MAREHEMU ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' |
Na Mzee wa Bonde
MBUNGE wa jimbo wa Kinondoni Jijini Dar es salaam, Idd Azan amewataka wanamuziki nchini kuiga mfano wa marehemu Abuu Semhando 'Baba Diana' kuwa mvumilivu katika kipindi kirefu alichokaa katika bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' tangu ilipoundwa na kupata umaarufu baadaye.
Mbunge huyo alizungumza hayo alipokuwa kitoa nasaha zake kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Kinondoni ambapo alisema marehemu alikuwa mwanzilishi wa bendi hiyo ambayo ilianza ikiwa haina umaarufu lakini kwa kushirikiana na wenzake ilipata umaarufu hivyo akawasihi wanamuziki kuiga mfano huo wa uvumilivu.
"Kwa kweli nimesimama hapa kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kinondoni wote walikuwa waje hapa kumzika kipenzi chao Abuu lakini wameshindwa na kwakuwa mimi ni mwakilishi wao nimewawakilisha...Kimsingi ningependa kutoa wito kwa wanamuziki waliobaki waige mfano wa marehemu katika suala zma la uvumilivu, alianza Twanga Pepeta ikiwa haina mashabiki alivumilia hadi leo Twanga ni bendi maarufu kama angeondoka angeweza lakini alivumilia hadi mauti umemchukua, wengine igeni mfano huo," alisema Bw. Azan ambaye alitoa ubani wa sh. 200,000.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Baraka Msilwa alisema marehemu ameacha pengo kubwa ambalo haawaamini kama litazibika katika kipindi kifupi ijacho kwa kuwa marehemu alikuwa ni kiungo kati ya uonozi na wanmuziki na kwamba likuwa akitoa ushuri mwingi wa kuieneleza bendi hiyo
Alisema kuwa marehemu licha ya kutoa ushauri pia alikuwa akisaka vipaji vya wanamuziki wengine na kuchukulia na bendi hiyo hiyo kifo chake kitaacha pengo kubwa ambalo liadumu muda mrefu hadi kuzibika hivyo kama viongozi wa bendi hiyo wameguswa mno na kifo chake.
Miongoni mwa watu waliohudhuria ni baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo wakiwemo wacheza shoo na Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijiji Profesa Maji marefu, mwakilishi wa TOT Plus mkoani Tanga, Salim Bawazir na watu wengine ambao waliupokea msiba huo kwa majonzi makubwa.
No comments:
Post a Comment