Said Zuke wa kwanza kushoto akiangalia madawa ya kulevya akiwa na Kamanda wa polisi mkoani Tanga ACP Liberatus Sabas |
Said Zuke akifungua furushi hilo la madaya ya kulevya. |
Hapa Said Zuke akiijaribu madawa hayo ya kulevya akihakiki kama ni yenyewe. |
Madawa haya ni yenyewe na ni makali sana. |
Zuke na Ofisa wa Operesheni mkoani Tanga ASP Ussa na askari mwingine wa Ant-Robbery wakiangalia madawa hayo. |
JESHI la Polisi mkoani Tanga, linawashikilia watu wawili wakazi wa Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye uzito wa kilo 50.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo ACP Liberatus Sabas alisema kuwa watu hao walikamatwa Desemba 19 majira ya saa 9:30 katika kizuizi cha polisi Kabuku wilayani Handeni wakiwa kwenye gari dogo aina ya Mitsubish Pajero lenye namba za usajili KAW 276G.
Kamanda aliwataja watu hao kuwa ni Rashid Salim maarufu kwa jina la Chodoma (40) mkazi wa Magomeni Mwembechai Dar es salaam na Ismail Shebe (36) mkazi wa Kiwalani Jijini humo Dar es salaam.
Alisema watuhumiwa hao walikuwa wakitokea Jijini Dar es salaam kuelekea nchini Sudan kupitia Nairobi nchini Kenya wakitumia gari hilo ambalo lilikuwa na sehemu maalum iliyotengenezwa kuhifadhia madawa hayo.
Kamanda Sabas alisema watuhumiwa baada ya kupekuliwa Chodoma alikutwa na hati ya kusafiria yenye namba AB012971 iliyotolewa Agosti Mosi mwaka 2005 na Shebe alikuwa na hati AB293433 iliyotolewa Septemba 3, 2009.
Watuhumiwa hao kwa sasa wanashikiliwa katika kityuo kikuu cha polisi Chumbageni Jijini Tanga, kwa ajili ya mahojiano zaidi na kwamba wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara uchunguzi wa polisi utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment