Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Sunday, August 21, 2011

WANA-IJERIA WA COASTAL UNION HAWATACHEZA HADI HATI ZAO ZA KIMATAIFA ITC ZITUMWE TANGA

NEMBO YA COASTAL UNION ILIYOANZSIHWA MWAKA 1948 HADI LEO

KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOPAMBANA NA MTIBWA SUGAR NA KUTOKA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI AGOSTI 20 WAKATI WA UFUNGUZI WA LIGI KUU YA VODACOM.
KATIKA MCHEZO HUO COASTAL UNION ILIONEKANA KUPWAYA SEHEMU YA KIUNGO AMBAPO BAADA YA KUZUNGUMZA NA KOCHA WA TIMU HIYO AFIDH BADRU ALISEMA AMEATHIRIWA NA KUKOSEKANA KWA WACHEZAJI WAKE WAWILI WA KUTOKA NAIGERIA KIUNGO MZUIAJI FELIX AMECHI STANLEY NA KIUNGO MSHAMBULIAJI SAMUEL TONNYSON TEMI.

ALISEMA WACHEZAJI HAO AMBAO HATI ZAO ZA KIMATAIFA (ITC) BADO HAZIJATUMWA NA SHIRIKISHO LA SOKA LA NIGERIA (NFA) HIVYO KUSABABISHA WACHEZAJI HAO KUSHINDWA KUCHEZA KATIKA MCHEZO HUO.

"KUKOSEKANA KUCHEZA WACHEZAJI HAO NI PENGO KUBWA KWETU NA HILI LITATUFANYA TUATHIRIKE KISAIKOLOJIA KWANI KATIKA KIPINDI CHA KUJIANDAA NA MAZOEZI WALIKUWA WAMEZOEANA NA WENZAO HIVYO KOMBINATION ILIOPO SASA IMEVURUGIKA SABABU YA KUWAKOSA WACHEZAJI HAO.

HATA HIVYO MMOJA WA VIONGOZI WA KLABU HIYO ALISEMA KUWA WANAFANYA MIPANGO HATI HIZO ZITUMWE MAPEMA KABLA YA MCHEZO WAO NA SIMBA UTAKAOFANYIKA JUMATANO AGOSTI 24 KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI ILI WAWEZE KUFANYA VIZURI.

No comments:

Post a Comment