Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Friday, August 19, 2011

UHAMIAJI TANGA WAPIMA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA VVU NA UKIMWI

WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI MKOANI TANGA WAKISUBIRI KUPIMA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI NA VVU MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MKOA HUO ENEO LA JIRANI NA MAKTABA.

WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA WAKIMUHOJI KAMISHINA WA UHAMIAJI NCHINI DKT KAHAMBA JUU YA NAMNA IDARA HIYO ILIVYOAMUA KUWAPIMA WATUMISHI WAKE NCHI NZIMA.

"...HAPA TUNATAKA KUJUA IDADI YA WATUMISHI WETU WALIOATHIIKA ILI TUWEZE KUTEKELEZA WARAKA WA SERIKALI WA MWAKA 2007 JUU YA KUWATUNZA NA KUWALEA WATUMISHI WANAOISHI NA VVU NA UKIMWI...," ALISEMA KAMISHINA KAHAMBA

"...YAANI TUMEKUJA HADI HAPA KUWAPIMA HALAFU WASIJE HAPA MBONA TUTAWACHUKULIA HATUA WATUMISHI AMBAO HAWATAKI JAPO SUALA HILI NI HIARI LAKINI TUMEAMUA SISI KAMA SEHEMU YA JESHI BASI TUPIMANE BILA KUOGOPANA,..."

WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI MKOANI TANGA WAKIWA WAMEKAA KILA MMOJA AKIONGEA LAKE JUU YA KUINGIA KWA MAMA MNASIHI NASAHA HUMO NDANI ILI KUPIMA MAAMBUKI HAYO

Thursday, August 18, 2011

JENGO LA WATU WENYE VVU NA UKIMWI LAZINDULIWA BOMBO

MGANGA MKUU WA MKOA WA TANGA DKT ALLY ULEDI AKISOMA RISALA KATIKA UFUNGUZI WA JENGO LA KLINIKI YA MATUNZO NA MATIBABU YA WATU WENYE VVU NA UKIMWI KATIKA HOSPITALI YA BOMBO MKOANI TANGA.

BAADHI YA WATU MBALIMBALI WALIOFIKA KWENYE UZINDUZI HUO WA KLINIKI HIYO YA WAGONJWA WA VVU NA UKIMWI WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI AMBAPO KUSHOTO NI LULU GEORGE WA NIPASHE NA ANYEFUATA NI FATMA MATULANGA WA TBC.

MWAKILISHI WA SHIRIKA LA KIMARAEKANI CDC DKT STEFAN WIKTOR AKITOA SALAMU KUTOKA KWA WATU WA MAREKANI AMBAO WAMEFADHILI MRADI HUO WA UJENZI WA JENGO HILO KATIKA HOSPITALI HIYO  ALITEINAMA NI WAZIRI WA FYA DKT HADJI MPONDA NA PEMBENI YAKE NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. BENEDICTOR OLE KUYAN.

MEYA WA JIJI LA TANGA BW. OMARI GULEDI AKIHITIMISHA UZINDUZI HUO KWA KUELEZA KWAMBA ILI KUONDOA MRUNDIKANO WA WAGONJWA KAIKA HOSPITALI HIYO YA BOMBO, HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAPO MBIONI KUJENGA HOSPITALI YA WILAYA ENEO LA MASIWANI.

HAKUNA SHEREHE YA UZINDUZI IKAKOSA BURUDANI HAPA NI KIKUNDI CHA CASSA DANCING TROUPE WAKITOA BURUDANI KWA WAGENI MBALIMBALI WALIOFIKA KUSHUHUDIA UZINDUZI HUO

Tuesday, August 16, 2011

WACHINA WAANZA KUWEKA LAMI BARABARA YA TANGA/HOROHORO

ENEO LA BARABARA ILIYOANZA KUWEKWA LAMI NA KAMPUNI YA SINOHYDRO YA CHINA INAYOJENGA BARABARA YA TANGA/HOROHORO KWA KIWANGO CHA LAMI, HAPA NI ENEO LA MPERANI.

SEHEMU YA BARABARA ILIYOWEKWA TABAKA YA KWANZA YA LAMI (LEAYER) HII NI ENEO LA MTIBWANI AMBAYO TAYARI NAYO IMEWEKWA LAMI.

ENEO LA MPERANI LINAVYONEKANA KATIKA PICHA. NDUGU MSOMAJI WA BLOGU HII YA WATU NA MATUKIO YA MZEE WA BONDE, BARABARA HII HAWA WACHINA TAYARI WAMEANZA KUWEKA TABAKA YA KWANZA YA LAMI KATIKA ENEO KUANZIA MIKOCHENI AMBONI, HADI KUKARIBIA MTIMBWANI KWA KWELI BARABARA INAPENDEZA NA IKIMALIZIKA HOROHORO HADI MOMBASA ITAKUWA NI MASAA MAWILI TU KAMA MPAKANI HUTACHELEWESHWA.

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA MPAKANI MWA TANZANIA NA KENYA

OFISA USHURU NA FORODHA KATIKA MPAKA WA HOROHORO BW. DAVID KAMUKULA, AKIWAELEZA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA NAMNA WALIVYOWEZA KUDHIBITI UPITITAJI WA MAHINDI KWENDA NJE YA NCHI KAMA ILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.

BAADHI YA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOANI TANGA kutoka kushoto ni MRAKIBU MWANADAMIZI WA POLISI BW. NDAKI, DAVID LENGIA OFISA WA TAKUKURU NA BW. JOSEPH SEMWAIKO OFISA USALAMA WA TAIFA KUTOKA OFISI YA MKOA, WAKIMSIKILIZA MKUU WA IDARA YA USHURU NA FORODHA KATIKA ENEO LA HOROHORO.

KINU HIKI UNACHOKIONA HAPA CHINI NI NYUMBA AMBAYO IPO KENYA NA JIWE LILE KULEEE KUSHOTO NI NYUMBA YA TANZANIA NA BARABARA HII NDIYO WANANCHI WAMEACHA KAMA MPAKA UNAOGAWA NCHI YA TANZANIA NA KENYA LAKINI SHERIA INASEMA KWAMBA KUTOKA JIWE LA MPAKA HADI MAKAZI YA NCHI INATAKIWA WAACHE KIASI CHA MITA 200 LAKINI WANANNCHI HAWA WAMEAMUA KUJENGA KABISA KWENYE ENEO AMBALO NI NOMASSY LAND KAMA UNAVYOONA HAPA PICHANI.

MAKAZI WA KIJIJI CHA JASINI KILICHOPO KATIKA KATA YA MAYOMBONI WILAYANI MKINGA BI MWANAMKASI MBWANA NAYEMENYA MIHOGO NA NDUGU YAKE MWANAUANI, WAKITAYARISHA FUTARI YAO KATIKA ENEO AMBALO NI LA NCHI YA KENYA, HII INATOKANA NA WANANCHI HAWA KUJENGA KABISA MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA.

BAADHI YA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA TANGA WAKIWA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA JASINI AMBAKO WALIKWENDA KUFUATILIA NAMNA UVUSHAJI WA MAHINDI KWENDA NCHI JIRANI YA KENYA UNAVYOFANYWA KWA NJIA ZA PANYA KATIKA KIJIJI HICHO.

BAADHI YA MAOFISA HAO WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WAKIWA KATIKA ENEO LA BAHARI AMBALO NI NDANI KABISA YA KENYA WAKIANGALIA NAMNA WATU WANAVYOWEZA KUVUKA KUPELEKA BIDHAA AMBAZO HAZIJALIPIWA USHURU NA KUINGIZA BIDHAA AMBAZO HAZILIPIWI USHURU KUTOKA ENEO LA VANGA NCHINI KENYA.

BAADHI YA MAOFISA HAO WAKIZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA JASINI KUHUSIANA NA NAMNA WANAVYOWEZA KUDHIBITI UVUSHAJI WA MAHINDI NA BIDHAA AMBAZO HAZIJALIPIWA USHURU KATIKA ENEO HILO LA BAHARI MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA.

MUVI-SIDO WAZINDUA JARIDA LA NURU YA MAFANIKIO KWA WAJASIRIAMALI

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA ANAYESHUGHULIKIA HUDUMA ZA JAMII BW. NDIBALEMA KISHERU AKIZINDUA SHUGHULI ZA WADAU WA HABARI WA MRADI WA MUVI ULIOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA YCDP JIJINI TANGA, kushoto ni MENEJA WA SIDO MKOANI TANGA BW. SELEMANI MTANI NA kulia ni BW. JOSEPH MAKAZA MKURUGENZI WA HABARI WA MUVI.

WADAU WA HABARI NA MAWASILIANO WAKIFUATILIA KWA MAKINI UZINDUZI WA MRADI WA MUVI 

MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI HUO BW. NDIBALEMA KISHERU AMBAYE NI KATIBU TAWALA MKOANI TANGA (katikati) AKIJIANDAA KUKATA KAMBA MAAMULU YA KUZINDUA JARIDA LENYE HABARI ZA MAMBO MBALIMBALI KUHUSU HABARI ZA MASOKO KWA WAJASIRIAMALI NCHINI. WENGINE kushoto ni MKURUGENZI WA HABARI WA MUVI JOSEPH MAKANZA NA kulia ni BW. SELEMANI MTANI MENEJA WA SIDO

KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. NDIBALEMA KISHERU (katikati) AKISOMA JARIDA LA MRADI WA MUVI MARA BAADA YA KULIZINDUA HUKU MENEJA WA SIDO MKOANI TANGA BW. SELEMANI MTANI AKILIONESHA KWA WADAU WALIOHUDHURIA HAFLA HIYO YA UZINDUZI ILIYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA YCDP.

MAMBO YA MPAKANI FUTARI YAANDALIWA KENYA, YAPIKWA TANZANIA

MWANAMKASI MBWANA (anaye menya mihogo) MKAZI WA KIJIJI CHA JASINI KILICHOPO KATA YA MAYOMBONI WILAYANI MKINGA, AKITAYARISHA FUTARI YAKE YA MUHOGO AKIWA KATIKA MTI WA KIVULI AMBAO UPO NCHINI KENYA KISHA AKITAYARISHA FUTARI HIYO ANA KWENDA NYUMBANI KWAKE (NYUMA ALIKOKUPA MGONGO) HUKU ANAKOANGALIA NI KENYA MGONGONI KWAKE NI TANZANIA. MSOMAJI WA PICHA HII UKIANGALIA KWA MBALI PALE KWENYE UWA WA MAKUTI PANA JIWE JIWE HILO NI MPAKA KATI YA KENYA NA TANZANIA, SASA MWANAMKASI NA MDOGO YAKE MWANAUANI HAPA WANAPOTAYARISHA MUHOGO NI KENYA.

Thursday, August 11, 2011

KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHAZINDULIWA

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA BW. KIROBOTO AKIWA MMOJA YA WATU WALIHUDHURIA UFUNGUZI WA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA CASA KILICHOPO ENEO LA RASKAZONE

Monday, August 8, 2011

ASKOFU ANTHONY BANZI AZINDUA HUDUMA MPYA YA X-RAY TUMAINI HOSPITALI

MHASHAMU ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO KUU LA TANGA, ANTHONY BANZI AKIKATA UTEPE KUFUNGUA KITENGO KIPYA CHA IDARA YA MIONZI (X-RAY) KATIKA KITUO CHA AFYA TUMAINI. KUSHOTO KWAKE NI SISTER FROLA MUSHI MKUU WA KITUO HICHO.

JEWE LA MSINGI LA JENGO JIPYA LA IDARA YA MIONZI (X-RAY) TUMAINI HOSPITALI

MASHINE MPYA YA KISASA YA MIONZI (X-RAY) ILIYOZINDULIWA TUMAINI HOSPITALI

MASISTER WA JIMBO KUU LA KANISA KATOLIKI TANGA WAKIWA MIONGONI WALIOHUDHURIA UZINDUZI HUO

MTAALAMU WA IDARA YA MIONZI KATIKA HOSPITALI YA MKOA BOMBO DKT MATABA (kushoto) AKINONG'ONEZANA JAMBO NA MKURUGENZI WA WALEI WA KANISA HILO BW. SYLEVESTER MGOMA KATIKA UZINDUZI HUO

WATU MBALIMBALI NA WAFANYAKAZI WA KITUO HICHO CHA TUMAINI WAKIFUATILIA UZINDUZI HUO.

KATIBU WA KANISA KATOLIKI JIMBO KUU LA TANGA, SELESTIN KAGABA (wa kwanza kushoto) AKIFUATILIA KWA KARIBU UZINDUZI HUO

WAUGUZI WA KITUO HICHO NAO WALISHEHENESHA SHEREHE HIZO KWA KUHUDHURIA HUKU WAKIPIGA VIGELELE KILA ASKAFU ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NENO LA FARAJA KWAO NA HOSPITALI HIYO.

WATU WA KILA AINA WALIFIKA KWENYE UZINDUZI HUO

ALIYEVAA FULANA YA VIJUMBA JUMBA NI MTANGAZAJI WA REDIO ONE NA ITV MKOANI TANGA WILLIAM MNGAZIJA AKIFUATILIA KWA MAKINI UZINDUZI HUO PAMOJA NA WATU WENGINE MBALIMBALI.

Friday, August 5, 2011

CRDB YAWASAIDIA WAKULIMA WA KILIMO CHA MPUNGA KOROGWE

AOFISA WA BENKI YA CRDB LA MKOANI TANGA AKIANGALIA MOJA YA MASHAMBA YA MPUNGA WILAYANI KOROGWE AMBAYO BENKI HIYO IMEKUWA IKISAIDIA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KUWAINUA WAKULIMA. 



MFEREJI WA MAJI YANAYOKWENDA KWENYE MASHAMBA YA MPUNGA AMBAO UMEKARABATIWA KWA MAMILIONI YA FEDHA KWA AJILI YA KUWASAIDIA WAKULIMA WA MPUNGA WILAYANI KOROGWE KULIKOFANYWA NA BENKI HIYO YA CRDB


Monday, August 1, 2011

MWEZI UMEANDAMA WAISLAMU WOTE LEO WATAKUWA NA SWAUMU


TUNAWATAKIWA KILA LA KHERI WAISLAMU WOTE NA WAPENZI WA BLOGU HII YA WATU NA MATUKIO YA MZEE WA BONDE KATIKA MFUNGO HUU WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI AMBAO UMEANDAMA NA SIKU 29 SHAABANI HIVYO KUANZIA AUGOSTI MOSI WAISLAMU WOTE WA AFRIKA MASHARIKI WATAANZA KUFUNGA, TUNAWATAKIWA MFUNGO MWEMA NA MUNGU AWAEPUSHIE SABABU MBALIMBALI ZA KUACHA KUFUNGA KWA VYOVYOTE VILE, AMEEN.

Sunday, July 31, 2011

YANGA YAIKACHA COASTAL LEO KUOGOPA MAKWANJA

MABINGWA WA SOKA TANZANIA BARA, YANGA SPORTS CLUB WAMEINGIA MITINI KWA KUAHIRISHA MCHEZO WAO WA KIRAFIKI DHIDI YA 'WAGOSI WA KAYA' COASTAL UNION AMBAYO KWA SASA IPO FITI ASILIMIA 90 KUKABILIANA NA MIKIMIKI YA LIGI KUU YA VODACOM ITAKAYOANZA MWEZI UJAYO. YANGA WAMEAAHIRISHA MECHI HIYO WAKIELEZA KWAMBA KUCHEZA MCHEZO HUO KUTAVURUGA MAANDALIZI YAO YA MCHEZO WA NGAO YA HISANI HAPO AGOSTI 17 MWAKA HUU WATAKAPOCHEZA NA WAPINZANI WAO WAKUBWA SIMBA. HATA HIVYO HABARI ZILIZOZAGAA KATKA MITAA YA NGAMIANI ZINASEMA YANGA WAMEUKACHA MCHEZO HUO ULIOKUWA UPIGWE LEO KWENYE UWANJA WA CCM MKWAKWANI, KUTOKANA NA KUAMINI KWAMBA COASTAL NA SIMBA NI KITU KIMOJA HIVYO WACHEZAJI WA COASTAL WANAWEZA KUTUMIWA NA UONGOZI WA SIMBA KUWAAMUMIZA WACHEZAJI WAO ILI WASHINDWE KUCHEZA VYEMA SIKU HIYO YA NGAO YA HISANI, MANENO HAYO!!! 

HATIMAYE UBINGWA WA POOL WATOKA DAR WAENDA DODOMA

MBUNGE WA KIBAKWE MH. GEORGE SIMBACHAWENE (kulia) AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA FAINALI YA MASHINDANO YA SAFARI LAGER NATIONAL POOL CHAMPIONSHIRP MJINI DODOMA, AKIMKABIDHI MMOJA WA VIONGOZI WA MKOA WA DODOMA AMBAO WAMEKUWA MABIGWA WA MWAKA 2011

MGENI RASMI MH. GEORGE SIMBACHAWENE (MP) WA KIBAKWE AKIMKABIDHI KITITA CHA SH. MILIONI 5 KWA NAHODHA WA TIMU YA POOL YA MKOA WA DODOMA AMBAYO IMETWAA UBINGWA MWAKA HUU BAADA YA KUIFUNGA KINONDONI AMBAO NI MABIGWA WA MWAKA JANA, UBINGWA WALIOUTWAA JIJINI ARUSHA.

MWENYEKITI WA POOL TAIFA BW. ISAACK TCHOGOSHO AKIMKABIDH KITITA CHA SHILINGI MILIONI KIONGOZI WA MKOA WA MWANZA AMBAO WAMETWAA USHINDI WA TATU KATKA MASHINDANO HAYO.

MABINGWA WAPYA WA MASHINDANO YA SAFARI LAGER NATIONAL POOL CHAMPIONSHIRP MKOA WA DODOMA.

Saturday, July 30, 2011

BILION 121 ZAHITAJIKA KUKARABATI MRADI WA MAJI WA HTM HANDENI

ADAM MGANGA MPIGA NGOMA YA UFUNGILO AKIASHIRIA KUANZA KWA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI, JULY 28 MWAKA HUU.

WAHESHIMIWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI WAKIWA KATIKA MKUTANO WAO WA BARAZA LA MADIWANI (FULL-COUNCIAL) WILAYANI HANDENI.

WAGENI WAALIKWA, WATENDAJI NA WAANDISHI WA HABARI WAKIFUATILIA KIKAO HICHO AMBACHO PAMOJA NA MAMBO MENGINE WALIZUNGUMZIA SUALA LA UKOSEFU WA MAJI KATKA WILAYA HIYO AMBAPO MENEJA WA MRADI WA MAJI WA HTM INJINIA ALEX MSILANGA ALISEMA MRADI HUO UNAHITAJI KIASI CHA SHILINGI BILIONI 121 UKARABATI WAKE ILI KUTATUA TATZO LA MAJI HANDENI.

MADIWANI WAKIFUATILIA MKUTANO HUO WA BARAZA LA MADIWANI NA KUCHANGIA HOJA MBALIMBALI.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI BW. HASSAIN MWACHIBUZI (kulia), MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO BW. RAMADHANI DILIWA NA KULIA KWAKE NI MAKAMO WAKE.

NGOMA YA UFUNGILO HANDENI

ADAM ATHUMANI MGANGA MPIGA NGOMA YA UFUNGILO INAYOASHIRIA KUANZA KWA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI, MGANGA ALIANZA KUPIGA NGOMA HII TANGU MWAKA 1979 HADI SASA BAADA YA KUIRITHI KUTOKA KWA MZEE JUMA KIGWADUKE.

Tuesday, July 26, 2011

KAZI YA BWANA AFYA WA JIJI AIFANYA KALEMBO, UWASA HARAKA WAUZIBUA MFEREJI ULIOKUWA UKITIRIRISHA MAJI BARABARANI

MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI SAIDI KALEMBO AKIANGALIA NAMNA JIJI WASIVYOWEZA KUZIBUA MITARO AMBAYO INAWEZA KULETA MAGONJWA YA MILIPUKO. HAPA NI SEHEMU YA HOTELI YA SALZ NYUMA YA HOTELI YA SP JIRANI KABISA NA MLANGO WA KUINGILIA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA.

KALEMBO ATEMBELEA MFEREJI AFRITEX (CIC) UNAOMWAGA KEMIKALI ZA SUMU

MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOANI TANGA, MEJA JENERALI SAID KALEMBO (MWENYE TAI KATIKATI YA PICHA) AKIONYESHWA MFEREJI MAMA WA JIJI AMBAO HUANZIA KWENYE KIWANDA CHA AFRITEX NA KUTITIRISHA MAJI YANAYODAIWA KUWA NA KEMIKALI ZA SUMU.



Na Mwandishi Wetu,Tanga
MKUU wa mkoa wa Tanga Meja Jererali (Mstaafu), Said Kalembo ameuagiza uongozi wa Jiji la Tanga kuchukua hatua za haraka juu ya tatizo la viwanda vinavyotiririsha maji yenye kemikali na kusababsiha madhara kwa binadamu katika mfereji mama unaopita kata sita za Jiji hilo  kwenda baharini, unapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Akizungumza juzi wakati mkuu huyo na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya mkoa walipotembelea mfereji huo kuona namna maji yanayodaiwa kuwa na kemikali yakimwagwa kutoka viwandani na kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine wanaotumia mfereji huo kuufanyia usafi.

Awali Ofisa Afya wa Jiji hilo, Yusuph Gumbo akimsomea taarifa mwenyekiti huyo wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, alisema kuwa Julai 11 mwaka huu vibarua 14 waliokuwa wakifanya usafi kwenye mfereji huo kwa kuingia katikati, walipata madhara makubwa ya kuungua miguuni kwa kubabuka ngozi baada ya kuingiwa na maji yanayodhaniwa kuwa kemikali zenye sumu.

Alisema vibarua hao walipokuwa wakisafisha mfereji huo wenye urefu wa kilomita nane, licha ya kuvaa viatu virefu (Gum Boots) hata hivyo maji ya mfereji huo yaliwaingia na kujisikia kuwashwa baada ya muda wa masaa mawili walipotoka katika mfejei huo na kisha kuanza kubabuka na hali zao kuwa mbaya.

“Kwa vile vibarua wale walikuwa wakipokezana kuingia ndani ya mfereji  waliamua kutoka ili wenzao wengine waingie waendelee na usafi, lakini wale waliotoka mferejini baada ya kuvua viatu muwasho ulizidi na mmoja kati yao ambaye aliungua vibaya na ngozi ilibabuka na kufanya awe na vidonda kuanzia magotini hadi miguuni,” alisema Gumbo.

Aliongeza kwamba mfereji huo uliojengwa miaka ya 1970 kwa ajili ya kusaidia kutoa maji ya mvua na kuyapeleka maharini lakini sasa umekuwa ukitumiwa na viwanda kumwaga mabaki ya takataka zao na kuvitaja viwanda hivyo kuwa ni kiwanda cha nguo cha Afritex, Kiwanda cha kusindika samaki cha Sea Food Products, Kiwanda cha foma, Kiwanda cha Vioo (Tansilica), karakana ya Tanroads na karakana za magari zilizopo eneo la viwanda Gofu.

Hata hivyo, alisema hatua ambazo halmashauri ya jiji imechukua hadi sasa ni kuwapa notisi ya kisheria wenye viwanda hivyo na kuwataka kuwa na mitambo ya kusafishia majitaka wanayoyatiririsha kabla ya kumwagwa baharini na kiwanda cha Afritex tayari kimenunua mtambo huo lakini bado haujaanza kusafisha maji hayo.

Mwana mazingira wa Envirocare Haika mcharo ambaye ni ofisa habari wa taasisi hiyo inayojihusisha na suala la mazingira hapa nchini, alimweleza Mkuu wa huyo wa mkoa katika ziara hiyo kwamba serikali inatakiwa kuchukua hatua juu ya tatizo hilo kwa ajili ya kulinda viumbe hai vya baharini na binadamu na wananchi wanaoishi pembezoni mwa mfereji huo.

“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa kabla ya kufanya ziara hapa na kamati yako, juzi (Alhamisi) nilitembelea kiwanda cha Afritex nikiwa na waandishi wa habari kuona namna kiwanda hiki kinavyojiendesha hasa sual la mazingira tumeona maji yao wanayoyatitiisha lakini tunadhani wakati mwingine maji yanakuja kwenye mfereji huu bila kusafisha, ni vema serikali ya mkoa ikatilia mkazo suala hili mapema kabla ya athari kubwa haijapatikana,” alisema mcharo.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa mkoa alimwagiza viongozi wa Jiji pamoja na Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi kuhakikisha wanachukua hatua za haraka ikiwezekana kuvifungia viwanda walivyobainika kumwaga kemikali hizo zenye sumu kwani tayari madhara kiafya yamepaikana kwa vibarua hao waliobabuka ngozi kuliko kukaa na kulalamikia suala hilo.
MWISHO

MSHIKE MSHIKE WA KUDAKA ABIRIA STENDI YA TANGA

WAPIGA DEBE STENDI YA TANGA WAKIMNG'ANG'ANIA ABIRIA (DADA ALIYEKUWA NA KIPOCHI MWENYE ALIYEVAA SURUALI NYEUSI) KUPANDA KWENYE MABASI YAO KILA MMOJA AKITAKA KUMKATIA TIKETI YA KWENDA MOROGORO LEO ASUBUHI.