MBWANA MSUMARI MENEJA WA UWANJA WA MKWAKWANI NA MWENYEKITI WA MATAWI YA SIMBA MKOANI TANGA. |
MCHEZO KATI YA COASTAL UNION NA SIMBA YA JIJINI DAR ES SALAAM UTAKAOCHEZWA KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI JUMATANO WIKI HII AGOSTI 24, VIINGILIO VYA MCHEZO HUO TAYARI VIMETANGAZWA.
MENEJA WA UWANJA HUO ALISEMA VIINGILIO VYA MCHEZO HUO VITAKUWA NI VYA AINA TATU, SH. 300 KWA WATAKAOINGIA RASHA, SH. 5000 UPANDE WA MAGOLI (reli 1Sports) na (reli 2 Coastal) NA SH. 7,000 UPANDE WA BANDANI NA SEHEMU ZA MBILI.
MSUMARI ALISEMA VIINGILIO HIVYO VIMEPANGWA KWA PAMOJA NA UONGOZI WA CHAMA CHA SOKA MKOANI TANGA (TRFA) KWA KUZINGATIA KWAMBA SIMBA NI MOJA YA TIMU YA KIMATAIFA HIVYO HATA VIINGILIO VYAKE VINAKUWA VYA JUU ILI KULIFANYA PAMBANO HILO KUWA MAALUUM 'SPECIAL GAME'.
WAKATI HUO HUO, TIMU YA SIMBA TAYARI IMEWASILI MKOANI HAPA NA KUFIKIA KATIKA HOTELI YA NYINDA CLASSIC AMBAPO JUMANNE ASUBUHI ITACHUKUA MAZOEZI KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI NA JIONI YAKE KABLA YA KUSHUKA DIMBANI KUMENYANA NA COASTAL UNION AMBAYO IMEJICHIMBIA KATIKA MJI WA MWAMBANI KUJINOA NA PAMBANO HILO.
No comments:
Post a Comment