Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Sunday, October 23, 2011

SEKONDARI YA SHEMSANGA YAUNGUA TENA MOTO, SAFARI HII CHANZO CHAKE NI HITILAFU YA UMEME

SHULE YA SHEMSANGA INAYOMILIKIWA NA JUMUIYA YA WAZAZI WA CCM ILIYOPO WILAYANI KOROGWE IMEUNGUA MOTO NA KUSABABISHA HASARA INAYOKADIRIWA KUFIKIA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 10

MKUU WA SHULE YA SHEMSANGAGA BW. PASCHAL DEOGRADIUS AKIANGALIA HUKU HAAMINI MOJA YA CHUMBA AMBACHO KILIKUWA NI BWENI LA KULALA LA WANAFUNZI HAO.

MOJA YA BWENI AMBALO LIMETEKETEA KABISA KATIKA SHULE HIYO.

Thursday, October 20, 2011

AIRTEL YAKARIBIA KUWASHA MTANDAO WAKE KATA YA KIZARA, BUNGU KWA PROFESA MAJIMAREFU

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITWANGA, AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA KWAMKOLE KILICHOPO KATA YA KIZARA KUZUNGUMZIA SUALA LA MAWASILIANO YA SIMU ZA MIKONONI ALIPOFIKA KIJIJINI HAPO NA MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI BW. STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU.

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW CHARLES KITWANGA (KULIA) AKIWA NA MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI BW. STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU' WALIPOKUWA KWENYE KIJIJI CHA KWAMKOLE KATA YA KIZARA KUZUNGUMZIA UWEZEKANO WA WAKAZI WA KATA HIYO KUPATA MAWASILIANO YA SIMU ZA MIKONONI.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO WA KAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI YA AIRTEL BIBI BEATRICE SINGANO MALLYA, AKIZUNGUMZIA NAMNA KAMPUNI HIYO ITAWAONDOLEA KERO WANANCHI WA KATA YA KIZARA WANAOHITAJI HUDUMA YA SIMU ZA MIKONONI ILI WAWEZE KUTAMBUA BEI YA MAZAO YAO SOKONI. KUSHOTO NI NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITANGWA.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL BIBI BEATRICE SINGANO MALLYA, AKIWA KATIKA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO AKISISITIZA USHIRIKIANO BAINA YA WATAALAMU WA KAMPUNI HIYO WATAKAOFIKA KATIKA KIJIJI CHA KIZARA KUTAFUTA ENEO LA KUWEKA MINARA YA MAWASILIANO KWA AJILI YA HUDUMA YA WANANCHI WA KATA HIYO NA KATA JIRANI, NA WANANCHI ILI WAWEZE KUFANYA KAZI ZAO KWA URAHISI.

"JAMANI KAMPUNI YA AIRTEL IMEDHAMIRIA KWA MAKUSUDI KABISA KUHAKIKISHA INAFIKISHA MAWASILIANO KWA WANANCHI ILI WAWEZE KUONGEZA CHACHU YA UCHUMI" MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO ALIPOFIKA NA NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITWANGA.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL  BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKITOA MAELEZO YA NAMNA KAMPUNI HIYO ITAKAVYOANZA MCHAKATO WA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MINARA YA SIMU ZA KAMPUNI HIYO KATIKA KATA YA KIZARA WILAYANI KOROGWE.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKIWAELEZA WANANCHI WA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO NAMNA UTARATIBU UTAKAVYOTUMIKA KUWEKA MINARA YA SIMU KWA WAKAAZI WA KATA YA KIZARA WILAYANI KOROGWE

Sunday, October 16, 2011

VILA PARK LODGE NI MOJA YA HOTELI ZA KISASA WILAYANI KOROGWE

VILA PARK LODGE NI HOTELI YAKO YA KISASA KABISA ILIYOPO WILAYANI KOROGWE JIRANI NA OFISI YA MKUU WA WILAYA. KWA MALAZI, CHAKULA SAFI KABISA NA VINYWAJI VYA AINA YOTE UFIKAPO WILAYANI KOROGWE VILA PARK LODGE NI NYUMBANI KWAKO.

MOJA YA VYUMBA VYA VILA PARK LODGE

STENDI KOROGWE ADHA TUPU, MADEREVA WALALAMIKA UBOVU WANAPOINGIA, WASEMA WANALIPA FEDHA ZA BURE

STENDI YA KOROGWE PICHANI, UNAWEZA KUIONA ILIVYO

BASI LA MEDIDIAN LIKITOKA BAADA YA KUDAKA ABIRIA

YAANI KWA KWELI KITUO PESA ZIMEPOTEA HAPA MAANA KILITENGENEZWA MWAKA JANA MWEZI WA 11

ANGALIA BASI HILI LIKIPATA TABU MLANGONI LINAPOTOKA

Saturday, October 15, 2011

BUS LALETA KIZAAZAA, ABIRIA WANYESHEWA NA MVUA WAKIWA NDANI YA BUS HILO

KIZAAZAA NDANI LA BUS HILI LILILOKUWA LIKIFANYA SAFARI ZAKE KUTOKA TANGA KWENDA ARUSHA, KUFUATIA ABIRIA KUDAI FEDHA ZAO WAKATI WALIPOFIKA MAENEO YA KATI YA PONGWE NA MUHEZA AMBAKO MVUA ILIPOKUWA IKINYESHA BASI HILO LILIKUWA LIKIMWAGA MAJI KAMA LINAVYOONEKANA KATIKA PICHA HII

VITI VYA BASI HILI VIKIWA HAVINA WATU KUTOKANA NA KUVUJA SANA MAJI PEMBENI NA KATIKATIKA YA BASI HILO, HATUA AMBAYO ILISABABISHA KIZAAZAA KIKUBWA KWA ABIRIA WALIOKUWA WAKIENDA ARUSHA KUTOKA TANGA.

WANAFUNZI WAZAA WATOTO, MMOJA AFANYA MTIHANI NA MWANAYE

MKUU WA WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIMPA MTOTO WAKE MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MKALAMO WILAYANI HUMO MTOTO AMBAYE AMEMZAAA NA MWANAFUNZI MWENZAKE MARIAMU MOHAMED AMBAYE PIA NI MWANAFUZNI WA KIDATO CHA NNE AMBAYE HAKUWEZA KUFANYA MTIHANI HUO KWASABABU YA TATIZO HILO.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIWA AMEMSHIKA MTOTO ZAINA JACKSON WA MWANAFUNZI REHEMA MOHAMED AMBAYE NI MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KILOLE WILAYANI HUMO, KUSHOTO NI MWANAFUNZI HUYO AKIWA NYUMBANI KWAO ALIPOTEMBELEWA NA DC HUYO.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIWA AMEMBEBA MTOTO SALMA MUJIB HUKU AKIMTAZAMA MAMA WA MTOTO HUYO MARIAM MOHAMED AMBAYE NI MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MKALAMO ALIYESHINDWA KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA SEKONDARI MWAKA HUU.

AKAMATWA BAADA YA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

MWANAFUNZI wa shule ya sekondari Mkalamo iliyopo tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, Mujib Ziddy (19), amekamatwa na polisi mara baada ya kumaliza mitihani yake ya kidato cha nne iliyomalizika Alhamisi iliyopita, akituhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo waliokuwa wakisoma darasa moja.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa ni mtunza stoo ya shule hiyo na aliyekuwa akiishi hosteli ya shule hiyo pamoja na mwanafunzi huyo wa kike Mariamu Mohamed (19) ambaye ameshindwa kufanya mtihani huo baada ya kuwa na ujauzito ingawa alijifungua mtoto wa kike Septemba 5 mwaka huu na kachanga hicho kumpa jina la Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma.

Mwanafunzi huyo pamoja na familia yake aliyoongozana nayo na ile ya mwanafunzi wa kike, walifikishwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Erasto Sima kwa ajili ya kuhojiwa kabla ya kuchukuliwa na polisi, alisema kuwa alisema alijisikia vibaya sana mzazi mwenzake kukosa mitihani hiyo ambayo ameifanya licha ya awali kutaka kuzuiwa asifanye kutokana na kosa hilo.

"Kwa kweli nilijisikia vibaya Mariamu kushindwa kufanya mitihani kwasababu yangu, hatukujua kile tulichokuwa tukifanya pale shuleni, nakumbuka tulikuwa tukichukuana na kwenda kwenye moja ya darasa na kufanya mapenzi...Naomba niachiwe huru niweze kukatunza katoto kangu na matokeo yakitoka yakiwa nimefanya vizuri basi niweze kuendelea na masomo yangu," alisema Mujib alipokuwa akihojiwa ofisini hapo kwa Mkuu wa wilaya.

Mkuu wa shule hiyo Bw. Hemed Kimbute alikiri mbele ya mkuu wa wilaya kwamba wakati tukio hilo la binti huyo kupewa ujauzito na mwanafunzi mwenzake na shule kubaini Machi 23 mwaka huu, hawakuweza kutoa taarifa kwa bodi ya shule, Kijiji wala kata kwa ajili ya hatua zaidi ingawa ilipobainika mwanafunzi huyo, kumpa mimba mwenzake, alimtia kamba lakini alikosa ushirikiano na wazazi kumfikisha katika vyombo vya sheria.

"Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ni kweli nakiri sikutoa taarifa lakini baada ya tukio mimi nilimfunga kamba nikakosa ushirikiano wa wazazi lakini nasema kwa tukio hili bora nishike chaki nifundishe na ukuu wenu wa shule siutaki kusalimisha maisha yangu maana tukio hili nimepata mammbo magumu kule siwezi kuishi kwa mazingira yale yaliyopo kule," alisema Bw. Kimbute huku akiwa amehamaki mno kuhusu suala hilo.

Alipobanwa kuhusu vitisho alivyovipata baada ya tukio hilo, Mkuu huyo wa shule ambaye mkuu wa wilaya alikuwa akimtuhumu kwamba amehusika kuchangia kuwepo kwa tukio hilo, alisema sheria za shule zilizopo kuhusu kuwabana wanafunzi waliokuwa hosteli ya shule hiyo ndizo zinamweka pabaya na wanakijiji hatua ambayo ameona ni bora sheria zivunjwe kuliko kuzifuata kuhataraisha maisha yake. Katika hosteli ya shule hiyo wanafunzi wa kike wanaishi bila ya kuwa mwanaglizi usiku (Matron) kwa kuwa shule haina mwalimu mwanamke.

Baba wa Mujib alisema tangu binti huyo alipopata ujauzito huo na mwanae kuhusishwa na mimba hiyo, mwanafunzi huyo aliletewa nyumbani kwao katika kijiji cha Changalikwa ambako wanaishi naye hadi sasa na kwamba lengo lao, binti huyo mwanae atakapokuwa watamfanyia mipango ya kusoma kwa vile mwenye anataka kuenelea na masomo.

"Kwa kweli jambo hili limenisikitisha mno niliamini mwanangu Mujib nimemeleka shule kusoma kumbe mwenzangu ananiletea mtoto na mama yake, siyo jambo zuri la kufurahia kama mzazi nimempokea Mariamu na tunamlea hadi mtoto wake akikua basi na yeye tutampeleka shule," alisema Bw. Mujib Hussein.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo aliwalaumu wazazi wa pande zote kwa kuficha matukio ya namna hiyo ambayo mara nyingi yanalenga kukosesha haki ya msingi ya kusoma kwa mtoto wa kike na kwamba ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kuhakikisha wanafuata sheria kushughulikia matatizo ya watu wanaowapa ujauzito watoto wa shule huku ofisi yake ikiangalia namna atakavyoyashughulikia tabia kama hizo.

Wednesday, October 12, 2011

JULIO NA MAZOEZI KABAMBE YA COASTAL UNION, LENGO NI KUINASUA MKIANI

KOCHA JAMHURI KIHWELO 'JULLIO' AKIWEKA KONI IKIWA NI SIKU YAKE YA KWANZA KUINOA TIMU YAKE MPYA YA COASTAL UNION KWENYE UWANJA WA GYMKHANA AMBAKO TIMU HIYO INACHUKUA MAZOEZI.

WACHEZAJI WA TIMU YA COASTAL UNION WAKIW ANA KOCHA WAO JAMHURI KIHWELO 'JULIO' WAKIFANYA MAZOEZI KWENYE UWANJA WA GYMKHANA JIJINI TANGA AMBAKO TIMU HIYO INAFANYA MAZOEZI.

Tuesday, October 11, 2011

MBUNGE WA KOROGWE ATAKA MASHAMBA YA KATANI LIMITED YASIYOLIMWA WAPEWE WANANCHI WALIME MAHINDI

SHAMBA LA MKONGE LA KAMPUNI YA KATANI LIMITED LILILOPO KATIKA KIJIJI CHA LWENGERA DARAJANI KATA YA KWAGUNDA LIKIWA HALIONYESHI KULIMWA.

MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU' (KULIA) AKIELEZWA NA DIWANI WA KATA YA KERENGE BW. IDD SHEBILA (KATIKATI) JUU YA MAHITAJI YA WANANCHI YA ARDHI LAKINI KAMPUNI HIYO YA KATANI IMEHODHI MAENEO MAKUBWA LAKINI HAWALIMI HIVYO WAMETAKA SHAMBA HILO LIGAWIWE WANANCHI WALIME.

MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI PROFESA MAJIMAREFU (KULIA) AKIONESHA UKUBWA WA SHAMBA LA MAGUNGA ESTATE LA KATANI LIMITED AMBALO HALIJALIMWA  HALI AMBAYO ANATAKA LIGAWIWE KWA WANANCHI KWA AJILI YA KILIMO. KATIKATI NI DIWANI WA KATA YA KERENGE IDD SHEBILA NA KUSHOTO KABISA NI KATIBU WA MBUNGE HUYO BW. ANDREW NG'ANDU

WAFUKIWA NA KIFUSI WAKITAFUTA RUPIA WALIKUWA WAKICHIMBA CHOO NDANI, MMOJA AFA PAPO HAPO

MAMA ZAINA RAMADHANI AMBAYE NYUMBA YAKE KWA NYUMA ALIWAITA WATU WATATU WAMCHIMBIE CHOO KWA NDANI (NYUMBA YA MAKUTI INAYOONEKANA NYUMA YA PICHA) WATU HAO WALIPOANZA KUCHIMBA WAKAELEZA KWAMBA WAMEONA DALILI YA KUWEPO KWA RUPIA ZA KIJERUMANI HIVYO WAKAENDELEA KUCHIMBA.

HADI SHIMO LIKAFIKA KWENYE NYUMBA HII YA BATI, AMBAKO MTU MMOJA ANAYEITWA SALEH WAZIR ALIFUKIWA NA KIFUSI HUMO NDANI NA KUFA WAKATI MMOJA ANAYEITWA SIMON ALIFUNIKWA LAKINI BAHATI YAKE MIGUU YAKE ILIFUNIKWA AKAWAHI KUTOLEWA HUKU MWENZAO MMJA ANAYEITWA OTBORN ALIWAHI KUKIMBIA NA KUWAACHA WENZAKE.

HAONEKANAI KAKATWA NI MBUNGE WA KOROGWE VIJIJI PROFESA MAJIMAREFU AKIWA AMESHIKA TOCHI KUMULIKA CHINI YA SHIMO LILILOUA KATIKA KIJIJI CHA MNYUZI WILAYANI KOROGWE SEPTEMBA 15 MWAKA HUU.

NYUMBA AMBAYO SHIMO LIMETOKEZA KWA NDANI NA KUUA MTU MMOJA HUKO MNYUZI

Saturday, October 1, 2011

SHITA TANGA WAWASOMEA SWALA MAITI WALIOKUFA NA MV SPICE ISLANDERS ZANZIBAR

KATIBU WA BARAZA KUU LA KIISLAMU NCHINI (BAKWATA) MKOA WA TANGA SHEIKH MOHAMED RYIAMI (KUSHOTO) AKISOMA HOTBA KWENYE MSIKITI MKUU WA IJUMAA WA BARABARA YA 10 BAADA YA MASHEIKH NA WAUMINI WA DINI HIYO KUSWALIA MAITI WALIOKUFA KWA AJALI YA MAJINI KUFUTIA KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDERS VISIWANI ZANZIBAR MWEZI ULIOPITA NA KUUWA ZAIDI YA WATU 100, ALIYEMSHIKIA KIPAZA SAUTI NI USTAADH DONDO ALLY.

MASHEIKH WILAYANI TANGA WAKISOMA DUA KUWAOMBEA MAREHEMU WA MV SPICE ISLANDERS ILIYOZAMA VISIWANI ZANZIBAR MWEZI ULIOPITA NA KUUZA WATU ZAIDI YA 100, DUA HIYO NA SWALA YA MAITI ILISOMWA KWENYE MSIKITI MKUU WA IJUMAA JIJINI TANGA HIVI KARIBUNI AMBAYO IMEANDALIWA NA SHIRIKISHO LA TAASISI ZA KIISLAMU MKOANI TANGA (SHITA).

KATIBU WA BAKWATA MOHAMED RYIAMI (WA KWANZA KULIA) NA ANAYEMFUATA SHEIKH HUSSEIN HASHIMU WAKIONGOZA JOPO LA MASHEIKH NA WAUMINI WALIOFURIKA KWENYE MSIKITI WA IJUMAA ULIOPO BARABARA 10 JIJINI TANGA KUWASWALI MAREHEMU WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA MELI YA MV SPICE ISLANDERS ILIYOZAMA VISIWANI ZANZIBAR MWEZI ULIOPITA.

WAUMINI WAKISOMA VITABU KUWAOMBEA MAREHEMU WALIOFARIKI KWA AJALI YA MELI YA MV SPICE ISLANDERS ILIYOZAMA HUKO VISIWANI ZANZIBAR MWEZI ULIOPITA KWENYE MSIKITI MKUU WA IJUMAA JIJINI TANGA

MZEE WA BONDE NAYE ALIKUWEPO KUWAOMBEA MAREHEMU WALIOKUFA KWA AJALI YA MV ISLENDERS YA VISIWANI ZANZIBAR MWEZI LIOPITA (KULIA) NI USTAADH SALIMU BAWAZIR NAYE AKISOMA DUA KUWAOMBEA MAREHEMU HAO. caption

NILIPOTOKA NILIPATWA NA KIGUGUMIZI KUAMINI KWAMBA NI KWELI VIATU ALIVYOKUJA NAVYO BENEDICTOR KAGUA MTANGAZAJI WA REDIO MAARUFU JIJINI TANGA YA MASAFA YA FM YA 100.06 MWAMBAO FM A KAMA KWELI VIMEIBIWA NA KUACHIWA HIVI UNAVYOVIONA VYA YEBOYEBO, NI TUKIO AMBALO KILA MWISLAMU ANATAKIWA KULIPIGA VITA SIYO ZURI HATA KIDOGO.

KOROGWE WAZINDUA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA

KAIMU MKUU WA WILAYA YA KOROGWE METHEW NASEI AKISALIANA NA WANANCHI MARA ALIPOWASILI KWENYE VIWANJA VYA MAGOMA SHULENI KULIKOFANYIKA MAADHIMISHO YA UZINDUZI WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA AMBAPO KIWILAYA ZILIFANYIKA MAGOMA NA KUHUDHURIWA NA WATU WENGI

KAMANDA WA JWTZ AKIWA NA KIKOSI CHAKE CHA MGAMBO AMBACHO KIMEANZA MAFUNZO KATIKA KIJIJI HICHO CHA MAGOMA MARA NYINI WANA-MGAMBO NI JESHI LA AKIBA AMBAPO KATIKA SHEREHE HIZO ZA UZINDUZI WALINOGESHA SHEREHE HIZO KWA GWARIDE LAO ZURI.

KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KOROGWE (KUSHOTO) AKIWA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KOROGWE MR. MASEMBEJO WAKIANGALIA RATIBA YA SHEREHE ZA UZINDUZI WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU MAGOMA.

SHEREHE HIZO PIA ZILIKUWA NA NGOMA KUTOKA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAGOMA, MZUNGU HUYU WA KIMAREKANI AMBAYE NI MWALIMU WA KUJITOLEA NAE ALIUUNGANA NA WANAFUNZI WAKE KUCHEZA NGOMA YA WANAFUNZI HAO.

KIKOSI CHA WANA-MGAMBO KIKIWA KIMETULIA WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI AMBAYE NI MKUU WA WILYA YA MUHEZA BW. NASEI AKIHUTUBIA SHEREHE HIZO AMBAZO PAMOJA NA UJUMBE WA SERIKI KUHUSU MIAKA 50 YA UHURU PIA ALIWATAKA WANANCHI KUTUNZA CHAKULA KUJIKINGA NA NJAA.

Thursday, September 29, 2011

NAHODHA WA MELI YA KIGENI AKUTWA AMEJINYONGA BANDARI YA TANGA

NAHODHA WA MELI YA MV TIGER MONROVIA BW. PAKULSKI RADOSLAV ADAM (47) AKINING'INIA KWENYE MLINGOTI WA BENDERA KWENYE MELI HIYO BAADA YA KUJINYONGA USIKU WA KUAMKIA ALHAMISI BAADA YA MELI HIYO KUTIA NANGA KWENYE BAMDARI YA TANGA.

MWILI WA NAHODHA HUYO UKIONEKANA BAADA YA KUJINYONGA

MELI YA MVU TIGER IKIWA IMETIA NANGA KWENYE BANDARI YA TANGA

TIMU YA MAOFISA WA SERIKALI AKIWEMO MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOANI TANGA, RCO MOHAMED JAFAR (kulia mwenye glovu za bluu) AKIWA NA MAOFISA HAO KUCHUNGUZA MWILI WA MAREHEMU HUYO

NAHODHA ADAM AKIONEKANA KWENYE MTI HUO AKIWA AMEJINYONGA TAYARI

NAHODHA HUYO AKINING'INIA HUKU OFISA WA KIKOSI CHA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOANI TANGA, AFANDE JOHN AKIUTAZAMA MWILI HUO KUONA KAMA NI KWELI ALIJITUNDIKA HAPO AU ULIWEKWA NA MTU

MABAHARIA WA MELI HIYO PAMOJA NA MAOFISA WA SERIKALI WAKIUSHUSHA MWILI WA NAHODHA HUYO KUTOKA MAHALI AMBAKO ALIJINYONGEA KWENYE MELI HIYO

MELI YA TIGER INAVYOONEKANA PICHANI KATIKA ENEO LAKE LA NDANI JUU KABISA YA KICHWA CHA NAHODHA HUYO

MWILI WA NAHODHA HUYO UKIWA UMEFUNGWA TAYARI KWA KUTOLEWA NCHI KAVU KWENYE KUHIFADHIWA KWENYE HOSPITALI YA BOMBO.

MAOFISA HAO WAKIWA NA WAHUDUMU WA AFYA WA MAMLAKA YA BANDARI NCHINI BANDARI YA TANGA WAKIUBEBA MWILI KUUTOA NJE YA MELI HIYO WAKITUMIA BOTI NYINGINE

NAHODHA MSAIDIZI WA MELI HIYO BW. COLGOLF AKITOA MAELEZO KWA MAOFISA WA SERIKALI KUFUATIA KUJINYONGA KWA NAHODHA HUYO

MWILI UKIWA UMEFUNGWA VIZURI TAYARI KUPELEKWA KWENYE HOSPITALI YA BOMBO KUHIFADHIWA

MWILI UKIWA UMEBEBWA NA MAOFISA HAO NA KUUPAKIA KWENYE BOTI ILI WAUTOE NJE NA KUUPELEKA HOSPITALINI BOMBO

MAOFISA HAO WAKIUTOA MWILI HUO NJE YA BOTI WALIMOMPAKIA NA KUUPELAKA BOMBO HOSPITALI.

Na Mzee wa Bonde,Tanga
Nahodha wa meli ya kigeni akutwa amejinyonga melini
NAHODHA wa Meli ya shehena ya MV  Tiger Monrovia,Pakulski Radoslav Adam (47)  jana alikutwa akiwa amejinyonga ndani ya meli hiyo katika mazingira ambayo hayajajulikana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Constantine Massawe  alisema jana kuwa  kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana Alhamisi wakati meli hiyo ikiwasili katika bandari ya Tanga ikitokea Dar es salaam.


Alisema wafanyakazi wa meli hiyo wamesema kuwa  Nahodha huyo alipanda ngazi hadi kwenye nguzo za bendera ya meli hiyo na kujinyonga kwa kutumia kamba.


Alisema wanfanyakazi hao wamedai kuwa hawakuwa wamejua mwenzao alikokuwa hadi ilipofika  ilipofika alfajiri baada ya mmoja wa wafanyakazi melini kupanda juu na kuukuta mwili wake ukining’inia.

Alisema kufuatia tukio hilo, wafanyakazi hao wameweza kuwasiliana na ndugu zake walioko nchini Poland pamoja na mmliki wa meli hiyo ambao ili kujua nini kifanyike juu ya mwili huo
.

Mwandishi wa habari hizi alishihudia shughuli za utoaji wa mwili huo uliokuwa ndani ya meli iliyotia nanga mbali na bandari ya Tanga,zikifanywa na maafisa wa jeshi la Polisi,Bandari ya Tanga,uhamiaji,TRA pamoja na mawakala wa meli hiyo ambapo ilichukua zaidi ya masaa saba hadi kuutoa na kuupeleka Hospitali ya Bombo.


Wakala wa meli hiyo,Abas Mohamed wa kampuni ya CMA CGM (T) Ltd alisema imebeba makontena ya bidhaa mbalimbali ambazo zimetoka nchi za Ulaya na bara la Asia na kwamba ilipita Dar es salaam na ingekaa banadari ya Tanga kwa siku mbili kabla ya kwenda Mombasa na Colombo  nchini Malasia.


Afisa afya wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga,Happiness Byabato alisema baada ya kuufanyia uchunguzi mwili huo ambaini kuwa amejinyonga mwenyewe.


Kwa mujibu wa  Massawe ni kuwa  mwili huo umehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga,Bombo kusubiri maamuzi ya ndugu wa marehemu kama asafirishwe au azikwe Tanga.


Alisema pamoja na kwamba taarifa za awali zinaeleza kuwa nahodha huyo kajinyonga lakini jeshi hilo bado linafanya uchunguzi wa kitaalamu kujua chanzo cha tukio hilo.