Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Wednesday, January 12, 2011

KITUO CHA AFYA MOMBO CHAPATA GARI LA KUBEBA WAGONJWA, NI MSAADA KUTOKA HOTEL YA LIVERPOOL

GARI LA KUBEBA WAGONJWA JIPYA LILILOKABIDHIWA UONGOZI WA KITUO CHA AFYA MOMBO WILAYANI KOROGWE NA UONGOZI WA HOTELI MAARUFU YA LIVERPOOL ILIYOPO KATIKA MJI MDOGO WA MOMBO.

MKUU WA MKOA WA TANGA ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI GARI HILO LA WAGONJWA KATIKA KITUO CHA AFYA MOMBO, AKIJARIBU KULIWASHA KAMA ISHARA YA KULIZINDUA HUKU MKURUGENZI WA HOTELI YA LIVERPOOL AKIANGALIA.


MKUU WA MKOA AKISALIMIANA NA MKURUGENZI WA HOTELI YA LIVERPOOL MARA BAADA YA KUFIKA KATIKA KITUO CHA AFYA MOMBO TAYARI KWA KUKABIDHI GARI HILO LA WAGONJWA, WA TATU KUTOKA KULIA KWA MKUU WA MKOA NI MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI PROFESA MAJI MAREFU.


MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KOROGWE BW. LAMECK MASEMBEJO AKITOA TAARIFA FUPI YA NAMNA GARI HILO LITAKAVYOWEZA KUSAIDIA JAMII YA ENEO HILO LA MOMBO WAKIWEMO ABIRIA WANAOPATA AJALI KATIKA BARABARA KUU YA MOMBO/ MOSHI

MKUU WA MKOA AKIMPONGEZA MKURUGENZI WA HOTELI HIYO YA LIVERPOOL KWA MSAADA WAKE WA KUTOA GARI HILO AMBALO LITAWEZA KUPUNGUZA KERO YA KUSAFIRISHA WAGONJWA KUTOKA MJI MDOGO WA MOMBO HADI HOSPITALI YA WILAYA MAGUNGA KWA MATIBABU ZAIDI.

GARI LENYEWE HILO AMBALO LITASAIDIA WAGONJWA MBALIMBALI KWENDA KWENYE HOSPITALI KUPATA MSAADA MKUBWA WA MATIBABU MAKUBWA.

MKURUGENZI WA HOTELI YA LIVERPOOL NA MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA WA KWANZA KULIA WAKIANGALIA VIFAA VILIVYOMO NDANI YA GARI HILO LA WAGONJWA.

GARI HILI LINATAKIWA KUTUNZWA ILI LIWEZE KUSAIDIA WAGONJWA KWA MUDA MREFU.

No comments:

Post a Comment