Na Mashaka Mhando,Handeni
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Handeni la kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Abdallah Kigoda, amewataka Watanzania wasifanye ushabiki wa kisiasa kwa kuwachagua wapinzani akieleza kwamba sumu haijaribiwi kwa kuonjwa badala yake waendelee kukipa ridhaa chama hicho kwa kumchagua Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi leo.
Akizungumza katika siku ya mwisho ya kampeni ya takribani siku 70 katika kijiji cah Kwenjugo Magharibi B na kwenye uwanja wa CCM wilayani hapa, Dkt Kigoda alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kufahamu kwamba wanatakiwa kwenda kupiga kura leo wakiondoa ushabiki na badala yake wachague chama hicho kwasababu kimejenga misingi imara ya uongozi tangu ngazi ya shina hadi Taifa.
"Usichague upinzani kwa kufanya ushabiki wa kisiasa, ushabiki kweli upo lakini siyo kuuingiza kwenye masuala ya uchaguzi unapofanya ushabiki utakugharimu miaka mitano...Hivi kweli sumu inajaribiwa kwa kuonjwa hebu ndugu zangu mchagueni Rais Kikwete aendelee kuongoza nchi yetu na msipoteze kura zenu," alisema Dkt Kigoda na kuongeza
"CCM imetengeneza ilani ambayo itawawezesha Watanzania wote kupiga hatua katika nyanja mbalimbali na tatizo la maji ambalo limekuwa kero kaika maeneo meni nchini litatatuliwa kwa kiasi kikubwa...Miaka mitano iliyopita serikali imeweza kutekeleza ilani kwa umakini mkubwa, achaneni na wapinzania ambao hawana hata mjumbe wa kitongoji huku vijijini,".
Akizungumzia upinzania katika wilaya hiyo alisema kutokana na mshikamano wa wanachama na wapenzi wa CCM, vyama vya upinzani vilivyopo wilayani humo baada ya uchaguzi vitabaki kujiuliza na kutafuta njia nyingine ya kuwashawishi wananchi kutokana na sera za za kwamba chama hicho hakijafanya kitu na kutukana viongozi walizokuwa wakitumia wananchi hawakuwaelewa na waliwapuuza.
Alisema huwezi mwananchi wa Handeni leo ukimweleza kwamba hakuna kilichofanyika wakati kumekuwepo mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali hatua ambayo wanajivunia tangu alipoingia mwaka 1995 hali hiyo haikuwepo na kwamba ilani ya mwaka huu imeainisha mipango mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara hadi Singida kutokea wilayani humo.
Dkt. Kigoda alisema changamoto iliyokuwepo ya ukosefu wa maji, alisema pamoja na kwamba suala hilo ni la Kitaifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo tatizo hilo litabaki kuwa historia kutokana na ukarabati mkubwa wa mtaro mkubwa wa mradi wa maji wa HTM kutokea eneo la kijiji cha Tabora kilichopo wilayani Korogwe amako ndiko kulikuwa na chanzo, kufanyiwa matengenezo makubwa hadi eneo la Manga.
"Suala la maji mimi na wenzangu (madiwani) ndilo tutakalolifanya katika miaka mitano ijayo, ilani yetu imeaanisha kwamba mradi wa maji wa HTM utakarabatiwa kuanzia pale Tabora hadi Manga baada ya ukarabati na vyanzo vingine kuongezwa tatizo hili litakwisha" alisema Dkt Kigoda.
Nae Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Bw. David Mkude aliwataka wananchi wajiadhari na viongozi wa vyama ya upinzani ambao aliwalinganisha na wachezesha karata tatu mijini kwa kuwatapeli wananchi kwa maelezo ambayo hawawezi kuyafanya badala yake wanaropoka na kukashifu viongozi wa serikali.
MWISHO
No comments:
Post a Comment