Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Thursday, October 20, 2011

AIRTEL YAKARIBIA KUWASHA MTANDAO WAKE KATA YA KIZARA, BUNGU KWA PROFESA MAJIMAREFU

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITWANGA, AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA KWAMKOLE KILICHOPO KATA YA KIZARA KUZUNGUMZIA SUALA LA MAWASILIANO YA SIMU ZA MIKONONI ALIPOFIKA KIJIJINI HAPO NA MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI BW. STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU.

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW CHARLES KITWANGA (KULIA) AKIWA NA MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI BW. STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU' WALIPOKUWA KWENYE KIJIJI CHA KWAMKOLE KATA YA KIZARA KUZUNGUMZIA UWEZEKANO WA WAKAZI WA KATA HIYO KUPATA MAWASILIANO YA SIMU ZA MIKONONI.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO WA KAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI YA AIRTEL BIBI BEATRICE SINGANO MALLYA, AKIZUNGUMZIA NAMNA KAMPUNI HIYO ITAWAONDOLEA KERO WANANCHI WA KATA YA KIZARA WANAOHITAJI HUDUMA YA SIMU ZA MIKONONI ILI WAWEZE KUTAMBUA BEI YA MAZAO YAO SOKONI. KUSHOTO NI NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITANGWA.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL BIBI BEATRICE SINGANO MALLYA, AKIWA KATIKA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO AKISISITIZA USHIRIKIANO BAINA YA WATAALAMU WA KAMPUNI HIYO WATAKAOFIKA KATIKA KIJIJI CHA KIZARA KUTAFUTA ENEO LA KUWEKA MINARA YA MAWASILIANO KWA AJILI YA HUDUMA YA WANANCHI WA KATA HIYO NA KATA JIRANI, NA WANANCHI ILI WAWEZE KUFANYA KAZI ZAO KWA URAHISI.

"JAMANI KAMPUNI YA AIRTEL IMEDHAMIRIA KWA MAKUSUDI KABISA KUHAKIKISHA INAFIKISHA MAWASILIANO KWA WANANCHI ILI WAWEZE KUONGEZA CHACHU YA UCHUMI" MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO ALIPOFIKA NA NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITWANGA.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL  BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKITOA MAELEZO YA NAMNA KAMPUNI HIYO ITAKAVYOANZA MCHAKATO WA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MINARA YA SIMU ZA KAMPUNI HIYO KATIKA KATA YA KIZARA WILAYANI KOROGWE.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKIWAELEZA WANANCHI WA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO NAMNA UTARATIBU UTAKAVYOTUMIKA KUWEKA MINARA YA SIMU KWA WAKAAZI WA KATA YA KIZARA WILAYANI KOROGWE

No comments:

Post a Comment