Vipepeo ni moja kati ya vivutio vikubwa katika hifadhi asilimia ya misitu ya Amani ambayo imekuwa ikiwaingizia fedha nyingi baadhi ya wakazi ambao wanawafuga vipepeo hao kwa ajili ya kuwauza nje.
misitu minene inayopatikana katika hifadhi ya Amani wilayani Muheza ambayo mara nyingi ukipita huko unakuta vipepeo na wanyama wengine wagodo ikiwemo nyoka hatari.
Baadhi ya wakazi ambao hufanya shughuli zao katika msitu huo kama kulima iliki, pilipili manga na tangawizi ambazo hupatikana kwa wingi katika msitu huo.
Miti ya pilipili manga ikiwa imeuzunguka mti mwingine mkubwa, aina hiyo ya zao ni moja ya vivutio vikubwa vya kitalii kutokana na upanaji wake wa pilipili hiyo ambayo matawi yake huzunguka mti mkubwa kama unavyoonekana.
Blogu hii imedhaminiwa na Simba Video Coach
Kwa usafiri wa Dar es salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha, safiri kwa raha na Simba Mtoto Luxury Coach
Tuesday, November 9, 2010
Monday, November 8, 2010
Safari ya kuundwa baraza la mawaziri YAIVA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzani Dkt. Jakaya Kikwete ameridhia kuitishwa kwa bunge la 10 la jamhuri ya muungano ambalo sasa litafanyika kuanzia Novemba 12 hadi 17 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine litatumika kuapishwa kwa wabunge hao na kutoa fursa kwa Rais huyo kumchagua Wazii Mkuu na kuunda baraza lake la Mawaziri ambalo Watanzania wengi wana hamu ya kuona sura mpya zitakazoingia humo na kumsaidia kazi ya kuijenga Tanzania katika kipindi chake cha mwisho cha utawala wake wa miaka 10.
Makamo wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal aanza kazi rasmi
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Ghalib Bilal, akitia saini moja ya vitabu vilivyopo katika ofisi yake ikiwa ni ishara ya kuanza kazi rasmi baada ya kuapishwa.
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal akizungumza na wafnyakazi wa ofisi yake ambapo pamoja na kujitambulisha kwao, pia aliwaeleza kila mmoja kufanya kazi kwa kufiata kanuni, taratibu na sheria ili kutiminza wajibu wa kuwatumikia Watanzania.
NMB yakabidhi mipira kwa shule kumi za Jiji la Tanga
Ofisa Elimu sanaa na michezo wa Jiji la Tanga Baruti, akimkabidhi mwalimu Adelina wa Masiwani Shule ya msingi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Chumbageni (chini) wakihudhuria sherehe ya kukabidhiwa mipira kwa shule kumi za Jiji la Tanga na benki ya National Micro-finance bank (NMB) sherehe hizo zilifanyika katika shule hiyo ya Chumbageni Jijini Tanga. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Meneja wa NMB mkoani Tanga Mapunda.
Kitabu cha Business Cards Directory chaja 2011
Kitabu cha kwanza nchini Tanzania kitakachowaunganisha wafanyabiashara wote nchini Tanzania kitwaacho Business Cards Directory kinatarajiwa kuchapishwa toleo lake la kwanza mwakani ambacho hivi sasa kundi la watu mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wake Dr William Shao, wanakusanya kadi za wafanyabiashara hapa nchini.
Kwa mujibu wa Dr Shao ni kwamba wafanyabiashara watagharamia kiasi kidogo cha fedha na kwamba kadi hizo kupitia kirabu hicho kitaingizwa kwenye tovuti bure ya directory hiyo ambayo ni http://www.bizcard.co.tz/ humo utapata taarifa mbalimbali kuhusu mpango mzima wa business Cards Directory.
Kwa mawasiliano zaidi waweza kuwasiliana kwa email-info@bizcard.co.tz au mobile namba 0754-989837 au 0655-989837. Kwa mkoani Tanga waweza kuwasiliana na Mr Mashaka Mhando simu namba 0784/0767/0778/0713-471707 au email mashkando@hotmail.com.
Ewe Mfanyabiashara jitokeze uwe wa kwanza kutangaza katika kitabu hiki ambacho kitakusaidia kujulikana upo wapi badala ya kugawa business card ambayo mara nyingi huwa watu wanazipoteza katika kipindi kifupi unapompa sasa suluhisho la kadi hizo ni BUSINESS CARDS DIRECTORY...Karibuni wote.

Manchester bado pointi 2 kuifikia Chelsea
Manchester United 'almaaruf Man U' baada ya kuifunga Wolverhampton 2-1 katika mchezo mzuri na wa kupendeza ambao J.S. Park aliifungia timu yake hiyo goli la jioni lililoipa ushindi timu hiyo na kuikaribia kabisa Chelsea inayoongoza kwa kuwa na pointi 25 dhidi ya 23 za Manu U....Kidogo kidogo wataachia tu kama Yanga hapa Tanzania kwa Simba.
Balotell arudi uwanjani na kupiga bao 2
Mshambuli wa Manchestar City Mario Balotell (jezi 45) akishangilia baada ya kufunga bao la pili na la ushindi kwa timu yake leo baada ya kuifunga West Brominch bao 2-0, wengine pichani ni Tevez na Silva.
Arsenal yadunguliwa 0-1 na Newcastal
Mshambuliaji wa Newcastal Andy Caroll akishangilia bao aliloifungia timu yake baada ya mlinda mlango wa Arsenal Fabias kufanya uzembe wa kushindwa kuokoa mpira uliomgonga beki wake na mfungaji kufunga kirahisi kwenye uwanja wa Emerates mjini London.
Sunday, November 7, 2010
Mwandishi wa Mwananchi aukwaa udiwani pangani
Mwandishi wa Habari anayeaandikia gazeti la Mwananchi wilayani Pangani, John Semkande, ameibuka na ushindi mnono katika kinyang'anyiro cha udiwani kata ya Pangani Magharibi baada ya kumshinda mpinzani wake mkubwa Kitwana Seif wa Chama Cha Wananchi (CUF), Semkande ambaye aligombea kupitia CCM alipata kura 1,126 dhidi ya kura za Kitwana 589.
Akizungumza mara baada ya matokeo hayo Semkande ambaye alimshinda Abdalahaman aliyekuwa makamo mwenyekiti wa halmashauri ya Pangani, alisema kuwa atawatumikia wananchi wa kata hiyo kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya CCM waliyoinadi kuondoa kero zilizopokatika kata hiyo.
Alipoulizwa swali la kizushi kwamba kazi yake ya uanishi ataacha au la, Semkande alisema kuwa hawezi kuacha kwani pamoja na kufahamika katika harakati za kuwasaidia watu hata alipokuwa siyo kiongozi, pia kazi hiyo ilimuongezea umaarufu uliomfikisha hapo.
"Nitaandika tu habari hasa za halmashauri kama kutakuwa na wakuu wa idara wanachelewesha ilani yetu ya CCM kwa makusudi nitaandika kufichua ili mambo yaende si unajua kichaa kapewa rungu," alisema mheshimiw adiwani huyo.

Saturday, November 6, 2010
JK akimwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fredrick Werema ikiwa ni uteuzi wake wa kwanza tangu aapishe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano sherehe hizozilifanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo.
JK akila kiapo cha urais miaka mitano mingine
Rais Jakaya Kikwete akiapishwa na Jaji Mkuu nchini Augostino Ramadhani kutoka na kushinda urais kwa kupata asilimia 61.17 kaika matokeo ya jumla. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo.
Umati uliofika kushuhudia JK akiapishwa
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa Rais Dkt Jakaya Kikwete kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam
JK akikagua gwaride baada ya kuapishwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akikagua gwaride rasmi la vikosi vya ulinzi na usalama lililoandaliwa kwa ajili ya sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa uhuru Jijini Dar es salaam.
Friday, November 5, 2010
JK kuapishwa kesho uwanja wa Uhuru
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tikiti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dkt. Jakaya Kikwete, akionesha cheti cha ushindi wa mbio za urais uliohusisha wagombea saba wa vyama vya siasa vya upinzani kwa mashabiki na watu mbalimbali waliojiokeza kushuhudia NEC ikitangaza matokeo ya kinyang'anyiro hicho baada ya kutangazwa na Mwenyekiti wa NEC Jaji (Mstaafu) Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam, leo.
Lipumba ampongeza JK, amkabidhi ilani ya CUF
MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tikiti ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Rais Mteule Jakaya Kikwete kwa ushinda kinyang'anyiro cha urais kwa kupata takribani kura milioni 5.2 sawa na asilimia 61.17. Sherehe hizo zilifanyika kwenye ukumbi wa Karimmjee Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa NEC amtangaza JK kashinda
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa NEC Jaji Lewis Makame, leo alasiri amemtangaza rasmi mgombea wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kupata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17 ya kura halali zilizopigigwa ambazo ni 8,398,394 sawa na 97.36 akifuatiwa na Dkt Willbroad Slaa wa Chadema ambaye alipata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34.
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alishukuru kwa niaba ya wagombea wenzake licha ya kutoa ujumbe akiitaka tume ya taifa ya uchaguzi isijivunie matoeo hayo kutokana na idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura na kumkabidhi Rais mteule ilani ya CUF, alipata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06, mgombea wa APPT-Maendeleo Kuga mzirai alishika nafasi ya nne kwa kupata kura 96,933 sawa na asilimia 1.12.
Mshindi wa tano alikuwa Hashim Rungwe mgombea wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 26,388 sawa na asilimia 0.31, mgombea wa TLP Mutamwega mugaya alishika nafasi ya sita kwa kupata kura 17,482 sawa na asilimia 0.20 na mgombea wa UPDP Dovutwa Fahm ambaye alitangaza kujitoa alishika mkia kwa kujikusanyia kura 13,176 sawa na asilimia 0.15 ya kura zote halali zilizopigwa.
Katika matokeo hayo watu waliojiandikisha kupiga kura ni 20,137,303 waliopiga kura ni 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 na kura zilizoharibika ni 227,803 na kura halali zilikuwa ni 8,398,394 sawa na asilimia 97.36.

Lowasa naye akanusha kuhusika na uchakachuaji kura za Slaa
TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI NOVEMBA 5, 2010
Novemba 3,2010 mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt Willbroad Slaa aliwatuhumu makada 30 wa Chama Cha Mpinduzi (CCM) kuwa walifanya kikao cha kupanga kumwibia kura mjini Mwanza. Kati ya makada aliowatuhumu ni pamoja na mimi.
Napenda kuufahamisha umma kuwa habari hizi siyo za kweli kwasababu mwezi wote wa Oktoba nilikuwa jimboni kwangu nikifanya kampeni za kuwania ubunge jimbo la Mondoli. Sikupata kusafiri kwenda Mwanza hata siku moja, na siku iliyotajwa ya Oktoba 19, nilikuwa kwenye vijiji vya Mfereji na Enguiki nikifanya kampeni siku nzima.
Ukiacha tuhuma hizo, pia upo uvumi uliosambazwa kwambanilishiriki kikao cha mkakati wa kuchakachua kura, mjini Arusha kumsaidia mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt Batilda Burian, aweze kushinda kiti hicho. Nasema uvumi huo ni uzushi na siyo wa kweli.
Kutokana na yote haya, ninakwazika kwamba inaonekana katika nchi yetuumeanza kuingia utamaduni mpya wa kufanya siasa za uongo, uvumi, uzushi na kila aina ya hila kwa nia ya kujipatia ushindi. Kwa udhoefu wa mataifa mengine yaliyotuzunguka, ndani ya Afrika na sehemu nyinine duniani, amani hupotea kutokana na usambaji wa taairifa za uongo.
Mwasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alituachia amani na utulivu ambavyo ni tunu ya Taifa hili. Dalili zinazoonekana, kuna watu wanaelekea kuchoshwa na amani iliopo. Wanajianda kufanya vurugu, kuliiingiza taifa hili katika machafuko, na sijui wanafanya hivyo kwa maslahi ya nani.
Wito kwa Watanzania, ni kwamba tusiichoke amani. Amani tuliyonayo ndiyo iliyotutofautisha na mataifa mengi yaliyotuzunguka na kuifanya Tanzania nchi ya kupigiwa mfano. Tuelekeze nguvu zetu katika shughuli halali za kutuletea kipato zisizoharibu amani yetu. Tukiiharibu amani tuliyonayo, mwisho wa siku nchi yetu itatekeketea na sote hatutakuwa salama. Tutakuwa tumekwisha.
Mwisho, Namsihi Dk Slaa ajipe muda wa kuzifahamu vyema siasa za nchi hii. Asidanganywe na mahudhurio ya mikutano ya hadhara akadhani ndizo kura katika masanduku ya kupigia kura. Namsihi ajifunze zaidi jinsi ya kufanya siasa za kistaarabu bila kueneza, uvumi, uongo, chuki na uzushi vyenye kutetelesha amani ya nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.
EDWARD LOWASA, Mbunge Mteule jimbo la Mondoli.
Thursday, November 4, 2010
Slaa atoe ushahidi kama tumechakachua matokeo ya U-rais-Idara ya Usalama
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini Jack Mugendi Zoka akijitokeza kwa mara ya kwanza mbele ya Waandishi wa Habari nchini, kukanusha taarifa iliyotolewa na mgombea Urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt Willbroad Slaa almaarufu 'Mabunduki', kwama idara hiyo imehusika kuchakachua kura za Urais zilizopigwa na wananchi kwa kukipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho katika matokeo yanayotolewa na tume NEC mgombea wake Dkt Jakaya Kikwete anaongoza hadi sasa.
Zoka aliyemwakilisha Mkurugenzi wa idara hio Rashid Othman ambaye Dkt Slaa ametaka ajiuzulu kwaq kitendeo hicho, alisema kwamba hawahusiki kabisa na matokeo hayo ya kura zilizopigwa na wananchi na kwamba wamemtaka mombea huyo atoe ushahidi unaoonesha kwamba idara hiyo imehusika na 'uchakachuaji' huo wa matokeo hayo ya urais.
Katika tuhuma zake Dkt Slaa alisema anao ushahidi kwamba idara hiyo imehusika na hatua ya 'uchakachuaji' wa kura hizo kutkana na maokeo yanayotanazwa na NEC kuw ahayalingani na yale ambayo yeye kama ,mgombea matokeo aliyokuwa nayo hayalingani na yale yanayotangazwa akitolea mfano na jimbo la Maswa. Blogu hii ya Watu tunasema sisi tunaangalia je wananchi mnasemaje maana chombo hiki huwa hakitoki hadharani je kulikoni? toa maoni yako tuyajadili ukisoma habari hii.

Kuzunguka kote na Choper kura ndiyo hizi, Nimeibiwa hataaa.....!
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt Willbroad Slaa, akizungumza leo na vyombo vya habari vikiwemo vya nje (VOA) ambapo alitoa malalamiko yake kwamba haridhishwi na mwenendo wa utangazaji wa matokeo unaofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Dkt Slaa amehemwa! haamini kama ile Choper aliyokuwa akiitumia imezaa kura hizi zinazotangazwa na NEC.
Samwel Sita adaka fomu ya usipika tena
Mh Samwel Sitta akichukua fomu yake ya kugombea tena nafasi ya Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa mkurugenzi wa uchaguzi wa CCM Matson Chizzi kwa mara nyingine baada ya kuliongoza bunge lililopita kwa ufanisi mkubwa. Kila la kheri.
Rais mpya wa SMZ huyu hapa
Rais mpya wa awamu ya saba Dkt Ali Mohamed Shein akila kiapo chake cha Urais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar mheshimiwa Hamid Mahamuod huku rais aliyemaliza myda wake Aman Abeid Karume akishuhudia.
Wednesday, November 3, 2010
Wabunge wapya Korogwe hawa hapa
Wabunge Wateule, Yusuph Nassir 'Obama' (kushoto) ambaye ni mbunge wa Korogwe Mji na Stephen Ngonyani "Profesa Majimarefu' ambaye amepata kura nyingi kuliko mbunge yeyote wa CCM mkoani Tanga baada ya kuvuna kura 41,377 na kuwashinda wapinzani wake wawili waliogombea jimbo hilo. Hapa wabunge hao wakiwapungia mashabiki wao walipokwenda kwenye ofisi za halmashauri kufuatilia matokeo.
Tuesday, November 2, 2010
Mama Mongella ashindwa Ukerewe
Aliyekuwa mbunge wa Ukerewe kwa miaka dahali Bibi Getrude Mongella ameangushwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge katika jimbo hilo.
Breeking news.................!
Mwana-DADA machachari bungeni na mwenye mvuto wa asili, Halima MDEE ametangazwa rasmi kushinda jimbo la Kawe Jijini Dar es salaam baada ya kuwabwaga wapinzani wake.Taarifa kamili tutaziweka soon.
Mnyika anyakua rasmi UBUNGO
HATIMAYE mwansiasa kijana machachari John Mnyika baada ya kuvumilia kwa miaka mitano kufuatia kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2005, sasa ametangazwa rasmi kushinda katika jimbo la Ubungo kwa kujikusanyia kura 66,743 na kumshinda mpinzani wake wa karibu bi Hawa Ngumbi wa CCM ambaye amepata kura 50,554. Mnyika ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema nafasi aliyoishika baada ya mwenye nafasi hiyo Dkt Willbrod Slaa kugombea nafasi ya Urais.
Shein Rais mteule Zanziabr
Demokrasia imefuatwa bila tabu, baada ya wananchi wa Zanzibar kupitisha katiba ya maridhiano ya kusaidia na kumaliza mizozo ya uchaqguzi, hatimaye uchaguzi umefanyika kwa amani na Dkt Ali Mohamed Shein ameibuka na ushindi mkubwa na hivyo kusubiri kuapishwa kwa nafasi hiyo.
Rais wa vyombo vya anga, ashinda
Mbunge mteule wa jimbo la Tanga kupitia CCM Injinia Omari Rashid Nundu ambaye ni Rais wa Jopo la wataalamu wa vyombo vya anga duniani, ametangazwa kushinda jimbo hilo kwa kupata kura kibao dhidi ya wapinzani wake wa vyama vya upinzani.
'Zindabaa' agaragaza wapinzani Tanga
MGOMBEA wa ubunge jimbo la Tanga Mjini kupitia Chama Cha mapinduzi (CCM) Injinia Omari Rashid Nundu 'Zindabaa', ametangazwa rasmi kushinda ubunge jimbo hilo kwa kupata kura 40,225 na kuwashinda wagombea wengine wa upinzani waliogombea naye.
Akitangaza matokeo hayo leo hii majira ya saa 8:15 usiku kwenye ofisi za Jiji la Tanga, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo bw. John Maheke Gikene, alisema aliemfuata mgombea huyo ni Mussa Mbaruk wa CUF ambaye amepata kura 24,262, mgombea wa Chadema Kasimu Amari Mbaruk kura 5,750 na Mohamed Mwinyimatano wa UDP aliambulia kura 429.
Gikene alisema jumla ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni 179,325 kura halali zilizopigwa ni 72,212 wakati kura 275 ziliharibika.
Akitangaza matokeo ya kura za urais alisema mgombea wa PPT-maendeleo Kuga Mziray amepata kura 306, CCM Jakaya Kikwete amepata kura 42,628, Dkt Willibroad Slaa wa chadema amepata kura 7,353, Prof Ibrahim Lipumba wa CUF amepata kura 20,188, Hashimu Rugwe wa NCCR-mageuzi amepata kura 116, Mutamwega Mugaya wa TLP amepata kura 42 na Dovutwa fahm wa UPDP ameambulia kura 29.

Monday, November 1, 2010
Lema ambwaga Waziri wa JK A-town
Mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini (A-town) kwa tiketi ya Chadema Bw. Godbless Lema, amemshinda mpinzani wake wa karibu Bi Batilda Burian abaye ni Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira baada ya kupata kura 56,569 dhidi ya kura za Burian 37,460. pichani mbunge huyo mteule akionoka katika ofisi za manispaa ya Arusha baada ya kutangazwa mshindi.
Vicent afuata nyazo za Makongoro Mara
Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema Bw. vicent Nyerere leo ametangazwa kuwa mbunge mpya wa jimbo la Musoma mjini baada ya kupata kura 21,335, mgombea wa CCM Bw. Vedasto Manyinyi kura 14,072, Afande Mustafa Wandi wa CUF kura 253, Chrisant Nyakitita wa DP kura 53 na bi Tabu Said machibya aliambulia kura 19 tu. Nyerere anaweka historia ya ukoo wa baba wa taifa hili kutwaa ubunge kwa vyama vya upinzani. Mwaka 2000 mwenyekiti wa CCM Bw. Makongoro Nyerere alishinda ubunge jimbo la Arusha kupitia chama cha NCCR-Mageuzi.
'Aaah haya bwani nimekubali'
Bi Monica Mbega ambaye ni mkuu wa mkoa wa kilimanjaro, aliangushwa vibaya kwenye matokeo ya ubunge katika jimbo la Iringa mjini.
'Aliyemshinda mama Mbega huyu hapa'
Mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msingwa ametangazwa kushinda jimbo hilo kwa kupata kura 17,742 dhidi ya mpinzani wake wa CCM Bi Monica Mbega aliyepata kura 16,916 ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Shibuda kidede Maswa
Mgombea ubunge wa jimbo la Maswa magharibi Bw. John Magale Shibuda ametangazwa kuwa mshindi wa jimbo hilo baada ya kumshinda mpinzani wake mkubwa wa Chama cha Mapinduzi, Shibuda hakupata kiti hicho hivi hivi bali alidiriki hata kuwekwa ndani ufuatia vurugu zlizotokeza kwenye mikutano ya kampeni.
Haya matokeo Jiji Vipi?
Kazi ya kusubiri matokeo ilikuwa kubwa katika jimbo la Tanga mjini kama wanavyoonekana waandishi wa habari kutoka kulia mwenye kamera ni mwandishi wa TBC Fatuma Matulanga na kushoto ni Lulu George wa Nipashe wakisubiria matokeo hayo kwa hamu kubwa, taarifa za awali ni kwamba mgombea wa CCM Omari rashid Nundu ameshinda.
'Matokeo bado hayajatangaza maeneo mengi'
Mtangazaji wa ITV na RadioOne, Mgosi William Mngazija, akituma habari katika kituo chake kuwapasha namna matokeo yalivyochelewa kutangazwa huku akipata chai na kipande cha mhogo kwenye ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mkinga leo alasiri kabla ya kutangazwa matokeo.
Mwandishi akipata Chai
Mmiliki wa blogu ya watu, Bw. mashaka Mhando akipata chai kwenye jengo la ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mkinga wakati akisubiri matokeo ya ubunge, urais na udiwani wa jimbo hilo, hapo ilikuwa ni majira ya 9.30 alasiri leo.
Kitandula kidedea Mkinga
Mbunge mteule wa jimbo la Mkinga mkoani Tanga, Bw. Dastan Luka Kitandula akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mikakati yake ya kutekeleza lani ilani ya CCM baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ya jimbo hilo.
Dkt Kigoda apeta ubunge Handeni
Na Mashaka Mhando,Tanga
WAGOMBEA wa ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika majimbo ya Handeni, Mlalo na Mkinga, wameshinda kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuwabwaga wapinzani wao wa vyama vya CUF na Chadema waliokuwa na wagombea.
Wakitangaza kwa nyakati tofauti Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la handeni Bw. Hassain Mwachibuzi, alisema Dkt Abdallah Kigoda mbunge mkongwe wa CCM ameshinda baada ya kupata kura 31,497 dhidi ya mpinzani wake wa chama cha chadema Saleh Mbwetto aliyepata kura 5,907 na mgombea wa CUF Aidano Shundi aliambulia kura 4,947.
Jimbo la Mlalo msimamizi wa uchaguzi Bi Lucy Msofe alimtangaza mgombea wa CCM Brigedia jenerali (Mstaafu) Hassain Ngwilizi ambaye alipata kura 24,122 dhidi ya kura 5,337 za mpinzani wake wa karibu mwandishi wa habari wa siku nyingi Bw. Charles Kagonji wa chama cha chadema ambaye alijiunga na chama hicho baada ya kushindwa kwenye kura za maoni na Ngwilizi. Bw. Gogola Sechonge wa CUF aliambalia kura 1,695.
Jimbo la Mkinga, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Bw. Filbert Ngaponda, alisema bw. Dastan Luka Kitandula wa CCM ameshinda kwa kura 19,667 dhidi ya mpinzani wake wa CUF Bw. Bakari Mbega aliyeambulia kura 11,252 kati ya kura halali 30,919 kati ya watu 31,647 waliojitokeza kupiga kura kati ya watu 64,833 waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo hilo.
Akitangaza kura za rais Bw. Ngaponda alisema mgombea wa CCM Jakaya Kikwete alipata kura 22,803 sawa na asilimia 73.62, mgombea wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba alipata kura 6,484 mgombea wa chadema Dkt Willbroad Slaa kura 1,083 na mgombea wa PPT-Maendeleo Bw. Kuga mziray alipata kura 485.
Wagombea wengine ni wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 54, mgombea wa UPDP Bw. Dovutwa fahm kura 35 na mgombea wa TLP Bw. Mutamwega Mugaya aliambulia kura 33.

Rais wa TFF akimuaga Super Coach
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Leodger Chilla Tenga, alikuwa ni miongoni mwa maelfu waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Syllesaid Mziray kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni Jijini Dar es salaam na baadaye alihudhuria mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni.
Sunday akitoa heshima za mwisho
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Sunday Kayuni akitoa heshima zake za mwisho kuuaga mwili wa marehemu Syllesaid Mziray 'Super Coach' katika viwanja wa Biafra kinondoni Jijini Dar es salaam.
Mbunge mteule wa jimbo la Korogwe Mji
Mbunge mteule wa jimbo la Korogwe Mji Bw. Yusuph Nassir 'Obama' akishangilia ushindi wake akiwa na katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Bw. Gustav Muba katikati na kada wa CCM na Jumuiya ya UVCCM wilaya ya Korogwe.
Obama ashinda ubunge Korogwe Mji
Na Mashaka Mhando,Korogwe
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Korogwe Mji kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Yusuph Nasir almaarufu 'Obama', ametangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho katika uchaguzi uliofanyika jana baada ya kuwashinda wagombea wengine watatu wa vyama vya upinzani.
Akitangaza matokeo hayo leo saa 5:00 asubuhi Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bi Christina Midelo alisema Obama amepata kura 12,090 kati ya kura 15,346 ya wapiga kura wote waliojiandikisha na kura 62 ziliharibika.
Bi Midelo alisema kuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw. Kalistus Shekibaha alipata kura 1,720, mgombea wa Chama Cha Wananchi (CUF) Bw. Juma Mgogo alipata kura 400 na mgombea wa chama cha SAU Bw. Tony Kamuhanda aliambulia kura 225.
Akitangaza matokeo ya urais, Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema mgombea wa CCM Bw. Jakaya Kikwete aliongoza kwa kupata kura 10,761, Dkt Wilbrod Slaa wa Chadema alipata kura 3,435, Profesa Ibrahim Lipumba alipata kura 394, Bw. Kuga Mziray wa APPT-Maendeleo kura 110, NCCR-Mageuzi mgombea wake Bw. Hashim Rugwe alipata kura 19, mgombea wa TLP Bw. Mutamwega Mugaya alipata kura 5 na mgombea wa UPDP Bw. Dovutwa Fahm alipata kura 4.
Obama ambaye alimshinda Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Bw. Joel Bendera mara baada ya kutangazwa mitaa mbalimbali ya mji wa korogwe vijana mbalimbali waling'ara kwa kupanda pikipiki mitaani, mgombea huyo alisema atahakikisha changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo, atazifanyia kazi ikiwemo kutekeleza ahadi alizozitoa kama zilivyoaanishwa kwenye ilani ya CCM.

Mbunge Mteule wa jimbo la Tanga Injinia NUNDU
Mzee wetu Makamba akimwambia Injinia Rashid Nundu kwamba utakapokuwa mbunge wa Tanga huo mshahara utakaouacha uhakikishe unauanzishia mfuko wa maendeleo kweli.
Picha za kukumbukwa
Waandishi wa habari wakichapa mwendo wa umbali wa kilomita tano kwa mguu, baada ya kufukuzwa katika mkutano wa kura za maoni za wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM uliofanyika katika kata ya Kiomoni nje kidogo ya jiji la Tanga. Kutoka kushoto ni Lulu george wa Nipashe, Mashaka Muhando wa Majira, Dege Masoli wa Nipashe na Raymond Minja wa kituo cha Redio Mwambao cha jijini Tanga.
Kwa kweli picha hizi haziwezi kusahauliwa katika mchakato wa kura za maoni za CCM katika wilaya ya Tanga...Zimewekwa wakati huu baada ya watu mbalimbali kuomba tufanye hivi.
Kwa kweli picha hizi haziwezi kusahauliwa katika mchakato wa kura za maoni za CCM katika wilaya ya Tanga...Zimewekwa wakati huu baada ya watu mbalimbali kuomba tufanye hivi.
Tukubali kupokea matokeo
Uchaguzi umefanyika kwa amani karibu vituo vyote hapa nchini imeripotiwa kwamba watu wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba ya kumchagua kiongozi wanaetaka.
Kimsingi kila Mtanzania ametumia nafasi hiyo kumchagua kiongozi anayemtaka hii inamaana baada ya kura kujulishwa matokeo yatatangazwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi katika kila jimbo na yale ya urais yatatangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC.
Swali linakuja je viongozi wa vyama watakubali kupokea matokeo hayo, kwa upinzani tumewashuhudia viongozi wake wengi wakisema watakubali matokeo pindi yatakapotangazwa lakini matokeo hayo yaoneshe dalili kwamba hakuna hila zozote ambazo zimetumika kukipendelea chama tawala.
Mimi nadhani viongozi wa vyama vya siasa wawaeleze wanachama na mashabiki wa vyama vyao kukubali matokeo na mshindi akitangazwa kila mmoja afanye shughuli zake ili kuepusha matukio ya umwagaji damu kama ambavyo tumeweza kushuhudia katika nchi jirani kwa udhoefu unaonesha kwamba matokeo yanapotangazwa ndiyo mara nyingi vurugu za kupinga matokeo hayo zinapotokea hatua ambayo inatokea umwagaji wa damu na vifo.
Tanzania hatuwezi kufikia hapo kama watu wanataka mabadiliko hawakatazwi na kura zao ndiyo zitahukumu kwa waliokaaa madarakani lakini kutokana na hali ilivyo JK atakuwa amepata ushindi mkubwa kutokana na mwelekeo unavyoonekana na matokeo ya awali yanavyoonekana.
Mikoa kama Tanga, Lindi, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Tabora na Singida taarifa zake zinaonesha kwamba CCM imepata ushindi mkubwa na mikoa ya Rukwa, Mbeya, Arusha, Songea, Shinyanga, Mara na Mwanza Chadema kinaonekana kuongoza kwa kura.
Kila lahei Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki TANZANIA!

Subscribe to:
Posts (Atom)