Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, December 21, 2010

SHEHENA YA MADAWA YA KULEVYA YALIYOKAMATWA TANGA, HAYA HAPA

Said Zuke wa kwanza kushoto akiangalia madawa ya kulevya akiwa na Kamanda wa  polisi mkoani Tanga ACP Liberatus Sabas


Askari wa Kikosi cha Kupambana na Uhalifu (Ant-Robbery) Said Zuke (anayefungua furushi lililojaa madawa ya kulevya) mbele ya Waandishi wa Habari kushoto kwake ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga ACP Liberatus Sabas na maofisa wengine wa polisi wa kwanza aliyekaa ni mwandishi wa gazeti la Nipashe Lulu George akishuhudia shehena hiyo ya madawa ya kulevya iliyokamatwa na jeshi hilo.

Said Zuke akifungua furushi hilo la madaya ya kulevya.

Hapa Said Zuke akiijaribu madawa hayo ya kulevya akihakiki kama ni yenyewe.


Madawa haya ni yenyewe na ni makali sana.

Zuke na Ofisa wa Operesheni mkoani Tanga ASP Ussa na askari mwingine wa Ant-Robbery wakiangalia madawa hayo.

Na Mdau wetu
JESHI la Polisi mkoani Tanga, linawashikilia watu wawili wakazi wa Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye uzito wa kilo 50.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo ACP Liberatus Sabas alisema kuwa watu hao walikamatwa Desemba 19 majira ya saa 9:30 katika kizuizi cha polisi Kabuku wilayani Handeni wakiwa kwenye gari dogo aina ya Mitsubish Pajero lenye namba za usajili KAW 276G.

Kamanda aliwataja watu hao kuwa ni Rashid Salim maarufu kwa jina la Chodoma (40) mkazi wa Magomeni Mwembechai Dar es salaam na Ismail Shebe (36) mkazi wa Kiwalani Jijini humo Dar es salaam.

Alisema watuhumiwa hao walikuwa wakitokea Jijini Dar es salaam kuelekea nchini Sudan kupitia Nairobi nchini Kenya wakitumia gari hilo ambalo lilikuwa na sehemu maalum iliyotengenezwa kuhifadhia madawa hayo.

Kamanda Sabas alisema watuhumiwa baada ya kupekuliwa Chodoma alikutwa na hati ya kusafiria yenye namba AB012971 iliyotolewa Agosti Mosi mwaka 2005 na Shebe alikuwa na hati AB293433 iliyotolewa Septemba 3, 2009.

Watuhumiwa hao kwa sasa wanashikiliwa katika kityuo kikuu cha polisi Chumbageni Jijini Tanga, kwa ajili ya mahojiano zaidi na kwamba wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara uchunguzi wa polisi utakapokamilika.

GARI LAPINDUKA NA KUTEKETEA KWA MOTO MBEYA, SITA WAFA, 11 WAJERUHIWA VIBAYA


HAYA ONA HILI UNADHANI KUNA WATU WAMEPONA HUMU?


MAGARI KAMA HAYA NYAKATI HIZI ZA MWISHO WA MWAKA LAZIMA MADEREVA WAKE WAWE MAKINI VINGINEVYO YATAKUWA KAMA HIVI NA KUPOTEZA ROHO ZA WATU BURE.
         Na Mdau Thobias Mwanakatwe,Mbeya
WATU sita wamekufa kwa kuteketea kwa moto na wengine 11 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kwenda wilayani Makete mkoa mpya wa Njombe (Njoluma) kupinduka na hatimaye  kuwaka moto.
 
Tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa tano asubuhi limehusisha gari aina ya Rand Lover ambalo hata hivyo namba zake za usajiri hazijajulikana kutokana na kuteketea kwa moto.
 
Abiria walionusurika katika ajli hiyo ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya,wamesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Kimondo kata ya Ulenje wilaya ya Mbeya Vijijini ambapo ilikuwa imebeba abiria na kupakiza mafuta ya Petroli juu ya Keria na ndani ya gari.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Advocate Njombi amesema atatoa taarifa rasmi za tukio hilo baada ya kuletewa na askari ambao wapo eneo la tukio.
 
Hata hivyo Askari wa Kikosi cha Usalama Barabara wakizungumza na mdau wa Blogu hii kwa simu katika eneo la tukio wamesema waliokufa ni watu sita ambapo kati yao watoto wadogo ni wawili na watu wazima wanne.
 
Mmoja wa Majeruhi wa ajali hiyo,Hilda Japhet (25) mkazi wa Uyole Mbeya,akizungumza na mdau wa Blogu hii katika hospitali ya Rufaa Mbeya alikolazwa alisema kutokana na ajali hiyo watoto wake wawili wamekufa kwa kutetea na moto.
 
Daktari wa zamu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk.Dominick Chalu, alisema kufuatia tukio hilo wamepokea majeruhi kumi na moja ambao wamelazwa katika hospitali hiyo na kwamba wawili kati ya hao hali zao ni mbaya.
 
Aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni pamoja na watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano ambao ni Evance Stephen na Latifu Labiso mkazi wa Ntokela wilayani Rungwe.
 
Dk.Chalu aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Bahati Mwavipa (50) kazi wa Uyole Mbeya,Sara Charles (50) mkazi wa Rungwe,Victoria Sanga (10),Okoka Matamsi, mkazi wa Mwanjelwa Mbeya,Huruma Israel,Jane Mbalila,Vailet Stephen mkazi wa Kanyegele na Judy Erick mkazi wa Mbalizi-Mbeya.
 
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo,Okoka Matamsi, akizungumzia ajali hiyo alisema wakati wakiwa njia kuelekea wilayani Makete ghafla gari hilo lilipinduka na kuanza kuteketea kwa moto.
 
Matamsi ambaye alikuwa akizungumza huku akiwa amewekewa maji ya dawa (drip), alisema baada ya gari hilo kupinduka lilianza kuteketea kwa moto ambao ulikolezwa na mafta ya Petroli ambayo yalikuwa yamepakizwa juu ya keria baada ya kupasuka kutokana na ajali hiyo.
 
Alisema kutokana na ajali hiyo abiria ambao hawakujeruhiwa sana walipata upenyo wa kukimbia kutoka eneo moto ulipokuwa unawake na kusogea pembeni ambao walioungua ni wale ambao walishindwa kujinasua toka ndani ya gari hilo.
 
Kufuatia ajali hiyo wakati wa kaya Ulenje wamelitaka Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya kupiga marufuku kupakiza mafuta ya petrol na dieseli katika magari aina ya Rand Lover ambayo ndiyo yanafanya safari ya kutoka Mbeya kwenda Makete ili kuepusha vifo visivyokuwa vya lazima.
 
Wakati huohuo,abiria wawili kati ya watu waliojeruhiwa kufuatia ajali ya ndege ndogo iliyotokea juzi katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya wameruhusiwa baada ya hali zao kuwa nzuri.
 
Ndege hiyo ambayo ni ya kampuni ya Air Z tofauti na ilivyoelezwa juzi kuwa ni ya Tropical wakati siyo kweli yenye namba SH-PCN  U206F ilianguka majira ya saa 6;39 juzi katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege Mbeya kuelekea Dar es Salaam.
 
Majeruhi walioruhisiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri ni Muuguzi Frorence Stephen na Rubani wa ndege hiyo, Keyuln Fakhard raia wa Iran ambaye amechuliwa na kupelekwa Zanzibar.
 
Hata hivyo Dakrati wa Hospitali ya Rufaa kitengo cha Mifupa, Dk.Jons Chitemo, ambaye alivunjika mkono kutokana na ajali hiyo bado amelazwa na anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
MWISHO

Monday, December 20, 2010

WAZUNGU KUTOKA OHIO, TOLEDO WATEMBELEA WAJASIRIAMALI WA KIKUNDI CHA TWAN

MAMA NKUBA (katikati) AKIWA NA WAGENI WAO KUTOKA NCHINI MAREKANI KATIKA JIMBO LA OHIO KATIKA MJI WA TOLEDO AMBAO NI MJI DADA NA JIJI LA TANGA. KUSHOTO NI SHERRY DANSEL NA MWENZAKE MARTIN NAGGY.

MARTIN NAGGY (kulia) NA SHERRY DANSEL (kushoto) NA KATIKATI NI MWENYEJI WAO MEFAKH DIWANI

BI HUSNA AKIWA NA WAGENI WA KUTOKA TOLEDO.

MARTIN NAGGY ALIPOTEMBELEA MOJA YA WAJASIRIAMALI WA KIKUNDI CHA TANGA WOMAN ASSOCIATION GROUP (TWAN)


WANA-KIKUNDI CHA TWAN WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAGENI WAO WA KUTOKA NCHINI MAREKANI JIMBO LA OHIO TOLEDO.


BREAKING NEWS...AJALI NYINGINE YAUA SITA MBEYA

HABARI AMBAZO TUMEZIPATA MUDA HUU NI KWAMBA WATU SITA WALIOKUWA WAKISAFIRI KWENYE GARI DOGO KUTOKA MBEYA KWENDA WILAYANI MAKETE KATIKA MKOA MPYA WA NJOMBE, WAMEFARIKI BAADA YA KUPATA AJALI KISHA PETROLI WALIYOKUWA WAMEIBAKIZA JUU YA GARI KULIPUKA, TAARIFA ZAIDI TUTAWAPA PUNDE.

Sunday, December 19, 2010

MWANAFUNZI AFA KATIKA AJALI YA NDEGE MBEYA, WENGINE WAJERUHIWA

Wananchi wa eneo la Uyole lililopo nje kidogo ya Jiji la Mbeya wakiiangalia ndege iliyoanguka eneo hilo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watatu kujeruhiwa.


                        Na Thobias Mwanakatwe,Mbeya
MWANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Swilla iliyopo Mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya Vijijini, Godfrey Mpoli, amefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya ndege  ndogo waliyokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kwenda Dar Es Salaam kuanguka mjini hapa.
 
Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Tropical-Air Z yenye namba SH-PCN  U206F imeanguka majira ya saa 6;39 katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege Mbeya kuelekea Dar es Salaam.
 
Taarifa ambazo Blogu ya Watu na matukio imezipata ni kwamba ndege hiyo ilikodiwa na Mfuko wa Bima ya Afya kwa ajili ya kuja kumchukua Mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa ni marehemu.
 
Mwanafunzi huyo aliyefariki amemaliza kidato cha Nne mwaka huu katika shule hiyo ambapo alikuja kuchukuliwa kukimbizwa kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
 
Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya,Suma Kibopile, akizungumza na Blogu hii ,alisema kufuatia ajali hiyo wamepokea majeruhi watatu ambao ni pamoja na Daktari wa Rufaa kitengo cha Mifupa, Dk.Jons Chitemo, ambaye alikuwa akimsindikiza mwanafunzi huyo kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Kibopile alisema majeruhi wengine wa ajali hiyo ni Rubani wa ndege hiyo,Keyuln Fakhard raia wa Iran ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kupata mshituko baada ya kupata taarifa kuwa mwanafunzi aliyekuja kumchukua amefariki dunia na Muuguzi Frorence Stephen ambaye hata hivyo ametibiwa na kuruhusiwa.
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Venance Balama, ambaye alifiki eneo la tukio amesema kuwa ajali hiyo imeleta historia nyingine kwani mwaka 2006 kulitokea ajali ya ndege katika uwanja huo ambapo Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Juma Akukweti alipata ajali na kufariki wakati ametoka kuangalia soko la Mwanjelwa lililoungua mwaka huo.
 
Balama alisema ajali ya ndege iliyotokea jana nayo imekuwa siku chache tu baada ya kuungua kwa Soko kuu la Uhindini mapema mwezi huu.  

BREAKING NEWS...NDEGE YAANGUKA MBEYA NA KUUA MTU MMOJA WATATU WAJERUHIWA



HABARI AMBAZO ZIMETUFIKIA MUDA HUU ZINASEMA KUWA NDEGE NDOGO IMEANGUKA KATIKA ENEO LA UYOLE MBEYA NA MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA WATU WATATU WAMEJERUHIWA, HABARI KAMILI NA TUKIO ZIMA TUTAWALEETEENI PUNDE.

IDD AZAN AONGOZA MAZISHI YA ABUU SEMHANDO, MUHEZA

MAREHEMU ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA'
KOMRADHI WAPENDWA WASOMAJI WA BLOGU HII KUTOKANA NA SABABU AMBAZO ZIPO NJE YA UWEZO WETU TUMESHINDWA KUKUWEKEENI PICHA HII INATOKANA NA SABABU AMBAZO HAZIKUWEZA KUEPUKWA LICHA YA KUWEPO KATIKA ENEO LA TUKIO HADI MWISHO, ISIPOKUWA TUNAKULETEENI MAELEZO YA WATU MUHIMU WALIOZUNGUMZA KATIKA ENEO LA TUKIO HAPO CHINI, SAMAHANI SANA.

Na Mzee wa Bonde
MBUNGE wa jimbo wa Kinondoni Jijini Dar es salaam, Idd Azan amewataka wanamuziki nchini kuiga mfano wa marehemu Abuu Semhando 'Baba Diana' kuwa mvumilivu katika kipindi kirefu alichokaa katika bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' tangu ilipoundwa na kupata umaarufu baadaye.

Mbunge huyo alizungumza hayo alipokuwa kitoa nasaha zake kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Kinondoni ambapo alisema marehemu alikuwa mwanzilishi wa bendi hiyo ambayo ilianza ikiwa haina umaarufu lakini kwa kushirikiana na wenzake ilipata umaarufu hivyo akawasihi wanamuziki kuiga mfano huo wa uvumilivu.

"Kwa kweli nimesimama hapa kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kinondoni wote walikuwa waje hapa kumzika kipenzi chao Abuu lakini wameshindwa na kwakuwa mimi ni mwakilishi wao nimewawakilisha...Kimsingi ningependa kutoa wito kwa wanamuziki waliobaki waige mfano wa marehemu katika suala zma la uvumilivu, alianza Twanga Pepeta ikiwa haina mashabiki alivumilia hadi leo Twanga ni bendi maarufu kama angeondoka angeweza lakini alivumilia hadi mauti umemchukua, wengine igeni mfano huo," alisema Bw. Azan ambaye alitoa ubani wa sh. 200,000.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Baraka Msilwa alisema marehemu ameacha pengo kubwa ambalo haawaamini kama litazibika katika kipindi kifupi ijacho kwa kuwa marehemu alikuwa ni kiungo kati ya uonozi na wanmuziki na kwamba likuwa akitoa ushuri mwingi wa kuieneleza bendi hiyo

Alisema kuwa marehemu licha ya kutoa ushauri pia alikuwa akisaka vipaji vya wanamuziki wengine na kuchukulia na bendi hiyo hiyo kifo chake kitaacha pengo kubwa ambalo liadumu muda mrefu hadi kuzibika hivyo kama viongozi wa bendi hiyo wameguswa mno na kifo chake.

Miongoni mwa watu waliohudhuria ni baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo wakiwemo wacheza shoo na Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijiji Profesa Maji marefu, mwakilishi wa TOT Plus mkoani Tanga, Salim Bawazir na watu wengine ambao waliupokea msiba huo kwa majonzi makubwa.

DADPS KOROGWE YAMWAGA PIKIPIKI KWA MAAFISA UGANI

MMOJA WA MAOFISA UGANI WA KOROGWE AKIKAGUA PIKIPIKI

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA (wa pili kulia juu ya baraza) AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KOROGWE  KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI PIKIPIKI KWA MAOFISA UGANI. WA KWANZA KUSHOTO NI MJEMA MWETA OFISA KILIMO NA MIFUGO WA WILAYA YA KOROGWE.


MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIWASHA MOJA YA PIKIPIKI HIZO HUKU MAOFISA UGANI NA WATUMISHI WENGINE WA HALMASHAURI HIYO WAKIMUANGALIA.


MKUU WA WILAYA YA KOROGWE BW. ERASTO SIMA AKIWASHA MOJA YA PIKIPIKI HIZO.

HARAKATI KUELEKEA MAPINDUZI YA KIJANI………
DADPS  YAMWAGA  PIKIPIKI KWA MAAFISA UGANI KOROGWE
Na mdau Fatna Mfalingundi,Korogwe
Katika jitihada za kutekeleza dhana ya kilimo kwanza kwa vitendo,Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Kupitia mpango wa Maendeleo ya Kilimo wa Wilaya (DADPS) imegawa pikipiki zenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa Maafisa Ugani sita wa Kata za Dindira, Mazinde,Vugiri,Mkalamo na katika skimu ya umwagiliaji ya Mombo.
Akitoa taarifa ya pikipiki hizo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Mkuu wa Idara ya Kilimo,Mifugo na Ushirika Bw.Mjema Mweta alisema kuwa pikipiki hizo ni mwendelezo wa manunuzi ya pikipiki 14 ambazo tayari zimekwishanunuliwa na kwamba wanatarajia kununua sita nyingine katika mwaka huu wa fedha wa 2010/2011.
Bw.Mjema aliongeza kuwa lengo la Halmashauri ni kuwapatia Wagani wengi zaidi vyombo vya usafiri ili kuboresha ufanisi katika utendaji kazi wao ikiwemo kuwahudumia Wakulima wengi na kwa urahisi zaidi hivyo kuleta Mapinduzi ya kijani na hatimaye kupunguza umasikini.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bw.Erasto Sima aliyekuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo aliwataka Wagani hao kuzitumia pikipiki hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuweza kuleta tija katika Sekta ya kilimo na kuonya kuwa atakayekiuka malengo na kugeuza matumizi kama vile kuzifanya “bodaboda” au nyenzo ya kuzifikia “nyumba ndogo” zake atakiona cha Mtemakuni.
Nao Wagani hao walishukuru kwa kupatiwa vitendea kazi hivyo na kueleza kuwa vitawarahisishia sana utendaji kazi na kuongeza ufanisi kwani kabla ya kupatiwa nyenzo hizo za usafiri  ilikuwa ngumu sana kwao kuwafikia Wakulima wote wenye mashamba binafsi na mashamba darasa.Aidha waliahidi kuzitumia katika malengo yaliyokusudiwa. 

Saturday, December 18, 2010

ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' KUZIKWA KESHO SAA 4:00 ASUBUHI KIJIJINI KWAO KIBANDA WILAYANI MUHEZA,TANGA

MAREHEMU ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA'


PIKIPIKI AMBAYO MAREHEMU ALIKUWA AMEPANDA NA KUPATA AJALI MBAYA KATIKA ENEO LA AFRICANA MBEZI, TANGIBOVU.

GARI AINA YA BENZI LINALODAIWA KUHUSIKA NA KIFO HICHO LIKIWA LIMEINGIA KWENYE MTARO BAADA YA KUMGONGA 'BABA DIANA' KWA NYUMA YA PIPIKI YAKE.

MAREHEMU ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' AMBAYE NI MPIGAJI WA DRAMU KATIKA BENDI YA AFRICAN STARS BAND (kushoto) AKIFUATIWA NA KANKU KELLY NA MWISHO NI KING KIKI WALIPOFIKA KUHUDHURIA MAZISHI YA DKT RAMADHANI MTORO ONGALA.

Friday, December 17, 2010

MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA KOROGWE WAKIAPA LEO ASUBUHI

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KOROGWE BW. SADICK KALAGHE AKILA KIAPO HUKU WAKE ZAKE WAWILI (hawapo pichani) WAKIMSHUHUDIA KWENYE UKUMBI WA HALMASHAURI HIYO.

MAKAMO MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO BW. LUCA LOGAN KIRIKA NAYE AKILA KIAPO CHAKE LEO ASUBUHI.


DIWANI WA KATA YA MAGOMA HADIJA MSHAHARA NAYE AKILA KIAPO


MADIWANI WAKIPOZI KUSUBIRI KULA KIAPO.


MADIWANI WAKIPOZI KUSUBIRI KULA KIAPO.


MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILYA YA KOROGWE BW. LAMECK MASEMBEJO (kulia) AKISHUHUDIA KUAPISHWA KWA MADIWANI HAO.


MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI BW. STEPHEN NGONYAJI 'PROFESA MAJIMAREFU' (kushoto) AKIWA NA MWENYEKITI WA CCM WA KOROGWE VIJIJINI BW SALUM MALINGUMU WAKISHUGUDIA KUAPISHWA HUKO KWA MADIWANI.


OFISA HABARI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KOROGWE VIJIJINI BI FATNA MFALINGUNDI NAYE ALIKUWEPO KWENYE UKUMBI HUO AKISHUHUDIA KUAPISHWA HUKO.


OFISA HABARI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KOROGWE BI FATNA MFALINGUNDI, HAPA ALIKUWA AKIFUATILIA KWA KARIBU KABISA NAMNA ZOEZI ZIMA LA UAPISHAJI LINAVYOENDELEA.


BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI LI NA USALAMA WA WILAYA YA KOROGWE WAKIFUATILIA ZOEZI HILO LA UAPISHAJI LINAVYOENDELEA.


BW. MGAYA NAYE PIA ALIKUWEPO KWENYE UKUMBI HUO.


DKT RASHID SAID MGANGA MKUU WA WILAYA YA KOROGWE NAYE AKIFUATILIA ZOEZI HILO LA KUAPISHWA KWA MADIWANI.

MH.FIDELIS LAMTEY.HAKIM WA WILAYA YA KOROGWE AKIMUAPISHA MH.FREDERICK LENARD GAHU.DIWANI KATA YA VUGIRI JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI.

Wednesday, December 15, 2010

MAISHA YANAVYOENDELEA KATIKA VIJIJI VYETU

PATA UJUMBE WA NYUMBA HII KATI YA ZOTE ZILIZOPO KIJIJI CHA LUTINDI HAPA NI MTAA UJULIKANAO KWA JINA LA BETHANIA.


'MSHKAJI' AKIKATIZA NA BAISKELI YAKE LICHA YA MITAA HIYO YA LUTINDI KUWA NI SEHEMU YA MIINUKO LAKINI ALIWEZA KUENDESHA BAISKELI, WEWE HUWEZI HATA KIDOGO.


WANANCHI WA KIJIJI CHA LUTINDI AMBAKO NI MAAUFU SANA KWAKUWA NA HOSPITALI YA VICHWAA WAKIENDELEA NA SHUGHULI ZAO HAPA MAMA HUYU ANATOKA KUTAFUTA KUNI.


SHULE YA MSINGI LUTINDI, HILI NI DARASA LA KWANZA NA PILI LAKINI JE MMOMONYOKA HUU WA UDONGO HAUTALIANGUSHA MADARASA HAYA?


WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI LUTINDI WILYANI KOROGWE WAKIONEKANA KWA MBALI WAKIWA WANAKIMBIA KUOGOPA KAMERA.


Tuesday, December 14, 2010

WADAU BADO WAJADILI SUALA LA MAPENDEKEZO YA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA YA VYOMBO VYA HABARI YA MWAKA 2008

MKURUGENZI WA MISA-TAN BIBI ROSE HAJI AKIWA KWENYE MKUTANO WA KUJADILI MAPENDEKEZO YA WADAU KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA VYOMBO VYA HABARI, 2008 INAYOFANYIKA KWENYE HOTELI YA WHITE PARROT, KOROGWE MKOANI TANGA.


MWANA-SHERIA MOHAMED TIBANYENDELA AKIANDIKA UBAONI MADA MBALIMBALI ZINAZOJADILIWA KWENYE WARSHA HIYO YA MAPENDEKEZO YA WADSAU KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA VYOMBO VYA HABARI MWAKA 2008.