Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Friday, April 8, 2011

KALEMBO ATEMBELEA KIVUKO PANGANI KILICHOGONGWA

MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI (MSTAAFU) SAID KALEMBO AKIPATA MAELEZO KUTOKA KWA MTAALAMU WA KIVUKO CHA MTO PANGANI ABACHO KIMEGONGWA NA GARI LILILOPOTAKA KUTOKA KAIKA KIVUKO HICHO.

Thursday, April 7, 2011

OLE KUYAN AZINDUA MRADI WA MAJI PANGANI

MWANAKIJIJI CHA UBANGAA KILICHOPO WILAYANI PANGANI MKOANI TANGA, AKIMSOMEA KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. BENEDICT OLE KUYAN TAARIFA YA MRADI WA MAJI SAFI YA KUNYWA KWA WANANCHI WA KIJIJI HICHO KATIKATI NI MKUU WA WILAYA YA PANGANI BI ZIPORA PANGANI

KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. BENEDICT OLE KUYAN AKIZINDUA MRADI WA MAJI WA KIJIJI CHA UBANGAA KILICHOPO WILAYANI PANGANI HIVI KARIBUNI.

BAADA YA KUZINDUA MRADI WA MAJI KAIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. BENEDICT OLE KUYAN ALIMBANDIKA NDOO YA MAJI MAMA MMOJA KIJIJINI HAPO KAMA ISHARA YA KUZINDUA MRADI HUO.

Friday, March 4, 2011

MWANAMKE KUJIREMBA NA KUJIPAMBA

RAISA SAID AKICHAGUA UREMBO WA KUVAA NA KUJIPAMBA MWANAMKE KWENYE VIWANJA VYA TANGAMANO KULIKOFANYIKA SHEREHE ZA WIKI WA WALEMAVU.

MZUNGU AMBAYE JINA LAKE HALIKUPATIKANA MARA MOJA NAYE PIA ALIVUTIWA NA UREMBO WA KUJIPAMBA MWANAMKE ALIPONUNUA ILI NAYE AWE KAMA MWAFRIKA.

RAISA SAID NA RAFIKI YAKE WA KIZUNGU WAKIKUMBATIANA BAADA YA KILA MMOJA KUNUNUA UREMBO WA KUJIPAMBA MWANAMKE KWENYE VIWANJA HIVYO VYA TANGAMANO.

Monday, February 7, 2011

JAJI KIPENKA ATAKA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAWAELEWESHE WANANCHI TARATIBU ZA KIMAHAKAMA

WAKUU WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WALIKUWEPO KATIKA SHEREHE YA SIKU YA SHERIA NCHINI AMBAPO MGENI RASMI ALIKUWA JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA, JAJI MUSSA KIPENKA.

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA, JAJI MUSSA KIPENKA AKIZUNGUMZA KWENYE SHEREHE YA SIKU YA SHERIA ILIYOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA MAHAKAMA JIJINI TANGA.


HAKIMU MKAZI MFAWIDHI WA MAHAKAMA YA WILAYA MKOANI TANGA RM INCHARGE MR. CHUMA AKITOA UFAFANUZI WA MAMBO MBALIMBALI KUHUSU SIKU YA SHERIA ILIPOFANYIKA JIJINI TANGA.

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga, Jaji Mussa Kipenka, amewataka watumishi wa mahakama nchini kuwaelewesha wananchi kuhusu taratibu mbalimbali za mahakama wakati mchakato wa kutoe elimu kwa jamii ukiandaliwa.

Akizungumza katika siku ya sheria iliyofanyika kwenye viwanja vya mahakama Kuu kanda ya Tanga, Jaji Kipenka alisema wananchi kutokana na kutokujua taratibu za mahakama wamekuwa wakipoteza muda mwingi kutafuta haki ama kufungua kesi au kukata rufaa kuitafuta haki katika mamlaka zisizohusika.

“Changamoto kubwa iliyopo mbele yetu ni kuboresha eneo hili la elimu kwa umma ili taratibu na shuguli za mahakama ziwe wazi kwa wananchi…Hivyo ni vema sasa watumishi na watendaji wote wa mahakama wawajibike kwa kutoa maelekezo kwa wananchi kuhusu taratibu za mahakama pale zinapohitajika,” alisema Jaji Kipenka.

Hata hivyo, Jaji huyo alikiri kuwepo kwa tatizo la kuhusiana na sheria ya mwenendo wa mashauri ya kesi za madai ambazo amedai kutokana na taratibu zake imekuwa ni vigumu kueleweka hasa kwa mwananchi ambaye hajasomea fani ya sheria.

Akifafanua Jaji Kipenka alisema kwa kiwango kikubwa mapungufu yaliopo katika sheria hiyo yamekuwa yakisababisha ‘wadaawa’ (wanaofungua kesi za madai) kutofahamu hatua muhimu za kuchukua kabla au baada ya kufungua mashauri hayo ambayo wengi wamekuwa wakikosea sana.

“Elimu kwa umma ni changamoto kubwa kwa mahakama ya Tanzania na ipo haja ya kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na mahakama kuanzisha programu mahususi ya elimu kwa umma ili kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli zetu za kimahakama,” alisema Jaji Kipenka.

Katika sherehe hiyo iliyoongozwa na kuandaliwa vema na Msajili Mfawidhi wa wilaya wa mahakama Kuu kanda ya Tanga, Bw. Benedict Mwingwa, kauli mbiu yake kwa mwaka huu ilikuwa ni “Umuhimu wa elimu kuhusu mahakama kama hatua ya msingi ya utatuzi wa migogoro katika jamii”.

Wednesday, February 2, 2011

JANUARY MAKAMBA KUZINDUA MPANGO WA KUPATA KERO ZA JIMBO LAKE KUPITIA SMS KUTOKA KWA WANANCHI WAKE

Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya SMS Kati ya Wananchi wa Bumbuli na Mbunge wao, Ndugu January Makamba, yamezinduliwa tarehe 29 Januari 2011 kwenye Semina Elekezi aliyoitisha Mbunge huyo wa viongozi na watendaji wa vijiji na Kata wapatao 250 wa Jimbo la Bumbuli.

Mfumo huo utaanza kutumika tarehe 10 Februari 2011, baada ya kipindi cha elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya mfumo kuu kukamilika. Kwa kifupi, wananchi wanapaswa kutuma kero, maoni na ushauri kwa Mbunge ambaye kila siku, yeye na wasaidizi wake, watakuwa wanasoma meseji hizi na kuwajibu au kuwatafutia majibu.

Kama kuna taarifa za haraka ambazo inabidi Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri, au Mkuu wa Polisi wa Wilaya au Bwana Afya inabidi azijue, basi Mbunge atasaidia kuzifikisha kwa haraka zaidi. Huduma hii haiondoi haja ya Mbunge kuendelea kutembelea Jimbo na kuonana na watu wake. Ni kwamba, simu au SMS, kama njia rahisi ya mawasiliano, hakuna haja ya kuacha kuitumia wakati wananchi wenyewe wanaitumia sana.

 Inawezekana ikaonekana ni gharama kubwa kwa Mbunge lakini hata haiko hivyo, ni suala ya mazungumzo kati ya Mbunge na mitandao ya simu ili gharama iwe at cost na Mbunge bado anaweza kugharamia hili kwa nusu ya posho yake (wapo Wabunge ambao wamejitolea nusu mshahara kwa jambo moja au jingine - kwa Mbunge wa Bumbuli hili ni muhimu).

Saturday, January 29, 2011

KALEMBO AFUNGA MAFUNZO YA OPERESHENI UZALENDO MGAMBO JKT

MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI (MSTAAFU) SAID KALEMBO AKISAINI KITABU CHA WAGENI MARA BAADA YA KUFIKA KWENYE OFISI KUU YA KAMBI YA 835 KJ MGAMBO JKT WILAYANI HANDENI ALIPOKWENDA KUFUNGA MAFUNZO YA OPERERESHENI /UZALENDO'.


WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA NA WAGENI WENGINE WALIOALIKWA KUHUDHURIA UFUNGAJI WA MAFUNZO HAYO KWENYE KAMBI HIYO YA 835 KJ MGAMBO JKT.


MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI (MSTAAFU) SAID KALEMBO AKIKAGUA GWARIDE LA VIJANA WANAOMALIZA MAFUNZO YA OPERESHENI UZALENDO KATIKA KAMBI YA 835 KJ MGAMBO JKT WILAYANI HANDENI.


VIJANA WANAOMALIZA MAFUNZO YA OPERESHENI UZALENDO WAKIPITA KWA MWENDO WA KASI NA KUTOA HESHIMA KWA MGENI RASMI AMBAYE NI MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI MSTAAFU SAID KALEMBO.


VIJANA WAKILA KIAPO CHAO CHA UTII KWA TAIFA MARA BAADA YA KUMALIZA MAFUNZO YAO YA OPERESHENI UZALENDO.


Wednesday, January 26, 2011

BIASHARA ZA MITAANI KATIKA JIJI ZINAVYOONEKANA

BIASHARA MITAANI.

MANCHESTER HAISHIKIKI LIGI KUU UINGEREZA

DIRTIMIR BERBATOV AKISHANGILIA GOLI LA TATU NA USHINDI AKIWA PAMOJA NA MCHEZSAJI MWENZAKE CHOICHARITO.

CHICHARITO AKISHANGILIA GOLI LA KUSAWAZISHA LA MANCHESTER KABLA YA BERBATOV KUHITIMISHA GOLI LA USHINDI KWA TIMU YAKE.

Tuesday, January 25, 2011

LUTINDI INAVYOPONESHA WAGONJWA WA AKILI

MJI WA BERTHANIA ULIOPO KIJIJI CHA LUTINDI WILAYANI KOROGWE


MGONJWA WA AKILI ALIYEJITAMBULISHA KWA JINA LA HAMISI MKAZI WA NEGERO WILAYANI KILINDI AKIWA KATIKA DUKA MOJA LILILOPO JIRANI NA HOSPTALI YA WAGONJWA WA AKILI KATIKA KIJIJI CHA LUTINDI. WENGINE PICHANI NI WAANDISHI MNGAZIJA, LULU NA AFISA KILIMO NA MIFUGO WA KATA YA BUNGU, KILENGAWANA.


MGONJWA WA AKILI HAMISI AKIWA AMEPOZI KWA MAJIRANI ZAKE JIRANI NA HOSPITALI YAO YA LUTINDI, MAJIRANI WAMESEMA MGONJWA HUYO SASA ANAAFADHALI KULIKO MIAKA MITATU ILIYOPITA.


Wednesday, January 19, 2011

NI ADHA KUBWA YA MAJI WILAYANI HANDENI

ADHA NA SHIDA KUBWA YA MAJI KATIKA WILAYA YA HANDENI KAMA PICHANI WANAVYOONEKANA AKINA MAMA WAKIGOMBEA MAJI KATIKA ENEO LA CHANIKA.

MISURURU MIREFU YA NDOO ZA MAJI ZIKIWA ZIMEPANGWA ILI KUSUBIRI MAJI YATOKE KATIKA ENEO LA CHANIKA WILAYANI HANDENI.

HAKIMU ASIMAMISHA KESI KISA MOSHI KUSUMBUA MAHAKAMA KIASI CHA WATU KUSHINDWA KUPUMUA

MOTO UKIWAKA NA KUTOA MOSHI JIRANI NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MFAWIDHI WA WILAYA YA HANDENI KIASI CHA KUSABABISHA HAKIMU AWAAMURU POLISI KUWASAKA NA KUWAKAMATA WALIOCHOMA MOTO HUO.


ASKARI POLISI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA HANDENI AKIWAKAMATA WATU WALIOCHOMA MOTO NA KUSABABISHA MOCHI MKUBWA KUINGIA KATIKA MAHAKAMA HIYO KIASI CHA HAKIMU MKAZI BW. JONATHAN MGONGORA KUWAELEZA WANANCHI HAO KWAMBA KABLA YA KUCHOMA MOTO LAZIMA WAPATE KIBALI CHA HALMASHAURI.


Friday, January 14, 2011

BREAKING NEWS BASI LA SETELITE LAPATA AJALI!!!!

BASI LA SETELITE LILILOKUWA LIKITOKEA DAR ES SALAAM KWENDA TANGA, LIMEPATA AJALI BAADA YA KUPINDUKA KATIKA ENEO LA KIRAPURA NA WATU KADHAA WAMEJERUHIWA, HABARI KAMILI KUPATA IDADI YA WATU WALIOJERUHIWA NA MAJINA YAO, TUTAWATAJIENI PINDI YATAKAPOPATIKANA KUTOKA KWA WENYE MAMLAKA YA KUFANYA HIVYO.

Wednesday, January 12, 2011

MISHKAKI HII WAWEZA KULA?

WACHUUZI WA MISHKAKI KUTOKA KUSHOTO NI EMANUEL MKUMBO, ALLY AZIZ ALLY, ANETH GABRIEL NA NICOLAUS KARANJA WAKIUZA NYAMA KWENYE BARABARA MOJAWAPO MKOANI KIGOMA, JE NYAMA HIYO AINA YA 'BAFYUM 'WAWEZA KULA?

MKUTANO WA UWEKEZAJI TANGA ULIVYOFANA WATU MBALIMBALI WALIKABIDHIWA VYETU


BW. TARIMO WA ECKENFORDE AKIKABIDHIWA CHETI CHAKE CHA MMOJA YA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA ELIMU MKOANI TANGA NA WAZIRI WA UWEKEZAJI DKT MARY NAGU.



ALIYEKUWA MEYA WA JIJI LA TANGA (sasa mtu wa kawaida) SALIM KISAUJI (kushoto) AKIWA NA SWAHIBA WAKE BW. MABAMVUA ALIYEKUWA NAIBU WAKE SASA WOTE WALIKOSA NAFASI ZA UDIWANI BW. MABAMVUA ALIGOMBEA UDIWANI KATA YA DUGA AKASHINDWA NA BW. KISAUJI ALIGOMBEA UBUNGE AKASHINDWA. NAO WALIKUWEPO KWENYE MKUTANO HUO WA UWEKEZAJI ULIOFANYIKA KWENYE HOTEL YA MKONGE JIJINI TANGA.
WADAU MBALIMBALI WALIKUWEPO KWENYE MKUTANO WA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA AMBAO ULITUMIKA KUJADILI KWA KINA FURSA ZILIZOPO NA NAMNA AMBAZO ZITATUMIKA KWA KUWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WAKUBWA AMBAO WAMEKUWA NA MITAJI MIKUBWA.

MKUTANO HUO PIA BAADHI YA WATU WALIOTOA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDELEO YA MKOA HUO WALIKABIDHIWA VYETI VYA HESHIMA NA WAZIRI WA UWEZESHAJI DKT MARY NAGU KWENYE MKUTANO HUO.

TANGA YAPANIA KUALIKA WAWEKEZAJI WAKUBWA KUWEKEZA MIRADI MIKUBWA

WAZIRI WA UWEZESHAJI NA UWEKEZAJI DKT MARY NAGU AKIWA PAMOJA NA MBUNGE WA LUSHOTO BW. HENRY DAFFA SHEKIFU KWENYE MKUTANO WA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA ULIOFANYIKA KWENYE HOTELI YA MKONGE JIJINI TANGA,


MMOJA YA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA ELIMU JIJINI TANGA, BW. NARCIS TARIMO AMBAYE NI MKURUGENZI WA ECKENRFORDE SECONDARI ZILIZOPO JIJINI TANGA NAYE ALIKUWA MMOJA YA WATU WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO MKUBWA WA UWEKEZAJI.

WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKUBWA WALIKUWA WAKIONESHA BIDHAA AMBAZO WAMEKUWA WAKIZIZALISHA KATIKA MKOA WA TANGA KWENYE KUTANO HUO WA UWEKEZAJI.


MFUKO WA MASHIRIKA YA UMMA PPF NAO WALIKUWEPO KATIKA MKUTANO HUO WA UWEKEZAJI MKOANI TANGA WAKITAMBULISHA MFUMO WAKE MPYA WA UWEKEZAJI WA AMANA AMBAO UNAWAWEZESHA WATEJA KUJENGEWA NYUMBA KWA AJILI YA KUKOPESHWA KWA BEI NAFUU.


WANA-CCM WANAVYOPENDEZA PINDI WANAPOVAA MAVAZI YAO YA CHAMA

VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA TANGA WAKIWA KATIKA MOJA YA MIKUTANO YAO, WA KWANZA KUTOKA KULIA NI MWENYEKITI WA CCM KATA YA MAJENGO BW. DONDO ALI, KATIBU WA MIPANGO NA UCHUMI KATA YA DUGA SALIM BAWAZIR NA DIWANI WA VITI MAALUM TARAFA YA CHUMBAGENI SAIDA GHADAF.

MADIWANI TOKA KUSHOTO KHALID ABDALA KATA YA CENTRAL, DIWANI KATA YA MAJENGO MOHAMED WAKIWA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA.

VIJANA WA JIJI LA TANGA KUTOKA KULIA MIRAJ WANDI, KOMBO NA WENGINE WAKIWA KWENYE UKUMBI WA HALMASHAURI YA JIJI KUFUATILIA VIKAO VYA MADIWANI

MZEE WA BONDE AKIWA NA RAISA SAIDI KWENYE UKUMBI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA (Picha zote hizi 4 kwa hisani ya MDAU wa Blogu hii MIRAJ WANDI ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Tanga.

KITUO CHA AFYA MOMBO CHAPATA GARI LA KUBEBA WAGONJWA, NI MSAADA KUTOKA HOTEL YA LIVERPOOL

GARI LA KUBEBA WAGONJWA JIPYA LILILOKABIDHIWA UONGOZI WA KITUO CHA AFYA MOMBO WILAYANI KOROGWE NA UONGOZI WA HOTELI MAARUFU YA LIVERPOOL ILIYOPO KATIKA MJI MDOGO WA MOMBO.

MKUU WA MKOA WA TANGA ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI GARI HILO LA WAGONJWA KATIKA KITUO CHA AFYA MOMBO, AKIJARIBU KULIWASHA KAMA ISHARA YA KULIZINDUA HUKU MKURUGENZI WA HOTELI YA LIVERPOOL AKIANGALIA.


MKUU WA MKOA AKISALIMIANA NA MKURUGENZI WA HOTELI YA LIVERPOOL MARA BAADA YA KUFIKA KATIKA KITUO CHA AFYA MOMBO TAYARI KWA KUKABIDHI GARI HILO LA WAGONJWA, WA TATU KUTOKA KULIA KWA MKUU WA MKOA NI MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI PROFESA MAJI MAREFU.


MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KOROGWE BW. LAMECK MASEMBEJO AKITOA TAARIFA FUPI YA NAMNA GARI HILO LITAKAVYOWEZA KUSAIDIA JAMII YA ENEO HILO LA MOMBO WAKIWEMO ABIRIA WANAOPATA AJALI KATIKA BARABARA KUU YA MOMBO/ MOSHI

MKUU WA MKOA AKIMPONGEZA MKURUGENZI WA HOTELI HIYO YA LIVERPOOL KWA MSAADA WAKE WA KUTOA GARI HILO AMBALO LITAWEZA KUPUNGUZA KERO YA KUSAFIRISHA WAGONJWA KUTOKA MJI MDOGO WA MOMBO HADI HOSPITALI YA WILAYA MAGUNGA KWA MATIBABU ZAIDI.

GARI LENYEWE HILO AMBALO LITASAIDIA WAGONJWA MBALIMBALI KWENDA KWENYE HOSPITALI KUPATA MSAADA MKUBWA WA MATIBABU MAKUBWA.

MKURUGENZI WA HOTELI YA LIVERPOOL NA MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA WA KWANZA KULIA WAKIANGALIA VIFAA VILIVYOMO NDANI YA GARI HILO LA WAGONJWA.

GARI HILI LINATAKIWA KUTUNZWA ILI LIWEZE KUSAIDIA WAGONJWA KWA MUDA MREFU.