Na Mwandishi Wetu,Tanga
MKUU wa mkoa wa Tanga Meja Jererali (Mstaafu), Said Kalembo ameuagiza uongozi wa Jiji la Tanga kuchukua hatua za haraka juu ya tatizo la viwanda vinavyotiririsha maji yenye kemikali na kusababsiha madhara kwa binadamu katika mfereji mama unaopita kata sita za Jiji hilo kwenda baharini, unapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
MKUU wa mkoa wa Tanga Meja Jererali (Mstaafu), Said Kalembo ameuagiza uongozi wa Jiji la Tanga kuchukua hatua za haraka juu ya tatizo la viwanda vinavyotiririsha maji yenye kemikali na kusababsiha madhara kwa binadamu katika mfereji mama unaopita kata sita za Jiji hilo kwenda baharini, unapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Akizungumza juzi wakati mkuu huyo na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya mkoa walipotembelea mfereji huo kuona namna maji yanayodaiwa kuwa na kemikali yakimwagwa kutoka viwandani na kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine wanaotumia mfereji huo kuufanyia usafi.
Awali Ofisa Afya wa Jiji hilo, Yusuph Gumbo akimsomea taarifa mwenyekiti huyo wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, alisema kuwa Julai 11 mwaka huu vibarua 14 waliokuwa wakifanya usafi kwenye mfereji huo kwa kuingia katikati, walipata madhara makubwa ya kuungua miguuni kwa kubabuka ngozi baada ya kuingiwa na maji yanayodhaniwa kuwa kemikali zenye sumu.
Alisema vibarua hao walipokuwa wakisafisha mfereji huo wenye urefu wa kilomita nane, licha ya kuvaa viatu virefu (Gum Boots) hata hivyo maji ya mfereji huo yaliwaingia na kujisikia kuwashwa baada ya muda wa masaa mawili walipotoka katika mfejei huo na kisha kuanza kubabuka na hali zao kuwa mbaya.
“Kwa vile vibarua wale walikuwa wakipokezana kuingia ndani ya mfereji waliamua kutoka ili wenzao wengine waingie waendelee na usafi, lakini wale waliotoka mferejini baada ya kuvua viatu muwasho ulizidi na mmoja kati yao ambaye aliungua vibaya na ngozi ilibabuka na kufanya awe na vidonda kuanzia magotini hadi miguuni,” alisema Gumbo.
Aliongeza kwamba mfereji huo uliojengwa miaka ya 1970 kwa ajili ya kusaidia kutoa maji ya mvua na kuyapeleka maharini lakini sasa umekuwa ukitumiwa na viwanda kumwaga mabaki ya takataka zao na kuvitaja viwanda hivyo kuwa ni kiwanda cha nguo cha Afritex, Kiwanda cha kusindika samaki cha Sea Food Products, Kiwanda cha foma, Kiwanda cha Vioo (Tansilica), karakana ya Tanroads na karakana za magari zilizopo eneo la viwanda Gofu.
Hata hivyo, alisema hatua ambazo halmashauri ya jiji imechukua hadi sasa ni kuwapa notisi ya kisheria wenye viwanda hivyo na kuwataka kuwa na mitambo ya kusafishia majitaka wanayoyatiririsha kabla ya kumwagwa baharini na kiwanda cha Afritex tayari kimenunua mtambo huo lakini bado haujaanza kusafisha maji hayo.
Mwana mazingira wa Envirocare Haika mcharo ambaye ni ofisa habari wa taasisi hiyo inayojihusisha na suala la mazingira hapa nchini, alimweleza Mkuu wa huyo wa mkoa katika ziara hiyo kwamba serikali inatakiwa kuchukua hatua juu ya tatizo hilo kwa ajili ya kulinda viumbe hai vya baharini na binadamu na wananchi wanaoishi pembezoni mwa mfereji huo.
“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa kabla ya kufanya ziara hapa na kamati yako, juzi (Alhamisi) nilitembelea kiwanda cha Afritex nikiwa na waandishi wa habari kuona namna kiwanda hiki kinavyojiendesha hasa sual la mazingira tumeona maji yao wanayoyatitiisha lakini tunadhani wakati mwingine maji yanakuja kwenye mfereji huu bila kusafisha, ni vema serikali ya mkoa ikatilia mkazo suala hili mapema kabla ya athari kubwa haijapatikana,” alisema mcharo.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa mkoa alimwagiza viongozi wa Jiji pamoja na Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi kuhakikisha wanachukua hatua za haraka ikiwezekana kuvifungia viwanda walivyobainika kumwaga kemikali hizo zenye sumu kwani tayari madhara kiafya yamepaikana kwa vibarua hao waliobabuka ngozi kuliko kukaa na kulalamikia suala hilo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment