Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Tuesday, August 30, 2011

BLOGU YENU YA MZEE WA BONDE INAWATAKIWA KILA LAKHERI NA SIKUU YA ID EL FITR

WAISLAMU WOTE NCHINI JUMATANO WANASHEREHEKEA SIKUKUU YA ID EL FITR, HIVYO BLOGU HII YA MATUKIO YA MZEE WA BONDE, INAWATAKIWA KILA LA KHERI KATIKA SIKUKUU HIYO, TUNAWAOMBA NDUGU ZETU TUSIWE CHANZO CHA VURUGU KAIKA MAENEO YA BURUDANI, TUWE WASTAARABU NA WAKIMYA KAMA WAKATI WA MFUNGO WA MWEZI WA RAMADHANI.

Wednesday, August 24, 2011

COASTAL YAPEWA VIFAA VYA MICHEZO VYA THAMANI YA TSH MIL 2

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA DARWORLD LINKS LTD YA JIJINI DAR ES SALAAM, MODDY BAWAZIR (kulia) AKIMKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION AHMED AURORA VIFAA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 2 ILI KUHAMASISHA TIMU HIYO IMFUNGE SIMBA LEO.


MKURUGENZI WA KAMPUNI YA DARWORLD LINKS LTD YA JIJINI DAR ES SALAAM MODDY BAWAZIR (katikati) AKIMKABIDHI MWENYEKITI WA COASTAL UNION AHMED AURORA JEZI KWA AJILI YA MAKIPA KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO (kulia) NI STEPHEN MGHUTO MAKAMO MWENYEKITI WA KLABU HIYO.

WAANDISHI WA HABARI WALIOFIKA KWENYE MKUTANO WA KUKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA KLABU YA COASTAL UNION WAKIWA KAZINI KWENYE HOTELI YA TANGA BEACH HOTEL LEO ASUBUHI.

Monday, August 22, 2011

WANANCHI HAWA WANAWEZA WASILIPE KODI WAKISEMA HAWAKO KENYA WALA TANZANIA

JIWE HILI LINALOGAWANYA MPAKA KATI YA TANZANIA NA KENYA, HAPA UPANDE WA KULIA WA PICHA JIRANI KABISA NA JIWE HILO NI UA WA MAKUTI WA MWANNCHI WA TANZANIA ALIYEJENGA KARIBU KABISA NA JIWE HILO KATIKA KIJIJI CHA JASINI. KUSHOTO UNAANGALIA PAA LA NYUMBA YA MWANANCHI WA NCHI YA KENYA AMBAYE NAYE PIA ANATUMIA JINA HILO LA JASINI NA KIJIJI CHAO KIMEANDIKISHWA KATIKA MJI ULIOPO MAKAO MAKUU YA VANGA AMBAKO UNAVUKA BAHARI UNAINGIA KATIKA MJI HUO WA VANGA AMBAO UPO KIASI CHA KILOMITA TATU TU KUFIKA HUKO. UJENZI HUU KWA KAWAITA HAUKUBALIKI KATIKA MIPAKA YA KIMATAIFA KWASABABU UNATAKIWA JIWE HADI NCHI KUNA ACHWA NAFASI YA MITA ZAIDI YA 200 ENEO HILO LINA KUWA HURU 'NOMASY LAND'.

VIINGILIO PAMBANO LA COASTAL UNION NA SIMBA JUMATANO, VYATAJWA

MBWANA MSUMARI MENEJA WA UWANJA WA MKWAKWANI NA MWENYEKITI WA MATAWI YA SIMBA MKOANI TANGA.  

MCHEZO KATI YA COASTAL UNION NA SIMBA YA JIJINI DAR ES SALAAM UTAKAOCHEZWA KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI JUMATANO WIKI HII AGOSTI 24, VIINGILIO VYA MCHEZO HUO TAYARI VIMETANGAZWA.

MENEJA WA UWANJA HUO ALISEMA VIINGILIO VYA MCHEZO HUO VITAKUWA NI VYA AINA TATU, SH. 300 KWA WATAKAOINGIA RASHA, SH. 5000 UPANDE WA MAGOLI (reli 1Sports) na (reli 2 Coastal) NA SH. 7,000 UPANDE WA BANDANI NA SEHEMU ZA MBILI.

MSUMARI ALISEMA VIINGILIO HIVYO VIMEPANGWA KWA PAMOJA NA UONGOZI WA CHAMA CHA SOKA MKOANI TANGA (TRFA) KWA KUZINGATIA KWAMBA SIMBA NI MOJA YA TIMU YA KIMATAIFA HIVYO HATA VIINGILIO VYAKE VINAKUWA VYA JUU ILI KULIFANYA PAMBANO HILO KUWA MAALUUM 'SPECIAL GAME'.

WAKATI HUO HUO, TIMU YA SIMBA TAYARI IMEWASILI MKOANI HAPA NA KUFIKIA KATIKA HOTELI YA NYINDA CLASSIC AMBAPO JUMANNE ASUBUHI ITACHUKUA MAZOEZI KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI NA JIONI YAKE KABLA YA KUSHUKA DIMBANI KUMENYANA NA COASTAL UNION AMBAYO IMEJICHIMBIA KATIKA MJI WA MWAMBANI KUJINOA NA PAMBANO HILO.

Sunday, August 21, 2011

SIMBA KUFIKIA NYINDA CLASSIC, MASHABIKI KUWAPOKEA JUMATATU PONGWE

SIMBA BAADA YA KUHAMISHIA MICHEZOYAKE KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI JIJINI TANGA, TIMU HIYO YA WEKUNDU WA MSIMBAZI ITAPIGA KAMBI KWENYE HOTELI YA NYINDA CLASSIC ILIYOPO ENEO LA BOMBO EREA TAYARI KWA MPAMBANO WAKE NA COASTAL UNION HAPO SIKU YA JUMATANO ADOSTI 24.
KWA MUJIBU WA MWENYEKITI WA KLABU HIYO MH. ISMAIL ADEN RAGE ALISEMA KUWA BAADA YA TIMU HIYO KUIFUNGA TIMU YA JKT OLJORO YA ARUSHA BAO 2-0, JUMATATU ASUBUHI TIMU HIYO ITAONDOKA MJINI ARUSHA NA KUFIKIA KWENYE HOTELI YA NYINDA CLASSIC ILIYOPO KWENYE ENEO HILO KUJIANDAA NA PAMBANO LAKE HILO NA 'WAGOSI WA KAYA' COASTAL UNION'


"TUTAFIKIA KWENYE HOTELI YA NYINDA CLASSIC ILIYOPO ENEO LA BOMBO NA HAPO TIMU YETU ITAKUWA IKIKAA KILA TUTAKAPOKUWA NA MCHEZO KWENYE UWANJA HUO WA MKWAKWANI, TUMECHAGUA KUCHEZEA TANGA TUKIAMINI KWAMBA WATU WA TANGA NI WAKARIMU NA WATU WENYE UPENDO," ALISEMA RAGE AMBAYE NI MBUNGE WA JIMBO LA TABORA MJINI (CCM).


MWENYEKITI HUYO PIA AMETANABAISHA KUWA BAADA YA MCHEZO WAO NA COASTAL UNION, JIONI VIONGOZI WA SIMBA NA COASTAL WATAKUTANA FARAGHA KWENYE UKUMBI WA HOTELI YA TANGA BEACH RESORT KUZUNGUMZA 'UNDUGU' WAO ULIOLEGALEGA KWA MIAKA KADHAA KUTOKANA NA SABABU AMBAZO KILA TIMU HAIJUI SABABU YA MAHUSIANO YAKO KUWA KOMBO.


'BAADA YA MECHI TUTAKAA NA WENZETU HAWA KUJADILI KWA KINA MAHUSIANO YETU BAINA YAO KWASABABU HATUKO VIZURI KAMA ZAMANI ILIVYOKUWA TUKISHIRIKIANA HIVYO TUTATUMIA MUDA AMBAO SISI TUTAKUWA TANGA KUBORESHA MAHUSIANO YETU YA HALI NA MALI ILI TUWEZE KUSAIDIANA HATA KAMA TIMU HIZI, ZITAKUWA NA MATOKEO TOFAUTI BAADA YA MCHEZO WETU JUMATANO," ALISEMA RAGE.


WAKATI HUO HUO, MWENYEKITI WA MATAWI YA SIMBA MKOANI TANGA, MBWANA MSUMARI ALISEMA KUWA MASHABIKI NA WAPENZI WA TIMU HIYO WA JIJI LA TANGA WAMEPANGA KUWAPOKEA KWA HOI HOI NA VIFIJO KWENYE ENEO LA PONGWE WATAKAPOINGIA SIKU YA JUMATATU AMBAPO MSAFARA WA BASI LILILOWACHUKUA WEKUNDU HAO WA MSIMBAZI LITASINDIKIZWA NA MSAFARA WA PIKIPIKI NA BAISKELI HADI NYINDA ILIKOFIKIA.




WANA-IJERIA WA COASTAL UNION HAWATACHEZA HADI HATI ZAO ZA KIMATAIFA ITC ZITUMWE TANGA

NEMBO YA COASTAL UNION ILIYOANZSIHWA MWAKA 1948 HADI LEO

KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOPAMBANA NA MTIBWA SUGAR NA KUTOKA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI AGOSTI 20 WAKATI WA UFUNGUZI WA LIGI KUU YA VODACOM.
KATIKA MCHEZO HUO COASTAL UNION ILIONEKANA KUPWAYA SEHEMU YA KIUNGO AMBAPO BAADA YA KUZUNGUMZA NA KOCHA WA TIMU HIYO AFIDH BADRU ALISEMA AMEATHIRIWA NA KUKOSEKANA KWA WACHEZAJI WAKE WAWILI WA KUTOKA NAIGERIA KIUNGO MZUIAJI FELIX AMECHI STANLEY NA KIUNGO MSHAMBULIAJI SAMUEL TONNYSON TEMI.

ALISEMA WACHEZAJI HAO AMBAO HATI ZAO ZA KIMATAIFA (ITC) BADO HAZIJATUMWA NA SHIRIKISHO LA SOKA LA NIGERIA (NFA) HIVYO KUSABABISHA WACHEZAJI HAO KUSHINDWA KUCHEZA KATIKA MCHEZO HUO.

"KUKOSEKANA KUCHEZA WACHEZAJI HAO NI PENGO KUBWA KWETU NA HILI LITATUFANYA TUATHIRIKE KISAIKOLOJIA KWANI KATIKA KIPINDI CHA KUJIANDAA NA MAZOEZI WALIKUWA WAMEZOEANA NA WENZAO HIVYO KOMBINATION ILIOPO SASA IMEVURUGIKA SABABU YA KUWAKOSA WACHEZAJI HAO.

HATA HIVYO MMOJA WA VIONGOZI WA KLABU HIYO ALISEMA KUWA WANAFANYA MIPANGO HATI HIZO ZITUMWE MAPEMA KABLA YA MCHEZO WAO NA SIMBA UTAKAOFANYIKA JUMATANO AGOSTI 24 KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI ILI WAWEZE KUFANYA VIZURI.

BARABARA YA TANGA/SEGERA HADI KITUMBI KUKARABATIWA

BANGO HILI LA MKANDARASI WA KAMPUNI YA SBI JAPAN LIKIWA LIMEWEKWA KATIKA MAKUTANO YA BARABARA YA RING NA TAIFA (jirani na stesheni ya reli) KUASHIRIA KUANZA KWA UKARABATI WA BARABARA YA TANGA-SEGERA-KITUMBI YENYE UREFU WA KILOMITA 120 LENGO LIKIWA KUONGEZA UPANA WA BARABARA NA KUIONGEZA UBORA WAKE. MENEJA WA WAKALA WA BARABARA MKOANI TANGA INJINIA ALFRED NDUMBALO AMESEMA MKANDARASI HUYO TAYARI AMEANZA KAZI IYO AMBAYO ITAFANYIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI NA MIEZI SITA HADI KUKAMILIKA KWAKE. HATUA HIYO ITASAIDIA KUIFANYA BARABARA HIYO KUPITIKA VIZURI NA KUEPUSHA AJALI ZINASOBABISHWA WAKATI MWINGINE NA UFINYU WA BARABARA HIYO.  

Friday, August 19, 2011

BREEKING NEWS!!!!!!!!!!! SIMBA KUCHEZEA UWANJA WA MKWAKWANI MICHEZO YAKE




KIKOSI CHA SIMBA KILICHOTWAA NGAO YA HISANI YA JAMII KWA KUIFUNGA YANGA BAO 2-0


KLABU YA SIMBA YA JIJINI DAR ES SALAAM, ITAUTUMIA UWANJA WA MKWAKWANI KUCHEZEA MICHEZO YAKE YA LIGI KUU YA VODACOM INAYOTARAJIA KUANZA AUGOSTI 20 MWAKA HUU, KUFUATIA UWANJA WA TAIFA AMBAO ULIPANGA KUTUMIA MICHEZO YAKE KUFUNGWA NA SERIKALI BAADA YA KUHARIBIKA KWA MICHEZO YA LIGI YA KAGAME.

KWA MUJIBU WA HABARI KUTOKA KWA MWENYEKITI WA MATAWI YA SIMBA MKOANI TANGA MBWANA MSUMARI NI KWAMBA SIMBA ITAUTUMIA UWANJA WA MKWAKWANI KWA VILE WANACHAMA WA KLABU HIYO WA MJINI TANGA WAMEOMBA HIVYO KLABU HIYO KUKUBALI.

MSUMARI AMBAYE PIA NI MENEJA WA UWANJA WA MKWAKWANI ALISEMA KUWA AMEWASILIANA NA MWENYEKITI WA KLABU HIYO ISMAIL ADEN RAGE KWA NJIA YA SIMU ASUBUHI AKIWA DODOMA AMEMWAKIKISHIA KWAMBA KLABU HIYO ITATUMIA UWANJA WAKE.

"AMENIHAKIKISHIA KABISA KWAMBA WATATUMIA UWANJA WA MKWAKWANI BADALA YA ARUSHA AMBAKO WALISEMA WALIPOKUWA KWENYE TAMASHA LA SIMBA DAY HAWAKUPATA MAPATO YA KUTOSHA HIVYO KUONA NI VEMA WAKAHAMA UWANJA HUO NA KUUTUMIA UWANJA WETU," ALISEMA MSUMARI NA KUONGEZA KWAMBA KATIKA TAMASHA HILO SIMBA WALIPATA MILIONI 25 TU.

KAMA ITAKUWA HIVYO, MASHABIKI WA TANGA WATAWEZA KUPATA UHONDO MKUBWA HASA TIMU HIYO IKIJA KUPAMBANA NA MTANI WAKE YANGA AMBAYE JUZI WAMEMPA KIPACHO CHA MABAO 2-0, TUSUBIRI TUONE NA BLOGU YAKO HII ITALIFUATILIA KWA KARIBU SUALA HILI ILI LIWEZE KUKUJUZA.






UHAMIAJI TANGA WAPIMA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA VVU NA UKIMWI

WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI MKOANI TANGA WAKISUBIRI KUPIMA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI NA VVU MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MKOA HUO ENEO LA JIRANI NA MAKTABA.

WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA WAKIMUHOJI KAMISHINA WA UHAMIAJI NCHINI DKT KAHAMBA JUU YA NAMNA IDARA HIYO ILIVYOAMUA KUWAPIMA WATUMISHI WAKE NCHI NZIMA.

"...HAPA TUNATAKA KUJUA IDADI YA WATUMISHI WETU WALIOATHIIKA ILI TUWEZE KUTEKELEZA WARAKA WA SERIKALI WA MWAKA 2007 JUU YA KUWATUNZA NA KUWALEA WATUMISHI WANAOISHI NA VVU NA UKIMWI...," ALISEMA KAMISHINA KAHAMBA

"...YAANI TUMEKUJA HADI HAPA KUWAPIMA HALAFU WASIJE HAPA MBONA TUTAWACHUKULIA HATUA WATUMISHI AMBAO HAWATAKI JAPO SUALA HILI NI HIARI LAKINI TUMEAMUA SISI KAMA SEHEMU YA JESHI BASI TUPIMANE BILA KUOGOPANA,..."

WATUMISHI WA IDARA YA UHAMIAJI MKOANI TANGA WAKIWA WAMEKAA KILA MMOJA AKIONGEA LAKE JUU YA KUINGIA KWA MAMA MNASIHI NASAHA HUMO NDANI ILI KUPIMA MAAMBUKI HAYO

Thursday, August 18, 2011

JENGO LA WATU WENYE VVU NA UKIMWI LAZINDULIWA BOMBO

MGANGA MKUU WA MKOA WA TANGA DKT ALLY ULEDI AKISOMA RISALA KATIKA UFUNGUZI WA JENGO LA KLINIKI YA MATUNZO NA MATIBABU YA WATU WENYE VVU NA UKIMWI KATIKA HOSPITALI YA BOMBO MKOANI TANGA.

BAADHI YA WATU MBALIMBALI WALIOFIKA KWENYE UZINDUZI HUO WA KLINIKI HIYO YA WAGONJWA WA VVU NA UKIMWI WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI AMBAPO KUSHOTO NI LULU GEORGE WA NIPASHE NA ANYEFUATA NI FATMA MATULANGA WA TBC.

MWAKILISHI WA SHIRIKA LA KIMARAEKANI CDC DKT STEFAN WIKTOR AKITOA SALAMU KUTOKA KWA WATU WA MAREKANI AMBAO WAMEFADHILI MRADI HUO WA UJENZI WA JENGO HILO KATIKA HOSPITALI HIYO  ALITEINAMA NI WAZIRI WA FYA DKT HADJI MPONDA NA PEMBENI YAKE NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. BENEDICTOR OLE KUYAN.

MEYA WA JIJI LA TANGA BW. OMARI GULEDI AKIHITIMISHA UZINDUZI HUO KWA KUELEZA KWAMBA ILI KUONDOA MRUNDIKANO WA WAGONJWA KAIKA HOSPITALI HIYO YA BOMBO, HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA WAPO MBIONI KUJENGA HOSPITALI YA WILAYA ENEO LA MASIWANI.

HAKUNA SHEREHE YA UZINDUZI IKAKOSA BURUDANI HAPA NI KIKUNDI CHA CASSA DANCING TROUPE WAKITOA BURUDANI KWA WAGENI MBALIMBALI WALIOFIKA KUSHUHUDIA UZINDUZI HUO

Tuesday, August 16, 2011

WACHINA WAANZA KUWEKA LAMI BARABARA YA TANGA/HOROHORO

ENEO LA BARABARA ILIYOANZA KUWEKWA LAMI NA KAMPUNI YA SINOHYDRO YA CHINA INAYOJENGA BARABARA YA TANGA/HOROHORO KWA KIWANGO CHA LAMI, HAPA NI ENEO LA MPERANI.

SEHEMU YA BARABARA ILIYOWEKWA TABAKA YA KWANZA YA LAMI (LEAYER) HII NI ENEO LA MTIBWANI AMBAYO TAYARI NAYO IMEWEKWA LAMI.

ENEO LA MPERANI LINAVYONEKANA KATIKA PICHA. NDUGU MSOMAJI WA BLOGU HII YA WATU NA MATUKIO YA MZEE WA BONDE, BARABARA HII HAWA WACHINA TAYARI WAMEANZA KUWEKA TABAKA YA KWANZA YA LAMI KATIKA ENEO KUANZIA MIKOCHENI AMBONI, HADI KUKARIBIA MTIMBWANI KWA KWELI BARABARA INAPENDEZA NA IKIMALIZIKA HOROHORO HADI MOMBASA ITAKUWA NI MASAA MAWILI TU KAMA MPAKANI HUTACHELEWESHWA.

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA MPAKANI MWA TANZANIA NA KENYA

OFISA USHURU NA FORODHA KATIKA MPAKA WA HOROHORO BW. DAVID KAMUKULA, AKIWAELEZA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA NAMNA WALIVYOWEZA KUDHIBITI UPITITAJI WA MAHINDI KWENDA NJE YA NCHI KAMA ILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.

BAADHI YA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOANI TANGA kutoka kushoto ni MRAKIBU MWANADAMIZI WA POLISI BW. NDAKI, DAVID LENGIA OFISA WA TAKUKURU NA BW. JOSEPH SEMWAIKO OFISA USALAMA WA TAIFA KUTOKA OFISI YA MKOA, WAKIMSIKILIZA MKUU WA IDARA YA USHURU NA FORODHA KATIKA ENEO LA HOROHORO.

KINU HIKI UNACHOKIONA HAPA CHINI NI NYUMBA AMBAYO IPO KENYA NA JIWE LILE KULEEE KUSHOTO NI NYUMBA YA TANZANIA NA BARABARA HII NDIYO WANANCHI WAMEACHA KAMA MPAKA UNAOGAWA NCHI YA TANZANIA NA KENYA LAKINI SHERIA INASEMA KWAMBA KUTOKA JIWE LA MPAKA HADI MAKAZI YA NCHI INATAKIWA WAACHE KIASI CHA MITA 200 LAKINI WANANNCHI HAWA WAMEAMUA KUJENGA KABISA KWENYE ENEO AMBALO NI NOMASSY LAND KAMA UNAVYOONA HAPA PICHANI.

MAKAZI WA KIJIJI CHA JASINI KILICHOPO KATIKA KATA YA MAYOMBONI WILAYANI MKINGA BI MWANAMKASI MBWANA NAYEMENYA MIHOGO NA NDUGU YAKE MWANAUANI, WAKITAYARISHA FUTARI YAO KATIKA ENEO AMBALO NI LA NCHI YA KENYA, HII INATOKANA NA WANANCHI HAWA KUJENGA KABISA MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA.

BAADHI YA MAOFISA WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA TANGA WAKIWA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA JASINI AMBAKO WALIKWENDA KUFUATILIA NAMNA UVUSHAJI WA MAHINDI KWENDA NCHI JIRANI YA KENYA UNAVYOFANYWA KWA NJIA ZA PANYA KATIKA KIJIJI HICHO.

BAADHI YA MAOFISA HAO WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WAKIWA KATIKA ENEO LA BAHARI AMBALO NI NDANI KABISA YA KENYA WAKIANGALIA NAMNA WATU WANAVYOWEZA KUVUKA KUPELEKA BIDHAA AMBAZO HAZIJALIPIWA USHURU NA KUINGIZA BIDHAA AMBAZO HAZILIPIWI USHURU KUTOKA ENEO LA VANGA NCHINI KENYA.

BAADHI YA MAOFISA HAO WAKIZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA JASINI KUHUSIANA NA NAMNA WANAVYOWEZA KUDHIBITI UVUSHAJI WA MAHINDI NA BIDHAA AMBAZO HAZIJALIPIWA USHURU KATIKA ENEO HILO LA BAHARI MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA.

MUVI-SIDO WAZINDUA JARIDA LA NURU YA MAFANIKIO KWA WAJASIRIAMALI

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA ANAYESHUGHULIKIA HUDUMA ZA JAMII BW. NDIBALEMA KISHERU AKIZINDUA SHUGHULI ZA WADAU WA HABARI WA MRADI WA MUVI ULIOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA YCDP JIJINI TANGA, kushoto ni MENEJA WA SIDO MKOANI TANGA BW. SELEMANI MTANI NA kulia ni BW. JOSEPH MAKAZA MKURUGENZI WA HABARI WA MUVI.

WADAU WA HABARI NA MAWASILIANO WAKIFUATILIA KWA MAKINI UZINDUZI WA MRADI WA MUVI 

MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI HUO BW. NDIBALEMA KISHERU AMBAYE NI KATIBU TAWALA MKOANI TANGA (katikati) AKIJIANDAA KUKATA KAMBA MAAMULU YA KUZINDUA JARIDA LENYE HABARI ZA MAMBO MBALIMBALI KUHUSU HABARI ZA MASOKO KWA WAJASIRIAMALI NCHINI. WENGINE kushoto ni MKURUGENZI WA HABARI WA MUVI JOSEPH MAKANZA NA kulia ni BW. SELEMANI MTANI MENEJA WA SIDO

KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA BW. NDIBALEMA KISHERU (katikati) AKISOMA JARIDA LA MRADI WA MUVI MARA BAADA YA KULIZINDUA HUKU MENEJA WA SIDO MKOANI TANGA BW. SELEMANI MTANI AKILIONESHA KWA WADAU WALIOHUDHURIA HAFLA HIYO YA UZINDUZI ILIYOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA YCDP.

MAMBO YA MPAKANI FUTARI YAANDALIWA KENYA, YAPIKWA TANZANIA

MWANAMKASI MBWANA (anaye menya mihogo) MKAZI WA KIJIJI CHA JASINI KILICHOPO KATA YA MAYOMBONI WILAYANI MKINGA, AKITAYARISHA FUTARI YAKE YA MUHOGO AKIWA KATIKA MTI WA KIVULI AMBAO UPO NCHINI KENYA KISHA AKITAYARISHA FUTARI HIYO ANA KWENDA NYUMBANI KWAKE (NYUMA ALIKOKUPA MGONGO) HUKU ANAKOANGALIA NI KENYA MGONGONI KWAKE NI TANZANIA. MSOMAJI WA PICHA HII UKIANGALIA KWA MBALI PALE KWENYE UWA WA MAKUTI PANA JIWE JIWE HILO NI MPAKA KATI YA KENYA NA TANZANIA, SASA MWANAMKASI NA MDOGO YAKE MWANAUANI HAPA WANAPOTAYARISHA MUHOGO NI KENYA.

Thursday, August 11, 2011

KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHAZINDULIWA

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA BW. KIROBOTO AKIWA MMOJA YA WATU WALIHUDHURIA UFUNGUZI WA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA CASA KILICHOPO ENEO LA RASKAZONE

Monday, August 8, 2011

ASKOFU ANTHONY BANZI AZINDUA HUDUMA MPYA YA X-RAY TUMAINI HOSPITALI

MHASHAMU ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO KUU LA TANGA, ANTHONY BANZI AKIKATA UTEPE KUFUNGUA KITENGO KIPYA CHA IDARA YA MIONZI (X-RAY) KATIKA KITUO CHA AFYA TUMAINI. KUSHOTO KWAKE NI SISTER FROLA MUSHI MKUU WA KITUO HICHO.

JEWE LA MSINGI LA JENGO JIPYA LA IDARA YA MIONZI (X-RAY) TUMAINI HOSPITALI

MASHINE MPYA YA KISASA YA MIONZI (X-RAY) ILIYOZINDULIWA TUMAINI HOSPITALI

MASISTER WA JIMBO KUU LA KANISA KATOLIKI TANGA WAKIWA MIONGONI WALIOHUDHURIA UZINDUZI HUO

MTAALAMU WA IDARA YA MIONZI KATIKA HOSPITALI YA MKOA BOMBO DKT MATABA (kushoto) AKINONG'ONEZANA JAMBO NA MKURUGENZI WA WALEI WA KANISA HILO BW. SYLEVESTER MGOMA KATIKA UZINDUZI HUO

WATU MBALIMBALI NA WAFANYAKAZI WA KITUO HICHO CHA TUMAINI WAKIFUATILIA UZINDUZI HUO.

KATIBU WA KANISA KATOLIKI JIMBO KUU LA TANGA, SELESTIN KAGABA (wa kwanza kushoto) AKIFUATILIA KWA KARIBU UZINDUZI HUO

WAUGUZI WA KITUO HICHO NAO WALISHEHENESHA SHEREHE HIZO KWA KUHUDHURIA HUKU WAKIPIGA VIGELELE KILA ASKAFU ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NENO LA FARAJA KWAO NA HOSPITALI HIYO.

WATU WA KILA AINA WALIFIKA KWENYE UZINDUZI HUO

ALIYEVAA FULANA YA VIJUMBA JUMBA NI MTANGAZAJI WA REDIO ONE NA ITV MKOANI TANGA WILLIAM MNGAZIJA AKIFUATILIA KWA MAKINI UZINDUZI HUO PAMOJA NA WATU WENGINE MBALIMBALI.