MZEE WA BONDE ALIKUWA MIONGONI MWA WATU WALIOJITOKEZA KUPIMA 'NGWASUMA' KWENYE VIWANJA VYA TANGAMANO WAKATI WA SIKU YA UKIMWI DUNIANI DES MOSI KILA MWAKA |
USIWE NA WASIWASI ACHA NICHUKUE DAMU IMIMINE HUMU BAADA YA DAKIKA MBILI TU MAJIBU YATAKUWA TAYARI USIWE NA WASIWASI KWANI NDEGE HUWA UNACHUKUA HUKO MTAANI? |
NGOJA NIWEKE HAYA MAJI SASA HIVI MAJIBU YAKO YATAKUWA TAYARI KWANI UMEOA? |
MHESHIMIWA MAGRETH MKANGA MBUNGE WA VITI MAALUM ANAYEWAKILISHA MAKUNDI YA WALEMAVU NAYE ALIMUUNGA MKONO MZEE WA BONDE KWA KUPIMA NGWASUMA KWENYE SHEREHE HIZO. |
EEH WEWE MWANAMKE MBONA SINDANO YAKO INAUMA SANA MHH |
NYIE MNIANGALIE NIKIPIMA MAJIBU YANGU NIPE MWENYEWE HAPA WASISIKIE WATU WENGINE. |
MHESHIMIWA ALITEMBELEA MABANDA MBALIMBALI YALIYOKUWEPO UWANJANI HAPO. |
OFISA WA SHIRIKA LA AFRIWAG SISTER FORTUNATA (mwenye blauzi nyeusi) AKITOA MAELEZO KUHUSU KAZI ZINAZOFANYWA NA SHIRIKA HILO KWA MBUNGE WA VITI MAALUM MAGRETH MKANGA. |
MTAALAM WA SHIRIKA LA TAWG LINALOTOA HUDUMA ZA UKIMWI AKITOA MAELEZO KWA WANAUNZI JINSI YA NAMNA YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUO. |
UKISHAIVALISHA MPIRA KAMA HIVI NA KUITUMIA HAKIKISHA UNAITOA NA KITAMBAA ILI MAJIMAJI YASIKUPATE KWENYE KUCHA ENDAPO UTAKUWA UMEKATA KWA WAKATI HUO. |
HAKIKISHA USIFANYE MARA MBILI HUMO KWA HUMO NI MARA MOJA TU UKIFIKA MSHINDO UNAITOA NI MUHIMU USISAHAU HILI. |
HIVI VIATU MNATENGENEZA WENYEWE MAANA NI VIZURI KWELI. |
No comments:
Post a Comment