Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, November 30, 2010

TANGA USIKU INAVYOKUWA HAPA NI ENEO LA KITUO BANGI


BAADHI YA NGUZO ZA TAA ZILIZOPO KATIKA BARABARA YA PANGANI (TAIFA ROAD) ZIKIWAKA KATI YA NGUZO 48 AMBAZO HAZIWAKI KUTOKANA NA KUUNGUA LICHA YA TAA HIZO KUPIGIWA KELELE SANA KUTOKANA NAMKANDARASI WA KAMPUNI YA SKYTEEL YA ARUSHA KUSHINDWA KUMALIZIA KAZI HIYO LICHA YA HIZO WALIZOZITENGENEZA KUTOZISHUGHULIKIA PINDI ZINAPOUNGUA.

AJALI AJALI AJALI!!!! BARABARA YA SEGERA CHALINZE


TANGA LEO ASUBUHI HAPA NI STENDI KUU YA MABASI

ANKAL MICHUZI KUTOA MAFUNZO YA KUFUNGUA BLOGU DES 10 JIJINI DAR UKUMBI WA BASATA

ANKAL AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIWAELEZA WADAU WA JUKWAA LA SANAA NAMNA YA UMUHIMU WA WASANII KUJITANGAZA KWENYE BLOGU ZILIZOPO HAPA NCHINI.



ANKAL MICHUZI AKIWAONESHA WADAU WA JUKWAA LA SANAA JINSI YA KUWEKA VIDEO KWENYE U-TUBE KULIA KWA ANKAL NI BW. JABIR IDRISA MWANDISHI WA HABARI MKONGWE NCHINI.
  Ankal Michuzi (Issa Michuzi) ambaye ni mmoja wa waasisi wa mitandao ya habari ya jamii (blogs) hapa nchini amewashauri wadau wa sanaa hasa wasanii kuanza kuingia kwa kasi kwenye matumizi ya teknolojia hiyo kwani ni njia kubwa ya kujitangaza na kuuza kazi za sanaa kote duniani.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa leo Jumatatu,Michuzi ambaye blog yake ya www.issamichuzi.blogspot.com imepata umaarufu mkubwa kutokana na kutembelewa na watu wengi aliweka wazi kwamba,blogs zimekuwa zikitembelewa na watu mbalimbali duniani hivyo wasanii hawana budi kuzitumia ili kujitangaza, kusambaza kazi zao na hata kujitambulisha katika masoko ya kimataifa.

Alisema kwamba, blogs tofauti na aina nyingine za vyombo vya habari inatumiwa kuhifadhi picha nyingi na kazi mbalimbali, kupata taarifa kuhusu tasnia ya sanaa, kupokea mawazo ya wateja wa kazi za sanaa na hata kuwa na wasaa wa kuwasiliana na wasanii wengine na hivyo kupanuka kimawazo na kiujuzi.

Akizungumzia historia ya blogs,Michuzi alisema kwamba ni teknolojia mpya hapa nchini na kwamba,ilianza kwa kuandika habari za kawaida lakini leo hii ni tegemeo katika kupasha habari kwa uharaka zaidi, kuwafikia watu wengi kuliko vyombo kadhaa vya habari na kimbilio la jamii kwani imekuwa kama sehemu ya jamii katika masuala mbalimbali.

Kwa ujumla Michuzi aliwataka wasanii na wadau wa Sanaa kuamka na kuanza kutumia teknolojia hiyo kwani wasanii mbalimbali duniani si tu wamekuwa wakitumia blog katika kujitangaza na kutambulisha kazi zao bali pia wamekuwa wakimilki mitandao na technolojia mbalimbali za mawasiliano.

Katika kuonesha kwamba, teknolojia hiyo ni muhimu Michuzi ameahidi kuwapa mafunzo ya bure wadau wa Jukwaa la Sanaa juu ya kufungua na kumiliki blog ambayo yataendeshwa Ijumaa ya Desemba 10,2010 kwenye Ukumbi wa BASATA.Wadau wote wa Sanaa mnakaribishwa.

Monday, November 29, 2010

KAMANDA MAALIMU GURUMO ATOKA ICU ALAZWA SASA ALAZWA MWAISELA

MWANAMUZI MKONGWE WA MUZIKI WA DANSI NCHINI MAALIMU MUHIDIN GURUMO AMBAYE WIKI ILIYOPITA ALILAZWA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM KUTOKANA NA KUSUMBULIWANA UGONJWA WA MAPAFU KUJAA MAJI KABLA YA KUHAMISHIWA KWENYE WODI YA UANGALIZI MAALUMU ICU BAADA YA HALI YAKE KUWA MBAYA, MAPEMA LEO MCHANA HALI YAKE ILIBADILIKA NA KUWA NZURI NA KUTOLEWA KWENYE CHUMBA HICHO NA KULAZWA KATIKA WODI YA MWAISELA NAMBA 1.

PICHANI AMBAPO HATA HIVYO TUNASIKITIKA KWA KUTOONEKANA VIZURI (KOMRADHI) NI MZEE MAKASSY MMOJA YA WANAMUZIKI NGULI HAPA NCHINI AKIMJULIA HALI MWANAMUZIKI MWENZAKE ALIPOFIKA HOSPITALINI HAPO LEO.

MH. SOPHIA SIMBA NA NAIBU WAKE WAANZA KAZI RASMI WIZARANI

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO BI SOPHIA SIMBA AKIWA NA NAIBU WAKE BI UMMY ALI MWALIMU WAKIWASALIMIA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO BAADA YA KUWASILI WIZARANI HAPOMKUANZA KAZI LEO MCHANA.


MH. SOPHIA SIMBA AKITIA SAHIHI KITABU KILICHOPO KATIKA OFISI YAKE LEO ALIPOFIKA KUANZA KAZI RASMI KATIKA WIZARA HIYO.


NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO BI UMMY ALI MWALIMU NAYE AKIWEKA SAHIHI KITABU KILICHOKUWEPO KATIKA OFISI YAKE WIZARANI HAPO LEO MCHANA WALIPOFIKA KUANZA MZIGO.


CHILIGATI AMKABIDHI NYARAKA WAZIRI PROFESA TIBAIJUKA

ALIYEKUWA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MH. JOHN CHILIGATI AKIMKABIDHI MAKLABASHA NA NYARAKA MBALIMBALI WAZIRI MPYA WA WIZARA HIYO PROFESA ANNA TIBAIJUKA. MAKABIDHIANO HAYO YALIFANYIKA JANA WAKATI WAZIRI HUYO ALIPOFIKA KUANZA KAZI KATIKA WIZARA YAKE HIYO MPYA. KULIA NI KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO BW. PATRICK RUTABANZIBWA.

JK AKUTANA NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI KWA MARA KWANZA TANGU ALIAPISHE


RAIS JAKAYA KIKWETE AKIKUTANA NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI KWA MARA YAKE YA KWANZA TANGU ALIUNDE NA KULIAPISHA JUMAMOSI ILIYOPITA IKULU JIJIJI DAR ES SALAAM LEO.(PICHA NA FREDY MARO WA IKULU)


BORESHENI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI KWANZA BEI BAADAYE-KALEMBO

KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. PAUL AMANIEL CHIKIRA (SHOTO) NA ENG. REYMOND MHANDO AMBAYE NI MWENYEKITI WA TANGA-UWASA WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAONI YANAYOTOLEWA NA WADAU WA TANGA-UWASA.



MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJISAFI NA MAJITAKA YA JIJI LA TANGA (UWASA) ENG. JOSHUA MGEYEKWA AKISOMA MAPENDEKEZO YA KUONGEZA BEI YA MAJI KATIKA JIJI HILO LEO ASUBUHI.


MDAU WA MAMLAKA YA MAJISAFI NA MAJITAKA YA JIJI LA TANGA-UWASA BOB. NASSER MAKAU ALIKUWA NI MMOJA YA WA WADAU WALIOTOA MAONI KWENYE MKUTANO HUO ULIOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA MKUU WA MKOA LEO ASUBUHI.


SALIM BAWAZIR (kulia) MMOJA YA WADAU WAKUBWA WA TANGA UWASA AKITOA MAONI YA KUIPONGEZA MAMLAKA HIYO KWA KAZI NZURI INAYOFANYA YA KUSAMBAZA MAJI KWA WAKAZIZ WA JIJI LA TANGA NA VITONGOJI VYAKE.


MKURUGENZI WA WA EURA BW. FELEX NGAMLAGOSI AKIZUNGUMZA NA WADAU KWENYE MKUTANO HUO.


KALEMBO ALIPOTEMBELEA KIWANDA CHA NGOMENI KAMBA


MENEJA WA KIWANDA CHA NGOMENI KAMBA KILICHOPO WILAYANI MUHEZA (MWENYE SHATI NYEUPE), AKIMWELEZA MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI MSTAAFU SAIDI KALEMBO NAMNA WANAVYOZALISHA KAMBA HIZO NA UZIUZA NJE YA NCHI.


MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI (MSTAAFU) SAID KALEMBO AKIANGALIA MOJA YA KAZI ZINAZOFANYWA NA KIWANDA CHA KAMBA NGOMENI AINA YA KIKAPU KILICHOFUMWA VIZURI NA NYUZI ZA KAMBA ZA KATANI HIVI KARIBUNI ALIPOTEMBELEA WILAYA YA MUHEZA.


TAMISEMI YAIAGIZA HALMASHAURI KYELA KUMLIPA ALIYEKUWA MWENYEKITI WAKE

Na Mdau Thobias Mwanakatwe, Kyela
WIZARA ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeiweka katika wakati mgumu Halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya baada kuiagiza kumlipa stahili zake zote aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Timoth Kisugujila  kutokana na Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kumvua madaraka mwenyekiti huyo bila kuzingatia taratibu na sheria za TAMISEMI.
 
Kisugujila ambaye alikuwa diwani wa kata ya Makwale wilayani hapa, alivuliwa madaraka ya uenyekiti Novemba mwaka jana na kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kudaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kumwandikia barua aliyekuwa diwani wa kata ya Kyela mjini,Visk Mahenge kwamba udiwani wake umekoma kutokana na kata ya Kyeka kupandishwa hadhi kuwa Mamlaka ya Mji mdogo.
 
Katika barua yake aliyekuwa Mwenyekiti huyo wa halmashauri, yenye kumb Na KDC/1/09 ya Novemba 13 mwaka 2009  ilieleza  kuwa kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 kifungu cha 45 (1) inayoongoza uundwaji wa Mamlaka ya Miji Midogo inapelekea kumnyima fursa ya yeye diwani (Visk Mahenge) kuendelea na madaraka yake ya udiwani.
 
Kutokana na barua hiyo ya Kisugujila, madiwani waliokuwa na hoja ya kumuengua mwenyekiti walimuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Mhando Senyagwa aiitishe mkutano wa dharura ndani ya siku nne ambapo Mkurugenzi alifanya hivyo na madiwani hao kwa kauli moja wakamwazimia na kumuengua katika nafasi ya uenyekiti.
 
Baada ya azimio hilo la madiwani kufikiwa,Mkurugenzi wa Halmashauri,Senyagwa aliitisha kikao kingine cha Baraza la Madiwani na kumchagua Mwenyekiti mpya wa Halmashauri, Watson Majuni ambaye alikuwa Makamo Mwenyekiti na Diwani wa kata ya Kajunjumele ambaye aliidhinishwa rasmi kuwa Mwenyekiti.
 
Kikao hicho cha kumuidhinisha Mwenyekiti mpya wa Halmashauri hiyo,kilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, ambaye katika hotuba yake alisema amefurahishwa na uamuzi uliofikiwa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kumwadabisha Mwenyekiti wao,Kisugujila kwa kosa la kutumia madaraka yake vibaya.
 
Kwamujibu wa barua yenye kumbu Na.CHB.215/443/01/61 ya Novemba 5 mwaka huu iliyoandikwa na Waziri wa TAMISEMI, Celina Kombani kwenda kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela na nakala kupelekwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,imetoa maamuzi ya rufaa iliyokatwa na Kisugujila ya kupinga kuvuliwa uenyekiti wa halmashauri.
 
Katika maamuzi ya waziri yaliyozingatia sababu moja kati ya nne zilizotolewa na mlalamikaji (Kisugujila), kuwa taarifa ya Mkutano wa Baraza  la Madiwani lililomvua madaraka  haikuzingatia masharti ya Kanuni ya 3(c)  ya mwaka 1995 ya taratibu za kumuondoa madarakani  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya.
 
“Kuhusu sababu ya nne ya rufaa imedhihirika kuwa hakuna taarifa ya maandishi iliyopelekwa kwa Mkuu wa Mkoa na kwamba Mkuu wa Mkoa au mwakilishi wake hawakuhudhuria mkutano huo,kutokuwepo kwa Mkuu wa Mkoa au mwakilishi wake katika mkutano huo ni kukiuka masharti ya kanuni ya 3 (c) ya taratibu za kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Halmashauri,”imeeleza barua hiyo ya Waziri wa TAMISEMI ambayo NIPASHE inayo nakala yake.
 
Barua hiyo imeeleza kwa msingi huo uamuzi uliofanywa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela bila kuwepo Mkuu wa Mkoa au mwakilishi wake ni batili na hivyo waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa ameamua kuwa rufaa ya Kisugujila ya kupinga kuvuliwa Uenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo imekubaliwa.
 
Kwamujibu wa barua hiyo ya waziri wa TAMISEMI,imeendelea kueleza kuwa kwa kuwa muda wa vikao vya mabaraza umeishia mwezi Julai 2010, hivyo Kisugujila atahesabika kuwa alikuwa madarakani kuanzia tarehe alipovuliwa uenyekiti wa halmashauri hadi tarehe ya mabaraza yalipovunjwa.
 
Kutokana na uamuzi huo,Waziri wa TAMISEMI amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela,Mhando Senyagwa kumlipa stahili zake zote za uenyekiti Timoth Kisugujila,  kuanzia tarehe alipovuliwa madaraka hadi mwezi Julai 2010 mabaraza yalipovunjwa.
 
Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI aliyefahamika kwa jina moja la Maswi, alipozungumza na NIPASHE kwa simu alisema pamoja na kwamba suala hilo lipo lakini hawezi kulizungumzia na badala yake Katibu Mkuu wa TAMISEMI ndiye anapaswa kulitolea maelezo ya kina.
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela,Senyagwa alipofuatwa na NIPASHE ofisini kwake kuzungumzia sakata hilo ilishindikana kutokana na kupata shinikizo la damu ghafla ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya Kyela baada ya kupata ghafla ugonjwa wa shinikizo la damu.
 
Kwamujibu wa taarifa zilizopatikana toka hospitalini hapo ambazo zilielezwa na wauguzi wa hospitali hiyo ambao waliomba majina yao yasiandikwe gazetini walisema hali ya Mkurugenzi si nzuri na kwamba shinikizo la damu lilikuwa limepanda hadi kufikia 220 kwa 160.
 
Kuugua ghafla kwa Mkurugenzi huyo kumezua maswali mengi kutoka kwa wafanyakazi wa halmashauri hiyo hasa ikizingatia kuwa imekuja siku tatu tu baada ya kupokea barua hiyo toka wizarani.
 

GURUMO HALI YAKE BADO TETE, ALAZWA ICU

MWANAMUZIKI MKONGE WA MUZIKI WA DANSI NCHINI MAALIM MUHIDINI GURUMO AMBAYE NI KIONGOZI WA MSONDO NGOMA MUZIKI BAND, HALI YAKE BADO HAIRIDHISHI BAADA YA KULAZWA WIKI ILIYOPITA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM.

TAARIFA ZINASEMA KWAMBA AMEHAMISHIWA KATIKA WODI YA UANGALIZI YA WAGONJWA WALIOKUWA MAHUTUTI (ICU) YA HOSPITALI HIYO KUTOKANA NA KUSUMBULIWA NA UGONJWA WA MAPAFU KUJAA MAJI.
                                       

WAZIRI HAWA GHASIA ATINGA OFISINI KWAKE LEO APOKEWA KWA FURAHA


WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, BI. HAWA GHASIA AKILAKIWA NA KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO BW. GEORGE YAMBESI (KULIA) HUKU MKURUGENZI MKUU WA UTAWALA NA RASILIMALI WATU WA WIZARA HIYO BW. ALOYCE MSINGWA (KUSHOTO) AKIMKABIDHI SHADA LA MAUA KAMA FURAHA YA KUMKARIBISHA WAZIRI HUYO LEO KATIKA WIZARA HIYO BAADA YA KUAPISHWA JUMAMOSI ILIYOPITA.
                          

JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA CHADEMA NCHI NZIMA




JESHI LA POLISI NCHINI LIMEZUIA MIKUTANO YOTE AMBAYO ITAFANYWA NA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) ILIYOPANGWA KUFANYIKA NCHI NZIMA.

MKURUGENZI WA SHERIA, KATIBA NA HAKI ZA BINADAMU WA CHADEMA MH. TUNDU LISSU (MB) ALIWAELEZA WAANDISHI WA HABARI KATIKA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA CHAMA HICHO YALIOPO KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM, ALILALAMIKIA HATUA HIYO AKIDAI KUWA NI KINYUME NA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI.

MIKUTANO HIYO YA CHADEMA ILILENGA KUPITA KWA WANANCHI KUWASHUKURU NA KWAMBA PIA WALITAKA KUWAELEZA NAMNA UCHAGUZI MKUU WA WABUNGE, RAIS NA MADIWANI NAMNA WALIVYOHUDUMIWA KITENDO AMBACHO JESHI HILO LILIONA HUENDA KUKATOKEA UVUNJIFU WA AMANI.

SHEMEJI TIGANYA NA SHAHADA YAKE YA UZAMILI YA MAWASILIANO YA UMMA AKIWA SAUT MWANZA

MAOFISA HABARI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO) KUTOKA KUSHOTO BI. LYIDIA CHURI AKIWA AMEPOZI NA MWENZAKE BW. VICENT TIGANYA AMBAYE ALIWAHI KUWA OFISA HABARI WA MKOA WA TANGA KABLA YA KUREJESHA MAKAO MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM AMBAKO YUPO HADI SASA WAKIWA KWENYE VIWANJA VYA RAILA ODINGA VYA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AUGOSTINO (SAUT) MARA BAADA YA KUTUNUKIWA SHAHADA ZAO ZA UZAMILI MASTER OF ARTS IN MASS COMMUNICATION.


OFISA HABARI MKUU (MSTAAFU) ALIYEKUWA OFISI YA WAZIRI MKUU WAKATI HUO BW. JACOB TESHA WA PILI KULIA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA KWENYE VIWANJA VYA RAILA ODINGA YA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AUGOSTINO (SAUT) NA BAADHI YA MAOFISA HABARI WA HALMASHAURI, DARA ZA SERIKALI ZINAZOJITEGEMEA AKIWEMO BW. VICENT TIGANYA WA TATU KUTOKA KUSHOTO BAADA YA KUTUNUKIWA SHAHADA ZAO ZA UZAMILI MASTER OF ARTS IN MASS COMMUNICTAION YA CHUO HICHO.


Sunday, November 28, 2010

BUNDA UKEREWE JIMBO JIPYA KATOLIKI PADRE RENATUS NKWANDE ACHAGULIWA KUWA ASKOFU KUONGOZA JIMBO HILO




Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict xvi ametangaza rasmi kuundwa kwa jimbo jipya la katoliki la Bunda na Ukerewe. Jimbo la Bunda na Ukerewe linaundwa kutokana na vipande vya jimbo la Mwanza na Musoma. Katika hatua nyingine Papa amemteua Padre Renatus Nkwande kuwa Askofu wa jimbo hilo jipya.

Askofu mpya mteule huyo Nkwande ndoa yake ya mwisho kuifungisha ilikuwa ni Novemba 6 mwaka huu mjini Mwanza katika kanisa Katoliki la Bugando alipofungisha ndoa baina ya Bw. Joseph Sura na Mama Calvin ndoa ambayo aliibariki na kuwa ya mwisho hadi kuteuliwa kuwa Askofu nafasi ambayo ni kubwa. Mungu ambariki askofu huyo mpya.



MANCHESTER YASHIKA USUKANI LIGI UINGEREZA, YAIGAGADUA BILA HURUMA BLACKBURN 7-1

MSHAMBULIAJI HATARI WA KIBULGARIADIMITAR BERBATOV AKIIFUNGIA TIMU YAKE YA MANCHESTER UNITED BAO LA 7 DHIDI YA BLACKBURN
Timu ya soka na Manchester United ya ingereza leo imeshika usukani wa Ligi Ku ya Uingereza baada ya kutoa kipigo kikali dhidi ya imu ya blackburn ambapo katika mchezo huo mshambuliaji Berbatov aliibuka shujaa baada ya kuifungia timu yake magoli matano mengine yalifungwa na Luis Nani na Ji Sum Park.

Katika matokeo mengine Asenal iliyofungwa mfululizo mechi mbili za ligi kuu na ile ya ulaya leo ilizinduka na kuiuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Aston Villa.

Matokeo mengine ni haya hapa katika michezo ya jana..

UFUNGUZI CECAFA TUSKER CUP TANZANIA YAANZA KWA KIPIGO, YACHAPWA 1-0 NA ZAMBIA

KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS


KIKOSI CHA ZAMBIA CHIPOLOPOLO


RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKISALIMIANA NA WACHEZAJI WA KILIMANJARO STARS AKIONGOZWA NA NAHODHA SHADRACK NSAJIGWA FUSO

KIUNGO WA KILIMANJARO STARS MOHAMED BANKA (KULIA) AKICHUANA NA MCHEZAJI WA ZAMBIA THOMAS NYIRENDA TANZANIA ILICHAPWA BAO 1-0.

KOCHA WA KILIMANJARO STARS JAN POULSEN AKISALIMIANA NA KOCHA WA ZAMBIA MARA BAADA YA PAMBANO HILO KUMALIZKA.





Saturday, November 27, 2010

JK AWAAPISHA MAWAZIRI WA SERIKALI YAKE IKULU LEO

MAWAZIRI WAKIWA WAMEKAA IKULU LEO WAKISUBIRI KUAPISHWA KUTOKA KUSHOTO NI WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI, SHUKURU KAWAMBWA, WAZIRI WA KILIMO,CHAKULA NA USHIRIKA PROF. JUMANNE MAGHEMBE NA WAZIRI OFISI YA RAIS MAHUSIANO NA URATIBU MH. STEPHEN WASIRA.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI DKT. HARISON MWAKYEMBE AKIELEKEA KWENYE ENEO LA KUPISHWA IKULU LEO.



WAZIRI WA UJENZI BW. JOHN POMBE MAGUFURI, NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA  MH CHARLES KITWANGA 'MAWE MATATU', WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI PROF. ANNA TIBAIJUKA NA WAZIRI WA UCHUKUZI ENG. OMARI RASHID NUNDU 'ZINDABAA'.
 
NAIBU WAZIRI WA UJENZI PROF. HARISON MWAKYEMBE NA FAMILIA YAKE
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIMPONGEZA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI PROF. ANNA TIBAIJUKA BAADA YA KUAPISHWA NA ALIMKABIDHI NYARAKA MBALIMBALI ZA KUFANYIA KAZI IKULU LEO JIJINI DARE SALAAM.
 

ULAYA TABU BARAFU YAZIBA BARABARA UINGEREZA

MOJA YA BARABARA ZA UINGEREZA ZIKIWA KATIKA HALI YA BARAFU LEO ASUBUHI

MASIKINI MBWA HUYU YUPO KATIKA WAKATI MGUMU WA KUKATIZA KWENYE MLIMA MKUBWA WA BARAFU

JAMAA HUYU AKIKATIZA MITAA HUKU BARAFU IKIMDONDOKEA NA KUZIBA BARABARA
BARAFU imetanda katika mitaa mbalimbali ya kaskazini na mashariki ya Londan ambako shughuli mbalimbali ikiwemo wanafunzi hawajaenda shule asubuhi leo kutokana na barafu kutishia uhai na magari yamekuwa yakipita kwa tabu barabarani ingawa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa juu ya madhara makubwa yaliyorpotiwa kutokea.

Mechi za leo za mzunguko wa pili za kugombea kome la FA huenda zisifanyike na kiongozi wa mchezo wa ragbi kati ya timu ya Afrika Kusini na Uingereza uliokuwa ufanyike leo kwenye uwanja wa Twickenham umeaahirishwa hadi utakapopangiwa siku nyingine. Sorce BBC

SAMAKI ALIYEPOTEA MIAKA 60 ILIYOPITA ATENGEWA ENEO MAALUM KIGOMBE

SAMAKI AINA YA SILIKANTI AMBAYE AMEPOTEA DUNIANI MIAKA 60 ILIYOPITA. SAMAKI HUYU ANA HISTORIA HAPA DUNIANI NA PIA ANA UTI WA MGONGO KAMA BINADAMU HUPENDA KUISHI CHINI BAHARINI KIASI CHA MITA 200 MAPANGONI.
                              Na Mzee wa Bonde
WAKAZI wanaoishi katika mwambao wa pwani ya bahari ya hindi, wametakiwa kutunza rasilimali ziliozomo katika maeneo ambayo yametengwa maalum kwa ajili ya uhifadhi wa viumbe vya bahari ili kuboresha na kupanua uchumi wa wananchi licha ya kuwepo matuminzi endelevu ya rasilimali hizo.

Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za bahari na Maeneo Tengefu, Dkt Abdilahi Chande alisema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa wadau juu ya uundaji wa mpango wausimamizi wa hifadhi ya bahari ya Silikanti ya Tanga katika eneo la Kigombe ambako samaki huyo wa aina yake duniani amekuwa akipatikana hapo mara kwa mara.

Alisema hifadhi ya bahari ni muhimili mkubwa wa rasilimali zilizomo ndani yake hivyo jamii inayoishi kwewnye maeneo hayo wana wajibika kuwa walinzi wa rasilimali hizo ambazo zitaweza kusaidia vizazi vijavyo na pia kusaidia uchumi wa nchi kwa sehemu kubwa ya uhifadhi wa viumbe hiyo.

"Kama wananchi mnaoishi katika maeneo ya bahari bmnalo jukumu kubwaq la kusimamia rasilimali zilizomo ndani ya bahari kwa lengo la kuleta tija kwa maslahi ya wananchi...Usimamizi bora na shirikishi utalenga katika kupanua uchumi wa wananchi licha ya kuwepo kwa matumizi endelevu ya rasilimali hizo," alisema Dkt Chande.

Katika mkutano huo alisema malnego makuu ni ya kurejesha maoni na mawazo ambayo ya wananchi ambayo waliyatoa wakati wakifanya mikutano katika maeneo yao wanayoishi ambako waliweza kupata taarifa mbalimbali juu ya matumizi sahihi ya rasilimali, matatizo ya kiuchumi na kijamii pamoja na yale yanayoharibu mazingira ya baharini. Hivyo mkutano hio ungechambua na kupata mpango mkakati wa namna watakavyosimamia hifadhi hiyo ya Silikanti Kigombe.

Awali Kaimu Mhifadhi Mfawidhi wa Silikanti Kigombe Bw. Sylevester Kazimoto alisema kuwa serikali tayari imepitisha kwamba eneo la Kigombe liwe hifadhi tengefu kwa ajili ya samaki aina ya Silikanti ambaye alipotea duniani miaka 60 iliyopita kabla ya kuonekana tena nchini Afrika ya Kusini na baadaye kuonekana mwaka 2003 tangu atoweke katika eneo la bahari ya Kilwa mkoani Lindi.

Bw. Kazimoto alisema eneo la Mtakatifu Luciana nchini Afrika ya kusini lilitengwa kuwa eneo tengefu la samaki huyo  sehemu nyingine hapa nchini ni eneo la Mafia lililotengwa mwaka 1994, ghuba Mnazi iliyopo katika maiingilio ya mto Ruvu iliyotengwa mwaka 2000 na hifadhi ya silikanti ya Kigombe iliyotengwa mwaka 2009.

RAIS OBAMA ASHONWA NYUZI 12 MDOMONI, NI BAADA YA KUUMIA AKICHEZA BASKETBALL

RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI AKIJISHIKA MDOMO BAADA YA MADAKTARI WA IKULU YA WHITE HOUSE KUMSHONWA NYUZI 12, MWINGINE NI MLINZI WAKE.

RAIS BARACK OBAMA NA MKEWE MICHELLE WAKIFURAHI.

RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI
NA BBC
RAIS Barack Obama wa Marekani amepata ajali wakati akicheza mpira wa kikapu asubuhi leo Ijumaa  huko Fort McNair Washington DC na kulazimika timu ya madaktari wa Ikulu ya White House imshone nyuzi takribani 12.

Kabla ya kushonwa Rais huyo alilalamika maumivu ya mdomo baada ya kugongana na mmoja wa wachezaji wa timu pinzani walipokuwa kwenye uwanja huo na kusababisha Rais huyo akimbizwe na walinzi wake hadi kwa madaktari hao wa Ikulu.

"Baada ya kuumizwa na mchezaji wa upinzani wa timu nyingine alisikia maumivu makali kwenye mdomo wake wa chini... Rais akalazimika kushonwa nyuzi 12 na jopo la madaktari wa Ikulu ya White House," Msemaji wa ikulu hiyo Bw.Robert Gibbs alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Rais Obama alishonwa nyuzi za kawaida zilizopatikana kwa wakati tukio hilo likitokea nyuzi ambazo zilikuwa ndogo tofauti na zinazohitajika zilizopelekea kushonwa nyingi mdomoni. Kwa habari zaidi dondoka hapa chin
President Obama nursing his injury Mr Obama was seen nursing his injury through a window at the White House
Mr Obama was playing basketball with his personal aide Reggie Love - who played basketball for Duke University - and other members of his family on what is the thanksgiving holiday in United States.
He was photographed in a grey T-shirt and jogging bottoms leaving the basketball facility, holding his bottom lip.
A few hours later, reporters who had gathered on the White House driveway for the arrival of the Christmas Tree saw the president in an upstairs window, pressing what appeared to be a cold compress against his mouth.
The president has been a long time player of the sport, and has even been seen to take to the court with Cabinet members.

More on This Story

Related stories

BREKING NEWS MAWAZIRI WAPYA KUAPISHWA IKULU DAR!!!!

RAIS Jkaya kikwete anatarajiwa kuwaambisha mawaziri na manaibu wake katika sherehe itakayofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Kuapishwa kwa mawaziri hao kunafuatia Rais juzi kutangaza baraza hilo likiwa na sura mpya akiwemo Waziri wa Uchukuzi Eng. Omari Nundu. Vuta subira picha za mawaziri hao wakiapishwa zaja.....................

WAANDISHI WAKIWA KAZINI HUYU NA NOT BOOK HUYU NA CAMERA

MWANDISHI WA GAZETI LA NIPASHE MKOA WA TANGA LULU GEORGE AKICHUKUA 'NOTI' KUTOKA KWA WADAU WA BAHARI KUHUSU SAMAKI WA AJABU SILIKANTI

AIREEN MSUMARI MWANDISHI WA TBC MKOANI TANGA, AKIREKODI TUKIO LA WADAU WALIOKUWA WAKIZUNGUMZIA SUALA LA KUTENGWA ENEO LA KIGOMBEA KUWA HIFADHI YA SAMAKI AINA YA SILIKANTI