Uchaguzi umefanyika kwa amani karibu vituo vyote hapa nchini imeripotiwa kwamba watu wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba ya kumchagua kiongozi wanaetaka.
Kimsingi kila Mtanzania ametumia nafasi hiyo kumchagua kiongozi anayemtaka hii inamaana baada ya kura kujulishwa matokeo yatatangazwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katika kila jimbo na yale ya urais yatatangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC.
Swali linakuja je viongozi wa vyama watakubali kupokea matokeo hayo, kwa upinzani tumewashuhudia viongozi wake wengi wakisema watakubali matokeo pindi yatakapotangazwa lakini matokeo hayo yaoneshe dalili kwamba hakuna hila zozote ambazo zimetumika kukipendelea chama tawala.
Mimi nadhani viongozi wa vyama vya siasa wawaeleze wanachama na mashabiki wa vyama vyao kukubali matokeo na mshindi akitangazwa kila mmoja afanye shughuli zake ili kuepusha matukio ya umwagaji damu kama ambavyo tumeweza kushuhudia katika nchi jirani kwa udhoefu unaonesha kwamba matokeo yanapotangazwa ndiyo mara nyingi vurugu za kupinga matokeo hayo zinapotokea hatua ambayo inatokea umwagaji wa damu na vifo.
Tanzania hatuwezi kufikia hapo kama watu wanataka mabadiliko hawakatazwi na kura zao ndiyo zitahukumu kwa waliokaaa madarakani lakini kutokana na hali ilivyo JK atakuwa amepata ushindi mkubwa kutokana na mwelekeo unavyoonekana na matokeo ya awali yanavyoonekana.
Mikoa kama Tanga, Lindi, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Tabora na Singida taarifa zake zinaonesha kwamba CCM imepata ushindi mkubwa na mikoa ya Rukwa, Mbeya, Arusha, Songea, Shinyanga, Mara na Mwanza Chadema kinaonekana kuongoza kwa kura.
Kila lahei Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki TANZANIA!
No comments:
Post a Comment