Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Saturday, October 30, 2010

Msiwachague wapinzani kwa kufanya ushabiki

Na Mashaka Mhando,Handeni
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Handeni la kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Abdallah Kigoda, amewataka Watanzania wasifanye ushabiki wa kisiasa kwa kuwachagua wapinzani akieleza kwamba sumu haijaribiwi kwa kuonjwa badala yake waendelee kukipa ridhaa chama hicho kwa kumchagua Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi leo.

Akizungumza katika siku ya mwisho ya kampeni ya takribani siku 70 katika kijiji cah Kwenjugo Magharibi B na kwenye uwanja wa CCM wilayani hapa, Dkt Kigoda alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kufahamu kwamba wanatakiwa kwenda kupiga kura leo wakiondoa ushabiki na badala yake wachague chama hicho kwasababu kimejenga misingi imara ya uongozi tangu ngazi ya shina hadi Taifa.

"Usichague upinzani kwa kufanya ushabiki wa kisiasa, ushabiki kweli upo lakini siyo kuuingiza kwenye masuala ya uchaguzi unapofanya ushabiki utakugharimu miaka mitano...Hivi kweli sumu inajaribiwa kwa kuonjwa hebu ndugu zangu mchagueni Rais Kikwete aendelee kuongoza nchi yetu na msipoteze kura zenu," alisema Dkt Kigoda na kuongeza

"CCM imetengeneza ilani ambayo itawawezesha Watanzania wote kupiga hatua katika nyanja mbalimbali na tatizo la maji ambalo limekuwa kero kaika maeneo meni nchini litatatuliwa kwa kiasi kikubwa...Miaka mitano iliyopita serikali imeweza kutekeleza ilani kwa umakini mkubwa, achaneni na wapinzania ambao hawana hata mjumbe wa kitongoji huku vijijini,".

Akizungumzia upinzania katika wilaya hiyo alisema kutokana na mshikamano wa wanachama na wapenzi wa CCM, vyama vya upinzani vilivyopo wilayani humo baada ya uchaguzi vitabaki kujiuliza na kutafuta njia nyingine ya kuwashawishi wananchi kutokana na sera za za kwamba chama hicho hakijafanya kitu na kutukana viongozi walizokuwa wakitumia wananchi hawakuwaelewa na waliwapuuza.

Alisema huwezi mwananchi wa Handeni leo ukimweleza kwamba hakuna kilichofanyika wakati kumekuwepo mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali hatua ambayo wanajivunia tangu alipoingia mwaka 1995 hali hiyo haikuwepo na kwamba ilani ya mwaka huu imeainisha mipango mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara hadi Singida kutokea wilayani humo.

Dkt. Kigoda alisema changamoto iliyokuwepo ya ukosefu wa maji, alisema pamoja na kwamba suala hilo ni la Kitaifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo tatizo hilo litabaki kuwa historia kutokana na ukarabati mkubwa wa mtaro mkubwa wa mradi wa maji wa HTM kutokea eneo la kijiji cha Tabora kilichopo wilayani Korogwe amako ndiko kulikuwa na chanzo, kufanyiwa matengenezo makubwa hadi eneo la Manga.

"Suala la maji mimi na wenzangu (madiwani) ndilo tutakalolifanya katika miaka mitano ijayo, ilani yetu imeaanisha kwamba mradi wa maji wa HTM utakarabatiwa kuanzia pale Tabora hadi Manga baada ya ukarabati na vyanzo vingine kuongezwa tatizo hili litakwisha" alisema Dkt Kigoda.

Nae Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Bw. David Mkude aliwataka wananchi wajiadhari na viongozi wa vyama ya upinzani ambao aliwalinganisha na wachezesha karata tatu mijini kwa kuwatapeli wananchi kwa maelezo ambayo hawawezi kuyafanya badala yake wanaropoka na kukashifu viongozi wa serikali.
MWISHO

Msifanye ushabiki kwenye siasa-Dkt Kigoda

Mgombea ubunge jimbo la Handeni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Abdallah Kigoda, akijinadi kwa wapiga kura wake katika eneo la Kwenjugo Magharibi B wilayani humo leo asubuhi, pamoja na kuomba kura zake, diwani pia alimuombea kura Rais Jakaya Kikwete.

Friday, October 29, 2010

M'kiti wa Simba na vazi la mtaa wa Jangwani

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt Jakaya Kikwete akimtambulisha mgombea ubunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage ambaye pia ni mwenyekiti wa Wazazi wa mkoa huo na Mwenyekiti wa klabu ya Simba ya Jijini Dar es salaam ambayo sasa inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom ikiwa na pointi 24.

Wekundu wa Msimbazi sasa Juu

Kikosi cha timu ya Simba ya Jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu. Timu hiyo hivi sasa inaongoza ligi hiyo kwa kuwa na ponti 24 na Novemba 7 mwaka huu itashuka dimbani kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea kucheza na Majimaji ya mjini humo mchezo huo utakamilisha ratiba ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Thursday, October 28, 2010

Dkt Kigoda na mkandarasi wa maji

Mgombea ubunge wa jimbo la handeni mkoani Tanga Dkt Abdallah Kigoda akisalimiana na mkurugenzi wa kampuni ya Subhash Sing, Bw. Mahitan Sing mara baada ya kuzindua bwawa la maji eneo la Kwenjugo Magharibi wilayani humo.

Wednesday, October 27, 2010

Bw. Mashaka Mhando (kushoto) akipokea cheti chake cha kufudhu mafunzo ya siku tatu juu ya kuandika habari za uchaguzi mafunzo yaliyofanyika mjini Moshi kulia ni mchungaji Anatori Salawa.

Toledo Sekondari kuanza kufundisha somo la kompyuta

Na Mashaka Mhando,Tanga
SHULE ya sekondari ya Toledo iliyopo katika Jiji la Tanga, itaanza kufundisha wanafunzi wake somo la kompyuta kuanzia mwakani baada ya kupata msaada wa kompyuta zipatazo 37 kutoka kwa marafiki wa shule hiyo kutoka nchini Marekani na Uingereza.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa chumba cha maabara ya kompyuta, Mkuu wa shule hiyo Bw. Samwel Ndauka alisema shule hiyo inayotumia jina la mji mmoja nchini Marekani, alisema kuwa baada ya marafiki wao kuwapa msaada wa vifaa hivyo kisha walimu kupata mafunzo ya kompyuta, kuanzia mwakani watafundisha somo hilo.

Alisema shule hiyo iliyopata msaada wa kompyuta 25 kutoka shule ya sekondari ya Leyton ya nchini Uingereza kisha kupata konpyuta nyingine 12 kutoka shirika la ICT na walimu wao kupata mafunzo ya vifaa hivyo sasa wanalazimika kuanza kufundisha kompyuta kama somo ili wanafunzi waweze kujifunza na kutumia kuwasiliana na marafiki zao waliopo duniani.

Bw. Ndauka alisema dhima ya shule hiyo ni kuiweka katika ulimwengu wa teklonojia ya mawasiliano na kutoa elimu ya kisasa ambapo baada ya kuiweka shule yao katika mtandao waliweza kupata marafiki wa shule za Thomas Hepburn, Leyton na Yarborough ambayo imeifunguliwa shule hiyo tovuti ya http://www.toledo-school.com/.

Akizundua darasa hilo la kompyua Ofisa Elimu Sekondari wa Jiji la Tanga, Bw. kassim Sengasu aliwataka wanafunzi kutumia fursa hiyo ya kusoma vifaa hivyo na wajiepushe matuminzi ya kuingia katika mitandao isiyofaa badala yake wajifunze kuongeza ujuzi wa kompyuta kupitia mitandao ya elimu ili wamalizapo masomo yao waweze kujua matuminzi sahihi ya vifaa hivyo.
MWISHO

'Wanafunzi someni mtimize ndoto zenu'

Na mashaka Mhando,Tanga
WANAFUNZI wametakiwa kuwa makini kwa kujiwekea malengo katika muda wote wawapo shuleni ili kuhakikisha kila mmoja anatimiza ndoto zake kwa kuamua akiwa shuleni anataka kuwa nani mara amalizapo masomo yake.

Sanjari na hilo pia wanafunzi wametakiwa kujiepusha na vishawishi vitakavyowafanya washindwe kusoma hivyo ili kuvishinda wanatakiwa kuwa karibu na kufungamana na dini zao ambazo zitawaepusha na ugonjwa hatari wa ukimwi.

Akizungumza kwenye mahafali ya sita ya Shule ya Sekondari Wasichana ya Mtakatifu Christina, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Sokoine Profesa Aponilea Pereka alisema kuwa kumaliza kidato cha nne siyo mwisho wa harakati zao za kusoma hivyo ni vema wakalenga kuendelea na elimu ya juu itakayowahakikishia maisha bora.

"Mimi kama mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo nina wakaribisha sana hususan kwenye kitivo cha tiba ya mifugo ili mpate shahada na kuwa madaktari wa mifugo...Lakini hamuwezi kutimiza yote hayo kama mtashindwa kujiepusha na vishawishi vitakavyowaondolea ndoto zenu," alisema Profesa Pereka.

Awali akizungumza kwenye mahafari hayo Kaimu Mkuu wa shule hiyo Bi Mariam Pendo alisema moja ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili ni tatizo la wanafunzi kuwa na simu ambazo mara nyingi wamekuwa wakiwasiliana katika muda wa kujisomea hatua ambayo inawafanya washindwe kukabiliana na masomo.

"Tatizo la wanafunzi kuwa na simu shuleni watu wanaopaswa kulaumiwa ni wazazi, kwasababu wao ndiyo wanawanunulia na kuwapa kwa ajili ya mawasiliano, lakini shule yetu inauangalizi mzuri kuwapa simu wazazi watoto ni kuwafanya washindwe kusoma badala yake wanapiga na kusikiliza simu," alisema Bi Pendo.

Aidha, Mkuu huyo wa shule alisema kuwa tatizo jingine ni suala la vitabu vya kiada katika soko ambapo vitabu vingi vilivyopo sio imara na hivyo kusababisha gharama kubwa kwa shule kutokana na kununuliwa mara kwa mara kufuatia kuchakaa mapema kabla ya mihula ya mwaka kumalizika.
MWISHO

'Nyomi kwa Januari Makamba'

Umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Bumbuli kumsikiliza mgombea ubunge wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Dkt. Jakaya Kikwete alifika kufanya kampeni. Mbunge wa jimbo hilo ni Januari Makamba ambaye amepita bila kupingwa.

'ushindi upo'

Makada wa CCM wakitafari hali ya uchaguzi inavyokwenda, kutoka kushoto ni Athumani Zumo Bi Mariam Shamte na Elias Mpanda Katibu wa UVCCM wilaya ya Tanga. Hapa wapo kwenye uwanja wa shule ya msingi Mazoezi wilayani Korogwe ulipokuwa ukifanyika mkutano wa mgombea urais wa CCM Rais Jakaya Kikwete.
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kifungilo iliopo wilayani Lushoto,Tanga wakiwa kwenye mahafali ya kumaliza kidato cha Nne mwaka 2010.