Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Saturday, October 15, 2011
WANAFUNZI WAZAA WATOTO, MMOJA AFANYA MTIHANI NA MWANAYE
AKAMATWA BAADA YA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
MWANAFUNZI wa shule ya sekondari Mkalamo iliyopo tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, Mujib Ziddy (19), amekamatwa na polisi mara baada ya kumaliza mitihani yake ya kidato cha nne iliyomalizika Alhamisi iliyopita, akituhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo waliokuwa wakisoma darasa moja.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa ni mtunza stoo ya shule hiyo na aliyekuwa akiishi hosteli ya shule hiyo pamoja na mwanafunzi huyo wa kike Mariamu Mohamed (19) ambaye ameshindwa kufanya mtihani huo baada ya kuwa na ujauzito ingawa alijifungua mtoto wa kike Septemba 5 mwaka huu na kachanga hicho kumpa jina la Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma.
Mwanafunzi huyo pamoja na familia yake aliyoongozana nayo na ile ya mwanafunzi wa kike, walifikishwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Erasto Sima kwa ajili ya kuhojiwa kabla ya kuchukuliwa na polisi, alisema kuwa alisema alijisikia vibaya sana mzazi mwenzake kukosa mitihani hiyo ambayo ameifanya licha ya awali kutaka kuzuiwa asifanye kutokana na kosa hilo.
"Kwa kweli nilijisikia vibaya Mariamu kushindwa kufanya mitihani kwasababu yangu, hatukujua kile tulichokuwa tukifanya pale shuleni, nakumbuka tulikuwa tukichukuana na kwenda kwenye moja ya darasa na kufanya mapenzi...Naomba niachiwe huru niweze kukatunza katoto kangu na matokeo yakitoka yakiwa nimefanya vizuri basi niweze kuendelea na masomo yangu," alisema Mujib alipokuwa akihojiwa ofisini hapo kwa Mkuu wa wilaya.
Mkuu wa shule hiyo Bw. Hemed Kimbute alikiri mbele ya mkuu wa wilaya kwamba wakati tukio hilo la binti huyo kupewa ujauzito na mwanafunzi mwenzake na shule kubaini Machi 23 mwaka huu, hawakuweza kutoa taarifa kwa bodi ya shule, Kijiji wala kata kwa ajili ya hatua zaidi ingawa ilipobainika mwanafunzi huyo, kumpa mimba mwenzake, alimtia kamba lakini alikosa ushirikiano na wazazi kumfikisha katika vyombo vya sheria.
"Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ni kweli nakiri sikutoa taarifa lakini baada ya tukio mimi nilimfunga kamba nikakosa ushirikiano wa wazazi lakini nasema kwa tukio hili bora nishike chaki nifundishe na ukuu wenu wa shule siutaki kusalimisha maisha yangu maana tukio hili nimepata mammbo magumu kule siwezi kuishi kwa mazingira yale yaliyopo kule," alisema Bw. Kimbute huku akiwa amehamaki mno kuhusu suala hilo.
Alipobanwa kuhusu vitisho alivyovipata baada ya tukio hilo, Mkuu huyo wa shule ambaye mkuu wa wilaya alikuwa akimtuhumu kwamba amehusika kuchangia kuwepo kwa tukio hilo, alisema sheria za shule zilizopo kuhusu kuwabana wanafunzi waliokuwa hosteli ya shule hiyo ndizo zinamweka pabaya na wanakijiji hatua ambayo ameona ni bora sheria zivunjwe kuliko kuzifuata kuhataraisha maisha yake. Katika hosteli ya shule hiyo wanafunzi wa kike wanaishi bila ya kuwa mwanaglizi usiku (Matron) kwa kuwa shule haina mwalimu mwanamke.
Baba wa Mujib alisema tangu binti huyo alipopata ujauzito huo na mwanae kuhusishwa na mimba hiyo, mwanafunzi huyo aliletewa nyumbani kwao katika kijiji cha Changalikwa ambako wanaishi naye hadi sasa na kwamba lengo lao, binti huyo mwanae atakapokuwa watamfanyia mipango ya kusoma kwa vile mwenye anataka kuenelea na masomo.
"Kwa kweli jambo hili limenisikitisha mno niliamini mwanangu Mujib nimemeleka shule kusoma kumbe mwenzangu ananiletea mtoto na mama yake, siyo jambo zuri la kufurahia kama mzazi nimempokea Mariamu na tunamlea hadi mtoto wake akikua basi na yeye tutampeleka shule," alisema Bw. Mujib Hussein.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo aliwalaumu wazazi wa pande zote kwa kuficha matukio ya namna hiyo ambayo mara nyingi yanalenga kukosesha haki ya msingi ya kusoma kwa mtoto wa kike na kwamba ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kuhakikisha wanafuata sheria kushughulikia matatizo ya watu wanaowapa ujauzito watoto wa shule huku ofisi yake ikiangalia namna atakavyoyashughulikia tabia kama hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment