Korogwe Mr Kembo aliyevaa suti (kulia) akisisistiza gari litengenezwe haraka ili Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima awezekusafiria gari hilo ambalo lilikuwa haliwaki wakati akitaka kwenda vijijini kwa kazi za maendeleo

Tuesday, July 12, 2011

SHEREHE ZA IDADI YA WATU DUNIANI ZAFANA MUHEZA

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Meja Jenerali (mstaafu) Said Kalembo akisoma hotuba yake kwenye sherehe za kitaifa za maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani iliyoadhimishwa kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza ilikofanyika Kitaifa hapa nchini,kulia kwa Bw. Kalembo ni Waziri wa Fedha, uchumi na Mpango wa Maendeleo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Omar Yusuph Mzee, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilayani Muheza Bw. Peter Jambele.

Maofisa wa kamati ya ulinzi na usalama kutoka kushoto Kaimu RPC Tanga Mohamed Jafar, mwakilishi wa ofisi ya RSO mkoani Tanga, Mwakilishi wa magereza wakifuatilia kwa makini sherehe hizo.

Mkuu wa mkoa meja jenerali Said kalembo pamoja na waziri wa fedha, uchumi na mpango wa maendeleo wa serikali ya mapinduzi zanzibar Bw. Omar yusuph mzee wakiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za Tanga pamoja na wenyeviti wa halmsauri hizo mara baada ya Mkuu wa mkoa kusoma hutuba kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani iliyofanyika kitaifa wilaya ni Muheza.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Bw. Salim Sinani (kushoto) akiteta jambo na Meya wa Jiji la Tanga Bw. Omar Guled kwenye sherehe za idadi ya watu duniani zilizofanyika wilayani Muheza.

Saturday, July 2, 2011

COASTAL UNION YAPATA UONGOZI MPYA

VIONGOZI WAPYA WA KLABU YA COASTAL UNION WALIOCHAGULIWA LEO MAKAO MAKUU YA KLABU HIYO BARAARA 11 JIJINI TANGA, KUTOKA KUSHOTO NI ALBERT PETER (Mjumbe), SALIM AMIR (Mjumbe), AHMED HILAL 'AURORA' (Mwenyekiti), JAMES MWINCHANDE (Mjumbe) NA JULIUS BENJAMIN MJUMBE PIA MARA BAADA YA KUCHAGULIWA KWENYE MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI.

MWENYEKITI MPYA WA KLABU YA COASTAL UNION (kushoto) AKIVALISHWA KITAMBAA CHEKUNDU NA MMOJA YA WANACHAMA WA SIKU NYINGI WA KLABU HIYO MICHENI AHMED MICHENI BAADA YA KUTANGAZWA KUWA MSHINDI KISHA MWANACHAMA HUYO KUMPONGEZA KWA KUMVIKA KITAMBAA HICHO.

WANACHAMA WAKIWA TULI WAKIFUATILIA KWA MAKINI MATOKEO YA UCHAGUZI YAKITANGAZWA NA MWENYEKITI WA UCHAGUZI WA KLABU HIYO ABDALLAH YAHYA (hayupo pichani) WAKATI WA KUHESABU KURA ZILIZOPIGWA NA WAJUMBE WALIOFIKA KWENYE UCHAGUZI HUO.

WANACHAMA WA KLABU YA COASTAL UNION WAKIFUATILIA KWA MAKINI ZOEZI ZIMA LA UCHAGUZI LILILOVYOKUWA LIKIENDESHWA KATIKA KLABU HIYO HATUA AMBAYO IMEWEKA HISTORIA YA KLABU HIYO KUFANYA UCHAGUZI MKUU WA VIONGOZI WAKE BAADA YA MIAKA TISA TANGU ULIPOFANYIKA UCHAGUZI WA KIKATIBA MWAKA 2002.

MCHEZAJI WA SIKU NYINGI WA KLABU YA YANGA KITWANA MANARA (aliyesimama) AKITOA NASAHA ZAKE KAMA MMOJA YA VIONGOZI WA KAMATI YA UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI TFF AKIELEZEA TARATIBU ZILIZOSABABISHA HADI KLABU HIYO IKAFANYA UCHAGUZI WAKE HUO WA VIONGOZI.

MWENYEKITI MPYA WA KLABU YA COASTAL UNION AHMED HILAL 'AURORA' (wa pili kushoto) AKIWA NA WAJUMBE WAKE NA BAADHI YA WANACHAMA AKIWEMO KITWANA MANARA (kushoto kwake), STEVEN MGHUTO, ALBERT PETER NA MWENYE KANZU NI ALYEKUWA MWENYEKITI WA KLABU HIYO KAMATI YA MUDA MZEE TALHATA
Na Mashaka Mhando,Tanga
KLABU ya Coastal Union ya Jijini Tanga, leo imefanya uchaguzi wake wa kikatiba wa kuchagua viongozi wake watakaoiongoza klabu hiyo kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu baada ya miaka takribani taisa kuongozwa na kamati za muda.

waliochaguliwakatika mkutano huo ambao awali ulikuwa ufanyike wiki iliyopita lakini ulisimamishwa na TFF (shirikisho la soka nchini) baada ya kuwaengua wagombea saba ambao hawakuwa na sifa za kuwania nafasi hizo ni pamoja na Mwenyekiti Ahmed Hilal 'Aurora' ambaye hakuwa na mpinzani baada ya kujizolea kura 52 kati ya wajumbe 55 waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo.

Wajumbe waliochaguliwa kura zao zikiwa kwenye mabano ni pamoja na Kweli Nahashon (48), Albert Peter (47), Salim Amir (42), Julius Benjamin (42) na James Mwinchande ambaye alipata kura 36.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa kamati ya uchaguzi wa klabu hiyo Abdallah Yahya alisema kuwa watu waliojiandikisha kupiga kura kwa maana wanachama halali walikuwa 77 lakini kwenye uchaguzi huo wamefika wanachama 55 hivyo uchaguzi huo ulifanyika kutokana na koram ya wajumbe kutimia.

Alisema kwa mujibu wa katiba ya Coastal Union viongozi wanatakiwa kuwa tisa kwa maana Mwenyekiti, Makamo Mwenyeki na wajumbe saba lakini kutokana na kwamba kumebaki nafasi tatu za makamo mwenyekiti na wajumbe wa tatu uchaguzi mwingine utaitisha mara baada ya wanachama ambao walienguliwa kukamilisha taratibu za kuwasilisha vyeti wakikamilisha.

Wanachama ambao waliomba lakini walienguliwa ni pamoja na Makamo Mwenyekiti Steven Mghuto na Titus Bandawe, Yakob Nuru, Jawa Bakari Jawa, Ayub Athumani na Kilo Rashid.

Kwa mara ya mwisho klabu hiyo ilifanya uchaguzi wake wa kikatiba mwaka 2002 ambapo marehemu Zacharia Kinanda 'Arrigo Sacchi' aliachaguliwa kuwa Katibu Mkuu na wakati huo huo akiwa kocha mkuu wa timu hiyo na Mbwana Abushiri 'Director' akiwa mwenyekiti.
MWISHO

MASIKINI BANDARI YA TANGA HIVI NI KWELI WAFANYABIASHARA HAWAPENDI KUITUMIA SABABU YA TRA?

BANDARI YA TANGA INAVYOONEKANA PICHANI

BANDA LINALOFANYA BIASHARA YA MNADA WA SAMAKI LILILOPO ENEO LA DEEP SEA KATIKA JIJI LA TANGA NI MOJA YA ENEO LA SIKU NYINGI SANA PEMBEZONI MWA BANDARI YA TANGA.

SHAZI HILI LA SAMAKI LILIUZWA SH. 18,000, SAMAKI SASA HIVI WANABEI SANA NA HASA HII JULAI!

WADAU WATAKA TAMASHA LA FILAMU TANGAMANO LIFANYIKE KILA MWAKA

TAMASHA la wazi la sinema ambalo linafikia kelele chake leo kwenye uwanja wa Tangamano huku filamu iliyoongozwa na Single Mtambalike (Richie) na kuzalishwa na Suleiman Said Barafu ya Senior Bachelor ndiyo iliyofunga pazia la tamasha hilo huku wadau wa filamu wakiomba tamasha hilo lifanyike kila mwaka mjini hapa.

Tamasha hilo ambalo lilikuwa la wiki moja ambalo limedhaminiwa na Grand Malt Tanzania lilianza Juni 27 katika viwanja ya Tangamano Mjini Tanga, lilihudhuriwa na maelfu wa Jiji la Tanga na wilaya jirani ambao wameweza kuwaona wasanii waliokuwa wakiwaona tu luningani.

Filamu hiyo ambayo ilioneshwa kwenye uwanja huo ilitanguliwa na maelezo kutoka kwa muigizaji wake Jacob Steven maarufu kama JB ambaye ameshajizolea umaarufu mkubwa kupitia filamu kadha alizoigiza. 
 
 
 

FAX JAZZ INAVYOKONGA NYOYO ZA WATU TANGA HOTEL

WANA-MUZIKI WA BENDI MAARUFU JIJINI TANGA YA FAX JAZZ BAND AMBAYO IMEKUWA IKITUMBIZA KILA SIKU ZA ALHAMISI, IJUMAA, JUMAMOSI NA JUMAPILI KATIKA UKUMBI TANGA HOTELI AMBAKO MASHABIKI MBALIMBALI WA MUZIKI WA DANSI WAMEKUWA WAKIFURIKA. PICHANI NI MWIMBAJI KIDUCHU AKIWA NA MGOSIGWA AKIKUNG'UTA GITAA LA RYTHIM.

MSHABIKI MAARUFU WA MUZIKI UNAOAPIGWA TANGA HOTEL MR RASTA AKISAKATA MUZIKI WA FAX AKIWA NA MKEWE KWENYE UKUMBI HUO WA TANGA HOTEL.

MRATIBU WA UKIMWI WA JIJI LA TANGA MR MOSES NAYE HAKUBAKI NYUMA ALIKUTWA NA KAMERA YETU AKISAKATA MUZIKI WA FAX HUKU AKIMWAGA SERA ZA UPIMAJI WA HIARI WA VIRUSI VYA UGONJWA FAKIRI WA UKIWMI.

SHIRIKA LA SAHiRNGON YAJIKITA MUHEZA KUFUNDISHA NAMNA YA UFUATILIAJI WA FEDHA ZA KILIMO ZINAZOTUMWA NA SERIKALI WILAYANI HUMO

MRATIBU WA MTANDAO WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YA HAKI ZA BINADAMU KUSINI MWA AFRIKA (SAHiRNGON) MARTINA  KABISAMA (wa kwanza kushoto) AKIWA PAMOJA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA WILAYA YA MUHEZA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA KIROBOTO, ALEX MBEJO KWENYE MKUTANO WA WADAU WA KUFUATILIA FEDHA ZA KILIMO NA MIFUGO WILAYANI HUMO.

MRATIBU WA SHIRIKA LA SAHiRNGON MARTINA KABISAMA AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI ZA KUFUATILIA FEDHA ZA KILIMO WILAYANI MUHEZA KUTOKA KATA ZA TONGWE, KISIWANI NA NKHUMBA KWENYE MKUTANO ULIOFANYIKA KWENYE HOTELI YA AMBASSADOR WILAYANI HUMO.

WAJUMBE WA KAMATI ZA UFUATILIAJI WA FEDHA ZILIZOLETWA NA SERIKALI KWA AJILI YA KILIMO WILAYANI MUHEZA KUTOKA KATA ZA TONGWE, KISWANI NA KHUMBA WAKIMSIKILIZA MRATIBU WA SHIRIKA LA SAHiRNGON MARTINA KABISAMA (hayupo pichani) KWENYE MKUTANO ULIOFANYIKA WILAYANI MUHEZA.

SI KWAMBA WAMECHOKA AU WANASINZIA KUTOKANA NA UCHOVU WA KUKAA MUDA MWINGI LA HASHA! BALI WAJUMBE HAWA KUTOKA KATA ZA TONGWE, KISIWANI NA NKHUMBA WAKISIKILIZA KWA MAKINI NAMNA SERIKALI INAVYOWEZA KUTUMA FEDHA VIJIJINI NA WAKATI MWINGINE FEDHA HIZO HAZIONEKANI NA WALA HAZITUMIKI KWA MIRADI ILIYOKUSUDIWA HIVYO WAJUMBE HAO WAKAONEKANA HAWAELEWI UTARATIBU UNAVYOTUMIKA KUJUA FEDHA HIZO ZINAWEZEKANAJE KUFIKA BILA KUTUMIWA.

Friday, July 1, 2011

MASHINDANO YA POOL MKOANI TANGA KUANZA SPLENDID NA MAGROVE JULY 7 HADI 10 KWA VILABU VINANE KUCHUANA

MSIMU WA MASHINDANO YA KUTAFUTA KLABU BINGWA YA MCHEZO WAPOOL MKOANI TANGA UMEANZA, PICHANI NI MENEJA WA BIA YA SAFARI LAGER MKOANI TANGA MR. MBISE (kushoto) AKIWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA POOLTABLE MKOA WA TANGA (TARPA) SHABAN KIBELLOH WAKIWA KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA ZE CITY KULIKOKUWA NA 'SPEED POOL'

WATAALAM WA KAMPUNI YA INTERGRETED YA JIJI DAR ES SALAAM INAYOHUSIKA NA MATANGAZO YA BIA YA SAFARI LAGER WAKITOA MATANGAZO YAO KUHUSU KUANZA RASMI KWA MASHINDANO YA POOL MKOANI TANGA.

KATIKA MSIMU HUU WA MASHINDANO YA POOL KULIKUWA NA SHINDANO DOGO LA KUTAFUTA BINGWA ANAYEWEZA KUINGIZA KETE ZOTE 15 NDANI YA DAKIKA 3 TU NA PICHANI NI BINGWA ALIYEWEZA KUINGIZA KETE HIZO KWA KUTUMIA DAKIKA 2 NA SEKUNDE 32 HUYO SI MWINGINE NI ALLY SHARIFF MCHEZAJI WA KLABU YA KWAMINCHI. HII NI SPEED POOL.

HAPA MSHINDI WA SPEED POOL ALLY SHARIFF AKIWA NA MTANGAZAJI WA INTERGRETED BI LATIFA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA ZAWADI YAKE KISHA KUVALIA JEZI YAKE YA SAFARI LAGER HAPA AKIONGEA MANENO MAWILI MATATU NA LATIFA.

Thursday, June 30, 2011

UKUMBI UNAOFANYIA MIKUTANO YA BARAZA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA MDOGO

MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA WAKIENDELEA NA MJADALA WA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI HIYO, LEO KWENYE UKUMBI WA HALMASHAURI HIYO AMBAYO BAADHI YA WADAU WAMEULALAMIKIA UKUMBI HUO WAKIDAI KWAMBA NI MDOGO UNAPASWA KUJENGWA UKUMBI MKUBWA KWA FAIDA YA VIONGOZI WAJAO.
DIWANI WA KATA YA NKUMBA (wa kwanza kushoto) AKIWA NA DIWANI WA KATA YA TONGWE WAKISIKILIZA KWA MAKINI MJADALWA WA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KILICHOFANYIKA LEO KWENYE UKUMBI AMBAO NI MDOGO SANA WA HALMSHAURI HIYO.

Tuesday, June 28, 2011

TANGA CEMENT YATOA MSAADA WENYE THAMANI YA SHILINGI MIL 57 KWA KITUO CHA WALEMAVU MOROGORO

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA TANGA CEMENT ERIK WESTERBERG (mwenye shada la maua kulia) AKIMKABIDHI FUNGUO ZA BWALO LA KULIA CHAKULA NA JIKO PADRI BEATUS SEWANDO AMBAYE NI  MKURUGENZI WA KITUO CHA KUWAHADUMIA WALEMAVU CHA AMANI KILICHOPO WILAYANI MVOMELO MKOANI MOROGORO, MSAADA HUO UMEGHARIMU KIASI CHA SHILINGI MILIONI 57.

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA TANGA CEMENT ERIK WESTERBERG (mwenye shati nyeupe) AKISHIKANA MIKONO NA MMOJA YA WATOTO WANAOLELEWA KATIKA KITUO HICHO CHA AMANI, IMA KAMOTA.

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA TANGA CEMENT ERIK WESTERBERG (kushoto) AKISHIKANA MIKONO NA MAMA JOSEPHINE MAKITA AMBAYE NI MWANZILISHI WA KITUO HICHO CHA AMANI KILICHOPO WILAYANI MVOMELO MKOANI MOROGORO KATIKA HAFLA HIYO FUPI YA KUKABIDHI JENGO LA CHAKULA NA JIKO

Wednesday, June 22, 2011

KAMATI ANGALIENI MAHAKIMU WANAOKIUKA MAADILI YAO-JAJI MKUU AIAMBIA KAMATI YA WATUMISHI WA MAHAKAMA

JAJI  MKUU OTHMAN RASHID CHANDE AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA WATU,MISHI WA MAHAKAMA WA WILAYA ZA KOROGWE, HANDENI, KILINDI NA LUSHOTO KATIKA MKUTANO AMBAO ULIKUWA MAALUMU WA KUZINDUA KAMATI HIYO ULIOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO (IJA) KUSHITO KWA JAJI MKUU NI MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO BI SOPHIA MJEMA.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA (kushoto), KAMPTENI (mstaafu) SEIF MPEMBENWE DC HANDENI NA MKUU WA WILAYA YA KILINDI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI JAJI MKUU HAYUPO PICHANI AKIELEZEA UMUHIMU WA KAMATI YA UTUMISHI WA MAHAKAMA INAVYOWEZA KUTOA AHABU KWA MAHAKIMU WANAOKWENDA KINYUME NA SHERIA

MSAJILI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA BW. BENEDICTOR MWINGA (kushoto), HAKIMU MKUU MKAZI WA MAHAKAMA ZA MKOA WA TANGA BW. CHUMA WAKIFUATILIA KWA MAKINI TAARRIFA NA NA MAELESZO YA JAJI MKUU WA TANZANIA JAJI OTHMAN CHANDE HAYUPO PICHANI KWENYE MKUTANO WA KUZINUA KAMATI YA WAJUMBE HAO.

MAHAKIMU WAKAZI NA WA WILAYA WAKIMSIKILIZA JAJI MKUU KATIKA MKUTANO HUO AMBAO ULIFANIKA KWENYE CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA IJA WILAANI LUSHOTO.

WAJUMBE WA KAMAT HIYO YA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAKIMSIKILIZA JAJI MKUU HAWA NI VIONGOZI WA DINI NA WATU MASHUHURI KUTOKA KATIKA WILAYA HIZO.

Monday, June 20, 2011

UWANJA WA SABASABA TANGA ULIVYOJAA BAR NA NYAMA CHOMA

ENEO LA BANDARI AMBALO WATU WENGI WALIKUWA WAKIFIKA KUONA SHUGHULI ZA BANDARI YA TANGA WAKATI ULE WA SABASABA, LEO LIMEBAKI KUWA GEREJI TU.

UKUMBI HUU ULIKUWA SANA UNATUMIKA KWA MUZIKI ENZI MIMI NIKIWA MKUBWA NILIWAHI KUSHUHUDIA BENDI YA TANGA INTERNATIONAL CHINI YA NA MWIMBAJI WAKE MAHIRI KALOJI IKIPOOMOSHA MUZIKI WAKATI WA SABASABA LEO LIMEBAKI KUWA GOFU BADO MWEKEZAJI WA BAR HAJAPAONA LAKINI WAKIPAONA WANAWEZA KUPACHUKUA NASIKIA DJ MMOJA NI ENEO LAKE.

WADAU HAWA WA UWANJA WA SABASABA AMBAO SASA UMEJAA BAR AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIUZA VINYWAJI NA NYAMA CHOMA ZA KILA AINA UNAZOZIJUA HAPA DUNIANI WAKIONGOZWA NA KIONGOZI WAO MWENYE PUA KUBWA HAPA JAMAA HAWA, BAADA YA KUSHIBA SASA WANASHUSHIA VINYWAJI VYAO BAADA YA KULA NYAMA, AISEE WANAFAII KWELI.



UWANJA WA SABASABA ULIOPO ENEO LA GOFU JUU HIVI LEO UMEBAKI KUWA NA BAR, MAKANISA, GERAGE NA NYUMBA ZA KUSIHI BAADA YA KUFUNGWA MIAKA YA 1994 HADI LEO UMEKUWA NI UWANJA WA VINYWAJI NA NYAMA CHOMA.

ENEO HILI KWA MUJIBU WA UTAFITI NI KWAMBA KUNA BAR ZIPATAZO 49, MAKANISA 8, NYUMBA ZA KUISHI 12 NA GAREGE ZIPATAZO SITA.

UWANJA HUU HAPO ZAMANI KWA KWELI ULIKUWA KIVUTIO KIKUBWA KWA KUTANGAZA BIDHAA ZA MASHIRIKA, MAKAMPUNI YALIYOKUWEPO MKOANI TANGA NA PIA WANANCHI HASA WATOTO WALIKUWA WAKIPATA BURUDANI SAFI ZA KUSAFIRISHWA NA KITOLOLI PALE KWENYE BANDA ZA TRC ENZI HIZO NA UKIENDA KWENYE BANDA LA BANDARI WATU WALIKUWA WAKIINGIA KWENYE MFANO WA MELI AMBAYO ILIKUWA IKIWAFURAHISHA WENGI.

LEO HII KWENYE UWANJA HUO NI ENEO LA WATU WACHACHE NDIYO WANAOFIKA HUKO KUNYWA POMBE NA KULA KITI MOTO AMBACHO AMA KWA HAKIKA KUMEKUWEPO NA MABANDA MENGI AMBAYO YANASHINANA KUTENENEZA NYAMA HIYO AMBAYO INAONEKAN SASA KULIWA NA WATU WA DINI ZOTE KUTOKANA NA KWAMBA WAISLAMU NA WAKRISTO (wasabato) AMBAO HAWALI LAKINI NAO UTAWAKUTA WAKILA BILA HOFU.

JE MDAU WA MAENDELEO UNADHANI CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) AMBACHO NDICHO KINAMILIKI UWANJA HUU WA SABASABA WALIKUWA SAHIHI KUWAKODISHA WATU HAWA AU KINATAKIWA KUBUNI MRADI WA JENGO KUBWA AMBALO LITAKUWA KITEGA UCHUMI CHAO ITAKACHOWAINGIZIA FEDHA KWA AJILI YA KUWASAIDIA KATIKA KAMPENI ZA VYAMA VINGI AU MAWAZO YAKO NI NINI?

Sunday, June 19, 2011

ULIPATA KUMUONA ALUU ALLY AKICHEZA MPIRA?

KHALID ABDALLAH MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF (kushoto) AKIWA NA MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA NA TAIFA STARS ALUU ALLY 'SPOILER' AMBAYE KWA SASA YUPO NCHINI ABUDHABI BAADA YA KUSTAAFU KUCHEZA SOKA, HAPA WALIKUWA KWENYE UWANJA WAQ MKWAKWANI WAKIFATILIA MCHEZO WA KIRAFIKI BAINA NA YA COASTAL UNION NA TIMU MOJA YA MOMBASA.

MCHEZAJI WA COASTAL UNION SAID AKIJARIBU KUMTOKA MCHEZAJI WA TIMU YA MOMBASA ILIYOKUWA JIJINI TANGA KWA MCHEZO WA MMOJA WA KIRAFIKI NA TIMU HIYO, COASTAL ILISHINDA 2-1

KIWANDA CHA MBAO CHA SIKH SAW MILLS KWELI KIMEKUFA?

LANGO KUU LA KUINGILIA KATIKA KIWANDA CHA MBAO CHA SIKH SAW MILLS AMBACHO KWA SASA KINAONEKANA KUFA BAADA YA SERIKALI KUKIUZA KWA MWEKEZAJI MZAWA AMBAYE HATA HIVYO HAKUNA JITIHADA ZA KUKIFUFUA.

HIVI NDIVYO INAVYOONEKANA KWA NJE JENGO ZURI LA KIWANDA CHA SIKH SAW MILLS KILICHOKUFA.

Friday, June 17, 2011

RAS OLE KUYAN AONGOZA WATUMISHI TANGA KUPIMA UKIMWI

KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. BENEDICT OLE KUYAN AKIWAONGOZA WATUMISHI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA TANGA KUPIMA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI AMBAPO KATI YA WATUMISHI 77 WALIOHUDHURIA SEMINA YA UKIMWI 70 WALIPIMA AMBAPO KATI YA HAO 45 WALIPIMA NA KUCHUKUA MAJIBU YAO PAPO HAPO NA WENGINE WALIOBAKI HAWAKUCHUKUA MAJIBU YAO NA WATUMISHI 7 HAWAKWENDA KUPIMA KWA UWOGA.

Friday, June 10, 2011

Komradhi wasomaji wetu wa Blogu hii ya Mzee wa Bonde

Komradhi wasomaji wetu wa Blogu hii ya mzee wa Bonde ya watu na matukio kutokana na kutokuwepo hewani kwa muda mrefu hii inatokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wetu, tunawaomba radhi sana.

lakini katika kipindi ambacho hatutakuwa hewani tunafanya maboresho madogo katika Blogu hii ili siku ikianza kazi zake basi itoke kwa ufanisi na kukufahamisha matukio mbalimbali hapa Mkoani Tanga na nje ya mkoa huu na mengine nje ya nchi.

Asanteni Utawala blogu ya mzee wa bonde.