Na Mdau wetu Mbeya.
WATU 8 wamefariki dunia na wengine tisa 9 kujeruhiwa vibaya, baada ya gari walililokuwa wakisafiria kusindikiza maiti ya mtoto mchanga kupinduka na kutumbukia korongoni.
Katika ajali hiyo watu saba walikufa papo hapo na mmoja ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo alikufa baada ya kufia hospitalini alikokuwa akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya Rungwe Makandani.
Kamanda wa Polisi Mkoa Mbeya, Advocate Nyombi,akizungumza na waandishi wa habari jana alisema ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 9:30 alasili katika eneo la Uwanja wa ndege kijiji cha Ntokera Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Ajali hii imekuwa mbaya katika kipindi hiki cha mwanzano mwa mwaka 2011 ambapo Disemba 20 mwaka jana ajali nyingine iliteketeza wwatu sita walikufa ambao waliungua kwa katika barabara ya Mbeya-Makete baada ya gari aina ya Land Rover waliyokuwa wakisafiria iliyokuwa imebeba mafuta ya petro kupinduka na kasha kuwaka moto.
Kamanda Nyombi akielezea ajali ya juzi alisema chanzo cha ajali hiyo iliyohusisha gari yenye namba za usajili,T 692 ATV aina ya Toyota Hiace , ilitokana na kuharibika katika mfumo wa breki ambapo baadaye ilipoteza mwelekeo na kupinduka na kutumbukia korongoni.
Alisema gari hiyo ilikuwa na abiria 18 waliokuwa wakitokea Jijini Mbeya kwenda Wilayani Rungwe kwa ajili ya maziko ya mtoto mdogo wa miezi mitatu ambaye hata hivyo hakumtaja jina lake.
Kamanda Nyombi alisema katika maiti 8 ,ni mbili tu zimeweza kutambuliwa ambazo ni za Dereva wa gari hilo, aliyemtaja kwa jina moja tu la Martin na mwanamke aliyemtaja kwa jina la Cecilia Willfred (32),wote wakazi wa Jijini Mbeya.
Alisema maiti 6 bado hazijatambuliwa na kwamba zimehifadhiwa katika Hospitali ya serikali ya Makandana iliyopo wilayani Rungwe ambapo ndugu na jamaa watafika kuzitambua.
Nyombi alisema majeruhi 9 ambao hali zao zinadaiwa kuwa mbaya kutokana na wengi kupata majeraha makubwa sehemu mbalimbali ya miili yao wamelazwa katika hospitali nyingine ya misheni ya Igogwe wilayani humo.
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni David Abrahamu(30),Mary Mwashuya(29), wakazi wa Jijini Mbeya,Anna Seti,ambaye umri wake haukupatikana,pamoja na Eradi Mbewe(52)mkazi wa Jijini Mbeya na ambaye ni mmliki wa gari iliyopata ajali.
Wengine ni Pili Joseph(24),mkazi wa Ilomba,Niko Michael(26),Neema Kilian(38) wote wakazi wa Ilemi,Peter Annangisye(23) na Maltrida Fabiani(30) wote wakazi wa Mwanjelwa jijini hapa.