Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Saturday, October 29, 2011

MKUU WA MKOA ATEMBELEA MGODI WA KUZALISHA UMEME WA HALE, AKUTANA NA CHANGAMOTO

MKUU WA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA NEW PANGANI FALLS POWER STATION INJINIA PAKAYA MTEMAKAYA AKIMSOMEA TAARIFA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GALLAWA ALIPOTEMBELEA KAIKA MGODI WA KUZALISHA UMEME ULIOPO HALE WILAYANI KOROGWE.

WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KOROGWE PAMOJA NA MSAIDIZI WA MKUU WA MKOA WA TANGA, BW. JOSEPH SURA (KULIA), WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA LUTENI CHIKU GALLAWA (HAYUPO PICHANI) ALIPOTEMBELEA MGODI WA KUZALISHA UMEME HALE.

INJINIA PAKAYA MTEMAKAYA (ALIYENYOOSHA MKONO JUU) AKIMWELEZA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI CHIKU GALLAWA (KUSHOTO) NAMNA UZALISHAJI UNAVYOFANYIKA KWENYE MGODI HUO WA KUZALISHA UMEME HALE.


INJINIA PAKAYA MTEKAYA AKIMWELEZA MKUU WA MKOA NAMNA ABAVYO CHANAMOTO ZA UZALISHAJI UMEME ZINAVYOSABABISHA WAKAI MWININE WASHINDWE KUZALISHA KWA UFANISI

MKUU WA MKOA LUTENI CHIKU GALLAWA NA WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALMA YA WILAYA YA KOROGWE WAKITEMBEA NDANI YA MGODI WA UZALISHAJI UMEME WA HALE WILAANI KOROGWE AMBAKO WALIJIONEA KAZI MBALIMBALI ZINAZOFANIKA ZA UZALISHAJI UMEME.

INJINIA PAKAYA MTEMAKAYA AKIELEZA KWAMBA KITUO HICHO TANGU KIMEJENGWA MIAKA YA 1995 KIMEKUWA KIKIFANYA KAZI VIZURI ISIPOKUWA KOMPYUTA ZINAZOENDESHA MITAMBO ZIMEHARIBIKA NA HIVYO MITAMBO KUENDESHWA KWA KUTUMIA USIMAMIZI WA WATU

MKUU WA MKOA AKITOA MAELEKEZO YA NAMNA YA KUANGALIA CHANGAMOTO WANZOKABILIANA NAZO WATENDAJI WA MGODI WA KUZALISHA UMEME HALE HUKU WATENDAJI HAO WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI.

INJINIA MUSIMU MAKUNGA MSIMAMIZI WA MGODI WA KUZALISHA UMEME WA PANGANI FALLS AKITOA MAELEKEZO WA JINSI WANAVYOWEZA KUENDESHA MITAMBO HIYO YA KUZALISHA UMEME KATIKA MAJUKUMU YAO YA KILA SIKU.

MKUU WA MKOA NA WENYEJI WAKE WA MGODI WA KUZALISHA UMEME WALIPATA FURSA YA KUTEMBELEA MGODI WA ZAMANI WA KUZALISHA UMEME WA OLD PANGANI FALLS KWA KUPANDA KIBERENGE KAMA WANAVYOONEKANA KATIKA PICHA.

HAPA MKUU WA MKOA LUTENI CHIKU GALLAWA AKIWA NA MSAFARA WAKE WAKIANGALIA KINA CHA MAJI KATIKA BWAWA LILILOZUIWA KWA AJILI YA KUPELEKA MAJI KATIKA MGODI HUO

Friday, October 28, 2011

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA BARABARA YA TANGA/HOROHORO, BANDARI YA TANGA

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIUNDOMBINU INJINIA OMARI CHAMBO, AKITOA UFAFANUZI KWA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WALIOKUWA KWENYE MKUTANO KWENYE JENGO LA BANDARI HOUSE TANGA

WATENDAJI WA BANDARI YA TANGA WAKIFUATILIA KWA MAKINI MICHANGO YA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIUNDOMBINU INJINIA OMARI CHAMBO (KATIKATI) AKIELEZEA JAMBO KWA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WALIOTEMBELEA BANDARI YA TANGA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI

MJUMBE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU BW. HERBERT MNTANGI AMBAYE NI MBUNGE WA MUHEZA (BONDE) AKIWAELEKEZA WAJUMBE WENZAKE JINSI KISIWA KILICHOPO JIRANI NA BANDARI YA TANGA KINAVYOWEZA KUZIDISHA KUJAA KWA MCHANGA KATIKA BANDARI YA TANGA

HAPA WAJUMBE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WAKIWA NA WAFANYAKAZI WA BANDARI YA TANGA, WAKIPATA MAELEZO KATIKA ENEO LA KUINGIA KATIKA ENEO AMBALO LITAJENGWA BANDARI MPYA SEHEMU YA MWAMBANI

WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU NA WAFANYAKZI WA BANDARI YA TANGA, WAKITAZAMA ENEO AMBALO LITAJENGWA BANDARI YA KINA KIREFU KATIKA SEHEMU YA MWAMBANI

MTAALAMU WA TANROADS INJINIA EDWARD AKIWAELEKEZA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU JINSI KAMPUNI YA KICHINA YA SINOHYDRO ILIVYOJIDHATITI KATIKA KUHAKIKISHA INAMALIZA BARABARA YA TANGA/HOROHORO KUWEKA LAMI NA KUIMALIZA KWA WAKATI

WAHESHIMKWA WABUNGE WA KAMATI YA MIUNDOMBINU WAKITEMBEA KWA MIGUU KWENDA KUANGALIA DARAJA LA NDOYO AMBALO WACHINA WA KAMPUNI YA SINOHYDRO WAMELIJENGA KWA UBORA WA HALI YA JUU

MWENYEKITI WA KAMATI PETER SERUKAMBA (MBELE) AKIWAONGOZA WABUNGE WENZAKE KUTEMBELEA BARABARA YA TANGA/HOROHORO

Thursday, October 27, 2011

MKUU WA MKOA WA TANGA, ATEMBELEA VIWANDA NI ZIARA YAKE YA KWANZA TANGU ATEULIWE KUWA RC MPYA

MKUU WA MKOA WA TANGA, LUTENI (Mstaafu) CHIKU GALAWA (kushoto) AMEANZA ZIARA YA KUTEMBELEA VIWANDA VILIVYOPO JIJINI TANGA, KUONA SHUGHULI MBALIMBALI WANAZOZIFANYA IKIWA NI ZIARA YAKE YA KUJIFUNZA NAMNA VIWANDA VILIVYOPO HAPA VINAVYOKABILIWA NA MATATIZO, PICHA HII RC HUYO ALIIPIGA WILAYANI PANGANI ALIKOKWENDA KUTAMBULISHWA NA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA HUU, MEJA GENERALI SAID KALEMBO (katati) WALIYEKUWA NAYE NI MDAU WA TEKLONOJIA YA ELETRONIKI MOHAMED HAMMIE 'ANKO MO'.

Monday, October 24, 2011

KILA LA KHERI COASTAL UNION LEO ISHINDWE DHIDI YA POLISI DODOMA

KIKOSI CHA COASTAL UNION AMBACHO LEO KITAPAMBANA NA TIMU YA POLISI DODOMA KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI MAJIRA YA SAA 10:00 JIONI MCHEZO AMBAO UNATARAJIWA KUWA MKALI HASA KUTOKANA NA POLISI KUFUNGWA BAO 3-1 NA AZAM KWENYE UWANJA WA CHAMANZI JIJINI DAR ES SALAAM NA 'WAGOSI WA KAYA' KUWA KATIKA KIWANGO KIZURI TANGU WALIPOISARAMBATISHA VILLA SQUAD KWA MABAO 6-1 NA TIMU HIYO KUPUMZIKA MUDA MREFI HIVYO WATAINGIA UWANJANI WAKIW ANA ARI YA KUENDELEZA USHINDI CHINI YA KOCHA WAO MAHIRI JAMHURI KIHWELO 'JULIO'. MARA YA MWISHO TIMU HIZO KUCHEZA KWENYE UWANJA HUO ILIKUWA MWAKA 2008 AMBAPO POLISI WALIIFUNGA COASTAL BAO 1-0 BAO LILILOFUNGWA NA BANTU ADIMIN KIPINDI CHA PILI, JE COASTAL WATAFUNJWA MWIKO WA KUFUNGWA NA TIMU HIYO KWENYE UWANJA WAKE WA NYUMBANI?

UNAPOWAPA WATOTO CHAKULA SHULENI UWEZO WAO WA KUFIKIRI UNAONGEZEKA

WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI KATIKA SHULE YA MSINGI LWENGERA ESTATE WAKIWA KWENYE FOLENI YA CHAKULA MARA BAADA YA KUMALIZA VIPINDI VYAO VYA MASOMO SHULENI HAPO, WANAOWAANGALIA NI MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU' (MWENYE SUTI NYEUPE) ALIYEFIKA SHULENI HAPO KWENYE MAHAFALI YA DARASA LA SABA MWAKA HUU, WENGINE NI MAOFISA WA SHULE NA KATA YA KWAGUNDA ILIPO SHULE HIYO.

MMOJA WA WALIMU WA SHULE YA LWENGERA ESTATE AKIWAPAKULIA CHAKULA 'WALI' WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI WA SHULE HIYO MARA BAADA YA KUMALIZA VIPINDI VYAO VYA MASOMO.

"NTILIE MWINGI MWALIMU, LEO NINA NJAA MAANA NIMESOMA SANA' NDIVYO INAVYOELEKEA KUSEMA HIVI MWANAFUNZI WA DARASA LA AWALI LA SHULE YA LWENGERA ESTATE , BATULI RAJABU (KUSHOTO) AKIMWELEZA MWALIMU WAKE AMJAZIE CHAKULA HICHO.

WALI MAHARAGE WANAFUNZI HAWA WA DARASA LA AWALI LA SHULE YA MSINGI LWENGERA ESTATE WAKIPAKULIWA CHAKULA CHA MCHANA MARA BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAO SHULENI HAPO. UTARATIBU HUO NI MZURI KWANI UNAMFANYA MTOTO AFURAHI MASOMO NA WAKATI HUO KUKUA UWEZO WAKE WA KUFIKIRI NA KUKARIRI SABABU YA KUPATA CHAKULA SHULENI.

Sunday, October 23, 2011

SEKONDARI YA SHEMSANGA YAUNGUA TENA MOTO, SAFARI HII CHANZO CHAKE NI HITILAFU YA UMEME

SHULE YA SHEMSANGA INAYOMILIKIWA NA JUMUIYA YA WAZAZI WA CCM ILIYOPO WILAYANI KOROGWE IMEUNGUA MOTO NA KUSABABISHA HASARA INAYOKADIRIWA KUFIKIA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 10

MKUU WA SHULE YA SHEMSANGAGA BW. PASCHAL DEOGRADIUS AKIANGALIA HUKU HAAMINI MOJA YA CHUMBA AMBACHO KILIKUWA NI BWENI LA KULALA LA WANAFUNZI HAO.

MOJA YA BWENI AMBALO LIMETEKETEA KABISA KATIKA SHULE HIYO.

Thursday, October 20, 2011

AIRTEL YAKARIBIA KUWASHA MTANDAO WAKE KATA YA KIZARA, BUNGU KWA PROFESA MAJIMAREFU

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITWANGA, AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA KWAMKOLE KILICHOPO KATA YA KIZARA KUZUNGUMZIA SUALA LA MAWASILIANO YA SIMU ZA MIKONONI ALIPOFIKA KIJIJINI HAPO NA MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI BW. STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU.

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW CHARLES KITWANGA (KULIA) AKIWA NA MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI BW. STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU' WALIPOKUWA KWENYE KIJIJI CHA KWAMKOLE KATA YA KIZARA KUZUNGUMZIA UWEZEKANO WA WAKAZI WA KATA HIYO KUPATA MAWASILIANO YA SIMU ZA MIKONONI.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO WA KAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI YA AIRTEL BIBI BEATRICE SINGANO MALLYA, AKIZUNGUMZIA NAMNA KAMPUNI HIYO ITAWAONDOLEA KERO WANANCHI WA KATA YA KIZARA WANAOHITAJI HUDUMA YA SIMU ZA MIKONONI ILI WAWEZE KUTAMBUA BEI YA MAZAO YAO SOKONI. KUSHOTO NI NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITANGWA.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL BIBI BEATRICE SINGANO MALLYA, AKIWA KATIKA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO AKISISITIZA USHIRIKIANO BAINA YA WATAALAMU WA KAMPUNI HIYO WATAKAOFIKA KATIKA KIJIJI CHA KIZARA KUTAFUTA ENEO LA KUWEKA MINARA YA MAWASILIANO KWA AJILI YA HUDUMA YA WANANCHI WA KATA HIYO NA KATA JIRANI, NA WANANCHI ILI WAWEZE KUFANYA KAZI ZAO KWA URAHISI.

"JAMANI KAMPUNI YA AIRTEL IMEDHAMIRIA KWA MAKUSUDI KABISA KUHAKIKISHA INAFIKISHA MAWASILIANO KWA WANANCHI ILI WAWEZE KUONGEZA CHACHU YA UCHUMI" MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO ALIPOFIKA NA NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKLONOJIA BW. CHARLES KITWANGA.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL  BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKITOA MAELEZO YA NAMNA KAMPUNI HIYO ITAKAVYOANZA MCHAKATO WA KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MINARA YA SIMU ZA KAMPUNI HIYO KATIKA KATA YA KIZARA WILAYANI KOROGWE.

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA UMMA WA KAMPUNI YA AIRTEL BIBI BEATRECE SINGANO MALLYA AKIWAELEZA WANANCHI WA KIJIJI CHA BOMBO MAJIMOTO NAMNA UTARATIBU UTAKAVYOTUMIKA KUWEKA MINARA YA SIMU KWA WAKAAZI WA KATA YA KIZARA WILAYANI KOROGWE

Sunday, October 16, 2011

VILA PARK LODGE NI MOJA YA HOTELI ZA KISASA WILAYANI KOROGWE

VILA PARK LODGE NI HOTELI YAKO YA KISASA KABISA ILIYOPO WILAYANI KOROGWE JIRANI NA OFISI YA MKUU WA WILAYA. KWA MALAZI, CHAKULA SAFI KABISA NA VINYWAJI VYA AINA YOTE UFIKAPO WILAYANI KOROGWE VILA PARK LODGE NI NYUMBANI KWAKO.

MOJA YA VYUMBA VYA VILA PARK LODGE

STENDI KOROGWE ADHA TUPU, MADEREVA WALALAMIKA UBOVU WANAPOINGIA, WASEMA WANALIPA FEDHA ZA BURE

STENDI YA KOROGWE PICHANI, UNAWEZA KUIONA ILIVYO

BASI LA MEDIDIAN LIKITOKA BAADA YA KUDAKA ABIRIA

YAANI KWA KWELI KITUO PESA ZIMEPOTEA HAPA MAANA KILITENGENEZWA MWAKA JANA MWEZI WA 11

ANGALIA BASI HILI LIKIPATA TABU MLANGONI LINAPOTOKA

Saturday, October 15, 2011

BUS LALETA KIZAAZAA, ABIRIA WANYESHEWA NA MVUA WAKIWA NDANI YA BUS HILO

KIZAAZAA NDANI LA BUS HILI LILILOKUWA LIKIFANYA SAFARI ZAKE KUTOKA TANGA KWENDA ARUSHA, KUFUATIA ABIRIA KUDAI FEDHA ZAO WAKATI WALIPOFIKA MAENEO YA KATI YA PONGWE NA MUHEZA AMBAKO MVUA ILIPOKUWA IKINYESHA BASI HILO LILIKUWA LIKIMWAGA MAJI KAMA LINAVYOONEKANA KATIKA PICHA HII

VITI VYA BASI HILI VIKIWA HAVINA WATU KUTOKANA NA KUVUJA SANA MAJI PEMBENI NA KATIKATIKA YA BASI HILO, HATUA AMBAYO ILISABABISHA KIZAAZAA KIKUBWA KWA ABIRIA WALIOKUWA WAKIENDA ARUSHA KUTOKA TANGA.

WANAFUNZI WAZAA WATOTO, MMOJA AFANYA MTIHANI NA MWANAYE

MKUU WA WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIMPA MTOTO WAKE MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MKALAMO WILAYANI HUMO MTOTO AMBAYE AMEMZAAA NA MWANAFUNZI MWENZAKE MARIAMU MOHAMED AMBAYE PIA NI MWANAFUZNI WA KIDATO CHA NNE AMBAYE HAKUWEZA KUFANYA MTIHANI HUO KWASABABU YA TATIZO HILO.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIWA AMEMSHIKA MTOTO ZAINA JACKSON WA MWANAFUNZI REHEMA MOHAMED AMBAYE NI MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KILOLE WILAYANI HUMO, KUSHOTO NI MWANAFUNZI HUYO AKIWA NYUMBANI KWAO ALIPOTEMBELEWA NA DC HUYO.

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIWA AMEMBEBA MTOTO SALMA MUJIB HUKU AKIMTAZAMA MAMA WA MTOTO HUYO MARIAM MOHAMED AMBAYE NI MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MKALAMO ALIYESHINDWA KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA SEKONDARI MWAKA HUU.

AKAMATWA BAADA YA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

MWANAFUNZI wa shule ya sekondari Mkalamo iliyopo tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, Mujib Ziddy (19), amekamatwa na polisi mara baada ya kumaliza mitihani yake ya kidato cha nne iliyomalizika Alhamisi iliyopita, akituhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo waliokuwa wakisoma darasa moja.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa ni mtunza stoo ya shule hiyo na aliyekuwa akiishi hosteli ya shule hiyo pamoja na mwanafunzi huyo wa kike Mariamu Mohamed (19) ambaye ameshindwa kufanya mtihani huo baada ya kuwa na ujauzito ingawa alijifungua mtoto wa kike Septemba 5 mwaka huu na kachanga hicho kumpa jina la Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma.

Mwanafunzi huyo pamoja na familia yake aliyoongozana nayo na ile ya mwanafunzi wa kike, walifikishwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Erasto Sima kwa ajili ya kuhojiwa kabla ya kuchukuliwa na polisi, alisema kuwa alisema alijisikia vibaya sana mzazi mwenzake kukosa mitihani hiyo ambayo ameifanya licha ya awali kutaka kuzuiwa asifanye kutokana na kosa hilo.

"Kwa kweli nilijisikia vibaya Mariamu kushindwa kufanya mitihani kwasababu yangu, hatukujua kile tulichokuwa tukifanya pale shuleni, nakumbuka tulikuwa tukichukuana na kwenda kwenye moja ya darasa na kufanya mapenzi...Naomba niachiwe huru niweze kukatunza katoto kangu na matokeo yakitoka yakiwa nimefanya vizuri basi niweze kuendelea na masomo yangu," alisema Mujib alipokuwa akihojiwa ofisini hapo kwa Mkuu wa wilaya.

Mkuu wa shule hiyo Bw. Hemed Kimbute alikiri mbele ya mkuu wa wilaya kwamba wakati tukio hilo la binti huyo kupewa ujauzito na mwanafunzi mwenzake na shule kubaini Machi 23 mwaka huu, hawakuweza kutoa taarifa kwa bodi ya shule, Kijiji wala kata kwa ajili ya hatua zaidi ingawa ilipobainika mwanafunzi huyo, kumpa mimba mwenzake, alimtia kamba lakini alikosa ushirikiano na wazazi kumfikisha katika vyombo vya sheria.

"Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ni kweli nakiri sikutoa taarifa lakini baada ya tukio mimi nilimfunga kamba nikakosa ushirikiano wa wazazi lakini nasema kwa tukio hili bora nishike chaki nifundishe na ukuu wenu wa shule siutaki kusalimisha maisha yangu maana tukio hili nimepata mammbo magumu kule siwezi kuishi kwa mazingira yale yaliyopo kule," alisema Bw. Kimbute huku akiwa amehamaki mno kuhusu suala hilo.

Alipobanwa kuhusu vitisho alivyovipata baada ya tukio hilo, Mkuu huyo wa shule ambaye mkuu wa wilaya alikuwa akimtuhumu kwamba amehusika kuchangia kuwepo kwa tukio hilo, alisema sheria za shule zilizopo kuhusu kuwabana wanafunzi waliokuwa hosteli ya shule hiyo ndizo zinamweka pabaya na wanakijiji hatua ambayo ameona ni bora sheria zivunjwe kuliko kuzifuata kuhataraisha maisha yake. Katika hosteli ya shule hiyo wanafunzi wa kike wanaishi bila ya kuwa mwanaglizi usiku (Matron) kwa kuwa shule haina mwalimu mwanamke.

Baba wa Mujib alisema tangu binti huyo alipopata ujauzito huo na mwanae kuhusishwa na mimba hiyo, mwanafunzi huyo aliletewa nyumbani kwao katika kijiji cha Changalikwa ambako wanaishi naye hadi sasa na kwamba lengo lao, binti huyo mwanae atakapokuwa watamfanyia mipango ya kusoma kwa vile mwenye anataka kuenelea na masomo.

"Kwa kweli jambo hili limenisikitisha mno niliamini mwanangu Mujib nimemeleka shule kusoma kumbe mwenzangu ananiletea mtoto na mama yake, siyo jambo zuri la kufurahia kama mzazi nimempokea Mariamu na tunamlea hadi mtoto wake akikua basi na yeye tutampeleka shule," alisema Bw. Mujib Hussein.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo aliwalaumu wazazi wa pande zote kwa kuficha matukio ya namna hiyo ambayo mara nyingi yanalenga kukosesha haki ya msingi ya kusoma kwa mtoto wa kike na kwamba ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kuhakikisha wanafuata sheria kushughulikia matatizo ya watu wanaowapa ujauzito watoto wa shule huku ofisi yake ikiangalia namna atakavyoyashughulikia tabia kama hizo.

Wednesday, October 12, 2011

JULIO NA MAZOEZI KABAMBE YA COASTAL UNION, LENGO NI KUINASUA MKIANI

KOCHA JAMHURI KIHWELO 'JULLIO' AKIWEKA KONI IKIWA NI SIKU YAKE YA KWANZA KUINOA TIMU YAKE MPYA YA COASTAL UNION KWENYE UWANJA WA GYMKHANA AMBAKO TIMU HIYO INACHUKUA MAZOEZI.

WACHEZAJI WA TIMU YA COASTAL UNION WAKIW ANA KOCHA WAO JAMHURI KIHWELO 'JULIO' WAKIFANYA MAZOEZI KWENYE UWANJA WA GYMKHANA JIJINI TANGA AMBAKO TIMU HIYO INAFANYA MAZOEZI.

Tuesday, October 11, 2011

MBUNGE WA KOROGWE ATAKA MASHAMBA YA KATANI LIMITED YASIYOLIMWA WAPEWE WANANCHI WALIME MAHINDI

SHAMBA LA MKONGE LA KAMPUNI YA KATANI LIMITED LILILOPO KATIKA KIJIJI CHA LWENGERA DARAJANI KATA YA KWAGUNDA LIKIWA HALIONYESHI KULIMWA.

MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI STEPHEN NGONYANI 'PROFESA MAJIMAREFU' (KULIA) AKIELEZWA NA DIWANI WA KATA YA KERENGE BW. IDD SHEBILA (KATIKATI) JUU YA MAHITAJI YA WANANCHI YA ARDHI LAKINI KAMPUNI HIYO YA KATANI IMEHODHI MAENEO MAKUBWA LAKINI HAWALIMI HIVYO WAMETAKA SHAMBA HILO LIGAWIWE WANANCHI WALIME.

MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI PROFESA MAJIMAREFU (KULIA) AKIONESHA UKUBWA WA SHAMBA LA MAGUNGA ESTATE LA KATANI LIMITED AMBALO HALIJALIMWA  HALI AMBAYO ANATAKA LIGAWIWE KWA WANANCHI KWA AJILI YA KILIMO. KATIKATI NI DIWANI WA KATA YA KERENGE IDD SHEBILA NA KUSHOTO KABISA NI KATIBU WA MBUNGE HUYO BW. ANDREW NG'ANDU