Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Sunday, December 19, 2010

MWANAFUNZI AFA KATIKA AJALI YA NDEGE MBEYA, WENGINE WAJERUHIWA

Wananchi wa eneo la Uyole lililopo nje kidogo ya Jiji la Mbeya wakiiangalia ndege iliyoanguka eneo hilo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watatu kujeruhiwa.


                        Na Thobias Mwanakatwe,Mbeya
MWANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Swilla iliyopo Mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya Vijijini, Godfrey Mpoli, amefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya ndege  ndogo waliyokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kwenda Dar Es Salaam kuanguka mjini hapa.
 
Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Tropical-Air Z yenye namba SH-PCN  U206F imeanguka majira ya saa 6;39 katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege Mbeya kuelekea Dar es Salaam.
 
Taarifa ambazo Blogu ya Watu na matukio imezipata ni kwamba ndege hiyo ilikodiwa na Mfuko wa Bima ya Afya kwa ajili ya kuja kumchukua Mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa ni marehemu.
 
Mwanafunzi huyo aliyefariki amemaliza kidato cha Nne mwaka huu katika shule hiyo ambapo alikuja kuchukuliwa kukimbizwa kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
 
Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya,Suma Kibopile, akizungumza na Blogu hii ,alisema kufuatia ajali hiyo wamepokea majeruhi watatu ambao ni pamoja na Daktari wa Rufaa kitengo cha Mifupa, Dk.Jons Chitemo, ambaye alikuwa akimsindikiza mwanafunzi huyo kumpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Kibopile alisema majeruhi wengine wa ajali hiyo ni Rubani wa ndege hiyo,Keyuln Fakhard raia wa Iran ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kupata mshituko baada ya kupata taarifa kuwa mwanafunzi aliyekuja kumchukua amefariki dunia na Muuguzi Frorence Stephen ambaye hata hivyo ametibiwa na kuruhusiwa.
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Venance Balama, ambaye alifiki eneo la tukio amesema kuwa ajali hiyo imeleta historia nyingine kwani mwaka 2006 kulitokea ajali ya ndege katika uwanja huo ambapo Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Juma Akukweti alipata ajali na kufariki wakati ametoka kuangalia soko la Mwanjelwa lililoungua mwaka huo.
 
Balama alisema ajali ya ndege iliyotokea jana nayo imekuwa siku chache tu baada ya kuungua kwa Soko kuu la Uhindini mapema mwezi huu.  

No comments:

Post a Comment