Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, January 11, 2011

WAZIRI OMARI NUNDU ATEMBELEA BANDARI YA TANGA, AAMBIWA TRA HASA MFANYAKAZI ANAYEITWA BEN, NDIYE ANAYEIUA BANDARI HIYO


WAZIRI WA UCHUKUZI BW. OMARI NUNDU AKIZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA BANDARI YA TANGA ALIPOTEMBELEA KUJUA MATATIZO NA MAMBO MBALIMBALI AMBAYO YANAISIBU BANDARI HIYO. KUSHOTO KWAKE NI MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI NCHINI (TPA) BW. EPHREAM MGAWE.

WAFANYAKAZI WA BANDARI YA TANGA, WAKIMSIKILIZA WAZIRI WA UCHUKUZI, BW. OMARI NUNDU.

WAFANYAKAZI WA BANDARI YA TANGA, WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI WAZIRI NUNDU.

WAZIRI WA UCHUKUZI BW. OMARI NUNDU (KUSHOTO) NA MKURUGENZI WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI NCHINI (TPA) EPHREAM MGAWE, WAKIWASIKILIZA WAFANYAKAZI WAKITOA MALALAMIKO YAO JUU YA UFANISI WA KAZI WA BANDARI HIYO.


MMOJA WA WAFANYAKAZI HAO AKITOA MALALAMIKO YAKE JUU YA BANDARI HIYO AMBAYO ALIDAI MAMLAKA YA MAPATO (TRA) MKOANI TANGA IMEKUWA KIKWAZO KIKUBWA CHA BANDARI HIYO ISHINDWE KUFANYA KAZI KWA KUWANYANYASA WAFANYABIASHARA.


MFANYAKAZI HUYU AKIZUNGUMZA KWA HISIA KALI HUKU AKIOMBA MEZA IMLINDE KWA TUHUMA ANAZOTOA JUU YA TRA KUWASIMAMISHA WAFANYABIASHARA KILA WANAPOTOA MZIGO KATIKA BANDARI YA TANGA LICHA YA KUKAGULIWA BANDARI.


No comments:

Post a Comment