Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Monday, December 13, 2010

WAANDISHI, WANASIASA VIONGOZI WA DINI KATIKA WARSHA YA UHURU WA HABARI LEO KOROGWE

MZEE WA BONDE AKIWA MMOJA YA WASHIRIKI WA WARSHA YA UHURU WA HABARI KWA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI YENYE MIKOA YA ARUSHA, KILIMANJARO, MANYARA NA TANGA INAYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA WHITE PARROT KOROGWE. WENGINE NI CHARLES MASAYANYIKA TOKA MANYARA (kulia) NA RAMADHANI SIWAYOMBE (kushoto).


WADAU WAKISIKILIZA KWA MAKINI WAWEZESHAJI WAKIELELZEA HAKI YA KUPATA NA KUTOA HABARI.

WAWEZESHAJI WA WARSHA YA UHURU WA HABARI KUTOKA TAASISI YA MISA-TAN KUTOKA KUSHOTO NI MWANASHERIA BW. MOHAMED TIBANYENDERA NA MRATIBU WA WARSHA HIYO BW. ANDREW MALAWITI.


WADAU WAKINUKUU KILE WANACHOKIPATA KUTOKA KWA MWEZESHAJI.


MWEZESHAJI BW. TIBANYENDERA AKISISITIZA NAMNA YA SHERIA MBALIMBALI ZINAVYOELEZEA NAMNA YA UHURU WA HABARI.


MWENYEKITI WA WARSHA HIYO BW. ISMAIL MWISHASHI AMBAYE AMETOKEA WILAYANI PANGANI AKINUKUU KILE ALICHOSIKIA KWENYE WARSHA HIYO.

WADAU DIWANI WA KATA YA MANUNDU BW. ROBERT BAGO  (kushoto), GODFREY MUSHI KUTOKA IRINGA NA RAMADHANI SIWAYOMBE KUTOKA ARUSHA.

Sunday, December 12, 2010

MKUU HATUNUFAIKI NA MRADI HUU TUNAOMBA UTUSAIDIE

BANGO HILI LILISHIKWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA GOMBERO MTAA WA NAIROBI WAKATI MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI MSTAAFU SAIDI KALEMBO ALIPOFIKA NA KAMATI YAKE YA ULINZI NA USALAMA, LAKINI WANANCHI HAWA KABLA UJUMBE WAO HAUJAONWA NA KALEMBO MSHAURI WA MGAMBO WA WILAYA YA MKINGA ILIPOKWENDA KAMATI HIYO MEJA MURO ALIWASARAMBATISHA WANANCHI WALIOCHIKA BANGO HILI HIVYO RC HAKUPATA BAHATI YA KUSOMA BANGO HILI..

POULSEN AIWEZESHA KILIMANJARO STARS KUTWAA UBINGWA WA CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP BAADA YA KUILAZA IVORY COAST BAO 1-0


KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS KILICHOCHEZA LEO NA KUTWAA UBINGWA WA CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP BAADA YA KUIFUNGA IVORY COAST BAO 1-0 LILILOFUNGWA KWA NJIA YA PENALTI NA NAHODHA SHADRACK NSAJIGWA


SIKU MZEE WA BONDE ALIPOAMUA KUVUNJA UKIMYA TANGAMANO LAKINI HAIKUWA KAZI RAHISI

MZEE WA BONDE ALIKUWA MIONGONI MWA WATU WALIOJITOKEZA KUPIMA 'NGWASUMA' KWENYE VIWANJA VYA TANGAMANO WAKATI WA SIKU YA UKIMWI DUNIANI DES MOSI KILA MWAKA 


USIWE NA WASIWASI ACHA NICHUKUE DAMU IMIMINE HUMU BAADA YA DAKIKA MBILI TU MAJIBU YATAKUWA TAYARI USIWE NA WASIWASI KWANI NDEGE HUWA UNACHUKUA HUKO MTAANI?


NGOJA NIWEKE HAYA MAJI SASA HIVI MAJIBU YAKO YATAKUWA TAYARI KWANI UMEOA?


MHESHIMIWA MAGRETH MKANGA MBUNGE WA VITI MAALUM ANAYEWAKILISHA MAKUNDI YA WALEMAVU NAYE ALIMUUNGA MKONO MZEE WA BONDE KWA KUPIMA NGWASUMA KWENYE SHEREHE HIZO.


EEH WEWE MWANAMKE MBONA SINDANO YAKO INAUMA SANA MHH

NYIE MNIANGALIE NIKIPIMA MAJIBU YANGU NIPE MWENYEWE HAPA WASISIKIE WATU WENGINE.


MHESHIMIWA ALITEMBELEA MABANDA MBALIMBALI YALIYOKUWEPO UWANJANI HAPO.


OFISA WA SHIRIKA LA AFRIWAG SISTER FORTUNATA (mwenye blauzi nyeusi) AKITOA MAELEZO KUHUSU KAZI ZINAZOFANYWA NA SHIRIKA HILO KWA MBUNGE WA VITI MAALUM MAGRETH MKANGA.


MTAALAM WA SHIRIKA LA TAWG LINALOTOA HUDUMA ZA UKIMWI AKITOA MAELEZO KWA WANAUNZI JINSI YA NAMNA YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUO.


UKISHAIVALISHA MPIRA KAMA HIVI NA KUITUMIA HAKIKISHA UNAITOA NA KITAMBAA ILI MAJIMAJI YASIKUPATE KWENYE KUCHA ENDAPO UTAKUWA UMEKATA KWA WAKATI HUO.


HAKIKISHA USIFANYE MARA MBILI HUMO KWA HUMO NI MARA MOJA TU UKIFIKA MSHINDO UNAITOA NI MUHIMU USISAHAU HILI.


HIVI VIATU MNATENGENEZA WENYEWE MAANA NI VIZURI KWELI.


AZAM WAFUNGA UWANJA WA MKWAKWANI KWA AJILI YA UKARABATI SEHEMU YA KUCHEZEA 'PITCH', LENGO NI KUENDELEA KUUTUMIA MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU


MAFUNDI NA VIONGOZI WA AZAM FC AKIWEMO MENEJA WA UWANJA WA MKWAKWANI MBWANA MSUMARI (wa kwanza kushoto) WAKIANGALIA MAFUNDI WAKIENDELEA NA KAZI ZA UKARABATI WA PITCH YA UWANJA HUO AMBAO UMEFUNGWA TANGU NOVEMBA 26 MWAKA HUU.
Na Mzee wa Bonde,Tanga
TIMU ya Azam ya Jijini Dar es salaam, imeanza kurekebisha sehemu ya kuchezea (Pitch) ya uwanja wa Mkwakwani ili waweze kuendelea tena kuutumia uwanja huo katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza Januari 16 mwakani baada ya sehemu ya uwanja huo baadhi ya sehemu zake kuwa kipara kiasi cha wachezaji kushindwa kumiliki mpira.

Kutokana na timu hiyo ambayo imekubali kuutumia tena uwanja huo kama ilivyofanya katika mzunguko wa kwanza baada ya uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam kufungwa kupisha sherehe za kuapishwa kwa Rais, tayari umefungwa tangu Novemba 26 ambapo wataalamu wawili kutoka Dar es salaam wameanza kazi ya kuchimbua sehemu hiyo ya kuchezea ili waweze kupanda nyasi mpya.

Meneja wa uwanja huo, Mbwana Msumari aliwataja wataalamu hao kuwa ni Athumani Madenge na Idrisa Nassor ambao wanashirikiana na baadhi ya mafundi waliopo Jijini hapa kuahakikisha kwamba uwanja huo unarudi katika hali yake ya zamani ambao nyasi zake zilikuwa imara na hakukuwa na vipara.

Meneja huyo wa uwanja ambaye pia ni mwenyekiti wa Matawi ya Simba mkoani Tanga, alisema kuwa kazi inayofanyika kwa sasa ni kuchimbuliwa sehemu ya kuchezea yote na kuwekwa udongo mpya na mbolea maalumu kwa matuminzi ya uwanja na kisha kuoteshwa nyasi nyingine mpya ambazo zimetokea Mombasa nchini Kenya ambazo katika kipindi kifupi kijacho zitakuwa zimeshika vizuri tayari kwa mikimiki ya ligi hiyo na nyinginezo.

"Uwanja umechimbuliwa wote na kuwekwa udongo na umeoteshwa nyasi kutoka Mombasa, nyasi hizi zitaota kwa muda mfupi na uwanja wetu utakuwa bora kama zamani, hii ni hatua kubwa ambayo tunawashukuru sana wenzetu wa Azam kwa kuthamini na kutuunga mkono katika uwanja huu haya ni mafanikio ambayo watu wa Tanga tunatakiwa kuwaunga mkono bila kujali kwamba hii ni timu ya mkoa mwingine," alisema Msumari ambaye amekuwa mmoja ya wana michezo wenye ubunifu na mipango ambapo pia amefanikisha uwanja huo kupata kisima ambacho kitakachoondoa tatizo la ukosefu wa maji mara kwa mara.

hata hivyo, Meneja huyo aliviomba vilabu vingine visisite kuutumia uwanja huo kutokana na kuboreshwa na vile vile watu wa mkoa huo kufika kwa wingi kila inapofanyika michezo mbalimbali tofauti na maeneo mengine ambapo huwa wanafika pindi zinapocheza timu za Simba na Yanga tofauti na uwanja huo.

MKAPA ANOGESHA SHEREHE ZA MAHAFALI YA KWANZA YA SEKUCo LUSHOTO

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA AKIWASILI KWENYE VIWANJA VYA CHUO KIKUU CHA SEKUCo KILICHOPO WILAYANI LUSHOTO NA KUILAKIWA NA MAKAMO MKUU WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI PROFESA JOHN SHAO.

MKUU WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI AMBAYE PIA NI ASKOFU MKUU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA (KKKT) DKT ALEX MALASUSA.


ASKOFU MKUU WA KKKT DKT ALEX MALASUSA (kulia) AKISOMA DUA KUFUNGUA RASMI SHEREHE ZA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA SEKUCo.(kushoto) NI MAKAMO MKUU WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI PROFESA JOHN SHAO.


RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA (kushoto) AKIFUATILIA RATIBA YA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA SEKUCo KUSHOTO KWAKE NI MAKAMO MKUU WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI PROFESA JOHN SHAO


MWIMBAJI NYOTA KUTOKA NCHINI SWEDEN LENAMARIA KLIMGVOLL AKIWASALIMIA WAGENI WAALIKWA NA WAHITIMU WA CHUO KIKUU CHA SEKUCo KABLA YA KUTOA BURUDANI KATIKA UKUMBI HUO.


MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI PROFESA JOHN SHAO AKIZUNGUMZA KATIKAMAHAFALI HAYO


MKUU WA CHUO KIKUU CHA SEKUCo AMBACHO NI CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA TUMAINI DKT ANNET MUNGA AKIELEZEA HISTORIA YA KUANZISHWA KWA CHUO HICHO NA SIKU HIYO KUFANYA MAHAFALI YA KWANZA TANGU KIANZE  KUFUNDISHA


LENAMARIA AKIWABURUDISHA WAHITIMU NA WAGENI WALIOFIKA KWENYE MAHAFALI HAYO YALIYOFANYIKA DESEMBA 4 MWAKA HUU. MWIMBAJI HUYO HANA MIKONO YOTE.


RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA AKIHUTUBIA WAGENI WAALIKWA NA WAHITIMU WA CHUO KIKUU CHA SEKUCo ALIPOKUWA MGENI RASMI KWENYE MAHAFALI HAYO YALIYOFANYIKA DESEMBA 4 MWAKA HUU WILAYANI LUSHOTO, PICHA ZOTE NA MDAU RAMADHANI JUMA


Friday, December 10, 2010

...BREAKING NEWS...BASI LA HARAMBEE LACHINJA WATU WATATU, LILIKUWA LIKITOKA DAR KWENDA MOSHI

MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI SAID KALEMBO (SHOTO) AKIZUNGUMZA NA MKUU WA WILAYA KOROGWE BW. ERASTO SIMA.
HABARI zilizotufikia saa 4:12 usiku leo zilizomkariri Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bw. Sima ni kwamba basi la abiria la Harambee lililokuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda Moshi, limepinduka katika mji mdogo wa Mazinde wilayani korogwe na kuua watu watatu papo hapo na watu wengine 36 wamejeruhiwa vibaya na hali zao siyo nzuri.

Habari zaidi za tukio hili tutawajulisheni mara tutakapopata taarifa zaidi kesho asubuhi.

SHEREHE ZA MIAKA 49 YA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM LEO, WATANZANIA TUDUMISHE UZALENDO WA KUIPENDA NCHI YETU




Thursday, December 9, 2010

NICO BAMBAGA KUZIKWA LEO NYUMBANI KWAO MUSOMA

PICHANI NI KIKOSI CHA TIMU YA PAMBA YA MWANZA AMBACHO MAREHEMU NICO BAMBAGA (WA KWANZA KULIA WALIOKAA CHINI) ALIKUWA AKICHEZEA NA KUPATA UMAARUFU HADI UMAUTI WAKE,

MCHEZAJI HUYO ALIFANRIKI JUMATATU WIKI HII KATIKA HOSPITALI YA LUGALO JIJINI DAR ES SALAA KUTOKANA NA UGONJWA WA MAPAFU, BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIDIMIWE-AMIN

GARI AINA YA BENZ LINAUZWA MUONE BW. KANIKI NI BEI POA



GARI LINAUZWA WASILIANA NA BW. ALLY KANIKI WA MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM KWA MAWASILIANO ZAIDI YA KUNUNUA GARI HILO LA TAARIFA MBALIMBALI IKIWEMO BEI YA KUUZIA KWA SIMU NAMBA 0714 637849 AU 0713 871707

HAPA NI ENEO WATU WATAKUTANA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA UHURU

SEHEMU MAARUFU YA MATANUZI KATIKA JIJI LA TANGA...HAPA NI NYINDA UTAPATA MICHEMSHO, NYAMA CHOMA NA VINYWAJI VIKALI NA VYA RANGI YA DHAHABU. LEO ENEO HILI LITAKUWA NA WATU WATAKAOKUWA WAKISHEREHEKEA SIKUKUU YA UHURU, HONGEREENI MIMI NINA MSETO LEO SIKU YA TATU.

...BREAKING NEWS...ASHA BARAKA KUTETA NA PETER MSECHU...!

HABARI AMBAZO ZIMETUFIKIA MUDA HUU IKIWA TAIFA LINASHEREHEKEA MIAKA 49 YA UHURU AMBAYO KAULI MBIU YAKE NI MIAKA 49 YA UHURU TUDUMISHE UZALENDO, NI KWAMBA ASHA BARAKA MMILIKI WA BENDI YA THE AFRICAN STARS BAND 'WANA WA KUTWANGA NA KUPEPETA' ATAKUTANA NA MWIMBAJI PETER MSECHU MSHINDI WA PILI WA MASHINDANO YA TUSKER PROJECT FAME YALIYOMALIZIKA JUMAPILI ILIYOPITA NCHINI KENYA.

ACHA TUSUBIRI TUONE NINI KITAZUNGUMZA MIMI NA WEWE HATUJUI LABDA TUNAHISI KWAMBA MAMA HUYO 'KADA WA CCM' PENINE ANATAKA KUMJUMISHA KIJANA HUYO MAHIRI KWENYE BENDI YAKE ILI KUONGEZA NA KULETA RADHA KWENYE BENDI HIYO.

LEO NI SIKUKUU YA UHURU TUNASHEREHEKEA MIAKA 49 TANGU TUPATE UHURU MWAKA 1961

SHUJAA WA UHURU WA TANZANIA MEJA ALEXANDER GWEBE NYIRENDA AKIWA AMEPANDISHA MWENYE WA UHURU KATIKA KILELE CHA MLIM A KILIMANJARO IKIWA ISHARA YA MWENGE HUYO KUMULIKA MAADUI WALIOKUWA NJE YA MIPAKA YOTE YA TANZANIA. HII ILIKUWA SIKU MOJA KABLA YA TAREHE 9/12/1961

KILIMANJARO STARS YAIDUNGUA RWANDA 1-0 YAFUDHU NUSU FAINALI SASA KUCHEZA NA UGANDA IJUMAA

ZANZIBAR 'MAPINDUZI STARS' YATOLEWA KWA TAAAABU NA UGANDA, YAAGA MASHINDANO KAZI YABAKI KWA KILIMANJARO STARS.

SIKU YA MWISHO YA RAS CHIKIRA AELEZEA ALIVYOWEZESHA KUPATIKANA KWA GARI LA WAGONJWA BOMBO HOSPITALI

AMBULANCE MPYA YA HOSPITALI YA BOMBO IKIZINDULIWA LEO ASUBUHI HOSPITALINI HAPO NA MKUU WA MKOA MEJA JENERALI SAID KALEMBO

MKUU WA MKOA MEJA JENERALI (MSTAAFU) SAID KALEMBO AKIWA NA MGANGA MKUU MFAWIDHI WA HOSPITALI YA MKOA BOMBO DKT ALFRED MTATIFIKOLO AKIMUONESHA ZANA MBALIMBALI ZILIZOMO NDANI YA GARI HILO LA KISASA LILILONUNULIWA NA KAIBU TAWALA BW. PAUL CHIKIRA.

HAPA MGONJWA AKIWEKWA HUMU NDANI NI KUZURI KULIKO KULE WODINI CHEKI HAPA TUTAWEKA JUICE NA CHAI ATAKUWA ANAKUNYWA TU INGAWA KULE WODINI TUNAWAPA CHAKULA LAKINI HIKI CHA HUMU NDANI KITAKUWA BAABUU KUBWA...DKT MTATI ANAELEKEA KUMWELEZA HIVYO GENERAL KALEMBO. WEE ANGALIA TU PICHA.


HAPA KWA MFANO GARI LIMESHINWA KUWAKA KAMA LIMEISHIWA MAFUTA TUNACHOMEKA CABLE YA UMEME LINAFANYA KAZI KAMA NI OPERESHENI INAENDELEA HUMO NDANI YA GARI HILI SIYO MCHEZO TUMSHUKURU SANA MZEE CHIKIRA


KWA KWELI MKUU MANENO ULIYOSEMA NIMEYASIKIA NA NIMEELEWA KWAMBA GARI HILI LIMENUNULIWA KWA MSAADA WA (...) HALAFU TUTALITUNZA ILI LIWEZE KUTUMIKA MUDA MREFU UNAJUA HILI GARI LIMEFANYA HATA RAS AMEFIKA HAPA KWA MARA YA KWANZA HAJAWAHI KUFIKA NAKUMBUKA MOHAMED ABDULAZIZ ALIKUJA HAPAMWENYEWE NA WEWE HAPA SIKU YAKO YA KWANZA ALIKULETA KATIBU TARAFA YULE RAMADHANI SHEMNGWA AKAKUTAMBULISHA KWETU LAKINI HUYU BWANA HAKUWEPO LEO TUNAMUONA HAPA HALAFU ANASEMA KANUNUA YEYE HILI GARI...!


KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAGUNDUA UFISADI WA MABILIONI YA SHILINGI JENGO LA HALMASHAURI YA MKINGA

MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI (MSTAAFU) SAID SAID KALEMBO AKIMPONGEZA MKULIMA WA KIKUNDI CHA TUPENDANE BAMBA MWARONGO KILICHOPO KATA YA MTIMBWANI WILAYANI MKINGA ALIPOKUWA AKIKABIDHI MATREKA MADOGO (POWER TILLER) KWA VIKUNDI TISA MATREKTA YENYE THAMANI YA SH. 51,600,000 KWA VIKUNDI HIVYO.


HAIWEZEKANI HADI SASA JENGO HILI HALIJAKWISHA NA HILI NDUGU WAJUMBE LAZIMA TUANGALIE SUALA LA ZABUNI ZINAZOTOLEWA KWA MAJENGO YA SERIKALI KWA HAWA WAKANDARASI AMBAO HAWANA UWEZO KAMA ANGEKUWA NA FEDHA ANGEJENGA KWA FEDHA ZAKE HALAFU AKAIDAI SERIKALI BAADAYE, MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI MSTAAFU ALIPOKAGUA JENGO LA OFISI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKINGA AMBALO HADI SASA TAYARI LIMETUMIA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 1.9 NA HADI KUKAMILIKA LITAGHARIMU KIASI CHA SHILINGI BILIONI 2.4.


MGANGA WA WILAYA YA MKINGA MR KISHIWA AKISOMA TAARIFA YA UJENZI WA NYUMBA YA MGANGA NA KICHOMEO TAKA CHA ZAHANATI KATIKA KIJIJI CHA KIBIBONI KWA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA CHINI YA MWENYEKITI WAKE MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI (MSTAAFU) SAID KALEMBO ALIPOTEMBELEA WILAYA HIYO JUZI. NUMBA HIYO YA MGANGA NA KICHOMEO TAKA KWA MUJIBU WA BW. KISHIWA VIMEGHARIMU KIASI CHA SH. 24,985,900.


HAPA NI KITONGOJI CHA NAIROBI KIJIJI CHA GOMBERO AMBAKO WAJUMBE WA KAMATI HIYO WALIPOFIKA WALIPOKELEWA NA BANGO LA WANANCHI WANAOPINGA MRADI WA BOMBA LA MAJI SAFI WAKIWA NA MALALAMIKO KWAMBA MRADI HUO NI MBOVU LAKINI WALIZUIWA NA ASKARI WALIOKUWEPO NA KISHA MTAALAMU WA MAJI WA WILAYA (PICHANI) ALISOMA TAARIFA YAKE KWA MKUU HUYO WA MKOA KWAMBA MRADI UO UMEGHAIMU KIASI CHA SH. 41,485,540,00.


MWISHO MKUU HUYO WA MKOA ALIWAOMBA WANANCHI WILAYANI MKINGA KUKUBALI MABADILIKO KWA KUTOA MICHANGO YAO PANAPOJITOKEZA KAZI ZA UJENZI WA SHULE, ZAHANAI NA MIRADI YA MAENDELEO NA VLE VILE ALIWATAKA WALIME KISASA WAACHE KULIMA KWA MAZOEA.


Wednesday, December 8, 2010

RC KALEMBO KUINGIA MITAANI KUKAMATA WAZUNGU, NI BAADA YA UHAMIAJI MKOA KUNUKA RUSHWA

                        Na Mzee wa Bonde,Mkinga
MKUU wa mkoa wa Tanga, Meja Jenerali (Mstaafu) Said Kalembo, amesema ataingia mtaani akishirikiana na Kamanda wa polisi mkoani hapa, ACP Liberatus Sabas, kuwasaka na kuwakamata raia watatu wa kigeni, wanaorandaranda mkoani hapa bila shughuli maalum na Idara ya Uhamiaji mkoani hapa kushindwa kufanya hivyo kwa kile alichodai 'kupewa kitu kidogo'.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa iliyofanya kikao chake wilayani hapa jana, Mkuu huyo wa mkoa alisema analazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kuchoshwa na watumishi wa Uhamiaji mkoani hapa ambao amekuwa akipokea malalamiko mengi kwamba wanawaachia wageni waishi bila vibali na hata waliokuwa na vibali vilivyokwisha muda wake.

Alisema anazo taarifa kwamba wapo 'wazungu' watatu ambao wamekuwa wakizurura hovyo katika mitaa ya Jiji la Tanga, kuchukua wanawake na kuzunguka kwa visingio kuwa ni wawekezaji na  wanachokifanya mkoa huo haujui lakini idara ya uhamiaji wanaohusika na uchunguzi na kuwakamata watu wa namna hiyo hawafanyi chochote badala yake wazungu hao wanatanua mitaani.

Jamani hivi hawa uhamiaji vipi, kuna siku nitaaingia mitaani kuwakamata nitamuuomba RPC huyu niwe naye nitawakamata na kuwaweka ndani, Uhamiaji wapo lakini kila mtu anasema Msuya (Danny Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga) anakula rushwa...Sasa ukiona RC anaingia mtaa wakati wanaohusika wapo wanalipwa mshahara na serikali basi kuna tatizo na haiwezekani, hebu watu wa uhamiaji kama wapo shughulikieno hili ni aibu hizo rushwa zitawatokea puani," alisema Bw. Kalembo bila kuwataja wazungu hao.

Akizungumiza tuhuma hizo Bw. Msuya ambaye hakuhudhuria kikao hicho cha kamati ya usalama mkoa, alikiri kuwepo kwa wazungu hao lakini hata hivyo alikanusha kuhusika na rushwa akidai kwamba kama amekuwa akipokea rushwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ingekuwa imemkamata muda mrefu tangu malalamiko ya kupokea rushwa yanayomuandama mkoani hapa.

Aliwataja wazungu hao na kuanisha muda wa kwisha vibali vyao kuwa ni pamoja na Bw. Luitren Zijistra raia wa Uholazi anayefanya shughuli kiwanda cha maziwa na kibali chake kinamalizika Aprili 24 2012 na hana matatizo, mwingine aliyemtaja ni Bw. Zingaro Giussepe raia wa Italy ambaye kibali chake kimekwisha na Bw. Stephen Peter raia wa Ujerumani ambaye ana kibali cha Maendeleo ya Miundombinu ya Utalii.

"Unajua hawa wazungu wana vibali na huyu Stephen anakibali cha Toursim Infastructure Development amepewa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi na kinaisha Februari 26 mwakani sasa anavyozunguka hapa mjini maeneo ya Mkinga huko anaonekana hana kibali kumbe la na huyu Bw. Giussepe kweli kibali chake kimekwisha na mimi nimemwandikia barua Desemba 2 kumweleza kwamba hatutamuongeza tena na huyu Bw. Luitren sioni matatizo yake, lakini kama Mkuu wa mkoa anasema labda hawakumpa taarifa vizuri," alisema Bw. Msuya.

Bw. Msuya alikiri kwamba alishawahi kuitwa na Mkuu wa mkoa ofisini kwake akaelezwa kwamba amekuwa akijihusisha na rushwa mara kwa mara madai ambayo aliyakanusha ingawa Mwandishi wa Habari hizi aliwahi kuwanukuu baadhi ya wafanyakazi wake katika ofisi hiyo ambao walidai kuwa kazi zote zinazowahusu watu weupe mkuu huyo amekuwa akizifanya yeye.

"Bosi wetu akija Mhindi utakuta anawaita ofisini kwake hataki kutuachia kwa kweli amekuwa akipenda sana kufanya kazi za watu weupe wazungu huwa anawafuata huko huko kwenye viwanda hata kama vibali vyao vimekwisha Mkuu wa mkoa hasemi uongo bosi wetu hatusemi moja kwa moja anakula rushwa lakini hata sisi anatutia mashaka," alisema ofisa mmoja wa Uhamiaji aliyekuwepo ofisini jana.

FEDHA ZA KUNUNULIA SAMANI OFISI YA MBUNGE 'WA MBEYA ZATAFUNWA' NA WAJANJA, NI OFISI YA SUGU

                         Na  Thobias Mwanakatwe,Mbeya
FEDHA zilizotengwa na halmashauri ya Jiji la Mbeya mwaka 2004/2005 kwa ajili ya  kuhudumia ofisi ya Mbunge wa Mbeya Mjini ikiwemo kununulia samani mbalimbali kiasi cha sh. 2,870,360, zimebainika kuyeyuka kifisadi kwa vile samani hizo hazipo.
 
Kwamujibu wa nyaraka zilizopeleka na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kipindi hicho wakati huo ikiwa Manispaa kwenda katika ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya,zinaonyesha kuwa fedha hizo zilitumika kununulia samani za ofisi ya mbunge wa Mbeya Mjini pamoja na kuikarabati kazi ambayo haikufanyika.
 
Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Damson Ntangu akizungumza katika mahojiano na blogu hii ambayo ilitaka kufahamu fedha za kuhudumia ofisi za wabunge zinatumika vipi kwasababu ofisi ya mbunge wa Mbeya Mjini haina hata samani moja jambo ambalo hadi sasa limesababisha mbunge huyo kushindwa kukabidhiwa ofisi rasmi kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi.
 
Alisema ingawa bado haijawekwa wazi jukumu la kuzihudumia ofisi za wabunge ni la nani, lakini hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Mbeya kwa sasa Jiji, mwaka 2004/2005 ilitumia Sh.2,870,360 viti sita,Sofa kochi seti moja,meza kubwa moja,na zuria lenye ukubwa wa mita 15.
 
Ntangu alisema kutokana na hali hiyo madai yanayotolewa kwamba ofisi ya Mbunge wa Mbeya mjini haina samani wanaopaswa kulitolea maelezo ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambayo kwa mujibu wa nyaraka za barua ilieleza kuwa imetumia kiasi hicho cha fedha kununulia samani za ofisi hiyo.
 
Uchunguzi zaidi wa blogu hii umebaini kuwa  katika kipindi hicho pia kiasi cha  Sh,3,165,000 zilitolewa na serikali kuu ili zisaidie kuhudumia ofisi ya mbunge wa Mbeya mjini ambazo zilikabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya na pia nyaraka hizo zinaonyesha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2006/2007 hakuna fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuhudumia ofisi ya mbunge.
 
Wakati utata ukigubika katika ofisi ya Mbunge wa Mbeya mjini, kwa upande wa ofisi ya Mbunge wa Mbeya vijijini (CCM),Mch.Luckison Mwanjale,ofisi yake ipo bomba ambapo kulingana na nyaraka zilizopo ni kwamba kwa mwaka 2004/2005  Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini,ilitumia Sh.10,300,000 kwa ajili ya kutengeneza na kununulia samani za ofisi hiyo kazi ambayo imefanyika kwa umakini mkubwa.
 
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya,Juma Rashid Idd, akizungumzia suala hilo alisema kimsingi ofisi za wabunge zipo chini ya Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya ambao ndio wanapaswa kutolea maelezo na kwamba Halmashauri inachokifanya ni kutoa ofisi hizo lakini huduma zote kwa maana ya kununua samani siyo jukumu la halmashauri.
 
Mbunge wa Mbeya Mjini,(Chadema), Joseph Mbilinyi,hadi sasa bado hajakabidhiwa ofisi kuanza kazi kwasababu ofisi iliyokuwa ikitumika na aliyekuwa mbunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Benson Mpesya, haina samani hata moja .
 
Ofisi hiyo ilibainika kwamba haina samani zinazotakiwa baada ya mbunge huyo kwenda kwa Mkurugenzi wa Jiji,Juma Rashid Idd kwa lengo la kukabidhiwa rasmi ili aanze kazi za kuwatumikia wananchi wa Jiji la Mbeya.
 
Ofisi hiyo ya mbunge ambayo ipo katika majengo ya zamani ya Halmashauri ya Jiji yaliyopo karibu na kituo Kikuu cha Polisi Mbeya mjini, mbali na kukosa samani muhimu, lakini pia hakukuwepo na makablasha (files) ambayo hutumika kuhifadhia nyaraka mbalimbali za kiofisi,ikiwemo mipango iliyotekelezwa na inayotarajia kutekelezwa na mbunge.