HAYA ONA HILI UNADHANI KUNA WATU WAMEPONA HUMU? |
MAGARI KAMA HAYA NYAKATI HIZI ZA MWISHO WA MWAKA LAZIMA MADEREVA WAKE WAWE MAKINI VINGINEVYO YATAKUWA KAMA HIVI NA KUPOTEZA ROHO ZA WATU BURE. |
WATU sita wamekufa kwa kuteketea kwa moto na wengine 11 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kwenda wilayani Makete mkoa mpya wa Njombe (Njoluma) kupinduka na hatimaye kuwaka moto.
Tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa tano asubuhi limehusisha gari aina ya Rand Lover ambalo hata hivyo namba zake za usajiri hazijajulikana kutokana na kuteketea kwa moto.
Abiria walionusurika katika ajli hiyo ambao wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya,wamesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Kimondo kata ya Ulenje wilaya ya Mbeya Vijijini ambapo ilikuwa imebeba abiria na kupakiza mafuta ya Petroli juu ya Keria na ndani ya gari.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Advocate Njombi amesema atatoa taarifa rasmi za tukio hilo baada ya kuletewa na askari ambao wapo eneo la tukio.
Hata hivyo Askari wa Kikosi cha Usalama Barabara wakizungumza na mdau wa Blogu hii kwa simu katika eneo la tukio wamesema waliokufa ni watu sita ambapo kati yao watoto wadogo ni wawili na watu wazima wanne.
Mmoja wa Majeruhi wa ajali hiyo,Hilda Japhet (25) mkazi wa Uyole Mbeya,akizungumza na mdau wa Blogu hii katika hospitali ya Rufaa Mbeya alikolazwa alisema kutokana na ajali hiyo watoto wake wawili wamekufa kwa kutetea na moto.
Daktari wa zamu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk.Dominick Chalu, alisema kufuatia tukio hilo wamepokea majeruhi kumi na moja ambao wamelazwa katika hospitali hiyo na kwamba wawili kati ya hao hali zao ni mbaya.
Aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni pamoja na watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano ambao ni Evance Stephen na Latifu Labiso mkazi wa Ntokela wilayani Rungwe.
Dk.Chalu aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Bahati Mwavipa (50) kazi wa Uyole Mbeya,Sara Charles (50) mkazi wa Rungwe,Victoria Sanga (10),Okoka Matamsi, mkazi wa Mwanjelwa Mbeya,Huruma Israel,Jane Mbalila,Vailet Stephen mkazi wa Kanyegele na Judy Erick mkazi wa Mbalizi-Mbeya.
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo,Okoka Matamsi, akizungumzia ajali hiyo alisema wakati wakiwa njia kuelekea wilayani Makete ghafla gari hilo lilipinduka na kuanza kuteketea kwa moto.
Matamsi ambaye alikuwa akizungumza huku akiwa amewekewa maji ya dawa (drip), alisema baada ya gari hilo kupinduka lilianza kuteketea kwa moto ambao ulikolezwa na mafta ya Petroli ambayo yalikuwa yamepakizwa juu ya keria baada ya kupasuka kutokana na ajali hiyo.
Alisema kutokana na ajali hiyo abiria ambao hawakujeruhiwa sana walipata upenyo wa kukimbia kutoka eneo moto ulipokuwa unawake na kusogea pembeni ambao walioungua ni wale ambao walishindwa kujinasua toka ndani ya gari hilo.
Kufuatia ajali hiyo wakati wa kaya Ulenje wamelitaka Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya kupiga marufuku kupakiza mafuta ya petrol na dieseli katika magari aina ya Rand Lover ambayo ndiyo yanafanya safari ya kutoka Mbeya kwenda Makete ili kuepusha vifo visivyokuwa vya lazima.
Wakati huohuo,abiria wawili kati ya watu waliojeruhiwa kufuatia ajali ya ndege ndogo iliyotokea juzi katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya wameruhusiwa baada ya hali zao kuwa nzuri.
Ndege hiyo ambayo ni ya kampuni ya Air Z tofauti na ilivyoelezwa juzi kuwa ni ya Tropical wakati siyo kweli yenye namba SH-PCN U206F ilianguka majira ya saa 6;39 juzi katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege Mbeya kuelekea Dar es Salaam.
Majeruhi walioruhisiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri ni Muuguzi Frorence Stephen na Rubani wa ndege hiyo, Keyuln Fakhard raia wa Iran ambaye amechuliwa na kupelekwa Zanzibar.
Hata hivyo Dakrati wa Hospitali ya Rufaa kitengo cha Mifupa, Dk.Jons Chitemo, ambaye alivunjika mkono kutokana na ajali hiyo bado amelazwa na anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment