Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Saturday, January 28, 2012

MADAKTARI, WAUGUZI HOSPITALI YA BOMBO NAO, WAANZA MGOMO

WAFANYAKAZI WA KITENGO CHA UPASUAJI WA HOSPITALI YA BOMBO WAKIWA WAMEKAA NJE YA HOSPITALI HIYO KAMA SEHEMU YA MGOMO WAO WALIOUANZA LEO KATIKA HOSPITALI HIYO KUUNGA MKONO WENZAKO NCHI NZIMA.

MADAKTARI NA WAUGUZI WAKIWA WAMEKUSANYIKA KATIKA UKUMBI MDOGO WA KITENGO CHA MAZOEZI YA VIUNGO WAKISOMEWA TAARIFA YA KWANINI WANATAKIWA KUGOMA

BAADHI YA MADAKTARI NA WAUGUZI WAKISIKILIZA MKUTANO HUO.

WAKISIKILIZA KWA MAKINI MKUTANO HUO

HAWA NDIYO WALIOKUWA WAKISOMA BARUA ILIYOKUWA NA MADAI YA MADAKTARI AMBAYO WANAIDAI SERIKALI
Na Mzee wa Bonde,Tanga
MADAKTARI na wauguzi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo, nao wameanza mgomo wao jana, kuunga mkono wenzao waliogoma nchini kote kwa ajili ya kuishinikiza serikali iwalipe malimbikizo yao ikiwemo posho zao wakiwa kazini.

Mgomo huo umeanza jana ambapo huduma mbalimbali kwa wagonjwa zilisimama, na wagonjwa katika wodi ya wazazi walibaki pekee yao asubuhi bila kuwa na waauguzi wowote halkadhalika wagonjwa waliokuwa wodini ambao huwa wanapitiwa na madaktari kujua namna walivyolala, lakini waliamka bila kumuona daktari hali ambayo ilileta usumbufu mkubwa kwa wagonjwa hao.

Hata hivyo, katika kikao chao walichofanya jana katika hospitali hiyo kitengo cha viungo ambapo mwandishi wa habari hizi alifika eneo hilo bila kupata ushirikiano kutoka kwa madaktari huo, wakieleza kwamba waandishi waliokutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda walishindwa kumbana suala la msingi la kugoma kwao badala yake, wanazungumzia suala la uraisi wa 2015.

"Jamani nyie waandishi issue ni mgomo wa madaktari nyie mnazungumza na Waziri Mkuu suala la Urais hamuoni kwamba mnatumika katika masuala makubwa ya Kitaifa mnaingiza mambo ambayo hata wakati wenyewe haujafika, kwanini msimbane kuhusu mgomo na ni kwanini serikali inapiga chenga kukutana na viongozi wetu?," alihoji mmoja wa madaktari hao ambaye hakutaka jina lake lianikwe gazetini.

Abdallah Kubo mgonjwa aliyelazwa katika wodi ya Galanos, alilalamika kukosa matibabu baada ya kupata ajali juzi usiku ambako alifikishwa katika hospitali hiyo, majira ya saa tano usiku na kwamba alitarajia jana asubuhi angeonwa na daktari kisha kwenda kupatiwa x-ray kuangaliwa kama amevunjika katika viungo vyake.

"Kwa kweli mwili wangu unauma sana, nimeanguka na pikipiki baada ya kuwashiwa taa na gari kubwa kisha nikaparamia msingi nikaanguka nimeleta hapa sijitambui, nimeamka muda huu simuoni daktari, ndugu zangu wanataka nikapigwe x-ray lakini hatujaambiwa chochote twasikia leo (jana) madaktari wamegoma," alisema Kubo.

Mwanamke mwingine aliyejitambulisha kwa jina Bi Rose Mwaimu alisema alifika katika hospitali hiyo asubuhi jana, kwa ajili ya kuonana na daktari katika kitendo cha mazoezi ya viungo, lakini hakuweza kupata msaada wowote baada ya kuelezwa kwamba madaktari hawafanyi kazi
kufuatia mgomo waliouanza.

"Baba nimekuja hapa tangu asubhi nasubiri huduma lakini sijapata msaada wowote mguu wangu unaendelea kuvimba sijui sitafanyaje, kwa kweli tunaomba watuonee huruma jamani tunateseka," alisema Rose.

Alisema hospitali hiyo ya Bombo haina madaktari wa kutosha, hivyo mgomo huo utaathiri huduma za kiafya kutokana na kwamba wakati wakiwa wote hospitali hiyo huduma zao zimekuwa haziridhishi hivyo kugoma huko kutasababisha wagonjwa kupoteza maisha.

Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Dkt Mchomvu, alikiri mgomo huo kuanza katika hospitali hiyo leo (jana) lakini alisema huduma za dharura zitaendelea kama kawaida isipokuwa huduma nyingine wagonjwa hawatapata matibabu kama ilivyokuwa awali.

"Ni kweli tumegoma kuanzia leo (jana) kuunga mkono wenzetu nchini kote lakini huduma za Emergence  (dharura) zitaendelea iwapo kutakuwa na wagonjwa wa aina hiyo," alisema Dkt Mchomvu.

No comments:

Post a Comment