RAS PAUL CHIKIRA |
Na Mwandishi Wetu,Tanga
BAADHI ya wafanyakazi katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na hospitali ya mkoa ya Bombo waliokuwa chini ya Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, mwishoni mwa wiki walifanya sherehe kufurahia kustaafu kwa lazima kwa Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Paul Chikira.
BAADHI ya wafanyakazi katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na hospitali ya mkoa ya Bombo waliokuwa chini ya Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, mwishoni mwa wiki walifanya sherehe kufurahia kustaafu kwa lazima kwa Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Paul Chikira.
Wakizungumza katika sherehe hiyo iliyokuwa na wafanyakazi wapatao 26 kutoka sekta mbalimbali zilizokuwa chini ya RAS huyo na wengine wakitokea katika wilaya za Mkinga, Pangani, Handeni na Korogwe, walisema wanafurahia kiongozi huyo kuondoka kwa kuwa aliwachosha muda mrefu kufuatia kuwagawa katika makundi ikiwemo kupendelea watu wa kabila lake.
“Kwa kweli tumefurahi mno huyu bwana hakuna mtu aliyekuwa akimpenda wapo Wakuu wa Wilaya wametupigia simu kutuunga mkono katika sherehe hii kwa vile hata wao alikuwa mzigo kwao…Yupo DC mmoja alikubaliwa kwenda kusoma na Waziri Mkuu lakini RAS huyu hakumruhusu,” alisema mmoja wapo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazeti.
Wafanyakazi hao walisema pamoja na Bw. Chikira kutakiwa kuwa likizo tangu Desemba Mosi mwaka huu lakini wanamshangaa hadi leo yupo kazini licha ya Rais Jakaya Kikwete kumteua aliyekuwa msaidizi wa Waziri Mkuu Bw. Benedict Ole Kuyan kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa huo ambaye wafanyakazi hao wamefurahi wakidai ni kiongozi watakayempa ushirikiano mkubwa.
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu wafanyabiashara hao kufanya sherehe ikiwemo kuendelea kuwepo ofisini Bw. Chikira alisema wafanyakazi hao wana uhuru wa kidemokrasi kufanya sherehe hizo na akawatakiwa sherehe njema na suala la yeye (Chikira) kuendelea kuwepo ofisi hadi sasa amewaeleza waende kumuuliza Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo.
“Wafanye tu sherehe hiyo ni demokrasia yao siwezi kuwazuia ni utashi wao wachinje hata Ngamia, ngombe, Kondoo kusherehekea mimi kuondoka ni utashi wao na kueleza kwamba hadi leo nipo ofisini wamuulize Chief Secretary (Katibu Mkuu Kiongozi)yeye ndiye anajua mimi utumishi wangu wa umma unakoma lini?, alisema Bw. Chikira na kuhoji.
Alisema kwamba madai ya kuendesha ukabila kipindi chote alichokuwa RAS mkoani Tanga tangu mwaka 2004 alipohamia kutoka mkoani Morogoro, Bw Chikira alisema kuwa amefanyakazi yake kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa uma hivyo wafanyakazi hao kusherehekea ni mtizamo wao uliojaa chuki kwake.
Hata hivyo, alisema yeye ataendelea kuwepo ofisini kwake hadi Desemba 30 mwaka huu utakapokoma rasmi utumishi wake wa umma ingawa alipoulizwa kwamba kisheria alitakiwakuchukua likizo mapema mwezi huu alisema siyo lazima kufanya hivyo na hawezi kuondoka kwa shinikizo la wafanyakazi hao.
No comments:
Post a Comment