Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Sunday, August 21, 2011
SIMBA KUFIKIA NYINDA CLASSIC, MASHABIKI KUWAPOKEA JUMATATU PONGWE
"TUTAFIKIA KWENYE HOTELI YA NYINDA CLASSIC ILIYOPO ENEO LA BOMBO NA HAPO TIMU YETU ITAKUWA IKIKAA KILA TUTAKAPOKUWA NA MCHEZO KWENYE UWANJA HUO WA MKWAKWANI, TUMECHAGUA KUCHEZEA TANGA TUKIAMINI KWAMBA WATU WA TANGA NI WAKARIMU NA WATU WENYE UPENDO," ALISEMA RAGE AMBAYE NI MBUNGE WA JIMBO LA TABORA MJINI (CCM).
MWENYEKITI HUYO PIA AMETANABAISHA KUWA BAADA YA MCHEZO WAO NA COASTAL UNION, JIONI VIONGOZI WA SIMBA NA COASTAL WATAKUTANA FARAGHA KWENYE UKUMBI WA HOTELI YA TANGA BEACH RESORT KUZUNGUMZA 'UNDUGU' WAO ULIOLEGALEGA KWA MIAKA KADHAA KUTOKANA NA SABABU AMBAZO KILA TIMU HAIJUI SABABU YA MAHUSIANO YAKO KUWA KOMBO.
'BAADA YA MECHI TUTAKAA NA WENZETU HAWA KUJADILI KWA KINA MAHUSIANO YETU BAINA YAO KWASABABU HATUKO VIZURI KAMA ZAMANI ILIVYOKUWA TUKISHIRIKIANA HIVYO TUTATUMIA MUDA AMBAO SISI TUTAKUWA TANGA KUBORESHA MAHUSIANO YETU YA HALI NA MALI ILI TUWEZE KUSAIDIANA HATA KAMA TIMU HIZI, ZITAKUWA NA MATOKEO TOFAUTI BAADA YA MCHEZO WETU JUMATANO," ALISEMA RAGE.
WAKATI HUO HUO, MWENYEKITI WA MATAWI YA SIMBA MKOANI TANGA, MBWANA MSUMARI ALISEMA KUWA MASHABIKI NA WAPENZI WA TIMU HIYO WA JIJI LA TANGA WAMEPANGA KUWAPOKEA KWA HOI HOI NA VIFIJO KWENYE ENEO LA PONGWE WATAKAPOINGIA SIKU YA JUMATATU AMBAPO MSAFARA WA BASI LILILOWACHUKUA WEKUNDU HAO WA MSIMBAZI LITASINDIKIZWA NA MSAFARA WA PIKIPIKI NA BAISKELI HADI NYINDA ILIKOFIKIA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment