Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach

Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach

Wednesday, December 8, 2010

SHEREHE ZA WATU WENYE ULEMAVU ZILIVYOFANA JIJINI TANGA

MOJA YA MABANGO BORA KABISA AMBALO LILISHIKWA NA WATU KUTOKA WILAYA YA MKINGA HEBU SOMA UONE.


WAPIGA PICHA TULIKUWA WENGI MNO LAKINI MAMA HUYU ALIKUWA SIYO MCHEZO KILA TUKIO BOMBA UTAMKUTA.

HAWA NAO WALIKUWEPO NA BANGO LAO CHEKI.


KWELI ELIMU JUMUISHI INAHITAJIKA NA MAZINGIRA PIA YAWE RAFIKI.



NI KWELI HAKUNA KITU KWA AJILI YA WATU FULANI.

BILA UKIMWI INAWEZEKANA, UTASHI WA MTU.

MSHEREHESHAJI AU MSEMA CHOCHOTE (MC) DADA YETU MAMA BENDERA BAADA YA YOTE ALIPATA MUDA WA KUMSALIMIA MWALIMU BENDERA TANGA SCHOOL.


MSANII HUYU NAYE ALIKUWEPO NA ALICHEKESHA KWELI KWELI.


INAWEZEKANA KABISA DADA ANGU WOTE TUWEKE NIA INAWEZEKANA KABISA.


Tuesday, December 7, 2010

KOMRADHI HATUKUWEPO HEWANI SIKU YA JANA NA LEO HADI MUDA HUU, HII INATOKANA NA SABABU ZISIZOZUILIKA

MZEE WA BONDE NA RAFIKI YAKE MMOJA AMBAYE ANASOMA SHULE YA MSINGI MAZOEZI WILAYANI KOROGWE BAHATI MBAYA RAFIKI YAKE HUYU HAJIJUI JINA LAKE, NI MTOTO MWENYE MTINDIO WA UBONGO.

Sunday, December 5, 2010

UKIIGA UTAHARISHA ACHANA NA DEGE KUBWA

AAAH ZIMEANGUKA CHINI.....!


SIZIACHI NAZIOKOTA HAPA PASAFI KALEMBO SI WANAFANYA USAFI WA JIJI, HALAFU TUMBO LANGU ZURI SIYO KAMA LAKO...!

HAA NAPIGWA PICHA?...!

TIGO ILIPOSHEREHEKEA NA WAUZAJI WAKE WA TANGA NA KUWAPA ZAWADI

WAKALA WA KAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI YA TIGO TAWI LA TANGA BW. CHRISS AKITANGAZA UTARATIBU KATIKA SHEREHE ZA KUWAPONGEZA WAUZAJI WA KAMPUNI HIYO MKOANI TANGA SHEREHE ZILIZOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA POPATLAL JIJINI TANGA.

CHRISS AKIWA NA MSHINDI AMBAYE NI MUUZAJI BORA ALIYEPATA SIMU YA MKONONI.

CHRISS AKIWA NA MSHINDI ALIYESHINDA PIKIPIKI AMBAYO ILIKUWA NI ZAWADI KUBWA NA WENGINE WALISHINDA LAPTOP NA VITU VINGINE.

KALEMBO ALIPOKUTANA NA KAMANDA SIRRO KIFUNGILO

VIPI HABARI ZA MWANZA? MKUU WA MKOA WA TANGA MEJA JENERALI MSTAAFU SAIDI KALEMBO ALIPOKUTANA NA KAMANDA WA POLISI MKOANI MWANZA SACP SIMON NYAKORO SIRRO.

KAZI BADO IPO KUWATOA WATU KWENYE MAKAZI YASIYOKUWA BORA

NYUMBA YA MFUGAJI MMOJA WA KABILA LA KIMASAI KATIKA KIJIJI CHA KONJE WILAYANI HANDENI.


MFUGAJI HUYO HILI NI ZIZI LAKE LA NGOMBE, BADO SERIKALI INA KAZI KUBWA YA KUWAHAMISHA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUJENGA NYUMBA BORA.


Saturday, December 4, 2010

WAFANYA SHEREHE KUFURAHIA RAS KUSTAAFU KWA LAZIMA

RAS PAUL CHIKIRA
           Na Mwandishi Wetu,Tanga
BAADHI ya wafanyakazi  katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na hospitali ya mkoa ya Bombo waliokuwa chini ya Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, mwishoni mwa wiki walifanya sherehe kufurahia kustaafu kwa lazima kwa Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Paul Chikira.
Wakizungumza katika sherehe hiyo iliyokuwa na wafanyakazi wapatao 26 kutoka sekta mbalimbali zilizokuwa chini ya RAS huyo na wengine wakitokea katika wilaya za Mkinga, Pangani, Handeni na Korogwe, walisema wanafurahia kiongozi huyo kuondoka kwa kuwa aliwachosha muda mrefu kufuatia kuwagawa katika makundi ikiwemo kupendelea watu wa kabila lake.
“Kwa kweli tumefurahi mno huyu bwana hakuna mtu aliyekuwa akimpenda wapo Wakuu wa Wilaya wametupigia simu kutuunga mkono katika sherehe hii kwa vile hata wao alikuwa mzigo kwao…Yupo DC mmoja alikubaliwa kwenda kusoma na Waziri Mkuu lakini RAS huyu hakumruhusu,” alisema mmoja wapo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazeti.
Wafanyakazi hao walisema pamoja na Bw. Chikira kutakiwa kuwa likizo tangu Desemba Mosi mwaka huu lakini wanamshangaa hadi leo yupo kazini licha ya Rais Jakaya Kikwete kumteua aliyekuwa msaidizi wa Waziri Mkuu Bw. Benedict Ole Kuyan kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa huo ambaye wafanyakazi hao wamefurahi wakidai ni kiongozi watakayempa ushirikiano mkubwa.
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu wafanyabiashara hao kufanya sherehe ikiwemo kuendelea kuwepo ofisini Bw. Chikira alisema wafanyakazi hao wana uhuru wa kidemokrasi kufanya sherehe hizo na akawatakiwa sherehe njema na suala la yeye (Chikira) kuendelea kuwepo ofisi hadi sasa amewaeleza waende kumuuliza Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo.
“Wafanye tu sherehe hiyo ni demokrasia yao siwezi kuwazuia ni utashi wao wachinje hata Ngamia, ngombe, Kondoo kusherehekea mimi kuondoka ni utashi wao na kueleza kwamba hadi leo nipo ofisini wamuulize Chief Secretary (Katibu Mkuu Kiongozi)yeye ndiye anajua mimi utumishi wangu wa umma unakoma lini?, alisema Bw. Chikira na kuhoji.
Alisema kwamba madai ya kuendesha ukabila kipindi chote alichokuwa RAS mkoani Tanga tangu mwaka 2004 alipohamia kutoka mkoani Morogoro, Bw Chikira alisema kuwa amefanyakazi yake kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa uma hivyo wafanyakazi hao kusherehekea ni mtizamo wao uliojaa chuki kwake.
Hata hivyo, alisema yeye ataendelea kuwepo ofisini kwake hadi Desemba 30 mwaka huu utakapokoma rasmi utumishi wake wa umma ingawa alipoulizwa kwamba kisheria alitakiwakuchukua likizo mapema mwezi huu alisema siyo lazima kufanya hivyo na hawezi kuondoka kwa shinikizo la wafanyakazi hao.

POLISI MBEYA WAMKAMATA MWENYEKITI WA WAFANYABIASHA KISA AMEWAZUSHIA KUIBA BIDHAA ZAO WAKATI MOTO UKIWAKA

WAFANYABIASHARA WAKIHAHA KUKIMBIZA MALI ZAO BAADA YA SOKO LA UHINDINI KUUNGUA MOTO

          NA MDAU MWANAKATWE,MBEYA 
SAKATA la Polisi kudaiwa kuiba mali za wafanyabiashara wakati soko la Uhindini, Jijini Mbeya lilipokuwa likiteketea kwa moto limeingia katika sura mpya baada ya Mwenyekiti wa soko hilo,Emily Mwaituka kukamatwa na Polisi na kufunguliwa jalada la kesi akituhumiwa kulidhalilisha Jeshi hilo.
Mwenyekiti huyo ametiwa mbaroni siku moja tu baada ya soko hilo kuungua huku wafanyabiashara wakiendelea kuomboleza kufuatia hasara ya mamilioni ya fedha waliyoipata kutokana na moto kuteketeza soko hilo juzi.
Kukamatwa kwa Mwaituka kumefuatia madai aliyoyatoa juzi na kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa Polisi walishiriki kuiba mali za wafanyabiashara, ambazo zilikuwa zikiokolewa kutoka kwenye maduka ambayo yalikuwa hayajashika moto.
Akizungumza na blog hii muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mwaituka alisema alikamatwa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, ikiwa ni muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile ili kufanya tathimini ya tukio hilo la moto.
Mwaituka alisema wakati wa kikao hicho ambacho yeye alialikwa, alisema kuwa alishuhudia kwa macho yake magari ya Polisi yakisomba mali za wafanyabiashara zilizokuwa zikiokolewa kutoka kwenye maduka ambayo yalikuwa hayajashika moto.
Alisema baada ya kumalizika kwa kikao, Kamanda Nyombi alimkamata na kumpeleka Kituo cha Polisi kati, ambako alimkabidhi kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ili achukue maelezo yake.
Kwa mujibu wa Mwaituka, alipofikishwa kituoni hapo alitakiwa kutoa maelezo kuhusu madai aliyoyatoa, kuwa Polisi walishiriki kuiba mali za baadhi ya wafanyabiashara wenye maduka yaliyopo katika soko hilo lilipokuwa linateketea kwa moto.
"Kwenye kikao mimi nilisema kuwa niliona Defender nyeupe ya Polisi ikipakia bidhaa zetu, baada ya kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama kumalizika, RPC alinichukua, tukaenda naye hadi kituo cha Polisi akanikabidhi kwa Afisa wa upelelezi ili nitoe maelezo yangu, hapo nikafunguliwa jalada kuwa kwa kauli yangu ndani ya kikao eti nimelidhalilisha Jeshi la Polisi," alisema Mwaituka.
Hata hivyo Mwaituka hakutaka kuzungumzia zaidi suala hilo kwa madai kuwa ametakiwa arudi Polisi mchana kwa maelezo zaidi, ambapo aliwataka waandishi wasubiri hadi atakapototoka Polisi muda huo wa mchana.
"Tayari Polisi nimeshaandika maelezo yangu, wamesema wanaendelea na uchunguzi, hivyo wameniambia leo (jana) mchana niende tena Polisi, nawaomba msubiri nitoke huko mchana tutazungumza zaidi maana kwa sasa ninamambo mengi ya kufanya," alisema Mwaituka.
Blog hii ilipofika ofisini kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa kwa nia ya kutaka kuonana naye, alijibiwa na wasaidizi wake kuwa Kamanda Nyombi alikuwa amekwenda Tukuyu wilayani Rungwe ambako shughuli ya uchaguzi wa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani ilikuwa ikifanyika.
Hata hivyo mwandishi wa habari hii alijaribu kumpigia simu kupitia simu yake ya kiganjani, ambayo nayo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Kufuatia kukamatwa kwa Mwenyekiti huyo wa soko, wafanyabiasha wa soko hilo wamekuja juu na kuonya kuwa kama polisi wanataka kuwasha moto wa vurugu waendelee kumsumbua mwenyekiti wao kwasababu wanaamini kuwa alichokisema kuhusu polisi kuiba mali zao ni sahihi.
Wafanyabiashara hao walisema kama Polisi wanaona wanazushiwa suala hilo serikali ya mkoa wa Mbeya iunde tume huru kuchunguza suala hilo na wao wapo tayari kutoa ushahidi.
Usiku wa kuamkia juzi, soko kuu la Uhindini, lililopo katikati ya Jiji la Mbeya liliteketea kwa moto na kuwasababishia hasara kubwa wafanyabiashara wa soko hilo.
Wakati wa tukio hilo la moto, magari mawili ya Polisi yalitumika kubeba bidhaa zilizokuwa zikiokolewa kutoka ndani ya maduka ya wafanyabiashara na asubuhi yake wafanyabiashara walipokwenda Polisi kufuatilia bidhaa zao, hawakuridhika nazo kwa madai kuwa hazilingani na zile zilizokuwa zikipakiwa kwenye magari ya Polisi.
Hivi karibuni Mwaituka alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa alipofika Polisi juzi asubuhi alionyeshwa mabegi machache, vitenge na khanga, wakati usiku hule vilikuwa vikibebwa na vitu vingine vya thamani kama vile Televisheni, Komputa, pikipiki, majenereta na vingine vingi.

KILIMANJARO STARS YAIDUNGUA BURUNDI, YAFUDHU ROBO FAINALI


KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS


FURAHA WANAFUNZI WAKILA MAKANDE SHULENI KWAO

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KONJE ILIOPO WILAYANI HANDENI MKOANI TANGA WAKIFURAHI BAADA YA KUPATA CHAKULA CHA MCHANA AMBACHO KILIKUWA NI MAKANDE AU 'PURE'


WANAFUNZI WASHULE YA MSINGI KONJE WAKIPATA CHAKULA WAKIWA WAMEKAA KATIKA NYUMBA YA MWALIMU MKUU WA SHULE HIYO NA KUPATA MAKANDE HAYO


HAWA WENGINE WALIKUWA WAMEMALIZA KULA MAKANDE YAO LAKINI WALIPOMUONA MZEE WA BONDE AKIPIGA PICHA NAO WAKAFIKA ILI NAO WAUZE NYAGO


KIJANA AKIWA NA NONDO YAKE

MASHAKA KIBAYA AKIMPONGEZA MDOGO WAKE BAADA YA KUCHUKUA NONDO YAKE

USINGIZI HAUNA ADABU, UKISHIBA LAZIMA ULALE KIDOGO....!

BW. BEN 

!.....BREAKING NEWS...WAFANYAKAZI WA OFISI YA RAS TANGA WAANDAA SHEREHE, NI YA KUFURAHI RAS WAO KUSTAAFU.

KATIBU TAWALA (MSTAAFU) WA MKOA WA TANGA BW. PAUL AMANIEL CHIKIRA
BAADHI YA WAFANYAKAZI WALIOKUWA CHINI YA KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA, WAMEANDAA PATI KUBWA LEO KWENYE MOJA YA HOTELI ILIYOPO KATIKA JIJI LA TANGA KWA AJILI YA 'KUFURAHIA' HABARI KWAMBA RAS WAO BW. PAUL CHIKIRA AMESTAFU KWA MUJIBU WA SHERIA.

MMOJA YA WARATIBU WA SHERHR HIYO AMBAYE ALIMWELEZA MZEE WA BONDE KWAMBA SHEREHE HIYO ILIANZA JANA KWENYE ENEO MOJA YA SAHARE KISHA USIKU KUFUATIA NA MUZIKI KWENYE HOTELI YA TANGA HOTELI LAKINI SHEREHE RASMI ITAKUWA LEO AMBAKO KUTAKUWA NA DISKO PAMOJA NA NYAMA CHOMA NA MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA MMOJA WA MFANYAKAZI WA HOSPITALI YA BOMBO.

MRATIBU HUYO ALIMTONYA MZEE WA BONDE KWAMBA SABABU KUBWA YA KUANDAA SHEREHE HIZO, ALISEMA INATOKANA NA RAS HUYO KUWANYANYASA NA KUWAWEKA MAKUNDI WAFANYAKAZI HAO IKIWEMO KUPENDELEA WATU WA KABILA LAKE HATUA WALIYOIELELEZEA KWAMBA HAIKUWA IKIMFURAHISHA KILA MTU HIVYO FURAHA YAO WAMEONELEEA WASHEREHEKEE.

MRATIBU HUYO PAMOJA NA KUANDAA SHEREHE HIYO WAMEMSHANGAA KIONGOZI HUYO KUENDELEA KUWEPO OFISINI WAKATI ALITAKIWA TANGU DESEMBA MOSI MWAKA HUU AWE AMEANZA LIKIZO YA KUSTAAFU KWANI RAIS JAKAYA KIKWETE TAYARI AMEMTEA ALIYEKUWA MSAIDIZI WA WAZIRI MKUU BW. BENEDICT OLE KUYAN KUWA RAS MPYA WA MKOA WA TANGA KUANZIA DESEMBA 2 MWAKA HUU.

KUFUATIA KUCHELEWESHWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI, JESHI LA IVORY COAST LAFUNGA MIPAKA YAKE

                         Gbagbo na Ouatarra


Jeshi la Ivory Coast limefunga mipaka ya nchi hiyo na kuzuia vyombo vya habari vya nje kutoa matokeo ya uchaguzi wa nchi hiyo huku hali ya wasiwasi ikizidi kuongezeka kuhusiana na matokeo ya raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama ya Katiba kupinga matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi kuwa mgombea wa upinzani Alassane Ouattara ameshinda.

Wafuasi wa Rais Laurent Gbagbo walijaribu kuzuia kutoka kwa matokeo hayo yaliyocheleweshwa, wakidai umefanyika wizi wa kura katika eneo la kaskazini.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limetaka pande zote kuonesha uvumilivu.

"Mipaka yote, ya anga, ya ardhini na ya baharini imefungwa kwa watu na mizigo," amesema msemaji wa jeshi Babri Gohorou.

Mipaka hiyo itabaki katika hali hiyo mpaka tangazo lingine litakapotolewa, Bw Gohourou ameongeza.

Muda mfupi baadaye jeshi hilo lilitangaza "Kufungwa mara moja kwa matangazo ya vyombo vya habari vya kigeni" nchini humo ikiwemo CNN, France24 na Radio France International FM.

Tangazo la matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumapili, limecheleweshwa sana, na hivyo kusababisha kuwepo kwa hali ya wasiwasi nchini humo.

Wafuasi wa Rais laurent Gbagbo walijaribu kuzuia matokeo hayo kutoka, wakisema umefanyika wizi katika eneo la kaskazini ambapo Bw Ouattara ana umaarufu mkubwa.

Upande wa kaskazini unadhibitiwa na waasi wa zamani.

Thursday, December 2, 2010

WAPINZANIA WASHINDA IVORY COAST, MATOKEO YAZUIWA



MGOMBEA URAIS WA NCHI YA IVORY COAST BW. ALASSANE OUATTARA AKIFURAHI BAADA YA MATOKEO KUONESHA KWAMBA AMESHINDA UCHAGUZI WA RAIS WA NCHI HIYO KWA ASILIMIA 54%.

                               Na Mzee wa bonde na mashirika ya habari
KAMISHINA WA UCHAGUZI WA NCHI YA IVORY COAST BW. YOUSSOUF BAKAYOKO AMESEMA KUWA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA RDR BW. ALASSANE OUATTARA AMESHINDA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS WA NCHI HIYO LAKINI BARAZA LA KATIBA LENYE MAMLAKA YA KUTANGAZA MATOKEO HAWAJATANGAZA MATOKEO.

MTANGAZAJI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA BBC BW. JOHN JAMES ALIOPO KATIKA MJI MKUU WA NCHI HIYO ABIDJAN AMESEMA KUWA KUFUATIA KUTOTANGAZWA KWA MATOKEO HAYO GHASIA ZIMEANZA KUTOKEA BAADA YA MIILI MIWILI YA WATU KUOKOTWA WAKIWA WAMEKUFA.

WASAIDIZI WA RAIS ALIYEMALIZA MUDA WAKE BW. LAURENT GABGBO WAMEZUIA KUTANGAZWA KWA MATOKEO HAYO WAKIDAI KWAMBA BADO MATOKEO MENGINE KUTOKA KUSINI MWA NCHI HIYO HAYAJAKUSANYWA NA KUPIGA TAARIFA ZA USHINDI WA BW. OUATTARA.

KAMISHINA BAKAYOKO KATIKA TAARIFA YAKE ALISEMA KUWA BW. OUATTARA AMBAYE AMEJIPATIA UMAARUFU MKUBWA NCHINI HUMO, AMESHINDA KWA ASILIMIA 54 YA KURA ZOTE ZILIZOPIGWA JUMAPILI ILIYOPITA DHIDI YA ASILIMIA 46 ZA BW. GBAGBO.
Left: Laurent Gbagbo Right: Alassane Ouattara
Laurent Gbagbo (left)
  • Age: 65
  • Southerner, Christian
  • Former history teacher, now president
  • Took 38% of the first-round vote
Alassane Ouattara (right)
  • Age: 68
  • Northerner, Muslim
  • Economist and former prime minister
  • Took 32% of the first-round vote

NI URUSI KOMBE LA DUNIA 2018 NA QATAR 2022

NCHI ZA URUSI NA QATAR ZIMESHINDA UENYEJI WA KUANDAA KOMBE LA DUNIA KATIKA MCHUANO MKALI ULIOFANYIKA MAKAO MAKUU YA FIFA ZURICH USWISI.

URUSI IMESHINDA UENYEJI WA MWAKA 2018 BAADA YA KUPATA KURA 13 KATIKA MZUNGUKO WA PILI NA KUZIACHA NCHI ZA UHOLANZI-UBELIGIJI ZILIZOTAKA KUANDAA KWA PAMOJA ZILIPATA KURA 2 NA HISPANIA NA URENO PIA KUANDAA KWA PAMOJA ZILIAMBULIA KURA 7.

UINGEREZA ILIYOKUWA IMETAWALAKWENYE VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI VYA ULAYA VILIVYOKUWA VIKIIPIGIA CHAPUO ILITOLEWA KATIKA MZUNGUKO WA KWANZA BAADA YA KUPATA KURA 2 TU HUKU UHOLANZI NA UBELIGIJI WALIPATA KURA 4 HISPANIA NA URENO KURA 7 NA URUSI WALIPATA KURA 9.

SOMA MWENYEWE HAPA CHINI NAMNA KURA ZILIVYOKUWA....

2018 VOTING,
1st round: England 2 (eliminated), Netherlands-Belgium 4; Spain-Portugal 7; Russia 9
2nd round: Netherlands-Belgium 2; Spain-Portugal 7; Russia 13 (Russia obtain absolute majority)
 
KWA UPANDE WA QATAR JUMUIYA YA NCHI ZA KIARABU WALIIBUKA NA USHINDI KWA KUPATA KURA 14 KATIKA MZUNGUKO WA NNE NA KUISHINDA NCHI YA MAREKANI ILIYOPATA KURA 8.
 
QATAR AMBAYO ILIKUWA IMESHATANGAZA KWAMBA WANATAKA KUANDAA KWA KUFANYA MAAJABU YA KOMBE HILO KWA KUJENGA KIWANJA KITACHOTUMIKA KWENYE MASHINDANO HAYO NDANI YA BAHARI NA BAADA YA MASHINDANO HAYO KIWANJA HICHO WATAKIPELEKA KWENYE MOJA YA NCHI MASIKINI (sijui itakuwa Tanzania). PATA MATOKEO KAMILI JINSI KURA HIZO ZILIVYOPIGWA HAPA CHINI.
 
2022 VOTING
1st round: Australia 1 (eliminated); Japan 3; United States 3; South Korea 4; Qatar 11
2nd round: Japan 2 (eliminated); South Korea 5; United States 5; Qatar 10
3rd round: South Korea 5 (eliminated); United States 6; Qatar 11
4th round: United States 8; Qatar 14

KUUNGUA SOKO LA UHINDINI MBEYA, WAFANYABIASHARA WALALAMIKIA BIDHAA ZAO KUPORWA



WANANCHI WA JIJI LA MBEYA WAKIANGALIA MOTO UKITEKETEZA SOKO KUU LA UHINDINI LIKIUNGUA MOTO JUIZ USIKU
 


BAADHI YA WAFANYABIASHARA WAKIHAHA KUTAFUTA NJIA YA KUSALIMISHA MALI ZAO KATIKA MADUKA YALIYOKUWA JIRANI NA SOKO HILO (PICHA ZOTE NA MDAU WETU EMMANUEL LENGWA)
 

Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya
SOKO kuu la Uhindini lililopo katikati ya Jiji la Mbeya limeteketea kwa moto, huku Polisi  kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi wakidaiwa kushiriki kupora mali za wafanyabiashara ambao maduka yao yalikuwa yakiteketea. Hii ni mara ya pili kwa masoko makubwa kuteketea kwa moto jijini Mbeya ndani ya kipindi cha miaka minne, ambapo Desemba mwaka 2006, soko la Mwanjelwa nalo liliteketea kwa moto na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 800 kwa wafanyabiashara.
Moto huo wa jana uliowasababishia hasara kubwa wafanyabiashara wa soko hilo ulianza juzi majira ya saa 2:20 usiku na kuendelea kuteketeza maduka huku, Kikosi cha Zimamoto cha Halmashauri ya Jiji la Mbeya kikishindwa kuudhibiti moto huo.
Mdau wetu aliyefika mapema kwenye eneo la tukio alishuhudia baadhi ya wamiliki wa maduka wakihaha kuokoa mali zao ambapo vibaka nao walitumia fursa hiyo kukwapua bidhaa mbalimbali za maduka ya wafanyabiashara kwa kuyavunja hasa kutokana na kutokuwepo ulinzi madhubuti.
Wakati moto huo ukizidi kutanda katika soko hilo,gari la kwanza la Kikosi cha Zimamoto lenye namba za usajili SM 6039 liliwasili eneo la tukio majira ya saa 2:40 ambapo lilijaribu kuzima moto huo kwa dakika tano tu kabla ya kuishiwa maji.
Ubovu wa miundombinu hasa njia zan kuingia ndani ya soko hilo ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwa magari ya zimamoto kufanya kazi yake, hali iliyolazimu kuleta Tingatinga ambalo lilitumika kubomoa baadhi ya maduka ili kupata njia ya magari ya zimamoto kuingia ndani ya soko na kuendelea na kazi ya kuzima moto katika maduka yaliyokuwa yakiteketea kwa moto.
Gari jingine la kikosi hicho lenye namba SM 4524 liliwasili eneo la tukio saa 2:50 ambalo nalo kama ilivyokuwa kwa gari la awali pia liliishiwa maji hali iliyozua malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walianza kuwazomea askari wa kikosi hicho kwa uzembe.
Baadaye polisi wakiwa katika gari namba T 710 APB walifika eneo la tukio na kuanza kuwakamata vibaka ambao walikuwa wamechachama kuvunja maduka na kupora mali .
Hata hivyo Polisi hao walionekana wakizunguka baadhi ya maduka kuwazuia vibaka wasiibe lakini walizidiwa nguvu kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya vibaka ambao walifika eneo la tukio wakiwa zana za kubomolea milango.
Vibaka hao walifanikiwa kubomoa baadhi ya maduka yanayouza simu za mkononi na kuzikusanya kwa kuziweka kwenye mashuka waliyokuja nayo eneo la tukio.
Katika hali ya kushangaza magari ya polisi yenye namba za usajiri PT 1464 na PT 0796 yalionekana mara kadhaa yakisomba bidhaa za maduka yaliyokuwa yamevunjwa kabla ya kufikiwa na moto huo na kuzipeleka mahali kusipojulikana huku wananchi wakiamini kuwa bidhaa hizo zilikuwa zikipelekwa kituo cha polisi.
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na mdau wa globu hii jana asubuhi, wamedai kuwa mizigo iliyokuwa ikisombwa na magari hayo ya Polisi imeyeyuka.
“Usiku ule wakati bidhaa zetu ilikuwa ikipakiwa kwenye magari ya Polisi tulijua wanatusaidia kuokoa, lakini leo (jana) tulipowafuata watukabidhi bidhaa zetu, wanatuonyesha mabegi machache tu, kwa kifupi Polisi nao wameshiriki kuiba mali zetu,” alisema Mwenyekiti wa soko hilo, Emily Mwaituka.
Mwenyekiti huyo wa soko, alisema baada ya kuona hali hiyo, waliamua kuchukua hatua za kwenda kuonana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evance Balama ambaye aliwashauri kuwa wakamwone Mkurugenzi wa Jiji, Juma Rashid Idd  kwa kuwa soko hilo lipo chini ya Halmashauri ya Jiji hilo.
Mwaituka alisema walipofika kwa Mkurugenzi wa Jiji, aliwaeleza kuwa kulikuwepo na kikao cha Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhusiana na suala hilo, ambacho kilikuwa kimeitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,John Mwakipesile ofisini kwake kujadili suala hilo.
Hata hivyo mbali na magari ya Polisi, magari mengine yenye namba za kiraia nayo yalionekana katika shughuli za uokoaji wa mali, yakipakia bidhaa na kuondoka nazo.
Miongoni mwa magari yaliyoonekana yakipakia bidhaa kwenye maduka mbalimbali ni T 543 aina ya Nissan Patrol, T432 AEF, T 256 AEM, T 822, AGX, T 643 AMS aina ya Center, T 373 BBB aina ya Center, T257, ACK na T 695 ATS.


Tukio hilo la moto, lilisababisha baadhi ya watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka kutaka kujaribu kuingia katika Benki ya NMB tawi la Mbalizi Road iliyopo hatua tano kutoka sokoni hapo, hali iliyowalazimu Polisi kutumia nguvu ya ziada, ikiwemo mabomu ya machozi kuwatawanya vijana waliokuwa wameanza kujazana kwenye milango ya benki hiyo.
Na katika hatua nyingine, tukio hilo la moto lilimlazimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile  jana kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kwa ajili ya kujadili suala hilo.
Baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo ya ulinzi na Usalama, Mkuu huyo wa mkoa alizungumza na waandishi wa habari na katika hali isiyo ya kawaida, alisema kuwa anawasifu Polisi kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kudhibiti usalama wakati wa tukio la moto uliounguza soko la Uhindini.
“Nawapongeza Polisi kwa kazi kubwa waliyoifanya, kama sio wao hata maduka ambayo hayakuungua moto nayo yangevunjwa na vibaka, lakini pia nawapongeza Zimamoto kwa kufanikiwa kuudhibiti moto huo na mwisho naipongeza Halmashauri ya Jiji kwa ushirikiano waliouonyesha,” alisema Mwakipesile.
Alipotakiwa kuzungumzia madai ya Polisi na magari ya Polisi kushiriki kupora mali za wafanyabiashara wakati wa tukio hilo, Mwakipesile alisema mtu aliye na ushahidi autoe ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Alisema baada ya soko hilo kuteketea, ameagiza Halmashauri ya Jiji, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya na Wafanyabiashara waliothiriwa na moto huo kukaa pamoja na kuwapatia eneo jingine la kufanyia biashara wakati mipango ya kujenga upya soko hilo ikifanyika.
Alisema katika eneo hilo sasa litajengwa soko la kisasa kama ilivyo kwa Soko la Mwanjelwa ambalo baada ya kuungua hivi sasa linajengwa soko kubwa la kisasa kwa thamani ya Shilingi Bilioni 13 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.
Mwakipesile alisema kutokana na mipango ya kujenga upya soko hilo, hata wafanyabiashara wa maduka ambayo hayakuungua moto jana nao watahamishwa ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa katika eneo hilo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na kuwa hivi sasa timu ya wataalamu imeanza uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.
Hata hivyo taarifa za awali ambazo mwandishi wa habari hizi amezipata zinadai kuwa chanzo cha moto huo huwenda kikawa ni mamantilie wanaopika vyakula katikati ya soko hilo walisahau kuzima moto au ni hitlafu ya umeme hasa kwa kuzingatia kuwa moto huo ulianza sokoni hapo ikiwa ni muda mfupi baada ya kukatika kwa umeme katika mji wote wa Mbeya.
Jana Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alikataa kata kata kwa madai kuwa atatoa taarifa zaidi baadaye.
Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi,alifika eneo la tukio jana asubuhi kuwapa pole wahanga ambapo aliwaahidi kuwa atashirikiana nao kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu kuhakikisha kuwa wanapata maeneo mengine ya kufanyia biashara zao.

MAAMBUKIZI YA UKIMWI SASA WANAUME KUTAHIRIWA

MTANGAZAJI WA STAR TV NA REDIO FREE AFRIKA, KAKURU MSIMU AKIPIMWA MAGONJWA MBALIMBALI IKIWEMO UKIMWI, WATU WANATAKIWA PIA KUJENGA TABIA YA KUOPIMA MARA KWA MARA KUJUA AFYA ZAO.


UNAWEZA USIAMINI JUU YA SUALA LILILOIBUKA JANA KWENYE KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI AMBAKO KITAIFA YALIFANYIKIA MKOANI MOROGORO KULIKOIBUKA SUALA LA WANAUME KUTAIRI.

KWA WANAUME WA MIKOA YA PWANI HASA WENYE IMANI YA KIISLAMU HAWAWEZI KUELELWA SUALA HILO KWASABABU WAO KUTOKANA NA IMANI HIYO PINDI MTOTO WA KIUME ANAPOZALIWA BASI KABLA HAJATIMIZA SIKU 40 HUFANYIWA TOHARA (SUNA) KISHA HUTOLEWA NJE AMBAKO HUPIGIWA MAULIDI.

SASA SUALA LA KUTAIRI WANAUME LIMEKUJA KUKIWA NA HABARI KWAMBA WANAUME WENYE 'MIZUNGA' (AMBAO HAWAJATAIRIWA) WANATAKIWA KUFANYA HIVYO ILI KUJIEPUSHA NA UGONJWA HUO HATARI AMBAO BADO DAWA DUNIANI HAIJAPATIKANA. JAMANI HAYA SI MALIMWENGU BALI NI HADITHI ILIYOSADIKIKA NA KUSAWIRIWA NA VIONGOZI KWENYE KILELE CHA UKIMWI.

Wednesday, December 1, 2010

ULAYA WASIMAMISHA USAFIRI WA NDEGE KUTOKANA NA BARAFU KUZIDI

MOJA YA NDEGE IKIWA IMEZINGIRWA NA BARAFU NA NJIA YA KURUKIA NDEGE IKIWA IMETANDA BARAFU HIYO NDIYO HALI ILIOPO HUKO ULAYA.



BARAFU IMEENDELEA KULETA ADHA KUBWA KATIKA MIJI YA ULAYA BAADA YA KIWANJA CHA NDEGE CHA MJI WA GENEVA USWISI NA WATU NANE WANAHOFIWA KUFA NCHINI POLAND BAADA YA HALI YA HEWA KUBADILIKA NA KUTOKA NYUZI JOTO 20C HADI 4 F.

KUTOKANA NA HALI HIYO VIWANJA VYA NDENGE KATIKA MIJI YA UINGEREZA, PARISI NA USWISI VIMEFUNGWA ILHALI USAFIRI WA NDEGE KATIKA MIJI YA HISPANIA NA UJERUMANI UMEKUMBWA NA MATATIZO.

VIONGOZI MASHUHURI MBALIMBALI WALIKWAMA KUSAFIRI KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA ULAYA AKIWEMO WAZIRI MKUU WA HISPANIA JOSE LUIS RODRIGUEZ ZAPATERO ALICHELEWA KWENDA NCHI ZURICH, USWISI KUHUDHURIA MKUTANO WA SHIRIKISHO LA KABUMBU DUNIANI (FIFA) AMBAKO KULIKUWA NA UPIGAJI KURA KUCHAGUA MWENYEJI WA MASHINDANO YA SOKA YA DUNIA MWAKA 2018.

NCHINI URUSI KATIKA MJI WA KIBIASHARA WA MOSCOW NAKO KUMERIPOTIWA KUWA NYUZI JOTO LIMESHUKA KUTOKA NYUZI JOTO 23.6 C HADI KUFIKIA -10.5F HALI HIYO IMEINGIA KATIKA REKODI TANGU ILIPOTOKEA DESEMBA MOSI MWAKA 1831.

HUKO POLAND POLISI WA NCHI HIYO WAMETOA TAADHALI KWA WANANCHI WANAOISHI NYUMBANI KUACHA KUTOKA NJE BAADA YA WATU NANE KUGANDA KATIKA BARAFU NA KUFA.

BREAKING NEWS.................

!........SOKO KUU LA UHINDINI LILILOPO KATIKA JIJI LA MBEYA LIMEUNGUA MOTO, KWA MUJIBU WA MDAU WA BLOGU HII YA WATU NA MATUKIO BW. MWANAKWATE THOBIAS ANAELEZA MOTO HUO UMETOKEA USIKU NA TAARIFA ZAIDI TUTAWAJULISHENI IKIWEMO NA CHANZO CHA MOTO HUO NA HASARA ILIYOPATIKANA......!

BOZI BOZIANA KUFANYA ONESHO MKWAKWANI JUMAMOSI DES 4

BOZI BOZIANA AKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUWASILI NCHINI KUFANYA MAONESHO YAKE KWA KUSHIRIKIANA NA BENDI YA AFRICAN STARS TWANGA PEPETA.

DKT MWAKYEMBE AFURAHI KUFANYA KAZI NA MAGUFULI, ASEMA NI MCHAPAKAZI ASIYEKUBALI KUYUMBISHWA

NAIBU WAZIRI WA UJENZI DKT. HARRISON MWAKYEMBE

     


DKT HARRISON MWAKYEMBE AKIPONGEZWA NA WABUNGE WENZAKE MARA BAADA UA KUSOMA RIPOTI YA KAMATI ILIYOUNDWA KWA AJILI YA KUCHUNGUMZA SUALA LA RICHMOND

                       Na Mdau Thobias Mwanakatwe,Mbeya
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk.Harrison Mwakyembe, amesema amefurahisha  sana na uteuzi uliofanywa na Rais  Jakaya Kikwete na hasa kutokana na kumpangia wizara moja na Mhe.John Magufuri ambaye inafahamika kuwa ni kiongozi makini na mwenye misimamo asiyekubali kuyumbishwa katika utekelezaji wa kazi za umma.
 
Amesema hayo katika mahojiano na mdau huyu kwa simu muda mfupi baada ya kuapishwa jana/juzi na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dk.Mwakyembe alisema anajisikia vizuri sana kufanya kazi na Magufuri katika Wizara ya Ujenzi itakayoshughulikia ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege kwani ni kiongozi makini ambaye ana misimamo sana hasa katika suala la utekelezaji wa kazi za miradi maendeleo.
 
“Najisikia vizuri sana tena mno kufanya kazi na Magufuri kwani ni mtu ambaye ni mchapa kazi ambaye pia tumeshibana sana ,pia ni kiongozi ambaye ana msimamo katika kutumikia umma ambao unaeleweka asiyependa kuyumbishwa,”alisema Dk.Mwakyembe.
 
Dk.Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, alisema kimsingi ameupokea uteuzi wa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi kama changamoto kwake kwani kiongozi yeyote makini anapopewa jukumu kubwa kama la uwaziri inakuwa ni changamoto ambayo anatakiwa kuhakikisha anatimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi katika kuwaletea maendeleo wananchi.
 
Kuhusu ufisadi,Naibu Waziri huyo alisema kimsingi kwa kuwa suala la kupiga vita ufisadi na rushwa ni suala ambalo limetungiwa sheria kwa maana hiyo ndani ya serikali litaendelea kupigiwa kelele ili kuwepo na matumizi sahihi ya fedha za umma.
 
Dk Mwakyembe alianza kupata umaarufu kutokana na kuwa Mwenyekiti wa Kamati  Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura, iliyopewa Kampuni ya Richmond Development LLC, ya Hauston Marekani, ambapo aliyekuwa  Waziri Mkuu, Edward Lowassa,alitajwa kuhusika kuibeba kampuni hiyo kupata zabuni.
 
Dk. Mwakyembe katika ripoti yake, aliliambia Bunge kuwa, ushiriki wa karibu wa Lowassa katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura, si lazima uwe ushahidi kwamba kiongozi huyo wa kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond, lakini unaweza ukawa ushahidi wa staili yake ya kawaida kabisa ya uongozi katika kufuatilia masuala yote ya kitaifa kwa karibu, ikizingatiwa kwamba taifa lilikuwa katika kipindi kigumu cha ukosefu wa umeme.
 
“Mheshimiwa Spika, ushiriki huu wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura, si lazima uwe ushahidi wa kwamba kiongozi huyo wa kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa staili yake ya kawaida kabisa ya uongozi katika kufuatilia masuala yote ya kitaifa kwa karibu sana, tukizingatia kwamba nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme,” alisema Mwakyembe katika hatua moja ya awali ya ripoti yake.
 
Baadhi ya hoja zilizotajwa na Dk. Mwakyembe kuwa ziliishawishi kamati yake kuamini kuwa Lowassa alihusika kuibeba Richmond kupata zabuni hiyo, ni barua ya Katibu wa Lowassa ya Juni 21, 2006, B. Olekuyan, ya kuitaarifu Wizara ya Nishati na Madini kuwa Waziri Mkuu Lowassa amekubali mapendekezo na ushauri wa Waziri wa Nishati na Madini kama ulivyokuwa umeletwa.
 
“Aidha, baadhi ya nyaraka ambazo Kamati Teule ilipata katika uchunguzi wake zilionesha kuwa maelekezo na maamuzi mengi ya msingi yalikuwa yanafanywa na Waziri Mkuu badala ya wizara. Mfano ni barua kutoka Wizara ya Nishati na Madini kwenda kwa Waziri Mkuu tuliyoinukuu ukurasa wa 31 wa taarifa hii, ikitamka wazi kuwa GNT ilifanya majadiliano na Richmond Development Company LLC tarehe 8 hadi 16 Juni 2006 “kwa kuzingatia maelekezo” ya Waziri Mkuu,” alieleza Mwakyembe.
 
Kwamba, baada tu ya kupokea barua hiyo, Waziri wa Nishati na Madini aliandika dokezo kwa Katibu Mkuu wake akimtaka aiagize TANESCO iingie mkataba mara moja na Richmond Development Company LLC baada ya Waziri Mkuu kuidhinisha mapendekezo ya wizara.
 
Dk. Mwakyembe alisema kamati yake ilibaini kuwa hisia walizokuwa nazo viongozi wa ngazi mbalimbali wa TANESCO, uongozi wa kiimla wa wizara ulikuwa ukipata nguvu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
 
Kwamba kilichoonekana ni ukiukwaji wa sheria na utaratibu mzima wa uwajibikaji, na kwamba pamoja na dharura iliyokuwa ikilikabili taifa, serikali haipaswi kuwa kinara wa kuvunja sheria za nchi.
 
Aidha, Dk. Mwakyembe alisema kuwa baadhi ya mashahidi, wakiwemo waandishi wa habari waliinyoshea kidole Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa msingi wa ubabe uliokithiri wa Wizara ya Nishati na Madini katika kuibeba Richmond.
 
Alizitaja pia baadhi ya nyaraka ambazo kamati yake ilizipata katika uchunguzi wake, zilionyesha kuwa maelekezo na maamuzi mengi ya msingi yalikuwa yakifanywa na Lowassa badala ya wizara.
 
Alitoa mfano wa barua kutoka Wizara ya Nishati na Madini kwenda kwa Waziri Mkuu iliyonukuliwa ukurasa wa 31 wa ripoti ya kamati ikitamka kuwa Juni 8, 2006 GNT ilifanya majadiliano na Kampuni ya Richmond kwa kuzingatia maelekezo ya Lowassa.
 
Dk. Mwakyembe alilieza Bunge kuwa kamati yake pia ilibaini kuwa Julai 13, 2006 Waziri wa Nishati na Madini alimwandikia Katibu Mkuu wake kumweleza kuwa kwa mara nyingine amezungumza na Lowassa juu ya bei ya mitambo ya Aggreko.
 
Katika mazungumzo hayo, Lowassa alibaki na msimamo ule ule ulioelezwa na waziri kuwa aliagiza Richmond iulizwe kama inaweza kuzalisha Megawati 40 za umeme kwa bei isiyozidi senti 4.99 za Marekani na kama ikipatikana, basi ichukuliwe Richmond.
 
Dk. Mwakyembe ambaye wakati wote wa kusoma ripoti hiyo alionekana kutamka maneno bila kumung’unya, alisema kamati yake ililazimika kuwaita kwa mara ya pili Dk. Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na Katibu Mkuu wake, Mwakapugi, kwa ajili ya kuwahoji.
 
                                

HAPPY BIRTHDAY TO YOU MAMA KIKWETE

RAIS DKT JAKAYA KIKWETE AKIMLISHA KEKI MKEWE MAMA SALMA KIKWETE WAKATI WA HAFLA FUPI YA KIFAMILIA YA KUMPONGEZA MAMA SALMA KWA KUTIMIZA MIAKA 47, HAFLA ILIYOFANYIKA JANA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM (PICHA: NA FREDY MARO WA Ikulu)

NANI KAMA MAMA!!!!!!!?

WATAFUTWA KWA KUVUA MAJONGOO BAHARI

MAJONGOO BAHARI YAKIWA KWENYE OFISI ZA MACEMP ZILIZOPO JIJI LA TANGA.
                                  Na Mzee wa Bonde
IDARA ya Uvuvi kwa kushirikiana na Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Mwambao wa Pwani (MACEMP) Wilayani Mkinga, inawasaka wavuvi wanaodaiwa kuwa Wazanzibar wanaoendesha uvuvi haramu wa kutumia baruti na kuvua majongoo bahari yaliyozuiwa na serikali.

Wazanzibar hao wanaodaiwa wamefika katika vijiji mbalimbali vya ukanda wa bahari ya hindi ya wilayani hapa wakiwa na vibali vya kuvua samaki aina ya pweza, wanasakwa baada ya kubainika kuvua majongoo bahari yapatayo 82 yenye wastani wa uzito wa kilogram 132 na thamani ya shilingi mlioni 3.3.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Mratibu wa Mradi wa MACEMP Bw. Sylevester Givver alisema kuwa Wazanzibar hao walifika katika kijiji cha Mongavyeru kilichopo mpakani mwa Kenya na Tanzania kwa ajili ya uvuvi ujulikanao kwa jina la Dago, wamekuwa wakijihusisha na uvuvi haramu ukiwemo kuvua majongoo hayo bahari.

Alisema walifuatilia kwa kufanya doria usiku kuwasaka wavuvi haramu hao na ndipo walipofika kwenye nyumba moja huko Mongavyeru inayomilikiwa na mama aliyemtaja kwa jina la Tima Mohamed ambaye walipofika kundi la wanaume wavuvi walitoroka na hivyo kumtia mbaroni mwanamke huyo.

"Tulipompekua humo ndani tulikuta majongoo bahari yapatayo 82 yaliyokuwa na uzito kama kilogramu 132 hivi unajua majongoo haya kilo moja huuzwa kati ya sh. 20,000 hadi 25,000...Pia mle ndani tulikuta chupa 19 za gesi na chupa nne za baruti, ile nyumba ilikuwa imefungwa milango yote," alisema Bw. Givver ambaye wavuvi wilayani humo wamekuwa wakimsifu kwa jitihada zake za kuwapa mafunzo na mbinu mbalimbali za uvuvi wa kisasa.

Majongoo bahari kwa mujibu wa Givver, hivi sasa kuna mkakati wa kidunia uliopitishwa kuwalinda viumbe hao waliokuwa katika hatari ya kutoweka, wamekuwa wakiuzwa kwa wingi katika nchi za China, Hong Kong, Philipine na Vietnam ambako licha ya matuminzi ya chakula, utengenezaji peremende, soli za viatu na matumizi mengine, pia hutumika kutolea mahali kwa wanaume wanapotaka kuoa.

Hata hivyo, Ofisa huyo alisema mbali na kuwasaka wavuvi hao pia wamebaini kwamba wavuvi wanaotumia baruti na zana zilizokatazwa na serikali, wamekuwa wakitoka wilayani Tanga eneo la Kasera na Ngome Kisosora wanaotumia mwanya kuvua kwa kutumia baruti hatua ambayo tayari wanafanya doria ya mara kwa mara ili kudhibiti uvuvi huo.

MAJENGO YA ZAMANI KUFANYIWA UKARABATI PANGANI

Moja ya majengo makongwe ambayo ni kivutio kwa wageni  na kumbukumbu yaliyopo katika mji Mkongwe wa Pangani mkoani Tanga liliojengwa mwaka 1910. Taasisi ya Uzikwasa imechukua jukumu la kuyakarabati majengo hayo ili kumbukumbu hiyo muhimu isitoweke. PICHA NA RAMADHANI JUMA 
 
 
 
                              Na Mzee wa Bonde
TAASISI ya kiraia inayojishughulisha na masuala ya kijamii katika wilaya ya Pangani mkoani Tanga ya Uzikwasa imeanza kutekeleza mpango wa ukarabati wa majengo ya kale wilayani humo kwa lengo la kuyahifadhi ili yaendelee kuwa sehemu ya vivutio vya utalii na kumbukumbu ya wilaya hiyo kongwe.
 
Afisa ufuatiliaji na Tathimini wa taasisi hiyo Joseph Mushi alisema kuwa, wameamua kuchukua jukumu kama sehemu ya shughuli za kijamii na kwamba ukarabati huo utasaidia kuyafanya majengo hayo yaendelee kuwavutia watalii na kuhifadhi historia ya wilaya ya Pangani.
 
Alisema mpango huo ni mojawapo ya programu mbalimali za kijamii wanazozitekeleza kwa wakazi wa wilaya hiyo, ikiwemo ile ya kupambana na mimba za wanafunzi, pamoja na ndoa za umri mdogo.
 
Akielezea kampeni hiyo, mratibu wa Programu za kijamii wa taasisi hiyo Nickson Lutenda alisema kuwa, wakazi wa wilaya hiyo wameonesha mwamko mkubwa katika kampeni hiyo iliyolenga katika mabadiliko ya tabia kupitia njia za kuonesha filamu  na videkezo vya video.
 
“Wananchi wanafurahishwa sana katika vijiji vyote ambako tunaendesha programu hizo na tumeibua kesi nyingi sana za wanafunzi kukatisha masomo kwa kupewa  mimba…katika kijiji cha Mzambarauni baadhi ya wanafunzi waliokatisha masomo kwa kupewa mimba walitoa ushahidi wa wazi wa tatizo hilo” alisema.
  
Alisema kuwa, kwa ujumla taasisi hiyo imedhamiria  kupambana na matatizo yanayowakabili watoto na wanafunzi wa kike  wilayani humo, ikiwemo ndoa za kulazimishwa hasa kwa wasichana na wanafunzi wa kike, mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo, pamoja na ubakaji wa vikundi hali inayopelekea maambukizi ya ukimwi na kukwamisha vijana wengi kuendelea na masomo.

NHC WASOMBA MADAWATI BAADA YA KITUO CHA ELIMU CHA ENGUSERO KUSHINDWA KULIPA PANGO

ROLI LILILOKODISHWA NA KAMPUNI YA JUPITER WAKALA NA DALALI WA NHC MKOANI TANGA, LIKIPAKIA MADAWATI WANAYOSOMEA WANAFUNZI WA KITUO CHA ENGUSERO KILICHOPO ENEO LA GOFU BAADA YA MMILIKI WA KITUO HICHO KUSHINDWA KULIPA PANGO ANALODAIWA NA NHC HIVYO DALALI AMEAMUA KUSOMBA MADAWATI HAYO NA WANAFUNZI WAKISHANGAA NJE.


                 NA MZEE WA BONDE,TANGA
WANAFUNZI wanaosoma katika kituo cha Elimu cha Engusero cha Jijini Tanga wameutaka uongozi wa Kituo hicho kuwarudishia karo walizolipa kituoni hapo mwaka huu, ili wahamie katika vituo vingine kwa madai kuwa kituo hicho hakina walimu hali inayowafanya kila siku kufundishwa na mwalimu mpya.
 
Hali hiyo pia inadaiwa kumlazimu mkurugenzi wa kituo hicho PIUS YOHANA  kuingia darasani katika baadhi ya siku ambayo anakuwa amekosa hata mwalimu mmoja na kufundisha yeye mwenyewe licha kuwa haiwezi kazi hiyo.
 
Hayo yalibainishwa wanafunzi hao jana baada ya kituo hicho kunyang’anywa madawati na vifaa vingine kama kompyuta na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo ndilo linalomiliki majengo ya kituo hicho tawi la Sabasaba, kufuatia deni la shilingi milioni 1.1 alilokuwa akidaiwa mkurugenzi huyo kama kodi ya Pango.
 
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafunzi hao Mussa Kisoma, ada wanayotaka kurudishiwa na mkurugenzi huyo ni ile ya mwaka huu ambayo ni shilingi 280,000 kwa kila mwanafunzi, na kwamba kituo hicho kina takribani wanafunzi 400.
 
Ilidaiwa kuwa, baada ya kushindwa kulipa deni hilo kwa wakati, shirika la nyumba lilitoa tenda ya kutaifisha vifaa hivyo vya kujifunzia kwa kampuni ya udalali ya Jupiter, iliyofika kituoni hapo majira ya mchana na kuwatoa nje wanafunzi hao waliokuwa wanajisomea, kabla ya kuchukua madawati hayo na kompyuta na kuvipakiza katika lori.
 
Hata hivyo, wakati Jupiter wakitekeleza zoezi hilo , mkurugenzi huyo alifanikiwa kulipa deni hilo mara moja kwa mmliki huyo na kuruhusiwa kuendelea kutumia jengo hilo .
 
Meneja wa shirika la nyumba la Taifa Mkoani Tanga, Damas Ngoiya alithibitisha mpangaji huyo kulipa deni hilo na kuruhusiwa kurudisha vifaa vyake katika jengo hilo , ikiwa pia ni baada ya kuilipa kampuni ya udalali iliyofanya kazi ya kukusanya vifaa hivyo.
 
“Naomba wateja wajenge tabia ya kulipa mapema kodi zao…hakuna haja ya kufikia hatua ya kunyang’anyana kwa kuwa ni usumbufu hata kwetu sisi” alisema Ngoiya.
 
Akizungumzia madai ya wanafunzi hao kutaka warudishiwe karo zao ili wakasome katika vituo vingine, mkurugenzi huyo alisema kuwa, hawezi kulitolea majibu ya haraka suala hilo kwa kuwa wanafunzi hao wamekwishatimiza sehemu kubwa ya mwaka wa masomo ikiwa ni pamoja na kusoma silabasi zote kwa baadhi ya masomo.
 
“Kwa sasa niko katika vikao na wenzangu siwezi sina majibu ya ya moja kwa moja lakini kimsingi mwaka wa masomo karibu unaisha na baadhi ya masomo wamemaliza silabasi” alisema mkurugenzi huyo.
 
Hata hivyo, wanafunzi hao  waliandama hadi katika ofisi za elimu za jiji la Tanga kuwasilisha kilio chao hicho na kuahidiwa kuwa, uongozi wa jiji utalifanyia kazi suala hilo .