Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Saturday, July 2, 2011
COASTAL UNION YAPATA UONGOZI MPYA
KLABU ya Coastal Union ya Jijini Tanga, leo imefanya uchaguzi wake wa kikatiba wa kuchagua viongozi wake watakaoiongoza klabu hiyo kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu baada ya miaka takribani taisa kuongozwa na kamati za muda.
waliochaguliwakatika mkutano huo ambao awali ulikuwa ufanyike wiki iliyopita lakini ulisimamishwa na TFF (shirikisho la soka nchini) baada ya kuwaengua wagombea saba ambao hawakuwa na sifa za kuwania nafasi hizo ni pamoja na Mwenyekiti Ahmed Hilal 'Aurora' ambaye hakuwa na mpinzani baada ya kujizolea kura 52 kati ya wajumbe 55 waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo.
Wajumbe waliochaguliwa kura zao zikiwa kwenye mabano ni pamoja na Kweli Nahashon (48), Albert Peter (47), Salim Amir (42), Julius Benjamin (42) na James Mwinchande ambaye alipata kura 36.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa kamati ya uchaguzi wa klabu hiyo Abdallah Yahya alisema kuwa watu waliojiandikisha kupiga kura kwa maana wanachama halali walikuwa 77 lakini kwenye uchaguzi huo wamefika wanachama 55 hivyo uchaguzi huo ulifanyika kutokana na koram ya wajumbe kutimia.
Alisema kwa mujibu wa katiba ya Coastal Union viongozi wanatakiwa kuwa tisa kwa maana Mwenyekiti, Makamo Mwenyeki na wajumbe saba lakini kutokana na kwamba kumebaki nafasi tatu za makamo mwenyekiti na wajumbe wa tatu uchaguzi mwingine utaitisha mara baada ya wanachama ambao walienguliwa kukamilisha taratibu za kuwasilisha vyeti wakikamilisha.
Wanachama ambao waliomba lakini walienguliwa ni pamoja na Makamo Mwenyekiti Steven Mghuto na Titus Bandawe, Yakob Nuru, Jawa Bakari Jawa, Ayub Athumani na Kilo Rashid.
Kwa mara ya mwisho klabu hiyo ilifanya uchaguzi wake wa kikatiba mwaka 2002 ambapo marehemu Zacharia Kinanda 'Arrigo Sacchi' aliachaguliwa kuwa Katibu Mkuu na wakati huo huo akiwa kocha mkuu wa timu hiyo na Mbwana Abushiri 'Director' akiwa mwenyekiti.
MWISHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment