Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, February 7, 2012

SHIRIKA LA MASUALA YA HAKI ZA WATOTO NA SANAA KUFANYA KAMPENI KATA YA USAGARA KUELIMISHA JAMII HAKI ZA WATOTO

MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA UNITE TANZANIA CHILDREN LINALOSHUGHULIKA NA MASUALA YA AFYA YA MTOTO NA SANAA BI IRENE RAJAB MHANDO

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UNITE TANZANIA CHILDRENBI IRENE MHANDO

KATIBU WA SHIRIKA HILO BI DORO EZEKEL NTUMBO AKIWA KATIKA MAHOJIANO NA MWANDISHI WA HABARI HIZI KATIKA OFISI YAO ILIYOPO KATIKA JENGO LA READ CROSS

Na mzee wa Bonde,Tanga
SHIRIKA la Unite Tanzania linalojihusisha na afya ya mtoto na sanaa, limeandaa warsha kwa watendaji na wananchi katika kata ya Usagara Jijijini Tanga yenye lengo la kuijengea uwezo jamii kuhusu masuala yanayohusu haki mbalimbali za watoto ili waweze kuzitekeleza katika familia.

Sanjari na hilo, shirika hilo litaendesha kampeni kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo mabonanza ya watoto kwa kipindi cha miezi sita lengo likiwa kuhakikisha inapambana na vitendo vinavyowakosesha raha na haki watoto.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Bi Irene Mhando, akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, alisema kuwa lengo la mradi huo uliofadhiliwa na mtandao wa mashirika ya kiraia ya Foundation For Civil Society, alisema kwa kipindi cha miezi sita watajikita katika kata hiyo kuzungumzia kwa undani haki anazostahili kupata mtoto na vile vile kutambua vipaji vyao.

Alitaja makundi ambayo watakutana nayo katika kipindi hicho kuwa ni pamoja na watendaji wa mitaa, madiwani, polisi na wananchi wa kawaida katika mitaa mbalimbali ya kata hiyo ambapo wanatarajia kwamba itawajengea uwezo wa kutambua kwa nini jamii inapaswa kuwalea watoto kwa mtizamo mpana.

"Shirika litaendesha mradi wa kampeni ya haki ya mtoto katika kata ya usagara, kwa kipindi cha miezi sita watazungumza na wananchi, watendaji, polisi na makundi mengine ya jamii ili kuhakikisha malengo ya kuijengea uwezo jamii yanatimia ipasavyo na watoto wanaishi kama watu wengine," alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake, Katibu wa shirika hilo, Bi Doro Ntumbo, akijibu suala la kwanini wamechagua kata ya Usagara na siyo kata nyingine za Jiji hilo, alisema kuwa kata hiyo imekuwa na matukio mengi ya unyanyasaji wa mtoto hivyo kuendesha kampeni katika kipindi hicho kutasaidia kuongeza uelewa kwa jamii na matukio hayo mwisho wa siku kupungua.

"Ukitazama malengo ya mradi huu, kuwaongezea uelewa jamii kuhusu sera ya mtoto ya mwaka 2008, kubadilisha tabia za watu kuhusu namna wanavyotakiwa kuwapa haki watoto...Sasa kata ya Usagara tumeonelea tuanze nayo kwa vile masuala ya unyanyasaji yamekuwa yakikithiri hivyo kufika kwetu tutasaidia maana pia tutaunda mabaraza ya watoto, hii itasaidia kupunguza matukio ya ukiukwaji wa sheria za haki za mtoto," alisema Bi Ntumbo.
 


Friday, February 3, 2012

MAHARAMIA WACHOMA MOTO BOTI YA UVUVI KIGOMBE

MKUU WA MKOA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GALLAWA (mwenye kilemba) AKIMNYOOSHEA KIDOLE MKUU WA WILAYA YA MUHEZA BW. METHEW NASEI KWAMBA AHAKIKISHE WATU WALIOCHOMA MOTO BOTI YA UVUVI KATIKA MWAMBAO WA KIGOMBE WANAPATIKANA HARAKA.

WANANANCHI WA KIGOMBE WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA. WA KWANZA KULIA NI MSAIDIZI WA MKUU WA MKOA BW. JOSEPH SURA.

BOTI YENYEWE AMBAYO IMECHOMWA MOTO NA MAHARAMIA

MKUU WA MKOA WA TANGA MH GALLAWA AKIWA NA VIONGOZI WA WILAYA YA MUHEZA NA KIJIJI CHA KIGOMBE WALIPOMTEMBEZA KWENYE MWAMBAO WA PWANI KUONA ENEO LILILOHIFADHIWA KWA AJILI YA SAMAKI AINA YA SILIKANTI.


Na Mzee wa Bonde,Muheza
MAHARAMIA wanaoendesha uvuvi haramu katika mwambao wa bahari ya Hindi mkoani Tanga, wameichoma moto boti ya doria inayomilikiwa na Taasisi ya Hifadhi ya bahari ya Silikanti iliyopo katika kijiji cha Kigombe wilayani hapa.

Kuchomwa kwa boti hiyo iliyokuwa ikielea baharini katika eneo hilo la Kigombe, kunatokana na dori ya mara kwa mara inayofanywa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuwasaka maharamia wanaoendesha uvuvi haramu wa kutumia mabomu na nyavu ndogo zisizoruhusiwa, kumeelezwa kwamba ndiko kuliwapa hasira maharamia hao, wakachukua maamuzi hayo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kigombe Bew. Mwambi Haji alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa aliyefika katika kijiji hicho kupata maelezo ya kuchomwa kwa boti hiyo, alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni na hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Mhifadhi wa bahari ya Silikanti Bw. Sylevester Kazimoto alisema katika kipindi cha mwaka uliopita waliendesha doria 192 za baharini na nchi kavu iliyohusisha vyombo vya dola ambayo iliwezesha kukamatwa kwa wavuvi haramu wapatao sita.

Alisema pamoja na kuwakamata wavuvi hao pia walikamata vifaa vinavyotumika kwa uvuvi huo ikiwemo baruti 29, bunduki 17 za kuulia samaki, mitungi 31 ya kuzamia, makokoro 94, nyavu za utale 11 na samaki wa baruti kilo 124.

Akizungumza katika mkutano na wananchi waliofika katika ofisi ya hifadhi hiyo Mkuu wa Mkoa alisema kuwa kila wananchi analojukumu kubwa la kulinda na kuhifadhi rasilimali za bahari hivyo akawataka wataalamu wa hifadhi hiyo wakishirikiana na serikali ya kijiji kuandaa mpango wa kuorodhesha wavuvi wote na boti zao kisha kuziandika namba.

Alisema suala la uvuvi haramu hivi sasa linatakiwa kupigwa vita baada ya muda mrefu nchi yetu kuliacha bila kuwachukulia hatua watu wanaoendesha uvuvi haramu ambao licha ya kuharibu mazingira pia wanaleta matatiz ya kiafya kwa kuvua samaki wa aina hiyo.

Hata hivyo, mjumbe wa serikali ya kijiji hicho Bw. Hassain Bakari almtaka mkuu huyo wa mkoa kuingilia kati suala la wavuvi haramu kukamatwa kisha kesi zao kuishia hewani kwa maana ya polisi na mahakamani hatua ambayo inasababisha wavuvi hao kutawala mwambao wa bahari kwa kuendesha vitendo hivyo wakiamini kwamba, wakikamatwa kesi zao watazimaliza.

Thursday, February 2, 2012

MPIGA PICHA MAARUFU MKOANI TANGA ELIAS NGOSWE, AGONGWA AKIPIGA PICHA KWENYE MAHAFALI

Mmoja wa majeruhi waliogongwa na gari lenye namba T489 AGJ aina ya Toyota Bw. Elias Ngole almaarufu Ngoswe ambaye ni mpiga picha maarufu mkoani Tanga, aliyefika kwenye mahafali ya kidato cha sita katika shule hiyo ya Korogwe Girls akiwa amepakiwa kwenye bajaj kukimbizwa katika hospitali ya Magunga kwa matibahu.

Mwanafunzi Renata Renatus anayesoma kidato cha sita katika shule hiyo, akiwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe akihudumiwa na muuguzi alipofikishwa katika hospitali hiyo.

Gari lililosababisha ajali likiwa limebenuliwa ili kuwatoa majeruhi wa ajali hiyo ambayo imeleta usumbufu mkubwa kwa wanafunzi na wazazi waliofika.

Mkuu wa wilaya ya Korogwe (mwenye suti nyeusi) akiwa amemshika mwanafunzi Kibibi Mmasa (19) ambaye ndiye aliyeendesha gari hilo kwa kuliweka gea kisha gari hilo kurudi nyuma na kuwagonga wanafunzi wenzake na kuwasababisha majeraha makubwa 

Mwanafunzi Zahra Jumanne (19) akipelekwa wodini baada ya kupatiwa matibabu mwanafunzi huyo ni mmoja ya wahitimu walioumia sana.

Mwanafunzi Nancy James akiwa amelazwa katika hospitali hiyo ya Magunga akipatiwa matibabu na wauguzi wa hospitali hiyo.
Na Mzee wa Bonde,Korogwe
VILIO, majonzi na huzuni vilitawala leo asubuhi katika shule ya sekondari ya Wasichana Korogwe, kufuatia wanafunzi wapatao saba na mpiga picha mmoja wa kujitegemea, kujeruhiwa vibaya kwa kugongwa na gari lililokuwa likichezewa na mmoja ya wahitimu wa kidato cha sita aliyeweka gia ya kurudi nyuma na kisha gari hilo, kuwagonga wahitimu hao.

Tukio hilo lililotokea majira ya saa 10:20 asubuhi katika shule hilo, baada ya mwanafunzi mmoja Kibibi Mmasa anayesoma kidato cha sita shuleni hapo, kuingia katika gari la kaka yake lenye namba za usajili T489 AGJ ambaye alifika kushuhudia mahafali hayo, aliweka gia hiyo kisha gari hilo kurudi nyuma kwa mwendo kasi wa kilomita 120 kwa saa na kuwaparamia wahitimu hao waliokuwa wamejikusanya vikundi.


Wanafunzi waliojeruhiwa na hali zao kuelezwa zipo katika hali mbaya ni Zahra Jumanne (19) na mpiga picha wa siku nyingi Bw. Elias Ngole 'Ngoswe', wengine ni Renata Renatus (25), Sophia Godfrey (19), Victoria Mtwale (19), Nancy James (19) na Mwanamkonda Kapunda (19) ambao wote wanasoma kidato cha sita na ambao walikuwa wakitarajia kufanya mahafali ya kumaliza shule.


Mwandishi wa habari hizi alishuhudia gari hilo likiendeshwa na mwanafunzi huyo likitembea kwa kasi kurudi nyuma na kuanza kumgonga mpiga picha huyo ambaye alikuwa akizungumza na Mwandishi wa ITV na Redi One Bw. William Mngazija ambaye baada ya kuliona gari hilo aliruka pembeni lakini mwenzake alishindwa na badala yake gari hilo lilimgonga kisha kunasa chini yake na kuburuzwa hadi kiasi cha mita 30 gari hilo lililopogonga mti na kusimama.


Baada ya kugongwa mpiga picha huyo liligonga wanafunzi wengine ambao walikuwa wamejikusanya wakibadilishana mawazo namna watakavyosherehekea mahafali yao ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa benki ya posta nchini Bw. Sabasaba Moshingi ambapo mmoja Zahra aligongwa vibaya na kunasa chini ya gari hilo ambapo gari hilo lilipinduliwa ili kumnasua huko chini akiwa amevunjika miguu na kupata jeraha kubwa kichwani.


"Kaka alinituma mle ndani ya gari wakati nikichukua mzigo aliyonituma ghafla nikaona gari linakwenda, nikawa sijui kinachoendelea nikasikia makelele wenzangu wanapiga huko nje huku nikiwa nimekanyaga mafuta," alisema Kibibi huku akisihi viongozi wamweche kaka yake ambaye alishikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo. Kaka yake ni Hussein Mmasa.


Akizungumzia tukio hilo, Bw. Mngazija alisema kama si kupata ujasiri kuwa kusogea kulipisha gari hilo pengine naye angekuwa miongoni mwa watu waliojeruhiwa lakini ana mshukuru mungu kukwepa ajali hiyo.


"Nilikuwa nasalimiana na Ngoswe hatujaonana muda mrefu, sasa ghafla nikaliona gari linakuja kwa kasi nikaruka na kumuacha mwenzangu ambaye alisogea kwa nyuma badala ya kulikwepa matokeo yake likamgonga," alisema Bw. Mngazija na kuongeza kwamba alikwepa gari hilo likiwa limemfikia hatua mbili tu na kama siyo kuitwa kuelezwa gari kuja uswa wao, lingemgonga.


Mkuu wa wilaya ambaye alifika kwenye eneo hilo na baadaye kwenda hospitali kushughulikia tiba ya wanafunzi hao, alisema tukio hilo ni la kusikitisha na alishawahi kutoa taadhali kuhusu magari yanayokwenda kwenye sherehe kama hizo shuleni kwamba magari yaegeshwe kwenye maeneo maalum kuliko kuwekwa katika maeneo kama hayo ambayo yanaweza kutokea ajali kama hizo.


Wanafunzi hao, wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani hapa wakiendelea kupatiwa matibabu huku mmoja wao Zahra akiwekewa mtambo wa kumuongezea kupumua Oksijeni na wengine hali zao zinaendelea vizuri. Mahafali yaliendelea lakini hayakuwa na furaha kutokana na tukio hilo.

Tuesday, January 31, 2012

MAKAMU WA RAIS AFURAHISHWA NA SKIMU YA MOMBO

MAKAMU WA RAIS DKT MOHAMED GHALIB BILAL AKIKAGUA MIFEREJI YA MAJI KATIKA SKIMU YA MOMBO AMBAYO IMEONEKANA KUWASAIDIA WANANCHI WA MJI HUO KIASI CHA KUELEZA KWAMBA WANAPATA TANI 6.1 KWA HEKTA MOJA HATUA AMBAYO IMEWASAIDIA KUONDAKA NA UMASIKINI.

Monday, January 30, 2012

MH GALLAWA AWAPASHA MADAKTARI NA MANESI BOMBO, ASIYETAKA KAZI AONDOKE

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GALLAWA, ALIPOTEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TANGA, BOMBO AKIWA NA WENYEJI WAKE (KUSHOTO KWAKE0 MGANGA MKUU MFAWIDHI WA HOSPITALI HIYO DKT FRED MTATIFIKOLP ALIPOFIKANA KAMATI YAKE YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA KUANGALIA KAMA MADAKTARI NA WAUGUZI KAMA WAMEENDELEA KUGOMA.

KATIBU TAWALA WA KOA WA TANGA, BW. BENEDICT OLE KUYAN (KATIKATI) AKIWA NAYE NI MIONGONI MWA VIONGOZI WALIOFIKA KWENYE HOSPITALI HIYO. KUSHOTO KWAKE NI BREGEDIA GENERAL MWANGWAMBA.

BWANA AFYA MKUU WA MKOA WA TANGA BW. JUMANNE MAGOMA (KUSHOTO) AKIWEMO KWENYE MSAFARA HUO AKIWEMO MKUU WA MAGEREZA MKOA.

WANANCHI WALIOFURIKA KATIKA HOSPITALI HIYO WAKIWA KATIKA ENEO LA MAPOKEZI AMBAKO MKUU WA MKOA ALIFIKA NA KUINGIA KUMUONA DAKITARI WA WATOTO KAMA YUPO.
Na Mzee wa Bonde,Tanga
MADAKTARI na wauguzi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo, wametii amri ya serikali ya kuwataka kurejea kazini kufanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa lakini pamoja na kurejea huko, wameanza mgomo baridi wakiwa kazini.

Mwandishi wa habari hizi alifika katika hospitali hiyo asubuhi kufuatilia madaktari na wauguzi ambao hawakufika, lakini wote walifika na kwenda kwenye maeneo yao ya kazi kama kawaida.

Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo Dkt Fred Mtatifikolo, alipoulizwa kuhusu madaktari kurejea kazini alisema wameanza kazi jana na kwamba wote waliokuwa kwenye mgomo ulioanza katika hospitali hiyo Ijumaa wiki iliyopita kuunga mkono wenzao, wapo kazini na wanaendelea na kazi kama kawaida.

"Tuliitisha Roucall saa mbili asubuhi, tukakuta madaktari wote na wauguzi wamefika kazini, mgomo ulikuwepo hapa katika hospitali yetu Ijumaa na Jumamosi iliyopita lakini ulihusu madaktari hawa wa Intershirp kuunga mkono wenzao, lakini leo wote wapo kazini sasa kama hawafanyi kazi siwezi kujua kwa vile mimi kama Mganga Mkuu Mfawidhi siwezi kutembelea maeneo yote kuona utendaji wao wa kazi," alisema Dk Mtatifikolo.

Hata hivyo, pamoja na madaktari hao kurejesa kazini lakini kwa ujumla hawaonekani kufanya kazi kama kawaida na baadhi yao walisema kuwa suala la mgomo baridi lipo kwa vile wamelazinishwa kurejea kazini bila kusikilizwa huku wakiw ana madai yao ya msingi kama malimbikizo ya nyongeza zao za mishahara na posho nyingine.

"Sisi ni madaktari unapotulazimisha kufanya kazi bila madai yetu ya msingi kuyasikiliza na kutulipa kile tunachodai halafu unatutishia kutufukuza kazi sidhani kama umetatua mgogoro uliopo baina yetu na serikali, tutakuja kazini lakini suala la kufanya kazi ni jingine sisi tupo tupo tu hapa, hadi kieleweke kwa maana ya kwamba serikali ikubali kutulipa madai yetu, iache kusingizia siasa," alisema Dkt mmoja ambaye kama mwenzake walikataa kutaja majina yao wala kupigwa picha.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama walifika kwenye hospitali hiyo majira ya saa 6:00 mchana kutembelea wodi mbalimbali ikiwemo sehemu ya kupokelea wagonjwa wa nje kuona kama maeneo hayo madaktari kama walikuwa kazini na kisha baadaye mkuu huyo alizungumza na wafanyakazi wote wakiwemo madaktari wa hospitali hiyo.




Akizungumza na wafanyakazi hao mkuu huyo wa mkoa aliwaambia kwamba anayetaka kazi aendelee na kazi kama daktari hataki kazi aondoke apishe wengine ambao watafanya kazi kwa moyo wote wa kuwatibia wananchi wanaofika.

Saturday, January 28, 2012

MADAKTARI, WAUGUZI HOSPITALI YA BOMBO NAO, WAANZA MGOMO

WAFANYAKAZI WA KITENGO CHA UPASUAJI WA HOSPITALI YA BOMBO WAKIWA WAMEKAA NJE YA HOSPITALI HIYO KAMA SEHEMU YA MGOMO WAO WALIOUANZA LEO KATIKA HOSPITALI HIYO KUUNGA MKONO WENZAKO NCHI NZIMA.

MADAKTARI NA WAUGUZI WAKIWA WAMEKUSANYIKA KATIKA UKUMBI MDOGO WA KITENGO CHA MAZOEZI YA VIUNGO WAKISOMEWA TAARIFA YA KWANINI WANATAKIWA KUGOMA

BAADHI YA MADAKTARI NA WAUGUZI WAKISIKILIZA MKUTANO HUO.

WAKISIKILIZA KWA MAKINI MKUTANO HUO

HAWA NDIYO WALIOKUWA WAKISOMA BARUA ILIYOKUWA NA MADAI YA MADAKTARI AMBAYO WANAIDAI SERIKALI
Na Mzee wa Bonde,Tanga
MADAKTARI na wauguzi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo, nao wameanza mgomo wao jana, kuunga mkono wenzao waliogoma nchini kote kwa ajili ya kuishinikiza serikali iwalipe malimbikizo yao ikiwemo posho zao wakiwa kazini.

Mgomo huo umeanza jana ambapo huduma mbalimbali kwa wagonjwa zilisimama, na wagonjwa katika wodi ya wazazi walibaki pekee yao asubuhi bila kuwa na waauguzi wowote halkadhalika wagonjwa waliokuwa wodini ambao huwa wanapitiwa na madaktari kujua namna walivyolala, lakini waliamka bila kumuona daktari hali ambayo ilileta usumbufu mkubwa kwa wagonjwa hao.

Hata hivyo, katika kikao chao walichofanya jana katika hospitali hiyo kitengo cha viungo ambapo mwandishi wa habari hizi alifika eneo hilo bila kupata ushirikiano kutoka kwa madaktari huo, wakieleza kwamba waandishi waliokutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda walishindwa kumbana suala la msingi la kugoma kwao badala yake, wanazungumzia suala la uraisi wa 2015.

"Jamani nyie waandishi issue ni mgomo wa madaktari nyie mnazungumza na Waziri Mkuu suala la Urais hamuoni kwamba mnatumika katika masuala makubwa ya Kitaifa mnaingiza mambo ambayo hata wakati wenyewe haujafika, kwanini msimbane kuhusu mgomo na ni kwanini serikali inapiga chenga kukutana na viongozi wetu?," alihoji mmoja wa madaktari hao ambaye hakutaka jina lake lianikwe gazetini.

Abdallah Kubo mgonjwa aliyelazwa katika wodi ya Galanos, alilalamika kukosa matibabu baada ya kupata ajali juzi usiku ambako alifikishwa katika hospitali hiyo, majira ya saa tano usiku na kwamba alitarajia jana asubuhi angeonwa na daktari kisha kwenda kupatiwa x-ray kuangaliwa kama amevunjika katika viungo vyake.

"Kwa kweli mwili wangu unauma sana, nimeanguka na pikipiki baada ya kuwashiwa taa na gari kubwa kisha nikaparamia msingi nikaanguka nimeleta hapa sijitambui, nimeamka muda huu simuoni daktari, ndugu zangu wanataka nikapigwe x-ray lakini hatujaambiwa chochote twasikia leo (jana) madaktari wamegoma," alisema Kubo.

Mwanamke mwingine aliyejitambulisha kwa jina Bi Rose Mwaimu alisema alifika katika hospitali hiyo asubuhi jana, kwa ajili ya kuonana na daktari katika kitendo cha mazoezi ya viungo, lakini hakuweza kupata msaada wowote baada ya kuelezwa kwamba madaktari hawafanyi kazi
kufuatia mgomo waliouanza.

"Baba nimekuja hapa tangu asubhi nasubiri huduma lakini sijapata msaada wowote mguu wangu unaendelea kuvimba sijui sitafanyaje, kwa kweli tunaomba watuonee huruma jamani tunateseka," alisema Rose.

Alisema hospitali hiyo ya Bombo haina madaktari wa kutosha, hivyo mgomo huo utaathiri huduma za kiafya kutokana na kwamba wakati wakiwa wote hospitali hiyo huduma zao zimekuwa haziridhishi hivyo kugoma huko kutasababisha wagonjwa kupoteza maisha.

Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Dkt Mchomvu, alikiri mgomo huo kuanza katika hospitali hiyo leo (jana) lakini alisema huduma za dharura zitaendelea kama kawaida isipokuwa huduma nyingine wagonjwa hawatapata matibabu kama ilivyokuwa awali.

"Ni kweli tumegoma kuanzia leo (jana) kuunga mkono wenzetu nchini kote lakini huduma za Emergence  (dharura) zitaendelea iwapo kutakuwa na wagonjwa wa aina hiyo," alisema Dkt Mchomvu.

Thursday, January 19, 2012

WATENDAJI WA VIJIJI HANDENI, KILINDI WAPATIWA SEMINA ELEKEZI KUHUSU UTUNZAJI MAZINGIRA

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI BW. HASSAIN MWACHIBUZI, AKIZUNGUMZA KATIKA SEMINA ELEKEZI KWA WATENDAJI WA VIJIJI WA WILAYA ZA HANDENI NA KILINDI KUHUSU MASUALA YA AFYA NA MAZINGIRA ILIYOFANYIKA WILAYANI HUMO.

OFISA AFYA MKUU WA MKOA WA TANGA, BW. JUMANNE MAGOMA AKIZUNGUMZA KATIKA SEMINA HIYO KUELEZEA JINSI MKOA HUO ULIVYOJIPANGA KUHUSU USAFI KATIKA WILAYA ZAKE.

OFISA AFYA YA MZINGIRA KATIKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII BW. ANYITIKE MWAKITALIMA AKIZUNGUMZIA NAMNA WIZARA HIYO ILIVYOJIPANGA KUHAKIKISHA INASHUGHULIKIA SUALA LA USAFI NCHINI.

BW. MWAKITALIMA (KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BW. MASHAKA MHANDO MWANDISHI WA GAZETI LA MAJIRA (KATIKATI) NA BW. SONYO MWENKALE WA GAZETI LA NIPASHE.

RC GALLAWA ALIVYOTEMBELEA KIWANDA CHA SARUJI TANGA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA KIWANDA CHA SARUJI SIMBA CEMENT ALIPOTEMBELEA KUONA SHUGHULI ZA UZALISHAJI IKIWEMO CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO.

KIWANDA CHA SARUJI TANGA

OFISA MAWASILIANO NA WATEJA WA KIWANDA CHA SARUJI TANGA, BI MTANGA NOOR AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO NA MKUU WA MKOA KUHUSU KIWANDA HICHO KILIVYOWEZA KUTOA MISAADA KWA JAMII. KUSHOTO NI MKURUGENZI MKUU WA KIWANDA HICHO BW. ERIK WESTERBERG.

MH. GALLAWA ATAKA KIWANDA CHA SARUJI KUTAFUTA MAWAKALA KILA WILAYA MKOANI TANGA WA KUSAMBAZA SARUJI

 Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji (Tanga Cement) Bw Erik Westerberg mara alipowasili katika ofisi za kiwanda hicho alipofika kukitembelea kuona shunguli zao na changamoto zinazowakabili.

Na Mashaka Mhando,Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa amekitaka kiwanda cha saruji kilichopo Jijini Tanga, kuangalia uwezekano wa kuwa na mawakala wa kusambaza bidhaa hiyo kwa kila wilaya mkoni hapa, ili wananchi waweze kunufaika na ununuaji wa bei nafuu kuliko sasa.

Akizungumza mara baada ya kukitembelea kiwanda hicho kisha kusomewa taarifa ya kiwanda hicho, Mkuu huyo wa mkoa alimwambia Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Erik Westerberg kwamba kmekuwepo malalamiko ya muda mrefu ya wakazi wa mkoa wa Tanga, kwamba wamekuwa wakinunua saruji ya kiwanda hicho kwa bei kubwa wakati kiwanda hicho kipo mkoani kwao.

Alisema sababu kubwa ya malalamiko hayo ya wananchi ni kwamba kiwanda hicho kina wakala mmoja anayenunua kiwandani kisha saruji hiyo kuipeleka Zanzibar kisha ndipo anawapowauzia wauzaji wadogo waliopo mjini Tanga ambao wananunua kwa bei kubwa inayowalazimu na wao kuiuza sawa na mikoa mingine.

Bei ya saruji ya kiwanda hicho kwa mfuko mmoja Jijini Tanga unauzwa kati ya sh. 14,000 hadi 14,500, wakati saruji hiyo hiyo kutoka katika kiwanda hicho kwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dar es salaam mfuko mmoja huuzwa kati ya sh. 12,000 hadi 13,000 hali ambayo wananchi wa mkoa wa Tanga, kukiona kiwanda hicho hawana faida nacho licha ya kuwepo mkoani kwao.

"Kwanza nawapongeza sana kwa namna mnavyohifadhi mazingira na kazi mnavyozifanya, lakini kuna haya malalamiko ya muda mrefu kwa wakazi wa Tanga, kwamba saruji inauzwa na wakala mmoja anayesambaza baada ya kuinunua hapa, hivyo inavyouzwa huko mitaani inakuwa bei kubwa tofauti na miji mingine, sasa wanavyoona hivyo wanaona hawanufaiki na uwepo wa kiwanda hiki, naomba mfanye uwezekano wa kuwa na wakala kila wilaya za mkoa huu ili kuondoa suala hilo," alisema Mkuu wa mkoa huuyo/.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji huyo licha ya kukubali ombi la Mkuu wa mkoa kwa kueleza kwamba watafanya mchakato kwa kuyafanyia kazi maombi hayo, alisema kiwanda hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo suala la kukatika mara kwa mara kwa umeme kunakowapa hasara ya shilingi milioni 400 hadi 800 licha ya kulipa ankara ya umeme ya shilingi bilioni 1 kwa mwezi.

Vile vile alisema suala la kufungwa kwa matuminzi ya reli ya Tanga, kumewaathiri kwa kiasi fulani kusafirisha saruji mikoa ya kanda ya ziwa kwa maana kwamba njia ya reli ni bora zaidi kuliko njia ya barabara ambayo imekuwa na changamoto nyingi njiani.
 

Friday, January 13, 2012

MADC KOROGWE NA LUSHOTO WAKUTANA KUMALIZA TATIZO LA UHARIBIFU WA MSITU

WAKUU WA WILAYA ZA KOROGWE NA LUSHOTO PAMOJA NA KAMATI ZAO ZA ULINZI NA USALAMA PAMOJA NA VIONGOZI WA VIJIJI JIRANI KUTOKA TARAFA YA MAZINDE NGUA, WAKIWA KATIKA MKUTANO WA UJIRANI MWEMA KUJADILI TATIZO LA MSITU WA LUSHOTO, KUTOKA KULIA NI MKURUGENZI WA WILAYA YA LUSHOTO LUCY MSOFE, MKUU WA WILAYA YA KOROGWE ERASTO SIMA, MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO SOPHIA MJEMA NA DAS WA KOROGWE.

Wednesday, December 7, 2011

TUTUMIE FURSA ZILIZOPO KATIKA MKOA WETU WA TANGA-RC GALLAWA ASEMA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALLAWA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WILAYANI MUHEZA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU. WA KWANZA KUSHOTO MKUU WA WILAYA YA MUHEZA METHEW NASEI, MWENYEKITI WA CCM WILAYANI MUHEZA PETER JAMBELE NA KATIBU TAWALA WA TANGA BENEDICT OLE UYAN

Sunday, December 4, 2011

TAKUKURU FUATILIENI FEDHA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI HALMASHAURI-GALLAWA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (mstaafu) CHIKU GALLAWA AKIFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA MAOFISA WA TAKUKURU MAKAO MAKUU, MIKOA NA WILAYA ULIOFANYIKA HOTEL YA TANGA BEACH RESORT-TANGA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (Mstaafu) CHIKU GALLAWA (mwenye koti jekundu na sketi ya bluu) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA NGAZI YA JUU WA TAASISI YA KUZUAI NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU) MARA BAADA YA KUFUNGA MKUTANO WAO WA MWAKA.


Na Mashaka Mhando,Tanga
MKUU wa mkoa wa Tanga, luteni (mstaafu) Chiku Gallawa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuongeza kasi ya kufuatilia fedha zinazopelekwa na serikali katika halmashauri nchini ili ziweze kutumika vizuri kwenye miradi mikubwa ysa maendeleo iliyokusudiwa.

Akifunga Mkutano Mkuu wa mwaka wa takukuru kwenye hoteli ya Tanga beach Resort kwa maofisa wa taaisis hiyo kutoka mikoa yote ya tanzania bara, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa takukuru wamebeba dhamana kubwa ya kustawisha maendeleo kwa kufautilia watendaji kwenye halmasauri ambao wanatumia vibaya fedha zinazoolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo.

Amesema serikali hasa ya awamu ya nne, imekuwa ikitoa fedha nyingi katika halmashauri kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maeneleo hasa ya elimu, afya, barabara na kujenga majengo mbalimbali lakini fedha hizo wakati mwingine zimekuwa zikitumika visivyo na hivyo kuleta malalamiko kutoka kwa wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa pamoja na kuipongeza taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuokoa fedha za serikali kiasi cha shilingi bilioni 97.5, lakini ameitaka takukuru kuhakikisha inaongeza kasi ya mapambano ya rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi.

Kuhusu wananchi mkuu huyo wa mkoa amewataka kutoa ushirikiano kwa taaisis hiyo na waache kulalamikia masuala ya ufisadi wakati kama watatoa ushirikiano masula hayo yanaweza kudhibitiwa kwa watu kuogopa fedha za umma hatua ambayo mwelekeo wa taasisi hiyo inakoelekea na kwamba waongeze jitihada kutumia nyenzo walizokuwa nazo katika mapambano hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala la mapambano ya rushwa ikiwemo kuwafundisha watumishi wake kwenda sambamba na mabadiliko ya teklonojia katika masuala ya rushwa.
MWISHO

Wednesday, November 30, 2011

RC-TANGA AONGOZA KIKAO CHA KWANZA CHA BODI YA BARABARA TANGA

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI CHIKU GALLAWA AKIFUNGUA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA TANGA

BAADHI YA WAJUMBE WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA KUTOKA WILAYA YA KOROGWE WAKIONGOZWA NA DC WAKE BW. ERSTO SIMA (KATIKATI) WAKISIKILIZA KWA MAKINI UWASILISHAJI WA MADA MBALIMBALI KUHUSU BARABARA ZA MKOA WA TANGA

KAIMU MENEJA WA WAKALA WA BARABARA MKOA WA TANGA TANROADS INJINIA ALFRED NDUMBALO AKIWASILISHA TAARIFA YA UFANYAJI KAZI WA WAKALA HIYO KATIKA KIKAO CHA BODI YA BARABARA

MAOFISA WA MKOANI WAKIENDELEA NA ZOEZI LA KUREKODI ORODHA YA WAJUMBE WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA

BAADHI YA WAJUMBE KUTOKA WILAYA YA MUHEZA MBUNGE WA JIMBO LA MUHEZA BW. HERBERT MNTANGI (kulia) NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO BW. AMIR KIROBOTO

MAKAMO MPYA WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA TANGA BW. SALEH PAMBA (KUSHOTO), MWENYEKITI WA CCM MKOA WA TANGA BW. MUSSA SHEKIMWERI NA MWENYEKITI WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA NA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTEN CHIKU GALLAWA WAKIFUATILIA KWA MAKINI HOJA ZA KIKAO HICHO 

Friday, November 25, 2011

MWENGE WAKIMBIZWA TANGA KISHA WAKABIDHIWA MOROGORO

MKUU WA MKOA WA KUSINI PEMBA (aliyeshika Mwenge), MEJA (mstaafu) JUMA K TINDWA AKIMKABIDHI MWENYE WA UHURU MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (mstaafu) CHIKU GALLAWA MARA BAADA YA MWENGE HUO KUWASILI KATIKA UWANJA WA NDEGE UKITOKEA KISIWANI PEMBA.

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (mstaafu) CHIKU GALLAWA AKIWA TAYARI AMEUPOKEA MWENGE WA UHURU KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA KUSINI PEMBA, MEJA (mstaafu) JUMA TINDWA, ANAYEWATAZAMA NI MMOJA WA WAKIMBIZA MWENGE BW. DEOGRATIUS BULLAYI DAFI.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIPOKEA MWENGE WA UHURU KWA HESHIMA BAADA YA MKUU WA MKOA WA TANGA KUSOMA TAARIFA YAKE YA NAMNA MWENGE HUO UTAKAVYOKIMBIZWA KATIKA WILAYA ZA TANGA MJINI NA KILINDI, WA KWANZA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA MKINGA BW. RASHID NDAILE.

WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA TANGA WAKISHUHUDIA TUKIO LA KUKABIDHIWA MWENGE WA UHURU MWAKA HUU MKOANI TANGA AMBAO NI MAALUM KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU

MKUU WA MKOA WA MOROGORO BW. JOEL BENDERA AKIWA AMEUPOKEA MWENGE WA UHURU KUTOKA KWA KAIMU MKUU WA MKOA WA TANGA KAMPTENI (mstaafu) SEIF MPEMBENWE ALIYEUKABIDHI MWENGE HUO MKOANI HUMO KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA ALIYEKUWA NA MAJUKUMU MENGINE YA KITAIFA.

Tuesday, November 15, 2011

WANANCHI TANGA WATOA RAMBIRAMBI KWA WALIOKUFA KWA AJLI YA MELI YA MV SPICE ISLENDARS

MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GALLAWA AKIMKABIDHI MAKAMU WA PILI WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLI IDD HUNDI YA SHILINGI MILIONI 11.2 KAMA MCHANGO WA RAMBIRAMBI KWA WANANCHI WA ZANZIBAR KUFUATIA KUZAMA KWA MELI YA MV. SPICE ISLANDERS ILIYOZAMA MIEZI MIWILI ILIYOPITA.
Na Mashaka Mhando,Zanzibar
MKUU wa mkoa wa Tanga, luteni (mstaafu) Chiku Gallawa, amesema wananchi wa mkoa huo, waliupokea kwa masikitiko makubwa msiba wa wananchi waliokuwemo kwenye meli ya Mv Spice Islanders iliyozama miezi miwili iliyopita kwenye mkondo wa Nungwi Visiwani humo, na kwamba wameguswa hasa kutokana na ukaribu wake na visiwa hivyo.

Akizungumza juzi wakati wa kukabidhi rambirambi ya michango kwa ajili ya watu waliopeza maisha kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi, Seif Alli Idd, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa wanachi wa mkoa wa Tanga waliuopokea kwa masikitiko makubwa msiba huu mzito kutokana na mkoa huo kuwa na mahusiano ya karibu kutokana na kutenganishwa na bahari ya Hindi.

Alisema kuwa msiba huo utazidi kuwaunganisha wananchi wa mkoa huo na Visiwani humo katika kipindi chote cha raha, tabu na majonzi ya kuwakumbuka ndugu zao waliopoteza maisha kwenye jali hiyo na kwamba wataendelea kuwaombea ili mwenyezi Mungu awalale mahali pema peponi.

"Tanga na Zanzibar ni karibu sana na wanachi wa pande zote mbili wana mahusiano ya karibu sana.wameguswa na msiba huu na wameomba tuwasilishe pole nyingi sana pamoja na rambirambi hii ya hundi ya sh 11,288,250, msiba huu utazidi kuwaunganisha katika kipindi chote cha raha na taabu, wameomba mwenyezi mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu," alisema Mkuu huyo wa mkoa.

Luteni Gallawa aliwataka wale waliokabidhiwa dhima ya kusafirisha abiria katika vyombo vya usafiri wawe wanajali maisha ya watumiaji wao na kwamba wakati mwingine majanga ya namna hiyo yamekuwa yakiepukika lakini kutokana na wasafiishaji kujaza watu kupita kiasi hupelekea matatizo ambayo husababisha maafa kama yaliyotokea kwenye meli hiyo.

Kwa upande wake Makamu wa rais, alishukuru mchango huo kutoka kwa majirani zao wa karibu na kwamba rambirambi hiyo ni kielelezo tosha cha Muungano uliotukuka baina ya wananchi wa visiwani na bara kwa kujaliana katika shida na raha hasa katika ajali hiyo ambayo haiwezi kusauliwa kutoka na uwingi wa vifo vya watu waliopoteza maisha.

"Ulikuwa ni msiba mkubwa katika historia ya Zanzibar, watu 203 walithibitika kufariki na 619 waliokolewa, serkali zote mbili ya Muungano na ya Mapinduzi Zanzibar zilishirikana katika kipidi chote cha janga hili, na kuwasaidia wahanga hao," alisema Makamu huyo wa Rais.

Alisema tume imeundwa kuchunguza mkasa huu na serikali ya SMZ itatoa majibu yake hadharani kwa wananchi ili kuepusha janga kama hilo lisitokee tena na kwamba michango yote itapokelewa na kutumiwa kwa makusudi kwa kadri itakavoamriwa na serikali.

Ujumbe wa Tanga kwenda visiwani humo uliongozwa na Mkuu huyo wa mkoa, pia walikuwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa Bw. Mussa Shekimweri Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi, Mkuu wa wilaya ya Muheza Bw. Methew Nasei na mwakilishi wa wafanyabiashara mkoani Tanga Bw.Salim Abdallaziz  kutoka kampuni ya unga wa ngano ya Pembe.

Sunday, November 6, 2011

KUMBE KUNA SAMAKI WAKUBWA KIASI HIKI!

VIJANA WA KIJIJI CHA BAGAMOYO KILICHOPO WILAYANI KOROGWE WAKIVUA SAMAKI KATIKA DARAJA MOJA WAPO AMBALO LINAJENGWA NA KAMPUNI YA KICHINA YA SINOHYDRO, DARAJA HILO LIPO JIRANI NA MTO PANGANI AMBAO MAJI YA MTO HUO YAMEKATISHA BARABARA HIYO NA VIJANA HAO KUPATA NAFASI YA KUVUA SAMAKI

JUMA (KUSHOTO) NA SUFIANI WAKIVUA SAMAKI

ADAM NA SAID WAKIVUA SAMAKI KWA CHANDARUA KILICHOTOLEWA KWA AJILI YA KUJIKINGA NA MALARIA, LAKINI WANAKITUMIA KUVULIA SAMAKI.

VIJANA WAKIVUA HUKU WAKICHEZA KATIKA DARAJA HILO

SAMAKI WALIOVULIWA KATIKA DARAJA HILO

"...TUNAPATA SAMAKI HAPA, WEEE USICHEZE SI UNAWAONA HAWA...SHULE KWANINI BANA SI NAVUA NIKIUZA NITAPATA PESA...,ANASEMA GUMBO MLIMBO