Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, August 16, 2011

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA MPAKANI MWA TANZANIA NA KENYA

OFISA USHURU NA FORODHA KATIKA MPAKA WA HOROHORO BW. DAVID KAMUKULA, AKIWAELEZA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA NAMNA WALIVYOWEZA KUDHIBITI UPITITAJI WA MAHINDI KWENDA NJE YA NCHI KAMA ILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.

BAADHI YA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOANI TANGA kutoka kushoto ni MRAKIBU MWANADAMIZI WA POLISI BW. NDAKI, DAVID LENGIA OFISA WA TAKUKURU NA BW. JOSEPH SEMWAIKO OFISA USALAMA WA TAIFA KUTOKA OFISI YA MKOA, WAKIMSIKILIZA MKUU WA IDARA YA USHURU NA FORODHA KATIKA ENEO LA HOROHORO.

KINU HIKI UNACHOKIONA HAPA CHINI NI NYUMBA AMBAYO IPO KENYA NA JIWE LILE KULEEE KUSHOTO NI NYUMBA YA TANZANIA NA BARABARA HII NDIYO WANANCHI WAMEACHA KAMA MPAKA UNAOGAWA NCHI YA TANZANIA NA KENYA LAKINI SHERIA INASEMA KWAMBA KUTOKA JIWE LA MPAKA HADI MAKAZI YA NCHI INATAKIWA WAACHE KIASI CHA MITA 200 LAKINI WANANNCHI HAWA WAMEAMUA KUJENGA KABISA KWENYE ENEO AMBALO NI NOMASSY LAND KAMA UNAVYOONA HAPA PICHANI.

MAKAZI WA KIJIJI CHA JASINI KILICHOPO KATIKA KATA YA MAYOMBONI WILAYANI MKINGA BI MWANAMKASI MBWANA NAYEMENYA MIHOGO NA NDUGU YAKE MWANAUANI, WAKITAYARISHA FUTARI YAO KATIKA ENEO AMBALO NI LA NCHI YA KENYA, HII INATOKANA NA WANANCHI HAWA KUJENGA KABISA MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA.

BAADHI YA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA TANGA WAKIWA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA JASINI AMBAKO WALIKWENDA KUFUATILIA NAMNA UVUSHAJI WA MAHINDI KWENDA NCHI JIRANI YA KENYA UNAVYOFANYWA KWA NJIA ZA PANYA KATIKA KIJIJI HICHO.

BAADHI YA MAOFISA HAO WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WAKIWA KATIKA ENEO LA BAHARI AMBALO NI NDANI KABISA YA KENYA WAKIANGALIA NAMNA WATU WANAVYOWEZA KUVUKA KUPELEKA BIDHAA AMBAZO HAZIJALIPIWA USHURU NA KUINGIZA BIDHAA AMBAZO HAZILIPIWI USHURU KUTOKA ENEO LA VANGA NCHINI KENYA.

BAADHI YA MAOFISA HAO WAKIZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA JASINI KUHUSIANA NA NAMNA WANAVYOWEZA KUDHIBITI UVUSHAJI WA MAHINDI NA BIDHAA AMBAZO HAZIJALIPIWA USHURU KATIKA ENEO HILO LA BAHARI MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA.

No comments:

Post a Comment