Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Thursday, September 29, 2011

NAHODHA WA MELI YA KIGENI AKUTWA AMEJINYONGA BANDARI YA TANGA

NAHODHA WA MELI YA MV TIGER MONROVIA BW. PAKULSKI RADOSLAV ADAM (47) AKINING'INIA KWENYE MLINGOTI WA BENDERA KWENYE MELI HIYO BAADA YA KUJINYONGA USIKU WA KUAMKIA ALHAMISI BAADA YA MELI HIYO KUTIA NANGA KWENYE BAMDARI YA TANGA.

MWILI WA NAHODHA HUYO UKIONEKANA BAADA YA KUJINYONGA

MELI YA MVU TIGER IKIWA IMETIA NANGA KWENYE BANDARI YA TANGA

TIMU YA MAOFISA WA SERIKALI AKIWEMO MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOANI TANGA, RCO MOHAMED JAFAR (kulia mwenye glovu za bluu) AKIWA NA MAOFISA HAO KUCHUNGUZA MWILI WA MAREHEMU HUYO

NAHODHA ADAM AKIONEKANA KWENYE MTI HUO AKIWA AMEJINYONGA TAYARI

NAHODHA HUYO AKINING'INIA HUKU OFISA WA KIKOSI CHA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOANI TANGA, AFANDE JOHN AKIUTAZAMA MWILI HUO KUONA KAMA NI KWELI ALIJITUNDIKA HAPO AU ULIWEKWA NA MTU

MABAHARIA WA MELI HIYO PAMOJA NA MAOFISA WA SERIKALI WAKIUSHUSHA MWILI WA NAHODHA HUYO KUTOKA MAHALI AMBAKO ALIJINYONGEA KWENYE MELI HIYO

MELI YA TIGER INAVYOONEKANA PICHANI KATIKA ENEO LAKE LA NDANI JUU KABISA YA KICHWA CHA NAHODHA HUYO

MWILI WA NAHODHA HUYO UKIWA UMEFUNGWA TAYARI KWA KUTOLEWA NCHI KAVU KWENYE KUHIFADHIWA KWENYE HOSPITALI YA BOMBO.

MAOFISA HAO WAKIWA NA WAHUDUMU WA AFYA WA MAMLAKA YA BANDARI NCHINI BANDARI YA TANGA WAKIUBEBA MWILI KUUTOA NJE YA MELI HIYO WAKITUMIA BOTI NYINGINE

NAHODHA MSAIDIZI WA MELI HIYO BW. COLGOLF AKITOA MAELEZO KWA MAOFISA WA SERIKALI KUFUATIA KUJINYONGA KWA NAHODHA HUYO

MWILI UKIWA UMEFUNGWA VIZURI TAYARI KUPELEKWA KWENYE HOSPITALI YA BOMBO KUHIFADHIWA

MWILI UKIWA UMEBEBWA NA MAOFISA HAO NA KUUPAKIA KWENYE BOTI ILI WAUTOE NJE NA KUUPELEKA HOSPITALINI BOMBO

MAOFISA HAO WAKIUTOA MWILI HUO NJE YA BOTI WALIMOMPAKIA NA KUUPELAKA BOMBO HOSPITALI.

Na Mzee wa Bonde,Tanga
Nahodha wa meli ya kigeni akutwa amejinyonga melini
NAHODHA wa Meli ya shehena ya MV  Tiger Monrovia,Pakulski Radoslav Adam (47)  jana alikutwa akiwa amejinyonga ndani ya meli hiyo katika mazingira ambayo hayajajulikana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe  alisema jana kuwa  kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana Alhamisi wakati meli hiyo ikiwasili katika bandari ya Tanga ikitokea Dar es salaam.


Alisema wafanyakazi wa meli hiyo wamesema kuwa  Nahodha huyo alipanda ngazi hadi kwenye nguzo za bendera ya meli hiyo na kujinyonga kwa kutumia kamba.


Alisema wanfanyakazi hao wamedai kuwa hawakuwa wamejua mwenzao alikokuwa hadi ilipofika  ilipofika alfajiri baada ya mmoja wa wafanyakazi melini kupanda juu na kuukuta mwili wake ukining’inia.

Alisema kufuatia tukio hilo, wafanyakazi hao wameweza kuwasiliana na ndugu zake walioko nchini Poland pamoja na mmliki wa meli hiyo ambao ili kujua nini kifanyike juu ya mwili huo
.

Mwandishi wa habari hizi alishihudia shughuli za utoaji wa mwili huo uliokuwa ndani ya meli iliyotia nanga mbali na bandari ya Tanga,zikifanywa na maafisa wa jeshi la Polisi,Bandari ya Tanga,uhamiaji,TRA pamoja na mawakala wa meli hiyo ambapo ilichukua zaidi ya masaa saba hadi kuutoa na kuupeleka Hospitali ya Bombo.


Wakala wa meli hiyo,Abas Mohamed wa kampuni ya CMA CGM (T) Ltd alisema imebeba makontena ya bidhaa mbalimbali ambazo zimetoka nchi za Ulaya na bara la Asia na kwamba ilipita Dar es salaam na ingekaa banadari ya Tanga kwa siku mbili kabla ya kwenda Mombasa na Colombo  nchini Malasia.


Afisa afya wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Happiness Byabato alisema baada ya kuufanyia uchunguzi mwili huo ambaini kuwa amejinyonga mwenyewe.


Kwa mujibu wa  Massawe ni kuwa  mwili huo umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga,Bombo kusubiri maamuzi ya ndugu wa marehemu kama asafirishwe au azikwe Tanga.


Alisema pamoja na kwamba taarifa za awali zinaeleza kuwa nahodha huyo kajinyonga lakini jeshi hilo bado linafanya uchunguzi wa kitaalamu kujua chanzo cha tukio hilo.

                                                

Tuesday, September 27, 2011

UMEONA UJUMBE WA 'LANGU JICHO MGAHAWA'

WANANCHI WA KIJIJI CHA MAGOMA WILAYANI KOROGWE WAKIWEMO WATOTO WAKIPATA HUDUMA YA CHAKULA KWENYE MGAHAWA HUU AMBAO UMEKUWA NA MJUMBE MZITO KWA NJE KAMA UNAVYOONEKANA HAPA.

Sunday, September 11, 2011

MMILIKI WA BLOGU YA VIJIMAMBO VYA TANGA 'ANKO MO' APATA AJALI

MDAU MKUBWA WA MAWASILIANO YA ELETRONIKI MKOANI TANGA BW. MOHAMED HAMMIE RAJAB 'ANKO MO' AMBAYE ANAMILIKI BLOGU YA ANKO MO.BLOGSPOT.COM YENYE VIJIMAMBO VYA TANGA, AMEPATA AJALI MBAYA YA PIKIPIKI KATIKA MAENEO YA JIJI LA TANGA ALIPOKUWA KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA PILIPILI ZA KILA SIKU KUSAKA MATUKIO MAPYA. ANKO MO HIVI SASA YUPO WILAYANI PANGANI AKIPATA MATIBABU. BLOGU HII YA MZEE WA BONDE INAMPA POLE MNO NA INAMTAKIWA APONE HARAKA ILI AENDELEE NA SHUGHULI ZAKE KWA AJILI YA MKATE WA KILA SIKU.

Monday, September 5, 2011

WAANDISHI WAKIPIGWA MSASA JUU YA MASUALA YA UNYANYASAJI MOROGORO HOTEL

LEAH MWENYIKULE  MRATIBU WA WARSHA YA KUHUSU UNYANYAPAA NA UNYANYAPAA DHIDI YA WATOTO KWA AJILI YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI KUTOKA MIKOA YA TANGA, LINDI, MTWARA, MOROGORO, DODOMA, IRINGA, MBEYA NA DAR ES SALAAM INAYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA HOTELI YA MOROGORO, ILIYOANDALIWA NA PACT TANZANIA

BAADHI YA WASHIRIKI WAKIWA KWENYE CHUMBA CHA WARSHA


WASHIRIKI WAKIFUATILIA KWA MAKINI WARSHA HIYO

MZEE WA BONDE AKIINGIZA PICHA ZA WARSHA HIYO HUKU JIRANI YAKE MOHAMED ABDULAZIZ WA LINDI AKIINGIZA PICHA ZA CHANEL 10

MBUNGE WA TANGA, AZINDUA HOTELI MPYA YA NYUMBANI , ASEMA HAINA TOFAUTI NA ALIZOZIONA ULAYA

HOTEL MPYA YA NYUMBANI HOTEL & RESTAURANT  INAVYOONEKANA.

MGENI RASMI KATIKA SHEREHE FUPI YA UFUNGUZI WA HOTELI MPYA YA NYUMBANI HOTEL & RESTAURANT ENG. OMARI NUNDU (Katikati mwenye taji) AMBAYE NI MBUNGE WA TANGA, KULIA NI MKURUGENZI MTENDAJI WA HOTELI HIYO BW. ALOYCE KIMARO MBUNGE WA ZAMANI WA JIMBO LA VUNJO (CCM).

NAIBU MEYA WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA BW. MUZAMINI SHEMDOE AMBAYE NI DIWANI WA KATA YA MABAWA (wa kwanza kushoto) DIWANI WA KATA YA CENTRAL BW. KHALID ABDALLAH (katikati).

WADAU MBALIMBALI WALIFIKA KATIKA UZINDUZI HUO WA HOTELI YA NYUMBANI AKIWEMO MMILIKI WA HOTELI YA DOLPHIN INN ILIYOPO ENEO LA CHUDA BI ANNA MAARUFU ANNA DOLIPHIN (katikati) AKIWA NA RAFIKI ZAKE.

NAIBU MHARIRI WA GAZETI LA MWANANCHI BW. MIDRAJ IBRAHIMU (kushoto) AKIWA NA OFISA MMOJA WA JIJI LA TANGA KITENGO CHA BIASHARA NA MASOKO WAKIWA MIONGONI MWA WATU WALIOHUDHURIA UZINDUZI HUO.
Na Mzee wa Bonde,Tanga
MMILIKI wa hoteli mpya inayojulikana kwa jina la NYUMBANI Hotel & Restaurant Bw. Aloyce Kimaro aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, amewataka wafanyabiashara na wananchi wa Jiji la Tanga, kumuunga mkono katika uwekezaji wake mpya wa sekta ya hoteli ili kusaidia kuongezeka kwa pato la uchumi la mkoa wa Tanga.

Akitoa neno la shukurani kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopo mkabala ya jengo la posta katikati ya Jiji la Tanga, mbunge huyo wa zamani alisema alipata wazo la kufungua hoeli hiyo mkoani Tanga, kushirikiana na wana-jamii kuongeza pato la mkoa hasa kutokanana uwepo wa bandari na shughuli nyingine za kiuchumi.

Alisema kutokana na uwepo wa bandari na kukua kwa shughuli nyingi za kibiashara alionelea kufungua hoteli hiyo hivyo amewataka wananchi na wafanyabiashara kushirikiana naye kumsapoti katika kuhakikisha hoteli hiyo inatoa huduma za kisasa na za kimaaifa.

Bw. Kimaro ambaye anaendesha hoteli hiyo akiwa na wakurugenzi wengine Bw. John Kessy na Mansfeld, wanatarajia kufungua hoteli zenye jina hilo katika mikoa yote nchini ili kuhakikisha wanawekeza katika sekta hiyo wakiwa kama Watazania na kusaidia kukua kwa uchumi wa Tanzania. Hoteli hiyo ya Tanga inafuatia kuwepo kwa hoteli nyingne zenye jina hilo la nyumbani katika miji ya Mwanza na Moshi.

Akizindua hoteli hiyo Waziri wa Uchukuzi, Injinia Omar Nundu ambaye ni mbunge wa jimbo la Tanga, alisema katika kutembea kwake Ulaya hoteli hiyo inaingana kabisa na ambazo amezishuhudia na kwamba hoteli ya Nyumabni ni moja ya hoteli yenye hadhi kubwa mkoani Tanga na ambayo itafungua ukurasa mpya kwa wawekezaji wengine.

"Mbunge wenu mnajua nimemaliza huko Ulaya, lakini hoteli hii nilipoingai kwenye vyumba nimekuta vitu ambavyo nikiwa huko Ulaya kwenye mahoteli makubwa nimekutana na mambo makubwa mabyo yamo humu ndani, hii ni changamoto kwa wawekezaji wengine kuona umuhimu wa kuwekeza mahoteli makubwa kama haya katika Jiji letu," alisema Injinia Nundu.