Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Wednesday, October 27, 2010

Toledo Sekondari kuanza kufundisha somo la kompyuta

Na Mashaka Mhando,Tanga
SHULE ya sekondari ya Toledo iliyopo katika Jiji la Tanga, itaanza kufundisha wanafunzi wake somo la kompyuta kuanzia mwakani baada ya kupata msaada wa kompyuta zipatazo 37 kutoka kwa marafiki wa shule hiyo kutoka nchini Marekani na Uingereza.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa chumba cha maabara ya kompyuta, Mkuu wa shule hiyo Bw. Samwel Ndauka alisema shule hiyo inayotumia jina la mji mmoja nchini Marekani, alisema kuwa baada ya marafiki wao kuwapa msaada wa vifaa hivyo kisha walimu kupata mafunzo ya kompyuta, kuanzia mwakani watafundisha somo hilo.

Alisema shule hiyo iliyopata msaada wa kompyuta 25 kutoka shule ya sekondari ya Leyton ya nchini Uingereza kisha kupata konpyuta nyingine 12 kutoka shirika la ICT na walimu wao kupata mafunzo ya vifaa hivyo sasa wanalazimika kuanza kufundisha kompyuta kama somo ili wanafunzi waweze kujifunza na kutumia kuwasiliana na marafiki zao waliopo duniani.

Bw. Ndauka alisema dhima ya shule hiyo ni kuiweka katika ulimwengu wa teklonojia ya mawasiliano na kutoa elimu ya kisasa ambapo baada ya kuiweka shule yao katika mtandao waliweza kupata marafiki wa shule za Thomas Hepburn, Leyton na Yarborough ambayo imeifunguliwa shule hiyo tovuti ya http://www.toledo-school.com/.

Akizundua darasa hilo la kompyua Ofisa Elimu Sekondari wa Jiji la Tanga, Bw. kassim Sengasu aliwataka wanafunzi kutumia fursa hiyo ya kusoma vifaa hivyo na wajiepushe matuminzi ya kuingia katika mitandao isiyofaa badala yake wajifunze kuongeza ujuzi wa kompyuta kupitia mitandao ya elimu ili wamalizapo masomo yao waweze kujua matuminzi sahihi ya vifaa hivyo.
MWISHO

No comments:

Post a Comment