Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Thursday, January 19, 2012

MH. GALLAWA ATAKA KIWANDA CHA SARUJI KUTAFUTA MAWAKALA KILA WILAYA MKOANI TANGA WA KUSAMBAZA SARUJI

 Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji (Tanga Cement) Bw Erik Westerberg mara alipowasili katika ofisi za kiwanda hicho alipofika kukitembelea kuona shunguli zao na changamoto zinazowakabili.

Na Mashaka Mhando,Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa amekitaka kiwanda cha saruji kilichopo Jijini Tanga, kuangalia uwezekano wa kuwa na mawakala wa kusambaza bidhaa hiyo kwa kila wilaya mkoni hapa, ili wananchi waweze kunufaika na ununuaji wa bei nafuu kuliko sasa.

Akizungumza mara baada ya kukitembelea kiwanda hicho kisha kusomewa taarifa ya kiwanda hicho, Mkuu huyo wa mkoa alimwambia Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Erik Westerberg kwamba kmekuwepo malalamiko ya muda mrefu ya wakazi wa mkoa wa Tanga, kwamba wamekuwa wakinunua saruji ya kiwanda hicho kwa bei kubwa wakati kiwanda hicho kipo mkoani kwao.

Alisema sababu kubwa ya malalamiko hayo ya wananchi ni kwamba kiwanda hicho kina wakala mmoja anayenunua kiwandani kisha saruji hiyo kuipeleka Zanzibar kisha ndipo anawapowauzia wauzaji wadogo waliopo mjini Tanga ambao wananunua kwa bei kubwa inayowalazimu na wao kuiuza sawa na mikoa mingine.

Bei ya saruji ya kiwanda hicho kwa mfuko mmoja Jijini Tanga unauzwa kati ya sh. 14,000 hadi 14,500, wakati saruji hiyo hiyo kutoka katika kiwanda hicho kwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Dar es salaam mfuko mmoja huuzwa kati ya sh. 12,000 hadi 13,000 hali ambayo wananchi wa mkoa wa Tanga, kukiona kiwanda hicho hawana faida nacho licha ya kuwepo mkoani kwao.

"Kwanza nawapongeza sana kwa namna mnavyohifadhi mazingira na kazi mnavyozifanya, lakini kuna haya malalamiko ya muda mrefu kwa wakazi wa Tanga, kwamba saruji inauzwa na wakala mmoja anayesambaza baada ya kuinunua hapa, hivyo inavyouzwa huko mitaani inakuwa bei kubwa tofauti na miji mingine, sasa wanavyoona hivyo wanaona hawanufaiki na uwepo wa kiwanda hiki, naomba mfanye uwezekano wa kuwa na wakala kila wilaya za mkoa huu ili kuondoa suala hilo," alisema Mkuu wa mkoa huuyo/.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji huyo licha ya kukubali ombi la Mkuu wa mkoa kwa kueleza kwamba watafanya mchakato kwa kuyafanyia kazi maombi hayo, alisema kiwanda hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo suala la kukatika mara kwa mara kwa umeme kunakowapa hasara ya shilingi milioni 400 hadi 800 licha ya kulipa ankara ya umeme ya shilingi bilioni 1 kwa mwezi.

Vile vile alisema suala la kufungwa kwa matuminzi ya reli ya Tanga, kumewaathiri kwa kiasi fulani kusafirisha saruji mikoa ya kanda ya ziwa kwa maana kwamba njia ya reli ni bora zaidi kuliko njia ya barabara ambayo imekuwa na changamoto nyingi njiani.
 

1 comment:

  1. Afadhali maana,hata misaada hao saruji hutoa mikoa mingine na sio Tanga

    ReplyDelete